Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 11 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike na juhudi za Umoja wa Mataifa za kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na unaofanyika mtandaoni. Makala tunakupeleka katika ukanda wa Gaza, na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kuwapa sikio watoto wa kike akisema uwezo wa wasichana zaidi ya bilioni 1.1 duniani hauna kikomo lakini tunapokaribia mwaka 2030, wa mwisho kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, ulimwengu unaendelea kuwaangusha wasichana.Nchini Ethiopia hususan katika jimbo la Somali, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kuweza kujenga upya maisha yao wakati huu ambapo takwimu za shirika hilo zinaonesha kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 370 duniani kote wamekumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 15.Makala tunakupeleka Gaza ambapo mwaka mmoja wa vita nchini Gaza iliyochochewa na mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israeli Oktoba 7, 2023 na kisha Israeli kujibu mashambulizi yanayoendelea hadi leo, umekuwa ukimulika zaidi madhara ya vifo na majeruhi. Lakini sasa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limekusogezea madhara ya vita katika kilimo na ufugaji.Katika mashinani leo ikiwa ni Siku ya kimataifa ya Mtoto wa Kike tunaelekea nchini Tanzania kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo, kujifunza kutoka mtoto mmoja wa kike kuhusu haki za watoto.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • UNICEF nchini Ethiopia yarejesha matumaini kwa manusura wa ukatili wa kingono
    Nchini Ethiopia hususan katika jimbo la Somali, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kuweza kujenga upya maisha yao wakati huu ambapo takwimu za shirika hilo zinaonesha kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 370 duniani kote wamekumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 15. Sauti hiyo ya Nasteyo Sahane Layle, Meneja wa kushughulikia visa vya ukatili wa kijinsia dhidi ya akina mama, watoto na wanawake hapa Gode, jimboni Somali mashariki mwa Ethiopia akisema kuwa kazi kubwa tunayoifanya ni visa vinavyohusu ukatili wa kingono.Ni katika video ya UNICEF iliyochapishwa kuonesha kiza kinachokumba watoto wa kike hususan leo ambayo ni siku ya kimataifa ya mtoto wa kike.Hapa Gode, UNICEF imeanzisha kituo hicho cha kutoa huduma zote  na sasa kimekuwa ni kama eneo salama kwa manusura wa ukatili wa kingono.Anaonekana mmoja wa wasaka huduma kituoni hapa akifika tayari kupatiwa huduma, sura yake imefichwa ili kuficha utambulisho wako.Anapatiwa huduma ikiwemo kupimwa mapigo ya moyo na vipimo vingine na kisha kupatiwa dawa.Nasteyo anasema,“kinachotusikitisha zaidi ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 ambao walibakwa, na sasa mustakabali wao umeharibiwa.”Pamoja na Nasteyo, wahudumu wengine katika kituo hiki ni Nimo, Faduo, Ifrah na Hamdi, wote wanawake.Ni kutokana na huduma zao, manusura wanajiona wako salama kwani wanapatiwa huduma za kisaikolojia na nyingine muhimu wanazohitaji.Na kisha kupata tena uwezo wa kujiamini na kujenga upya maisha  yao. TAGS: AfyaAdditional: AfyaNews: Ukatili wa Kingono, EthiopiaRegion: AfrikaUN/Partner: UNICEF
    2 min
  • 10 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika malengo ya maendeleo endelevu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwema za Lebanon, afya ya akili na ripoti ya UNICEF kuhusu ukatili wa kingono. Katika kujifunza Kiswahili tunakuletea uchambuzi wa methali.Nchini Lebanon ujumbe wa jeshi la Umoja wa Mataifa la mpito nchini humo, UNIFIL, unasema mapigano kati ya jeshi la Israeli, IDF, na wanamgambo wa Hezbollah kusini mwa Lebanon yamekuwa na madhara kwa ujumbe huo kwani makao yake makuu huko Naqourra na maeneo ya karibu yameshambuliwa mara kwa mara tangu kuanza kwa mapigano kati ya pande hizo mbili.Leo ni siku ya afya ya akili duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake amesisitiza udharura wa kupatia kipaumbele afya ya akili pahala pa kazi.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema zaidi ya wasichana na wanawake milioni 370 walioko hai hii leo, walikumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 18.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu hii leo ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Mapenzi ni kikohozi hayawezi kufichika.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    12 min
  • Utoaji wa chanjo dhidi ya mpox nchini DRC
    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeanza chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya Nyani au MPOX  mwishoni mwa wiki iliyopita. Hii ni hatua muhimu ya kuongeza juhudi zinazoendelea za kupambana na mlipuko wa ugonjwa huo ambao DRC inachangia asilimia 90 ya wagonjwa wote zaidi ya 18,000 duniani. Lengo sasa ni kuokoa maisha, limesema shirika la  Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, kanda ya Afrika. Shuhuda wetu wakati wa kuanza kazi ya kutoa chanjo alikuwa mwandishi wetu wa Mashariki mwa DRC, George Musubao kutoka Goma, jimboni Kivu Kaskazini.
    4 min
  • 09 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani ikiwa ni siku ya posta duniani tunaangazia huduma za posta na juhudi za mashirika za kukabiliana na Mpox nchini DRC. Makala tunasalia huko huko DRC kufuatilia uzinduzi wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo huo, na mashinani tunakupeleka nchini Lebanon.Leo siku ya posta duniani huduma ambayo ilionekana kuwa itasambaratika kufuatia ujio wa maendeleo ya teknolojia ya intaneti lakini wenyewe wasimamizi wa huduma hii duniani wanasema licha ya mtikisiko sasa mambo yanashamiri, siri kubwa ikiwa ni ubia badala ya ushindani.Ukisikia makovu yasiyofutika ni ya simulizi hii utakayoisikia kuhusu familia moja huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupoteza watoto wanne kutokana na ugonjwa wa homa ya nyani au mpox huku mustakabali wao ukisalia mashakani kwani bado hawafahamu hali itakuwa vipi kwenye familia yao, baba na mama wakipambana na ugonjwa huo.Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo chanjo dhidi ya mpox imeanza.Na mashinani tutaelekea Lebabon ambapo, tutasikia simulizi ya Wahiba mwanamke mkimbizi kutoka Syria anayeishi Lebanon, ambaye      sasa amelazimika kuikimbia Lebanon kufuatia mashambulizi nchini humo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • Shirika la Umoja wa Mataifa la Posta lahimili changamoto kwa kugeuza changamoto kuwa fursa
    Leo siku ya posta duniani huduma ambayo ilionekana kuwa itasambaratika kufuatia ujio wa maendeleo ya teknolojia ya intaneti lakini wenyewe wasimamizi wa huduma hii duniani wanasema licha ya mtikisiko sasa mambo yanashamiri, siri kubwa ikiwa ni ubia badala ya ushindani. Tunasherehekea miaka 150 ya shirika la Umoja wa Mataifa la Posta, UPU, tunatambua umuhimu wa moja ya mifano ya mapema zaidi ya ushirikiano wa kimataifa. Ni Masahiko Metoki, Mkurugenzi Mkuu wa UPU katika ujumbe wake wa siku hii adhimu akiongeza kuwa..“Kile kilichoanza na wanachama 22 sasa inajumuisha nchi 192, kikionesha uthabiti wa ushirikiano wa kimataifa.”Miaka 150 wamekumbana na changamoto, vita, majanga mabadiliko ya kasi ya teknolojia ya kidijitali. Lakini wanafanya nini?“Leo hii UPU inaongoza juhudi za kufanya huduma za posta kuwa za kisasa na bora. Inatoa fursa kwa nchi kushirikishana ufahamu, kusaka majawabu na kukabili changamoto za sasa. Moyo wetu wa ushirikiano ndio umetusaidia kugeuza vikwazo kuwa fursa na kufanya huduma za posta kuendana na dunia inayobadilika.”Na zaidi ya yote…“Awali tuliona ongezeko la mawasiliano ya kidijitali kuwa ni tishio kwani kiwango cha utumaji wa barua kwa njia ya posta kilipungua. Lakini sasa tunaona fursa za utajiri. Mtandao mkubwa wa UPU umesaidia kupanuka kwa huduma mbali mbali ikiwemo biashara mtandao, huduma za kifedha, kijamii na kidijitali, ikihakikisha ufikiaji wa kila mtu duniani hata wale walio ndani zaidi hawaachwi nyuma.”Kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, UPU imehimili changamoto kwa kuwa bunifu, jumuishi na kusongesha ushirikiano wa kimataifa.“Katika siku hii muhimu, hebu na tusherehekee na tupongeze kazi ya shirika la Posta duniani ya kuondoa umbali na kuunganisha dunia.”
    3 min
  • Ugonjwa wa Mpox ‘umepoteza’ watoto wanne wa familia moja DRC
    Ukisikia makovu yasiyofutika ni ya simulizi hii utakayoisikia kuhusu familia moja huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupoteza watoto wanne kutokana na ugonjwa wa homa ya nyani au mpox huku mustakabali wao ukisalia mashakani kwani bado hawafahamu hali itakuwa vipi kwenye familia yao, baba na mama wakipambana na ugonjwa huo. Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iliyochapishwa kwenye mtandao wa Instagram unatupeleka Mbandaka, mji ulioko jimboni Equateur, kaskazini-magharibi mwa DRC.Dkt. Douglas Noble Mkurugenzi Mshiriki, UNICEF ndiye mwenyeji wetu hapa kwani ametembelea kituo cha matibabu ya mpox hapa Mbandaka.“Tuko hapa Mbandaka, ambapo kuna idadi kubwa zaidi ya wagonjwa wa mpox. Tumetembelea kituo cha matibabu, na ni huzuni kusikia hadithi ya familia moja yenye watoto sita, ambapo wanne walifariki dunia kwa  mpox. Watoto wawili wako vizuri kwenye kituo cha watoto. Baba na mama bado wako kituo cha matibabu”"Ni kwa kuzingatia madhara ya ugonjwa wa mpox kwa watoto  na  jamii nchini DRC ndio maana Dkt. Noble anasema..“Simulizi kama hizi zinatufanya tutambue uzito wa ugonjwa huu kwa watoto na jinsi unavyoathiri jamii. Wito wetu ni kuwahamasisha watu na kujenga uwezo wao ili waweze kudhibiti hali hii.”Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC inatajwa kubeba asilimia 90 ya wagonjwa wote 18,815 walioripotiwa duniani kote.
    2 min
  • 08 OKTOBA 2024
    Mnamo mwaka wa 2020, Umoja wa Mataifa ulipotimiza miaka 75 tangu kuanzishwa, pamoja na maadhimisho wakati huo ulimwengu ulianzisha mazungumzo ya kimataifa kuhusu matarajio na hofu kuhusu zama zijazo. Huo ndio ukawa mwanzo wa mchakato ambao hatimaye, miaka minne baadaye, hivi majuzi umefanyika Mkutano wa Zama Zijazo. Lakini kwa kuwa mikutano na mipango mingine ilishafanyika katika siku za nyuma, je huu nao unaweza kuwa ni mvinyo wa zamani katika chupa mpya kwa hiyo hautakuwa na mchango mkubwa chanya kwa dunia? Kuyajadili haya na mengine mara baada ya mkutano huo wa zama zijazo kukamilika jijini New York, Marekani, Anold Kayanda wa Idhaa hii aliketi na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Veronica Nduva aliyeshiriki mkutano huo.
    10 min
  • Wiki mbili za kusaka usalama DRC, mkimbizi asimulia madhila na atakacho.
    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, imesalia katika mgogoro kwa miaka mingi, hali ambayo imewasababishia raia mateso ya hali ya juu zaidi yakiwemo mauaji, utekaji nyara, na kuteketezwa kwa nyumbaa zao. Mapigano hayo pia yamewafungisha viragozaidi ya watu milioni 6.4 nchini humo, na kulazimisha familia kutafuta usalama katika makazi ya muda yaliyojaa pomoni. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeonya kuwa mgogoro huu uliodumu kwa muda mrefu na ukiukwaji wa haki za binadamu ni mwiba kwa wakimbizi hawa wa ndani.  Cicey Kariuki na taarifa zaidiRusayo ni eneo lililo na makazi ya muda ya wakimbizi   mjini Goma katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Miongoni mwa  wakimibizi wa ndani wanaishi kwenye makazi haya ni Sebororo, mwanamke mwenye  miaka 38 akitembea na watoto wake.Sebororo pamoja na wananawe watano wanaishi kwenye makazi ya pamoja na familia nyingine 90 huku wakisubiri kutengewa nyumba katika eneo hilo. Mama huyu anaeleza jinsi alivyojikuta katika makazi ya wakimbizi. Anasema,“tulianza kukimbia kuktoka kule tarehe tano mwezi wa kumi, awali walikuwa wanakuja lakini hawakuua watu, lakini leo hii wanaua watoto,wanaume na wanawake, sisi yalitushinda maanake wengine walikuwa pia wanatekweteza mimea.”Sebororo na watoto wake watano walitembea kwa wiki mbili kutafuta usalama, baada ya wapiganaji kuvamia kijiji chao cha Kiseguru katika Mkoa wa Kivu Kaskazini. Katika nusu ya kwanza ya mwaka wa 2024 pekee, zaidi ya watu 940,000 walilazimika kukimbia kutokana na ukatili, uliofanywa na makundi mengi yenye silaha yasiyo ya kiserikali huku familia nyingi zikifurushwa mara kadhaa. Kwa sasa anachokitamani zaidi Sebroro ni amani. “Haja yetu sisi ni watusaidie kwa kusimamisha vita ili turejee kwetu kwa sababu watu wanaisha.”Anasema.Kufurika kwa watu katika makazi haya ya muda kumezua  wasiwasi mkubwa miongoni mwa wahudumu wa kibinadamu kufuatia hatari ya kuenea kwa magonjwa, ikiwa ni pamoja na virusi vya homa ya nyani au mpox.Ruven Menikdiwela, Kamishna Msaidizi wa Operesheni wa UNHCR ambaye alitembelea eneo hilo na kukutana na familia mbalimbali za wakimbizi na kusikiliza wasiwasi wao, anasema, “leo asubuhi, nilizungumza na mwanamke huyu ambaye ana watoto wadogo watano. Alitembea kwa wiki mbili kufika katika eneo hili, bado anasubiri huduma, bado anasubiri watoto wake watibiwe, na bado anasubiri chakula. Ninatambua kwamba hii ni hali ya kawaida kwa watu wote wanaoishi katika eneo hili. Kila mmoja ana majanga yake binafsi, kwa hivyo hizi siyo tu takwimu, bali kuna hadithi za kibinafsi nyuma ya kila moja ya hizi takwimu na majanga ya kibinafsi na majanga yanayoendelea pia, kwa sababu hatuoni suluhisho lolote kwenye mustakabali.”Katika ziara yake kwenye makazi haya, Ruven Menikdiwela, pia alifanya vikao na wadau kadhaa akiwemo Waziri mkuu, mamlaka za mkoa na mashirika ya umoja wa Mataifa. Ujumbe wake ulikuwa wazi kwamba amani ndiyo suluhisho endelevu na dhabiti zaidi, na inahitajika kwa dharura. “Pande zote zinapaswa kukutana na kujadiliana kutoa fursa kwa amani, ili watu hawa wote, mamilioni ya watu waliolazimika kuhama, waweze kurudi nyumbani au kuunganishwa na jamii mahali walipo, na waweze kuishi kwa amani pamoja kama jamii moja.”
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners