Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Kambi ya huduma za macho ya UNICEF yawezesha watoto kuona vema
    Nchini Kenya, Idara ya Taifa ya Ulinzi wa Jamii kwa kushirikiana na Baraza la Kitaifa la watu wenye ulemavu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, wameendesha kambi ya kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto.  Mmoja wa wanufaika wa juhudi hii ni Candy, msichan wa  mwenye umri wa miaka 7 ambaye ana ualbino.Akiwa mwingi wa matumaini, Eric Odhiambo Okeyo, baba mzazi wa mtotohuyo alimpeleka kwenye kambi hiyo  jijini Kisumu ambapo alifanyiwa uchunguzi na matibabu.Baada ya kufanyiwa uchunguzi, Candy alielekezwa kwa daktari wa macho  ili abaini aina ya miwani ambayo ingemfaa.“Mtoto alipoanza shule niligundua kwamba mwendo wake katika masomo ulikuwa wa polepole sana na pia alikuwa analamika kwamba haoni anachoandika mwalimu. Hata akienda kucheza  niliona kwamba alikuwa akifunga macho mara kadhaa. Ilikuwa inanikosesha amani kwa sababu nilihisi kuwa alikuwa akiteseka,” amesema Eric.Mpango huu wa kielelezo wa UNICEF na wadau wake unashughulikia changamoto zinazowazuia watoto wenye ulemavu na familia zao kupokea msaada muhimu wanaohitaji wakati wa majanga na dharura.Akiwa mwingi wa furaha, Eric anasema, “imechukua muda wa miaka sita ambapo nimekuwa nikizunguka tu kuhusu miwani. Mahali nilipoenda hapo awali, niliambiwa kulipia shilingi elfu arobaini ($313) lakini sikuweza kupata hiyo pesa. Nimefurahi kwamba leo nimepewa bila gharama yoyote.”Baada ya uchunguzi na mawaidha mbalimbali katika hii kambi, Eric na mwanaye Candy hawakuweza kuificha furaha yao kwa kupata suluhisho la tatizo ambalo limewaathiri kwa miaka sita.Hatimaye, Candy alipewa miwani yake maalum ili kumsaidia kuona vizuri zaidi.“Nimefurahia sana sina jukumu tena la  kutafuta pesa za kununua miwani. Na nimefurahi pia mtoto wangu atakuwa na wakati rahisi. Amefurahia kabisa na anaipenda sana miwani yake. Amesema anajihisi vizuri. Kwa sababu ana miwani, natumaini anaweza kucheza bila shida yoyote, bila kujali kuhusu jua kwa sababu miwani inamkinga.”
    3 min
  • 16 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazi siku ya chakula duniani ikitupeleka jijini Roma Italia kufuatilia maadhimisho yake. Pia tunakupeleka nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani mashirika wanhaha kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto. Makala tunakwengda nchini DRC na mashinani Sierra Leone, kulikoni?Washiriki wa Sherehe za kimataifa za mwaka huu wa 2024 za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula zilizofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) jijini Roma Italia wamesisitiza haja ya upatikanaji wa vyakula mbalimbali vya kutosha, vyenye lishe, bei nafuu na salama.Nchini Kenya, Idara ya Taifa ya Ulinzi wa Jamii kwa kushirikiana na Baraza la Kitaifa la Watu wenye ulemavu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, wameendesha kambi ya kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto ikiwemo Candy mwenye umri wa miaka 7 ambaye ana ualbino. Baba yake alifika kwenye kambi hiyo na anatusimulia kupitia video ya UNICEF Kenya.Makala inatupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia harakati za shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP la kusaidia wanawake wakimbizi kuondokana na ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika.Mashinani tunamsikia Mpishi Mkuu Fatmata Binta kutoka kabila la wafugaji wanaohamahama la fulani nchini Sierra Leone anaeleza jinsi ushirikiano wake na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, kuhusu ni kwa jinsi gani FAO umemwezesha kusambaza manufaa ya fonio, nafaka asili ya Afrika , inayoweza kuwa suluhisho la changamoto za ukosefu wa chakula na tabianchi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya chakula duniani yaangazia haki ya chakula salama chenye lishe na cha bei nafuu
    Washiriki wa Sherehe za kimataifa za mwaka huu wa 2024 za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula zilizofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) jijini Roma Italia wamesisitiza haja ya upatikanaji wa vyakula mbalimbali vya kutosha, vyenye lishe, bei nafuu na salama.Ni maadhimisho ambayo yamewaleta wadau wa kilimo na chakula kutoka kote duniani lakini  yanakuja huku kukiwa na mvutano na mizozo ya kimataifa na majanga ya tabianchi ambayo ni miongoni mwa mambo yanayochangia changamoto ya mamia ya mamilioni ya watu duniani kote kukabiliwa na njaa na mabilioni ya watu kushindwa kumudu chakula bora, FAO inaeleza katika taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wake wa wavuti.Katika hotuba yake ya ufunguzi Mkurugenzi Mkuu wa FAO, QU Dongyu, amesema mifumo ya kilimo cha chakula inabidi "kusaidia wakulima wadogo, wakulima wa ngazi ya familia na wafanyabiashara wadogo katika mnyororo wa thamani ambao katika nchi nyingi ni wa msingi katika kufanya vyakula vyenye lishe, vya aina mbalimbali vipatikane kwa wote, na kuhifadhi tamaduni za jadi za chakula.” Ujumbe huo wa mkuu wa FAO unafanana na ujumbe wa Papa Francis ambaye amesisitiza wafanya uamuzi wa kisiasa na kiuchumi katika ngazi ya kimataifa lazima wasikilize matakwa ya wale walio chini kabisa katika mnyororo wa chakula.Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia video amesema, "kuna kitu hakiko sawa katika ulimwengu ambao njaa na utapiamlo ni ukweli wa maisha kwa mabilioni ya watoto, wanawake na wanaume." Akasema ulimwengu usio na njaa unawezekana, lakini "mifumo ya chakula inahitaji mabadiliko makubwa," ili kuwa na ufanisi zaidi, ujumuishi, mnepo na endelevu.Gérardine Mukeshimana, Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ametoa wito wa "uwekezaji wa haraka, wa pamoja na thabiti kwa wakulima maskini wa vijijini kutambua kwa ngazi ya chini kabisa haki yao ya msingi ya chakula chenye lishe." Akabainisha kuwa wakulima wadogo wanazalisha karibu nusu ya chakula cha dunia, ingawa pia wanakabiliwa na njaa na umaskini.Mfalme Letsie III wa Lesotho, ambaye ni Balozi Mwema Maalum wa FAO katika upande wa lishe anaeleza anavyoiunga mkono FAO kwa “kujaribu kuwa mtetezi mwaminifu na mwenye kujitolea katika masuala ya lishe, katika masuala ya uhakika wa chakula.” Anasema, “na mara kwa mara, mimi hutembelea sehemu nyingine za bara la Afrika nikivaa kofia yangu ya FAO, hasa kuhimiza serikali na viongozi kama bara kuwekeza zaidi katika masuala ya lishe na masuala ya uhakika wa chakula.”. 
    2 min
  • 15 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani kesho ikiwa ni siku ya chakula duniani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatili juhudi za FAO za kuhakikisha haki ya chakula kwa maisha bora na mustakabali bora kwa wananchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Licha ya mashambulizi, awamu ya pili ya chanjo kwa watoto dhidi ya polio huko Gaza iliyoanza jana imeendelea leo Jumanne eneo la kati mwa Gaza na hadi sasa watoto wapatao Elfu 93 wenye umri wa chini ya miaka 10 wameshapatiwa dozi ya pili.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP hii leo linatoa wito wa msaada wa dharura kuepusha janga la kibinamu eneo la kusini mwa Afrika kutokana na ukame uliochochewa na El- Niño.Na ubia mpya wa kutokomeza watu kukosa utaifa umezinduliwa huko Geneva, Uswisi ukilenga kutokomeza hadhi hiyo inayoathiri mamilioni ya watu duniani. Zaidi ya nchi 100, mashirika ya kiraia, taasisi zinazopigia chepuo kuondokana na hadhi hiyo, wanazuoni na wadau wengine wameanzisha ubia huo ikiwa ni kuendeleza kampeni ya muongo mmoja iliyopatiwa jina Mimi ni wa! Au I Belong.Mashinani leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya wanawake wa vijijini, ninampisha  Motshekile Mlalazi, mkulima kutoka Gokwe, kaskazini mwa Zimbabwe, ambaye kupitia video ya FAO anatueleza kuhusu mbinu yake ya kilimo hai ya kuchanganya mazao aliyojifunza kizazi hadi kizazi ilivyochangia  katika lishe bora, bayoanuwai ya kilimo, na pia kuongeza kipato.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • Wagonjwa majeruhi wa vita 16 wahamishwa kutoka hospitali ya Kamal Adwan kuwapeleka katika hospitali ya Al-Shifa
    Operesheni ya vikosi vya jeshi la Israel inayoendeea Kaskazini mwa Gaza kwa njia ya anga na ardhini kukabiliana na wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas yamelifanya eneo hilo kukatwa na sehemu zingine za Gaza, kwa kiasi kikubwa raia wakikosa huduma za msingi kama chakula, elimu na matibabu. Hospitali karibu zote Gaza Kaskazini hazifanyi kazi na iliyosalia ni Kamal Adwan nayo ikitoa huduma kwa kiasi kidogo sana kutokana na ukosefu wa vifaa, wahudumu wa afya na mafuta. Majeruhi wa vita wamezidi uwezo wa hospitali hiyo ndio maana ikaamua kuomba msaada kutoka shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kuhamisha majeruhi hao kwenda hospitali Al-Shifa mjini Gaza. Katika makala hii Flora Nducha anamulika zoezi hilo la kuhamisha majeruhi.
    4 min
  • UNICEF yatoa mafunzo ya kutengeneza sodo kwa kijana mkimbizi wa dani nchini Sudan
    Sodo au taulo za kike, vile vile pedi,  ni muhimu kwa wanawake na  wasichana, lakini wengi hawawezi kuzipata wakati wa vita na ukimbizi. Leo tunakutana na Samer, mvulana huyu ambaye akiwa na umri wa miaka 16 tu, kwa msaada wa klabu ya  usafi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, anatengeneza na kusambaza sodo kwa wanawake na wasichana katika maeneo ya wakimbizi wa ndani jimboni Atbara, nchini Sudan. Msaada wa kifedha kutoka  Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF, vilabu vya usafi vya UNICEF, na Shirika la Marekani la misaada ya maendeleo USAID,  vijana wakimbizi wa ndani wanawezeshwa kupata suluhisho kwa changamoto za usafi wanazokutana nazo, wakati wa vita na ukimbizi. Mmoja wa vijana hawa wakimbizi ni Samer mvulana mwenye umri wa miaka 16, ambaye amefundishwa kutengeneza sodo na sasa, anazisambaza bure kwa wanawake na wasichana wakimbizi wa ndani katika jimbo la Atbara, nchini Sudan.Nikataka kujua jinsi Samer anatengeneza sodo hizo…"Nashona kati ya vipande kumi na tano hadi ishirini kwa siku. Kwanza, nakata sponji au sifongo, kisha naweka ndani ya kitambaa. Naishona na kuongeza kifungo ili kuifunga vizuri."Kwa nini Samer, katika umri wa miaka 16, anatengeneza sodo"Hiki ndicho wasichana na akina mama wanachohitaji zaidi wakati wa ukimbizi, lakini hakipatikani. Ikiwa hawatumii sodo, huenda wasiweze kusafiri au kutembea kwa uhuru. Kwa hiyo, nazitengeneza na kuwapatia bure kwa ajili yao kutumia. Kwa sababu ya vita, watu hawana pesa za kununua pedi, kwa hiyo nazitengeneza na kuzisambaza. Sodo hizi zinaweza kufuliwa na kutumika tena. Pedi nyingi ni   hutumiwa mara moja tu, na watu wanalazimika kununua mpya kila wakati."Je nini kilimpa Samer hamasa ya kutengeneza sodo, na anajisikia vipi anapoifanya kazi hii?"Nilipojiunga na warsha ya UNICEF, nilianza kusaidia familia yangu kwa kuwatengenezea sodo. Napokea vifaa kutoka  kiwanda cha UNICEF. Nilipoanza kutengeneza sodo, nilihisi furaha kujua kuwa kuna watu wanaozihitaji. Baadhi yao, hawana pesa na wanakabiliwa na changamoto. Sijihisi aibu kwa kile ninachofanya, kwa sababu kutimiza mahitaji ya watu ni muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote."
    3 min
  • 14 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya katika ukanda wa Gaza yakiwa ni pamoja na chanjo dhidi ya polio huku mashambulizi ya Israel yakiendelea, na kuwahamisha wagonjwa majeruhi. Pia tunaangazia mchango wa wakimbizi Sudan kwa jamii, na ndoa za utotoni Zambia.Mashambulizi yakiendelea kurindima kutoka pande hasimu, jeshi la Israeli na wanamgambo wa Hamas huko Gaza, na Hezbollah huko kusini mwa Lebanon, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na awamu ya pili ya chanjo dhidi ya Polio Ukanda wa Gaza, huku huko Lebanon ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura ikisihi raia wasilengwe.Sodo au taulo za kike, vile vile pedi, ni muhimu kwa wanawake na      wasichana, lakini wengi hawawezi kuzipata wakati wa vita na ukimbizi. Leo tunakutana na Samer, mvulana huyu ambaye akiwa na umri wa miaka 16 tu, kwa msaada wa klabu ya usafi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, anatengeneza na kusambaza sodo kwa wanawake na wasichana katika maeneo ya wakimbizi wa ndani jimboni Atbara, nchini Sudan.Makala inatupeleka Kaskazini mwa Gaza kwenye moja ya operesheni ngumu na hatari ya kuwahamisha wagonjwa majeruhi wa vita 16 katika hospitali ya Kamal Adwan kuwapeleka katika hospitali ya Al-Shifa mjini Gaza, wakati operesheni ya kijeshi ya Israel ikiendelea.tutaelekea Zambia kumsikia kiongozi wa jamii ya Chewa, Mashariki mwa Zambia anayeongoza mapambano dhidi ya ndoa za utotoni.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • Awamu ya 2 ya chanjo dhidi ya Polio Gaza yaanza licha mashambulizi
    Mashambulizi yakiendelea kurindima kutoka pande hasimu, jeshi la Israeli na wanamgambo wa Hamas huko Gaza, na Hezbollah huko kusini mwa Lebanon, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na awamu ya pili ya chanjo dhidi ya Polio  Ukanda wa Gaza, huku huko Lebanon ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura ikisihi raia wasilengwe. Naanzia eneo la kati mwa ukanda wa Gaza ambako asubuhi ya leo Jumatatu awamu ya pili ya chanjo dhidi ya polio imeanza ikilenga watoto 591 700 wenye umri wa chini ya miaka 10,  watakaopatiwa dozi ya pili ya chanjo hiyo kufuatia kuthibitishwa kwa polio Gaza mwezi Agosti mwaka huu.Chanjo inatolewa licha ya ripoti za makombora kurushwa kwenye shule moja iliyogeuzwa makazi ya wakimbizi huko Nuseirat na katika hospitali moja huko Deir Al-Balah ambako mahema kadhaa yaliteketezwa kwa moto wakati watu wamelala.Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, Louise Wateridge akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa amesema, “nimekuwa kwenye simu na mfanyakazi mwenzangu tangu saa 9 alfajiri ya leo. Alikuwa amejihifadhi kwenye hospitali ya Al Aqsa. Ni mmoja wa watu wengi ambao wamepoteza kila kitu. Hema lao limeteketezwa. Tumeona picha na video, inaonekana makazi ya familia nyingi yameteketezwa kwenye moto huu mkubwa, na yeye amenaswa kwenye zahma na mashambulizi. Inatia kiwewe hata kusikiliza hali anayokumbana nayo.”Picha za mnato pamoja na video kutoka UNRWA zinaonesha wafanyakazi wa uokoaji wakisaka manusura kwenye eneo la hospitali ya Al Aqsa, huku mahema yakiwa yanateketea na nondo zimesambaratika. Maiti walioteketezwa kwa moto walikuwa wamefunikwa kwa blankenti.Na nikigeukia Lebanon, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X, zamani Twitter inasema chuki kati ya Israeli na wanamgambo wa Hezbollah, inaendelea kusababisha vifo, majeruhi na ukimbizi.Mashambulizi yanayoripotiwa kulenga makazi ya watu ambako wakimbizi wamesaka hifadhi. Inataka pande kinzani ziheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu na kwamba raia na miundombinu ya kiraia isilengwe.Naye Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi akizungumza Geneva, Uswisi hii leo amesema kwa mara nyingine tena suala la kutofautisha kati ya raia na wapiganaji limekuwa halina maana, akimulika jinsi raia wanavyokimbia mashambulizi ya angani kutoka jeshi la Israeli huko Lebanon.
    4 min
  • FAO yaleta nuru kwa wafugaji walioathiriwa na vita Gaza
    Mwaka mmoja wa vita katika ukanda wa Gaza iliyochochewa na mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israeli Oktoba 7, 2023 na kisha Israeli kujibu mashambulizi yanayoendelea hadi leo, umekuwa ukimulika zaidi madhara ya vifo na majeruhi. Lakini sasa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limekusogezea madhara ya vita katika kilimo na ufugaji na ndio makala yetu ya leo ikisimuliwa na Assumpta Massoi.
    4 min
  • Guterres: Ni wakati muafaka sisi kuwasikiliza wasichana
    Ikiwa le oni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kuwapa sikio watoto wa kike akianza ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii akisema uwezo wa wasichana zaidi ya bilioni 1.1 duniani hauna kikomo lakini tunapokaribia tarehe mwaka 2030, wa mwisho kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, ulimwengu unaendelea kuwaangusha wasichana.“Wasichana wanachangia zaidi ya asilimia 70 ya maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi, VVU” anasema Guterres na kwamba wana uwezekano mara mbili zaidi wa wavulana kukosa elimu au mafunzo. Na ndoa za utotoni bado zimeenea, huku takriban msichana mmoja kati ya watano duniani akiolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18. Kotekote duniani, mafanikio yaliyopatikana kwa bidii ya usawa wa kijinsia yanafutwa na vita dhidi ya haki za kimsingi za wanawake na wasichana, na kuhatarisha maisha yao. kuzuia uchaguzi wao, na kuweka kikwazo cha mustakabali wa wasichana.Kwa kutumia kaulimbiu ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo ni ‘Dira ya Msichana’ kwa Zama Zijazo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasema, wasichana tayari wana dira ya ulimwengu ambamo wanaweza kustawi. Wanafanya kazi kugeuza maono hayo kuwa vitendo, na kutaka sauti zao zisikike. Ni wakati muafaka sisi kusikiliza. Ni lazima tuwape wasichana nafasi kwenye meza, kupitia elimu, na kwa kuwapa rasilimali wanazohitaji na fursa za kushiriki na kuongoza.Ujasiri, matumaini na uamuzi wa wasichana ni nguvu ya kuzingatia. Ni wakati wa ulimwengu kuchukua hatua na kusaidia kubadilisha maono na matarajio yao kuwa ukweli.
    2 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners