Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UNICEF Kenya wafanikisha mapambano dhidi ya kipundupindu Lamu
    Serikali ya Kaunti ya Lamu katika pwani ya kaskazini ya Kenya, kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), wanaendesha shughuli ya kuwafikia wanajamii ili kubadilishana taarifa kuhusu jinsi watu wanaweza kuwalinda watoto na familia zao dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na kutoa huduma za maji, vifaa vya kujisafi na usafi kwa jamii zilizoathirika. Kutoka katika video iliyoandaliwa na UNICEF.Wamekaa chini ya mti, wanawake kwa wanaume. Nyuma ni nyumba ya makuti na matumbawe, Lamu, Pwani ya Kenya. Muelimishaji wa masuala ya afya anawaeleza namna ya kuweka mazingira safi ili kupambana na kipindupindu. Mwanajuma Kahidi yamewahi kumkuta. Anaposema Cholera anamaanisha hiyo hiyo kipindupindu iliyokuwa imetishia Uhai wake na familia yake.“Nilipopata maambukizi ya Kipindupindu nilihisi siko sawa kwa sababu nilikosa nguvu na nikakosa raha na nikapoteza nuru ya macho ndio nikakimbilia hospitali. Huo ugonjwa ulipitia kwenye maji na chakula. Mimi na watoto wangu tulipatwa na kipindupindu. Mimi nilichukua siku tatu. Watoto wangu wote mmoja baada ya mwingine walichukua siku nane nane. Madaktari wanajibidiisha sana juu yetu. Baada ya siku kadhaa wanajitokeza na kutuuliza, je mnafanya juhudi tulizowaambia?”Leila Abrar ni Mshauri katika UNICEF anayehusika na mabadiliko ya tabia katika jamii anasema, "kiwango cha ufahamu ni cha juu zaidi kuliko tulipokuwa tunaanza uelimishaji. Na pia tunaambiwa kuwa kiwango cha unawaji mikono kimeongezeka. Mabadiliko ya kijamii na tabia kwa kweli yanahusu kushirikisha jamii, kuwezesha jamii.
    3 min
  • 01 NOVEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko katika ukanda wa Gaza na masuala ya afya nchini Kenya. Makala inatupeleka nchini DRC kumsikia mkimbizi mjasiriamali na mnufaika wa pesa taslimu kutoka WFP, na mashinani tunakupeleka nchini Lebanonon kwa waathirika wa vita.Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, hali ya usalama na kibinadamu huko Ukanda wa Gaza inazidi kuzorota huku raia na hata wafanyakazi wa kutoa misaada wakisalia wamepigwa butwaa kwani mashambulizi kutoka Israeli yanaendelea kila uchao.Serikali ya Kaunti ya Lamu katika pwani ya kaskazini ya Kenya, kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), wanaendesha shughuli ya kuwafikia wanajamii ili kubadilishana taarifa kuhusu jinsi watu wanaweza kuwalinda watoto na familia zao dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na kutoa huduma za maji, vifaa vya kujisafi na usafi kwa jamii zilizoathirika. Kutoka katika video iliyoandaliwa na UNICEF.Makala George Musubao, mwandishi wetu wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC anazungumza na mkimbizi Esther Josephine aliyeko kambi ya Bulengo nje kidogo ya mji wa Goma, jimboni Kivu Kaskazini ambaye amenufaika na msaada kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP.Mashinani tutakuwa Lebanon, kumsikia mama aliyenusurika kifo na wanawe kutokana na makombora ya Israel.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • Raia na hata wahudumu wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza wamekata tamaa
    Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, hali ya usalama na kibinadamu huko Ukanda wa Gaza inazidi kuzorota huku raia na hata wafanyakazi wa kutoa misaada wakisalia wamepigwa butwaa kwani mashambulizi kutoka Israeli yanaendelea kila uchao. Naanzia ndani ya hospitali ya Kamal Adwan  kaskazini mwa Gaza, mtoto aliyejeruhiwa amebebwa akilia kwa uchungu. Kwingineko mgonjwa mwingine anatolewa kwenye gari la wagonjwa! Ni taswira iliyozoeleka sasa Gaza.Louise Wateridge ambaye ni Afisa Mwandamizi wa Masuala ya Dharura katika shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa kutoka Gaza Kati amesema hali si hali.Anasema, “mambo kwa kweli yanazidi kuwa mabaya hapa. Kukata tamaa ni kila mahali. Namaanisha, watu unaozungumza nao, na wafanyakazi wenzangu niliozungumza nao hawajui sasa wafanye nini. Hawafahamu waende wapi. Unaweza kusikia nyuma yangu milio ya makombora ikiendelea.”Bi. Wateridge akaendelea kusema kuwa, “kutokuwa na matumaini ndio neno pekee lililosalia Gaza. Unafahamu watu milioni 2.2. Inabidi umkumbushe kila mtu kwamba wamenasa. Hakuna njia ya kutoka nje ya Ukanda wa Gaza na mashambulio ya mabomu yanaendelea mchana kutwa na usiku kucha.”Hali ikiendelea hivyo hii leo huko katikati mwa Gaza, hapo jana jeshi la Israeli lilishambulia na kuharibu kwa kiasi kikubwa ofisi ya UNRWA iliyoko Ukingo wa Magharibi, ofisi ambayo ilikuwa inategemewa zaidi katika kutoa msaada kwa wakimbizi zaidi ya 14,000 wa kipalestina wanaoishi katika kambi ya Nur Shams.UNRWA kupitia mtandao wa X imesema kitendo cha kushambulia ofis iza UN lazima kikome na badala yake zilindwe wakati wote.
    2 min
  • ZMBF na harakati zao za kukabili udumavu Zanzibar
    Zanzibar Maisha Bora Foundation iliyoko Tanzania Zanzibar, iliyoanzishwa mwaka 2021 tayari inajinasibu na harakati za kusongesha afya ya watoto halikadhalika kupinga udhalilishaji wa kijinsia, masuala ambayo Umoja wa Mataifa kila uchao unasaka wadau wa kuunga mkono ili dunia pawe pahala salama kwa kila mtu na kila mtu aweze kustawi. Ni kwa kutambua hilo, Assumpta Massoi wa Idhaa hii alipopata fursa ya kuzungumza na Muasisi na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Bi. Mariam Mwinyi ambaye pia ni Mke wa Rais wa Zanzibar, wakati wa ziara yake hapa Umoja wa Mataifa hivi karibuni aliona vema Bi. Mwinyi atufafanulie kwa kina wanachofanya, na alianza na kwa kueleza sababu ya kumulika lishe bora kwa watoto Zanzibar.
    6 min
  • 31 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina mada kwa kina inayotupeleka Zanzibar nchini Tanzania kupata ufafanuzi wa jukumu la “Zanzibar Maisha Bora Foundation” akitueleza Bi. Mariam Mwinyi ambaye pia ni Mke wa Rais wa Zanzibar, wakati wa ziara yake hapa Umoja wa Mataifa hivi karibuni. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno HEREREZA.Kwa mujibu wa ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo na mashirika yake lile la mpango wa chakula (WFP) na la chakula na kilimo (FAO), uhaba mkubwa wa chakula unatarajiwa kuongezeka kwa ukubwa na ukali katika nchi na maeneo 22 duniani. Ripoti hiyo inaonya kwamba kuenea kwa migogoro, hasa katika Mashariki ya Kati inasukuma mamilioni ya watu ukingoni.Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Matthias Schmale, amelaani vikali shambulio la jana usiku lililotekelezwa na Jeshi la Urusi ambapo jengo la makazi la ghorofa nyingi lilipigwa katika mji wa Kharkiv, wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine.Na ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya majiji, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amewapigia chepuo vijana akitaka sauti zao na mawazo yao kupewa nafasi kwani  kuanzia harakati za chinichini hadi maabara za uvumbuzi, vijana wanasukuma hatua kabambe kukabiliana na      tabianchi,  wanaunga mkono ujumuishaji wa nishati mbadala, kazi zisizozalisha hewa chafuzi na usafiri safi wa umma, ambayo ni mambo yanayochangia kuunda miji endelevu ambapo kila mtu anaweza kustawi.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno HEREREZA!Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • 30 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Anold Kayanda akimulika masuala ya amani na usalama hususan Gaza; afya ya ubongo kwa wanamichezo; biashara ya ndizi kaukau huko India na dansi na kujitambua huko Trinidad na Tobago.Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina,  UNRWA, Philippe Lazzarini amemwandikia barua Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kusaka mshikamano na nchi wanachama baada ya Bunge la Israeli Jumatatu hii kupitisha miswada ya kusitisha shughuli za shirika hilo.  Flora Nducha na maelezo zaidi.. Hoja ya ubongo kutikisika (concussion) wakati wa michezo imeibuka katika siku za karibuni na kulazimu Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) kuingilia kati ili kudadavua kwa kina. Akiwa uwanjani akitazama mpira wa Daktari Tarun Dua, Mkuu wa Kitengo cha Afya ya Ubongo WHO, anaeleza kwa muhtasari kuhusu tatizo hilo kupitia taarifa ya Cecily Kariuki.Katika makala, Assumpta Massoi anakupeleka barani Asia, kusikia jinsi wazo la biashara kutoka familia moja lilivyoleta nuru kwa kaya zaidi ya 20.Mashinani tunamulika jinsi dansi kulivyomweka huru mtoto mkimbizi kutoka Venezuela huko nchini Trinidad na Tobago.
    10 min
  • Mwelekeo ni kutengeneza kaukau za ndizi zenye ladha ya kitunguu na nazi
    Uwekezaji rahisi kabisa kwa familia ya Didiki huko nchini India umekuwa na manufaa kwa kaya zaidi ya 20. Zao la ndizi ambalo awali hawakuweza kuongeza thamani ipasavyo lilikuwa na manufaa kidogo kiuchumi. Somo la biashara likamfungua fikra Didiki hadi kupata msaada kutoka Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo IFAD kwa ushirikiano na serikali ya India. Msaada umepanua biashara, vijana wamepata ajira, familia zimeongeza kipato na sasa mpango ni kufikia kaya zaidi ya 60,000. Ni kwa vipi? Ungan ana Assumpta Massoi kwenye makala hii.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners