Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Tiba Salama Digital Health App shirika linalotumia teknolojia kutekeleza SDGs
    Tiba Salama Digital Health App shirika la kijamii la lilalolenga kutumia teknolojia kutekeleza Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs katika kutoa huduma za afya kwa wanawake wajawazito, wanaolea na watoto.Lengo kuu ni kupunguza na hatimaye kuondoa kabisa vifo vya wajawazito na watoto wadogo kwa kuoresha huduma za afya hususani kwa maeneo ya pembezoni yenye upatikanaji hafifu wa huduma za msingi za afya.Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza Simon Mashauri, Mkurugenzi na Mwazilishi wa shirika hilo lenye makao yake makuu mkoani Tanga, kaskazini mashariki mwa Tanzania.
    4 min
  • Mwaka 1 wa vita Mashariki ya Kati: Ni wakati wa amani Gaza, asema Guterres
    Leo ni mwaka mmoja tangu vita ianze huko Gaza, Mashariki ya Kati baada ya wanamgambo wa kipalestina, Hamas kushambulia Israeli na kuua waisraeli 1250 pamoja na wageni, kisha Israeli kujibu mashambulizi yaliyoripotiwa kuua hadi sasa zaidi ya wapalestina 41,000 ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pamoja na wakuu wa mashirika mbali mbali ya chombo hicho wametoa wito kutaka kukoma kwa vita hiyo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi. Antonio Guterres huyu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake kwa njia ya video leo ikiwa in mwaka mmoja, anasema hii ni siku kwa jamii ya kimataifa kurejelea tena kwa sauti kubwa zaidi kulaani kwetu kwa vitendo vya kuchukiza vya Hamas ikiwemo utekaji nyara wa siku ile.Hamas waliteka nyara zaidi ya watu 250. Guterres amesema katika kipindi cha mwaka mmoja amezungumza na familia ambazo ndugu zao wanashikiliwa mateka hadi sasa. Amezungumzia pia machungu yaliyoibuka baada ya vita kuanza. Sasa anasema ni wakati wa kuachilia huru mateka. Wakati wa kunyamazisha bunduki. Wakati wa kukomesha machungu yaliyogubika ukanda huo. Wakati wa amani, sheria ya kimataifa na haki. Umoja wa Matiafa umejizatiti kufanikisha malengo hayo. Pisha nikupishe za manusura, magari ya wagonjwa na viwewe ni hali ya kawaida Gaza kwa mwaka mmoja sasa.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya ulimwenguni, WHO, pamoja na kusaidia waathiriwa wa vita, linashirikiana na mashirika ya kiraia kusaidia wale wanaosaidia manusura, mathalani madereva wa magari ya wagonjwa, wahudumu wa afya ambao waliathiriwa na kile walichokiona wakati wakisafirisha mahututi au kutambua maiti kwenye vifusi.Lile la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limemnukuu Abu Majdi mpalestina mwenye umri wa miaka 80 akisema baada ya mwaka mmoja wa ukimbizi, joto kali na baridi kali, hadi lini tutaendelea kuhimili ukimbizi huu? Hadi lini tutapata haki na maisha yetu?Naye Kaimu Mkuu wa Ofisi ya UN ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA  Joyce Msuya anasema hakuna takwimu zinazoweza kueleza bayana madhila ya kimwili, kiakili na kijamii ya vita hiyo.
    3 min
  • 07 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani Flora Nducha anamulika mwaka mmoja tangu kuanza kwa vita mpya huko Gaza, ambapo viongozi wa Umoja wa Mataifa na mashirika wanatoa kauli zao. Leo ni mwaka mmoja tangu vita ianze huko Gaza, Mashariki ya Kati baada ya wanamgambo wa kipalestina, Hamas kushambulia Israeli na kuua waisraeli 1250 pamoja na wageni, kisha Israeli kujibu mashambulizi yaliyoripotiwa kuua hadi sasa zaidi ya wapalestina 41,000 ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pamoja na wakuu wa mashirika mbali mbali ya chombo hicho wametoa wito kutaka kukoma kwa vita hiyo.Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, imesalia katika mgogoro kwa miaka mingi, hali ambayo imewasababishia raia mateso ya hali ya juu zaidi yakiwemo mauaji, utekaji nyara, na kuteketezwa kwa nyumbaa zao. Mapigano hayo pia yamewafungisha viragozaidi ya watu milioni 6.4 nchini humo, na kulazimisha familia kutafuta usalama katika makazi ya muda yaliyojaa pomoni. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeonya kuwa mgogoro huu uliodumu kwa muda mrefu na ukiukwaji wa haki za binadamu ni mwiba kwa wakimbizi hawa wa ndani.  Makala inaelekea  nchini Tanzania kuangazia Tiba Salama Digital Health App, shirika la kijamii la lilalolenga kutumia teknolojia kutekeleza Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs katika kutoa huduma za afya kwa wanawake wajawazito, wanaolea na watoto. Mashinani ikiwa dunia Jumamosi iliyopita iliadhimisha siku ya mwalimu duniani, nafasi ni yake mshindi wa tuzo ya UNESCO-Hamdan kutoka Togo, Mwalimu Komlan Abalo Braly wa shule ya sekondari Tchitchao, akielezea juhudi za kuboresha ufundishaji katika shule hiyo.
    12 min
  • Boti yazama Ziwa Kivu, UN yashikamana na waathiriwa
    Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan jimboni Kivu Kaskazini kwenye mji mkuu, Goma, Alhamisi ya Oktoba 3 iligubikwa na kiza nyakati za asubuhi baada ya boti kuzama kwenye Ziwa Kivu. Ilikuwa inasafiri kutoka Minova, jimboni Kivu Kusini. Zahma hii imesababisha vifo kwa mujibu wa vyombo vya habari huku Umoja wa Mataifa nao ukitoa kauli. Mwenyeji wetu huko Goma aliyeshuhudia tukio hilo ni George Musubao. 
    4 min
  • UNESCO: Tunapaswa kuthamini sauti za walimu kote duniani
    Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa  wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu. Kama tunavyofahamu, siku yenyewe ya Kimataifa ya Walimu ni kesho Oktoba 5 kama ilivyo ada ya kila mwaka lakini katika makao makuu ya UNESCO hapa Paris Ufaransa, maadhimisho yamefanyika leo kuelekea mkesha wa siku hii muhimu kwa elimu ya ulimwengu.Miongoni mwa waliozungumza ni Mkurugenzi Msaidizi Mkuu wa Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Stefania Giannini, ambaye ameitumia nafasi hii kusisitiza kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni 'Kutambua sauti za walimu.'Anasema, “walimu ni uti wa mgongo wa mifumo ya elimu na mawakala wakuu wa mabadiliko ya kubuni sera za elimu na kufanikisha SDGs. Tunapaswa kuthamini sauti za walimu; hili ndilo lengo kuu la Siku ya Kimataifa ya Walimu mwaka huu.”Kulingana na takwimu zilizotolewa na UNESCO, dunia inahitaji walimu wa ziada milioni 44 ili kufikia elimu ya msingi na sekondari kwa wote ifikapo mwaka 2030. Ingawa mahitaji ya walimu ni makubwa zaidi katika baadhi ya maeneo, uhaba wa walimu ni wa kimataifa.Walimu wanajiondoa kwenye taaluma hii kwa kiwango mara mbili zaidi ya miaka mitano iliyopita, hasa katika elimu ya sekondari. Hii inatokana na hali zao za kazi, zikiwemo mishahara midogo, mzigo mkubwa wa kazi, na ukosefu wa ushiriki katika maamuzi yanayohusu elimu. Akiiangizia changamoto hii, Mkurugenzi wa Kimataifa wa Elimu na Maendeleo ya Vijana katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Bi. Pia Britto, aliyejiunga katika hafla ya leo kwa njia ya video akiwa Pakistani amesema,"Leo nilikuwa na fursa nzuri ya kuzungumza na walimu wengi, ikiwa ni pamoja na mwalimu Tahseen Bashir hapa Islamabad, ambaye amenieleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na kufundisha madarasa mengi, uhaba wa vifaa vya kujifunzia, na changamoto za kutoweza kufundisha namna wanavyodhamiria. Lakini pia amenieleza jinsi alivyofurahi kuona wanafunzi wake wakifaulu. Wakati sauti ya mwalimu inaposikilizwa na wakati sauti za walimu zinapopewa kipaumbele, wanajiona kama wadau katika kuboresha elimu kwa wakati wote, na hatua hizo zinahitajika ili kuleta mabadiliko chanya hasa katika hali ngumu zaidi."Siku hii ya kimataifa ya walimu ni mahususi kwa ajili ya kutambua na kusherehekea mchango muhimu wa walimu ulimwenguni kote katika kutoa elimu bora na kujenga mustakabali wa jamii. Pia, ni fursa ya kuangazia changamoto wanazokabiliana nazo walimu.Kutoka hapa Paris Ufaransa, mimi ni Cecily Kariuki..
    3 min
  • 04 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Lebanon, na kesho ikiwa ni Siku ya walimu Dunia tunakupeleka Paris, Ufaranza kutsikia toka UNESCO. Makala tunafuatili ajali ya boti iliyozama katika ziwa Kivu nchini DRC na mashinani tunakupeleka Burundi, kulikoni? Mashirikika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya nchini Lebanon wakati mashambulizi ya anga ya Israel yakiendelea kushika kasi na kuwafungisha virago maelfu ya watu, wengi wakikimbia nchi jirani ya Syria ambako nako si shwari.Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa  wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu.Makala inakupeleka huko Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako janga la kuzama kwa boti ya abiria na mizigo liligubika eneo hilo Alhamisi asubuhi za huko.Na mashinani kupitia video ya WHO Afrika, tunamsikia Dkt. Dieudonné Niyongere akizungumza kuhusu msaada muhimu wa washirika katika kuimarisha juhudi za kukabiliana na mlipuko wa Mpox nchini Burundi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
    12 min
  • UN: Lebanon inakabiliwa na zahma kubwa wakati mashambulizi ya Israel yakiendelea
    Mashirikika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya nchini Lebanon wakati mashambulizi ya anga ya Israel yakiendelea kushika kasi na kuwafungisha virago maelfu ya watu, wengi wakikimbia nchi jirani ya Syria ambako nako si shwari. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO linasema hali nchini Lebanon ni janga la kibinadamu watu wengi wamejeruhiwa , wengine kupoteza maisha na mfumo wa afya umelemewa.Kupitia ukurasa wake wa  X Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema katika jitihada za kuwasaidia waathirika ndege ya kwanza ya msaada wa vifaa vya kitabibu vya upasuaji, dawa na vifaa tiba vingine imewasili mapema leo mjini Beiruti na vifaa hivyo vitatosha kuwatibu maelfu kwa maelfu ya watu na kuokoa maisha yao na ndege nyingine mbili zitawasili baadaye leo.Kwa upande wake Shirika la Umoja wa  Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema maelfu ya watu wanaendelea kukimbia mashambulizi ya makombora ya Israel na wengine wakivuka mpaka kwa miguu kuingia Syria kusaka uslama. Pamoja na kwamba linafanya kila liwezekanalo kuwasidia , limesema msaada zaidi unahitajika kukabiliana na wimbi la watu wanaoendelea kufurushwa.Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva wao “ Wamelaani vikali mashambulizi yanayotekelezwa kwenda Israel na makundi yenye silaha yasiyo ya kiserikali yaliyopo Lebanon ambayo yamesababisha watu 63,000 kutawanywa nchini Israel. Wamesema wahusika lazima wawajibishwe na watu waliotawanywa wapewe msaada na ulinzi.”Hata hivyo wamesisitiza kwamba“ Israel haiwezi kutumia uhalifu huo kama sababu ya kuhalalisha uhalifu wao nchini Lebanon unaojumuisha vitendo vya machafuko yenye lengo la kuleta hofu miongoni mwa raia wanaowashambulia.”Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, chini ya muda wa mwezi mmoja idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Lebanon imeongezeka mara tatu na zaidi ya watu 1,600 wameuawa  na wengine takriban 346,000 kujeruhiwa wakiwemo watoto 127.
    3 min
  • 03 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC kumulika ugonjwa wa homa ya nyani au mpox. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za machafuko Lebanon, Haiti na Sudan. Katika kujifunza Kiswahili Onni Sigalla anafafanua maana ya neno “NGEJA” Mashariki ya Kati, nchini Lebanon hali inaendelea kuwa tete amesema mratibu maalum wa Umoja wa mataifa nchini humo Jeanine Hennis Plasschaert. Kupiti ukurasa wake wa mtandao wa X amesema umekuwa usiku mwingine wa kutoka kulala mjini Beiruti milipuko ikighubika mji huo bila tahadhari, raia      wakikumbwa na taharuki bila kujua mustakbali wao.Mtaalamu mhuru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Sudan Radhouane Nouicer, leo ametoa wito kwa jeshi la Sudan (SAF), Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na wanamgambo wenye silaha kuchukua hatua za haraka kuhakikisha ulinzi wa raia mjini Khartoum, huku kukiwa na ongezeko la uhasama na ripoti za kutatanisha za mauaji ya kiholela.Na zaidi ya watu laki 7, sasa ni wakimbizi wa ndani nchini Haiti huku zaidi ya nusu ya idadi hiyo ni watoto, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.Ripoti inasema kuna ongezeko la asilimia 22 la watu waliofurushwa makwao, ambapo machafuko ya magenge ya uhalifu yamewalazimisha watu 110,000 kuzikimbia nyumba zao katika miezi saba iliyopita pkee. IOM imesema ongezeko hilo linasisitiza haja ya msaada zaidi wa kibinadamu kwa ajili ya waathirika.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “NGEJA”?Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
    12 min
  • Vivian Joseph: Taasisi ya Watoto Afrika ni fursa kwa kila mtoto kufikia uwezo wake
    Moja ya malengo ya Umoja wa Mataifa  ya maendeleo endelevu SDGs ani lengo namba 4 la kuhakikisha elimu bora kwa kila mtoto. Hata hivyo bado katika nchi  nyingi hususan zinazoendelea watoto wengi hasa wenye ulemavu wanakosa fursa za kufikia uwezo wao kutokana na changamoto za kupata elimu iwe rasmi au isiyo rasmi na hivyo kusalia nyuma. Umoja wa Mataifa umekuwa ukizichagiza nchi na jamii kuchukua hatua  ili kubadili mwelekeo huo. Nchini Tanzania kijana Vivian Joseph ni miongoni mwa walioitikia wito wa hatua na akaanzisha taasisi isiyo ya kiserikali ya Watoto Afrika Initiative nili kusaidia watoto  wenye changamoto ikiwemo ulemavu waweze kupata fursa hiyo ya elimu. Katika makala hii amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa kuhusu taasisi hiyo akianza kwa kufafanua wanachokifanya.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners