Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 29 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kuwasikia vijna ambao wanashiriki kongamano la vijana, wakieleza kuhusu mkataba wa zama zijazo na mchango wao katika kuutekeleza mashinani mwao. Pia tunakuletea muhtasari wa habar iza Sudan, Kura ya Knesset kuhusu UNRWA, na Siku ya kimataifa ya huduma, na mashinani.Baada ya Bunge la Israel hapo jana Oktoba 28 kupiga kura ya kuizuia Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) kufanya shughuli zake katika maeneo yote yaliyoko chini ya Israel, viongozi wa Umoja wa Mataifa kuanzia Katibu Mkuu Antonio Guterres wameendelea kupaza sauti kwamba kuizuia UNRWA ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa na italeta zahma kwa maisha ya watu katika eneo hilo la Mashariki ya Kati. Katibu Mkuu Guterres amesema analileta suala hili kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na atahakikisha Baraza hilo muda wote linakuwa na taarifa kwa kadri hali inavyoendelea.Ujumbe Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa  wa kutafuta ukweli nchini Sudan umesema katika ripoti yake mpya ya kina leo kwamba Vikosi vya wanamgambo wa RSF, ambavyo vimekuwa vikipigana na Jeshi la Sudan (SAF) katika mzozo unaoendelea nchini humo, vinahusika na kufanya ukatili wa kingono kwa kiasi kikubwa katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wao, ikiwa ni pamoja na ubakaji wa makundi na kuwateka nyara na kuwaweka kizuizini waathiriwa katika hali ambayo ni sawa na utumwa wa ngono.Na leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Usaidizi na Matunzo, makadirio mapya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi (ILO), yaliyotolewa leo yanaonesha takribani wanawake milioni 708 duniani kote wako nje ya nguvu kazi zenye ujira kwa sababu ya majukumu ya kutoa usaidizi au matunzo bila malipo. Utafiti huo umefanywa katika nchi 125.Mashinani leo tutakwenda katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Al Matar huko Kassala, Sudan, kusikiliza ujumbe kutoka kwa Ted Chaiban, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, aliyefanya ziara kambini humo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    11 min
  • WFP: Bila msaada wa kibinadamu Wasudan watakufa kwa njaa
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa. Vita vya kikatili nchini Sudan vimesababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani, imeandika WFP katika ukurasa wake wa X leo Oktoba 28 na kufafanua zaidi kwamba mtu mmoja kati ya watu wawili nchini humo anatatizika kupata mlo kila siku.WFP inaeleza kuwa njaa imethibitishwa Kaskazini mwa Darfur na mahitaji ya kibinadamu ni makubwa sana.Kabla ya taarifa hii ya leo ya WFP, jana kupitia pia ukurasa wa mtandao wa X, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Cindy McCain ambaye hivi karibuni alikuwa Sudan mojawapo ya maeneo yenye njaa zaidi duniani, ambapo watu milioni 25 wanakabiliwa na njaa kali ameandika kwamba WFP iko Sudan inatoa msaada wa kuokoa maisha lakini wanahitaji kwa haraka mambo matatu ambayo ni kuwafikia watu ili kuwasaidia, misaada kuweza kupita katika kila kivuko na usaidizi zaidi wa kimataifa kwa Wasudani walio katika mazingira hatarishi.Kwa miaka mingi, Sudan imekuwa ikisumbuka na migogoro. Mgogoro wa hivi karibuni zaidi, ulioanza Aprili mwaka jana 2023, umezua janga baya zaidi duniani la watu kuhama makwao na janga kubwa zaidi la njaa duniani linalosambaa Sudan, Sudan Kusini na Chad.
    2 min
  • Ushindi wa tuzo ya mtu bora wa mwaka wa UN ni ushindi kwa watu wa Kajiado wanaonufaika na mradi wetu - Kipeto
    Kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited wamiliki wa mradi wa nishati ya umeme itokanayo na upepo ya Kipeto Energy iliyoko Kaunti ya Kajiado nchini Kenya wamejitwalia tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa. 2024”Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo anasema ushindi huo ni kwa watu wa Kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambao ni wanaufaika wakubwa wa mradi kwani sio tu umewaletea umeme, bali pia umewainua kiuchumi na kijamii kwa miradi mingine mbalimbali kama inabobainisha makala hii iliyoandaliwa na Flora Nducha..
    4 min
  • 28 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia janga la nja linalokumba wananchi waathirika wa mizozo nchini Sudan, na simulizi za walinda amani wa UNIFIL nchini Lebanon. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Haiti, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, (WFP) leo kwa mara nyingine tena limetahadharisha kwamba bila msaada wa kibinadamu nchini Sudan, mamia ya maelfu wanaweza kufa kwa njaa.Kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, ambapo, katikati ya mvutano unaoongezeka kati ya Lebanon na Israel, walinda amani walioko katika makao makuu ya UNIFIL huko Naqoura wamekuwa wakivumilia mazingira magumu. Ushuhuda wa hivi karibuni kutoka kwa walinda amani hao unaonesha ukubwa wa changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwemo vitisho vilivyoongezeka kutoka kwa shughuli za kijeshi za Israel zilizo karibu na eneo hilo, vizuizi vya kusafiri, na changamoto za uendeshaji wa shughuli.Makala inatupeleka Nairobi Kenya kwa washindi waliotwaa tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa 2024” ambao ni kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited wamiliki wa mradi wa nishati ya upepo ya Kipeto Energy iliyoko Kaunti ya Kajiado nchini Kenya.Katika mashinani mashinani leo tutakuwa Haiti ambapo nafasi ni yake Andre Rose, mama wa kijana Kerby, akieleza jinsi msaada wa kifedha unaotolewa na Shirika la UNICEF umekuwa mkombozi kwa familia yake iliyolazimika kukimbia makazi yao kutokana na ghasia za magenge ya uhalifu nchini Haiti.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
    10 min
  • Walinda amani wa UNIFIL nchini Lebanon wasimilia kinachowakabili mashambulizi ya Israel yakiendelea
    Kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, ambapo, katikati ya mvutano unaoongezeka kati ya Lebanon na Israel, walinda amani walioko katika makao makuu ya UNIFIL huko Naqoura wamekuwa wakivumilia mazingira magumu. Ushuhuda wa hivi karibuni kutoka kwa walinda amani hao unaonesha ukubwa wa changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwemo vitisho vilivyoongezeka kutoka kwa shughuli za kijeshi za Israel zilizo karibu na eneo hilo, vizuizi vya kusafiri, na changamoto za uendeshaji wa shughuli. Kupitia video ya  Kikosi hicho cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, tunaona picha ya makao makuu yake huko Naqoura, Lebanon. Hapa tunaona ofisi za walinda amani hao, karibu na ofisi hii kuna mnara wa ulinzi, sehemu yake ikiwa imeharibiwa na mlipuko. Meja Kalpani Fernando anaelekeza kwenye mnara huo akieleza kilichotokea.“Ghafla, tuliona, na kusikia mlipuko. Kisha tukaona vumbi kubwa likitokea na moshi mweusi. Tulikimbia ndani ya ofisi, na ndani ya sekunde chache, mlipuko wa pili ulitokea. Kisha wanajeshi wawili kati ya kikosi changu walijeruhiwa walipokuwa wakifanya kazi katika Kituo cha Uangalizi cha 6. Walikuwa nje ya Kituo cha Uangalizi wakati huo, na walijeruhiwa kutokana na mlipuko wakati huo. Kisha nikafunga lango, na tukawapeleka hospitalini ndani ya muda wa dakika mbili hadi tatu.”Ingawa mzozo huu umesababisha madhara kwa afya ya walinda amani hawa, huku baadhi yao wakipata upasuaji kutokana na majeraha, bado wanaendelea kuwa na dhamira ya kuhudumu katika ujumbe wa kulinda amani. Mmoja wao ni Koplo Wickramage akisema….‘‘Wakati nilipokuwa kwenye zamu katika Kituo cha Uangalizi cha 6, kulitokea mlipuko na nikajeruhiwa kwenye sehemu ya nyuma ya bega langu. Nilihamishwa haraka kwenye hospitali ya UNIFIL. Nimefanyiwa upasuaji, na ninaendelea na matibabu. Sasa, ninapata nafuu na natumai kuungana na walinda amani wa Sri Lanka hivi karibuni ili kurudi kuhudumu katika UNIFIL.”Mbali na majukumu yao ya kawaida, wafanyakazi wa afya wa UNIFIL wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii, wakitoa huduma si tu kwa walinda amani waliojeruhiwa bali pia kwa raia walionaswa katikati mwa mapigano hao kama anayoeleza Luteni Kanali Shilpi Mankotia,“Mbali na huduma za kawaida za matibabu, siku hizi tunatoa msaada na huduma kwa majeruhi na manusura waliolengwa kimakosa, ikiwa ni pamoja na raia na wahudumu wa kibinadamu. Nilikuwa kwenye likizo niliposikia kuhusu mzozo  unaoendelea kwa sasa. Nilirudi kazini mara moja kutoka India. Nilifika Beirut usiku wa manane na baada ya kupambana kwa siku saba, hatimaye niliweza kurudi kwenye kituo changu cha kazi.”
    3 min
  • Ushindi wa mradi di wa Kipeto UN n ushindi wa wananchi wa Kajiado: Mnufaika
    Kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited inayoendesha Mradi wa Kipeto Energy jana Siku ya Umoja wa Mataifa ilitwaa tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa.”Mradi wa Kipeto wa kampuni hiyo unatoa nishani ya umeme kwa kaya 250,000 katika eneo la Esilanke kaunti ya Kajiado nchini Kenya ukizalisha megawati 100 za umeme tangu 2021 ambazo zinaingizwa kwenye gridi ya taifa, lakini pia unasaidia kuwajengea wananchi nyumba bora na kuwapa huduma muhimu ya maji. Stela Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amezungumza na mmoja wa wanaufaika wa mradi huo wa nishati ya upepo ya Kipeto kuhusu faida za mradi huo,  na anaanza kwa kujitambulisha..
    4 min
  • Grandi: Msaada wa haraka unahitajika DRC wakati wakimbizi wanaendelea kufungasha virago
    Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wanaendelea kukimbilia Uganda kukwepa machafuko nchini mwao, huku rasilimali zikikaribia kikomo. Ameonya Kamishina mkuu wa  shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi, akiwa ziarani nchini Uganda hivi karibuni kwenye kambi inayohifadhi wakimbizi wa DRC na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuongeza msaada.Wakimbizi wanaokimbia mzozo  nchini DRC wanashuhudia matukio ya kutisha ya mauaji na ubakaji amesema Grandi, alipotembelea kambi ya ......aliyetembelea kambi za wakimbizi, Uganda na kusimuliwa hadithi za uchungu mkubwa“Sijawahi kusikia simulizi za machungu na hofu kama hizi za mauaji, ubakaji wa watoto mbele ya mama zao, wanawake wajawazito kukatwa vipande na makundi yenye silaha, na hofu kutawala maeneo yote ya Mashariki mwa Congo.”Kutokana na hali hii, Grandi anasema amani ndiyo inahitajika zaidi kwa sasa ili kumaliza dhuluma zinazowakumba wakimbizi wa Congo.“Ni wakati sasa jamii ya kimataifa ijitolee kwa dhati kusaidia Congo kutoka kwenye hali hii. Nilifanya kazi kama afisa wa eneo zaidi ya miaka 30 iliyopita Mashariki mwa Congo, na hali haijabadilika kimsingi.”Uganda inahifadhi jumla ya wakimbizi...... wengi wakiwa kutoka DRC, Sudan na Sudan Kusini.
    2 min
  • 25 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na ujumbe wa Filippo Grandi wa UNHCH ambaye yuko ziarani Uganda. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini DRC, kulikoni?Hali Gaza inaendelea kuwa tete wakati ucheleweshwji wa kuhamisha wagonjwa hususan watoto wanaohitaji msaada wa haraka wa huduma za afya imekuwa ni hukumu ya kifo kwao huku maelfu ya watu wakiendelea kukosa mahitaji ya muhimu ya kila siku ikiwemo chakula kama mkate, yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa.Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wanaendelea kukimbilia Uganda kukwepa machafuko nchini mwao, huku rasilimali zikikaribia kikomo. Ameonya Kamishina mkuu wa  shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi, akiwa ziarani nchini Uganda hivi karibuni kwenye kambi inayohifadhi wakimbizi wa DRC na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuongeza msaada, kama inavyoeleza taarifa ya Bosco Cosmas.Makala inayotupeleka Nairobi Kenya kwake Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi akizungumza na mmoja wa wanaufaika wa mradi wa nishati ya upepo ya Kipeto Energy unaoendeshwa na kampuni ya Craftskills Wind Energy International Limited ambayo jana Siku ya Umoja wa Mataifa ilitwaa tuzo ya “Mtu Bora wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa” inayotolewa kila mwaka.Mashinani leo tutaelekea Beni, Kivu Kaskazini kusikia jinsi MONUSCO unavyowasaidia wanawake walio katika mazingira magumu, mmoja wao ni Salome Tatsopa ambaye ni mnufaika wa masomo ya ufundi wa cherahani akitueleza matumani yake baada ya mafunzo hayo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • UN: Hali si hali tena Gaza vifo vyatawala hospitali na kwa raia hata mkate ni adimu kupatikana
    Hali Gaza inaendelea kuwa tete wakati ucheleweshwji wa kuhamisha wagonjwa hususan watoto wanaohitaji msaada wa haraka wa huduma za afya imekuwa ni hukumu ya kifo kwao huku maelfu ya watu wakiendelea kukosa mahitaji ya muhimu ya kila siku ikiwemo chakula kama mkate, yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeonya kwamba idadi ya watoto wanaohamishwa Gaza kwa ajili ya huduma za dharura za matibabu imeshuka sana hadi kufikia mtoto mmoja kwa siku na kusema kiwango hiki kikiendelea itachukua zaidi ya miaka 7 kuhamisha watoto 2500 wanaohitaji huduma ya dharura ya matibabu.Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa UNICEF James Elder amesema “matokeo yake watoto wanakufa Gaza sio tu kutokana na mabomu na risasi na makombora yanayofurusmishwa lakini kwa sababu hata kama miujiza inatokea , hata kama mabomu yanalipuka na nyumba kuporomoka, na vifo kuongezeka watoto wananusurika, lakini kisha wanazuiliwa kuondoka Gaza Kwenda kupokea huduma za afya zitakazookoa maisha yao.”Ameongeza kuwa tangu Januari hadi Mei mwaka huu kwa wastan watoto 296 walihamishwa kwa mwezi kwenda kupata matibabu lakini tangu kufungwa kivuko cha Rafah idadi imeshuka hadi watoto 22 kwa mwezi.Kwa upande wake shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA linasema maisha ya kawaida yanazidi kuwa jinamizi kwani kukidhi mahitaji ya msingi kama chakula ni mtihani mkubwa wengi mathalani katika mji wa Deir al-Balah hata mkate ambao ni chakula kikuu kupatikana ni changamoto,Kila mtu katika Ukanga wa Gaza anakabiliwa na hatari ya baa la njaa kutokana na kuendelea kwa mashambulizi ya mabomu, ghasia, kuharibiwa kwa mashamba na wahudumu wa kibinadamu kushindwa kuwafikia wenye uhitaji.Wataalam wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu nao wamesema wanahofia hali mbaya ya Wapalestina wenye ulemavu ambao wamekwama Gaza, wakionya kwamba watu hao wenye ulemavu wanakabiliwa na hatari za ulinzi ikiwemo kutoepuka kifo na majeraha wakati wa mashambulizi ya vikosi vya Israel na hili ni janga juu ya janga wamesema.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA likimulika Ukingo wa Magharibi limesema “Makumi ya jamii zinakabiliwa na ongezeko la mashambulizi na vikwazo vya kufikia ardhi yao wakati wa mavuno ya mizeituni ya mwaka huu. Kati ya matukio yote yanayohusiana na walowezi, matukio 104 yamesababisha hasara au uharibifu mkubwa wa mali tangu kuanza kwa mwezi huu wa Oktoba ”.
    2 min
  • 24 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina mada inayotupeleka nchini Kenya kuzunguza na uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mada tofauti ikiwemo uwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno HEKEMUA.Uchambuzi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) uliotolewa leo jijini New York, Marekani katika Siku ya Kimataifa ya Polio, unaonesha kwamba asilimia 85 ya watoto 541 waliokumbwa na polio duniani mwaka wa 2023 wanaishi katika nchi 31 zenye mifumo dhaifu, zinazokabiliwa na mizozo, halikadhalika zilizo hatarini.Umoja wa Mataifa ulijengwa na ulimwengu, kwa ajili ya ulimwengu, ndivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, alivyouanza ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku ya leo ya Umoja wa Mataifa.Na leo Oktoba 24 huko Kazan nchini Urusi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amehutubia mkutano wa viongozi wa kundi la BRICS yaani Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini akisisititiza amani duniani akizitaja Gaza, Lebanon, Ukraine na Sudan, akiwaambia wajumbe wa BRICS, “tunahitaji amani nchini Sudan, huku pande zote zikinyamazisha bunduki zao na kujitolea katika njia ya kuelekea amani endelevuKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno HEKEMUA!  Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    12 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners