Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 23 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi ya Israeli kaskazini mwa Gaza unaoleta changamoto za kuendelea na chanjo ya polio, na virusi vya Marburg nchini Rwanda. Makala tunakupeleka nchini Uganda na mashinani nchini Lebanon, kulikoni?Mashambulizi makali ya anga kutoka kwa jeshi la Israel, idadi kubwa ya watu kutawanywa na ukosefu wa fursa ya kufika Gaza Kaskakzini vimelazimisha kuahirishwa kwa kameni ya chanjo kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Duniani WHO, la kuhudumia watoto UNICEF na la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWAMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani amewapongeza wahudumu wa afya wa nchini Rwanda kwa kazi kubwa wanaoyoifanya kukabiliana na ugonjwa wa Marburg. Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza hisia zake hizo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya afya katika mji Mkuu wa nchi hiyo, Kigali.Ndoa za utotoni,ubakaji na kutelekeza watoto, haya ndio matatizo yaliyokuwa yanaripotiwa mara nyingi zaidi kwa kuathiri watoto katika makazi ya wakimbizi katika wilaya Kyegegwa magharibi mwa Uganda. Hata hivyo, kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF na ufadhili kutoka wahisani wa Uingereza UKaid, maelfu ya wazazi katika makazi ya wakimbizi na jamii zinazohifadhi waakimbizi katika wilaya ya Kyegegwa wamepewa mafunzo juu ya malezi bora ili kuondoa ukatili dhidi ya watoto, wanawake, na wasichana.Mashinani tunabisha hodi Lebanon, kumsikia Farah, Mkimbizi wa ndani anayepokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, baada ya kujifungua kwenye hema, akieleza alichokabiliana nacho.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • Mbinu bora za malezi zimebadilisha maisha katika Wilaya ya Kyegegwa - UNICEF Uganda
    Ndoa za utotoni,ubakaji na kutelekeza watoto, haya ndio matatizo yaliyokuwa yanaripotiwa mara nyingi zaidi kwa kuathiri watoto katika makazi ya wakimbizi katika wilaya Kyegegwa magharibi mwa Uganda. Hata hivyo, kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto  UNICEF na ufadhili kutoka wahisani wa Uingereza UKaid, maelfu ya wazazi katika makazi ya wakimbizi na jamii zinazohifadhi waakimbizi katika wilaya ya Kyegegwa wamepewa mafunzo juu ya malezi bora ili kuondoa ukatili dhidi ya watoto, wanawake, na wasichana. Leo tuko katika wilaya ya Kyegegwa nchini Uganda ambapo, kwa msaada wa UNICEF,  wafanyakazi wa kijamii, kamati za ulinzi na ustawi  wa watoto, na kikosi cha polisi; wote wamepewa mafunzo mwafaka ili kuhakikisha ulinzi wa watoto unaofaa na wa kudumu, na tunakutana na Agnes Karungi mama mwenye umri wa miaka ishirini na  mmoja wa wanufaika wa mradi wa malezi bora. Mbali na kukumbana na changamoto za kuwa mama kijana, mwanaye Agnes, ni mwenye ulemavu na zaidi ya hayo akatengwa na familia yake kwa kuzaa akiwa angali mwanafunzi.Cecily Kariuki anaeleza zaidi katika makala hii..
    4 min
  • UN: Mashambulizi ya anga ya Israel yalazimisha kampeni ya chanjo kusitishwa Gaza Kaskazini
    Mashambulizi makali ya anga kutoka kwa jeshi la Israel, idadi kubwa ya watu kutawanywa na ukosefu wa fursa ya kufika Gaza Kaskakzini vimelazimisha kuahirishwa kwa kameni ya chanjo kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Duniani WHO, la kuhudumia watoto UNICEF na la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA. Asante Anold, kampeni hiyo iliyoahirishwa ilitakiwa kuanza leo n ani duru ya mwisho ya chango ya kampeni iliyolenga kuwachanja watoto 119,279 kote Gaza Kaskazini kwa dozi ya pili ya chanjo ya polio aina ya nOPV2, lakini hali ya sasa imefanya iwe vigumu kwa familia kupeleka watoto wao kwenye vituo vya chanjo, na kwa wahudumu wa afya kuendesha huduma kwa usalama.Mashambulizi ya makombora yanayoendelea dhidi ya miundombinu ya kiraia yamepunguza maeneo yanayokubaliwa kwa usitishaji wa uhasama kwa mnajili ya masuala ya kibinadamu kuwa kwenye Jiji la Gaza pekee, ikilinganishwa na wakati wa awamu ya kwanza ya chanjo iliyofanyika tarehe 1-12 Septemba 2024.Hali hii inahatarisha kufikiwa kwa lengo la angalau asilimia 90 ya watoto kuchanjwa, jambo ambalo ni muhimu ili kukomesha usambaaji wa virusi vya polio na kulinda afya za watoto.WHO na UNICEF wamesema kuwa kucheleweshwa kwa chanjo ya polio kunaweza kuongeza hatari ya virusi kuenea zaidi Gaza na maeneo Jirani na kuchelewesha utoaji wa dozi ya pili ya chanjo ndani ya wiki sita kunapunguza uwezo wa chanjo hiyo kuimarisha kinga za watoto na kuzuia maambukizi.Tangu  duru ya pili ilipoanza tarehe 14 Oktoba 2024, jumla ya watoto 442,855 wenye umri wa chini ya miaka kumi wamefanikiwa kuchanjwa katika maeneo ya kati na kusini mwa Gaza.UNICEF na WHO wanatoa wito kwa pande zote zinazohusika katika mzozo kutekeleza usitishaji mapigano  wa kibinadamu na kuhakikisha kuwa raia, wahudumu wa afya, na miundombinu ya kiraia kama shule na hospitali inakingwa dhidi ya mashambulizi.Mashirika hayo yamesisitiza umuhimu wa kuanza tena kampeni ya chanjo mara moja ili kuzuia kupooza kwa watoto na kuimarisha kinga dhidi ya polio.Katika juhudi za kuhakikisha huduma bora, takribani watoto 357,802 pia walipatiwa virutubisho vya vitamini A kama sehemu ya juhudi za kuunganisha chanjo ya polio na huduma zingine muhimu za afya.Mashirika ya WHO na UNICEF ymesisitiza kuwa kusitisha vita na kuwezesha chanjo ni hatua muhimu ili kuzuia mlipuko wa polio kuendelea na kulinda afya ya watoto wote Gaza.
    3 min
  • Dkt. Tedros: Heshima kwa wahudumu wa afya wa Rwanda wanavyopambana na Marburg
    Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani amewapongeza wahudumu wa afya wa nchini Rwanda kwa kazi kubwa wanaoyoifanya kukabiliana na ugonjwa wa Marburg. Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza hisia zake hizo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya afya katika mji Mkuu wa nchi hiyo, Kigali."Ninawapongeza wahudumu wa afya waliojitolea ambao wamejiweka hatarini kuokoa wenzao, na ambao wameendelea kufanya kazi licha ya hatari. Na ninaenzi wale ambao tumewapoteza."Pia Dkt. Tedros akaeleza kuwa yeye na wenzake wamefurahishwa na namna ya utoaji huduma ambayo haijawahi kutumiwa katika mlipuko ya magonjwa ya namna hii barani Afrika akitolea mfano wagonjwa wawili aliowashuhudia wakiendelea vizuri kwamba waliokolewa kwa kuwekewa mipira iliyopeleka hewa ndani ya mwili.“Tunaamini hii ni mara ya kwanza kwa wagonjwa wenye virusi vya Marburg barani Afrika kuingiziwa na kutolewa mpira wa hewa. Wagonjwa hawa wangefariki dunia katika milipuko ya hapo awali. Hii inaonesha kazi ambayo Rwanda imefanya kwa miaka mingi kuimarisha mfumo wake wa afya, kukuza uwezo wa huduma muhimu na msaada wa kuokoa maisha ambao unaweza kutumiwa katika huduma za kawaida za hospitali na katika dharura.”
    2 min
  • Kuanza tena kwa shughuli za Redio RTNC kutawawezesha kupigana dhidi ya taarifa potofu na za uongo - MONUSCO
    Umoja wa Mataifa unaendelea kuunga mkono serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC katika kukabili habari potofu na za uongo hususan huko mashariki mwa nchi ambako vikundi vilivyojihami vinaendelea kushambulia raia na kupambana na jeshi la serikali. Hivi karibuni Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, umeipatia kituo cha Taifa cha Redio na Televisheni, RTNC huko Beni jimboni Kivu Kaskazini jengo na vifaa vyenye thamani ya takriban dola elfu hamsini za Kimarekani. Hatua hiyo iliwezesha RTNC kuanza tena matangazo yake. Mwandishi wetu wa DRC, George Musubao alifika kituoni hapo kuzungumza na wahusika na wanufaika.
    6 min
  • 22 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC kufuatilia kazi za kituo cha Taifa cha Redio na Televisheni, RTNC huko Beni jimboni Kivu Kaskazini za kakabiliana na habari potofu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Cairo, Misri, imebainisha kwamba athari za vita zimerudisha nyuma maendeleo huko Gaza kwa takriban miaka 69. Ripoti hiyo iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP na  Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi na Kijamii kwa Asia Magharibi imeonya kwamba bila kuondoa vikwazo vya kiuchumi na kuwekeza katika maendeleo, uchumi wa Palestina unaweza kushindwa kurejesha viwango vya kabla ya vita na kusonga mbele kwa kutegemea misaada ya kibinadamu pekee.Kiongozi wa timu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Marburg Dkt. Janet Diaz ameeleza kwamba uongozi thabiti wa serikali ya Rwanda umewezesha kufanya uamuzi wa haraka na kuchukua hatua kuanzisha mwitikio wa sekta mbalimbali dhidi ya mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo wa Marburg nchini humo.Na uongozi wa Kikosi cha Muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) umeendelea kusisitiza kwamba pamoja na changamoto zilizopo, walinda amani wa UNIFIL wanaendelea kufanya kazi kwa karibu na jamii za kusini mwa Lebanon ili kuwezesha utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa wenye uhitaji. Hivi karibuni kumekuwa na mashambulizi dhidi ya walinda amani hao wa Umoja wa Mataifa yanayotekelezwa na majeshi ya Israeli.Mashinani kupitia video ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya Kibinadamu na misaada ya dharura OCHA tunamuangazia mmoja wa watu waliokimbia makazi yao akiwa katika shule ya Al Rimal, akielezea changamoto wanazokutana nazo katika kukabiliana na hali ngumu inayowakabili raia wa Gaza.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • Nadipo: Asante WFP kwa mradi wa mizinga ya nyuki sasa familia yangu inatabasamu
    Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.Katika kaunti hii vumbi linalotimuka katika eneo tambarare lisilo na miti linakufanya kujiuliza je Nini kizuri kinaweza kufanyika hapa kwenye ukame uliotamalaki? Lakini cha kustaajabisha ni kwamba kwa kuwezeshwa mengi yanawezekana ikiwemo njia bora za kuhakikisha uhakika wa chakula na hata kubadili maisha ya watu kama anavyosema mkulima wa nyuki Nadipo Lotelei mnufaika wa mradi wa mizinga ya nyuki kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. “Hatua iliyochukuliwa na WFP kutupatia mizinga ya nyuki imekuja kama nyota ya jaha kwangu kwa sababu  siwezi kutembea umbali mrefu kutokana na ajali niliyopata. Mradi huu umenisaidia sana mimi ili kuweza kusaidia watoto wangu na mke wangu. Mke wangu ameweza kuanzisha biashara ya duka kutokana na faida niliyopata ambayo sasa inatumika kama chnzo cha kipato cha mahitaji ya kaya yetu.”Nadipo ni miongoni mwa wafuga nyuki 1,900 katika kaunti ya Turkana ambao wamepewa mafunzo ya ufugaji nyuki na vifaa kupitia mradi wa WFP kwa ushirikiano na shirika binafsi la HIVE ambalo mwenyekiti mtendaji wake ni Christopher Nzuki. “Tunahusika katika ufungaji na usambazaji wa vifaa. Na wakati huohuo tunatoa mafunzo kwa wafugaji nyuki na kisha kuwapatia masoko. Tunachukua kila kitu wanachozalisha.”Ufugaji wa nyuki wa kisasa si kazi kubwa, na pia unatumia nafasi ndogo na maji kidogo. Nyuki huchavusha asilimia 80 ya miti ya maua ikiwemo mazao ya chakula. Huzalisha asali, nta, mafuta na sumu, bidhaa ambazo huuzwa kwa gharama kubwa sokoni. Kwa sasa WFP inasaidia karibu wafugaji wa nyuki 5,000 katika kaunti 9 nchini Kenya lakini lengo ni kuwafikia wengi zaidi na mradi huu kama anavyosema afisa wa WFP Timothy Koskei. “Dhamira yetu mwisho wa yote ni kuwafikia wastani wa wafuga nyuki 10,000 katika kaunti 9 na kuvuna takriban tani 600 za asali.” Kwa mujibu wa WFP nyuki wana uwezo mkubwa na wanaweza kutoa mavuno mengi ambayo ni neema kwa familia sisizojiweza katika maeneo haya kame. Mkurugenzi wa WFP nchini Kenya Lauren Landis anasema mradi umezaa matunda. “Hivi sasa tunasikia kutoka miongoni mwa wanaufaika ambao awali walikuwa wakipokea msaada wa chakula ,ambao sasa sio tu wanazalisha asali  kwa ajili ya faida bali pia wanafikiria kuongeza ununuzi wa pembejeo zaidi kutoka kwa Hive. Hivyo tunachokishuhudia ni mchakato ulio wazi ambapo mtu anatoka kuwa mpokea msaada na kuwa mteja, kuwa mpokeaji wa faida na si mpokeaji wa msaada wa chakula.”Kwa mafanikio haya WFP inasema itaendelea kupanua wigo wa mradi huu ili kunufaisha familia nyingi zaidi.
    4 min
  • Mlo shuleni ulibadilisha maisha yangu- Mkurugenzi wa WFP Somalia
    Kila siku, mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda shule wakiwa na njaa, wengi wao wakiteseka na utapiamlo sugu ambao huathiri ukuaji wa kiakili na utendaji wao katika masomo. Wanaobahatika huweza tu kumaliza masomo yao na kufanikiwa maishani kutokana na programu ya ‘mlo ya shuleni’ inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP). Mfano wa wanufaika hao ni El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa sasa wa WFP nchini Somalia. "Mimi ni zao la mlo wa shule," hayo ni maneno ya El-Khidir Daloum ambaye ana shukrani tele kwa WFP kwa kuendesha programu ya ‘mlo shuleni’ iliyomfaidisha  alipokuwa mwanafunzi. Hivi sasa, akiwa Mkurugenzi wa WFP nchini Somalia, Daloum ameweka dhamira ya kazi yake kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa wote. Je Daloum aliifahamu vipi programu ya mlo shuleni ya WFP kwa mara ya kwanza?“Tulipofika pale, tukakuta ni shule ya bweni, wakati huo wazazi wetu hawangeweza kugharamia shule hiyo. Kwa hivyo, shule ilifanya ushirikiano kati ya serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa Chakula Duniani (WFP). Na hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya  kwanza kuonja dagaa wa Kijapani, maziwa ya unga kutoka Uholanzi, na jibini ya Denmark, yote yaliletwa kwetu kupitia mlo wa shule.”Je Daloum anadhani maisha yake yangekuwa vipi kama WFP isingetoa mlo shuleni?“Nikiwaza kuhusu kizazi changu, hasa wale waliokuwa katika shule za bweni, bila ushirikiano huo kati ya serikali ya nchi yangu na WFP, hatungeweza  kumaliza elimu yetu. Ndio maana nakwambia kwamba mimi ni zao la mlo shuleni kutoka kwenye shule ya msingi kwenda katika shule ya kati na hatimaye sekondari, yote haya matatu yalifaulu kutokana na mlo shuleni.”
    2 min
  • 21 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa COP16 katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia na ufugaji nyuki Turakana nchini Kenya. Pia tunakupeleka nchini Somalia kufutilia programu wa WFP wa mlo shuleni na mashinani inatupeleka nchini Lebanon.Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng’oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili.Kila siku, mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda shule wakiwa na njaa, wengi wao wakiteseka na utapiamlo sugu ambao huathiri ukuaji wa kiakili na utendaji wao katika masomo. Wanaobahatika huweza tu kumaliza masomo yao na kufanikiwa maishani kutokana na programu ya ‘mlo ya shuleni’ inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP). Mfano wa wanufaika hao ni El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa sasa wa WFP nchini Somalia.Makala inatupeleka Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame ambako mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.Mashinani fursa ni yake Waffiyah Diyah kutoka Lebanon ambaye ni muathirika wa vita vilivyolazimisha maelfu ya watu kufangasha viragoanaelezea hali ya familia yake baada ya kukimbia mashambulizi na kupoteza kila kitu, lakini sasa anapokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM).Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners