Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Je wewe ni mmoja wa waathirika wa usugu wa viuavijiumbe maradhi, au Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa, UVIDA?
    Leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kando ya mjadala mkuu wa UNGA79, viongozi wanakutana kwenye Mkutano wa Ngazi ya Juu ukimulika usugu wa viuavijiumbe maradhi, Antimicrobial Resistance, kwa kiswahili ikiitwa pia UVIDA, au Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa. Katika taarifa ya Pamoja iluyotolewa kwenye mkutno huo na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO, la mazingira UNEP, la chakula  na kilimo FAO na shirika la afya ya Wanyama duniani WOAH, usugu wa viua vijiumbe maradhi unahusika moja kwa moja na vifo milioni 1.3 na kuchangia vingine milioni 5 kila mwaka.Unaweza kujiuliza ni nini na kwa nini ni muhimu wakutane? Bosco Cosmas, wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Profesa Mshiriki wa Vimelea Vya Magonjwa katika Chuo Kikuu cha Sayans iza Afya Bugando, mkoani Mwanza, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.
    7 min
  • 26 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika hospitali ya kanda Bugando, mkoani Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania kumulika chanzo na madhara ya usugu wa vimelea dhidi ya dawa au UVIDA. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na katika kujifunza Kiswahili tunabisha hodi nchini Zimbabwe, kulikoni?Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa leo kandoni mwa mjadala mkuu ulioingia siku ya tatu moja ya mada zinazopewa uzito ni usugu wa vijiuavijiumbe maradhi au Anti-Microbial Resistance (AMR). Katika taarifa ya Pamoja iluyotolewa kwenye mkutno huo na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO, la mazingira UNEP, la chakula  na kilimo FAO na shirika la afya ya Wanyama duniani WOAH, usugu wa viua vijiumbe maradhi unahusika moja kwa moja na vifo milioni 1.3 na kuchangia vingine milioni 5 kila mwaka.Pia katika katika Mjadala Mkuu wa baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA79 miongoni mwa waliopanda katika mimbari leo kuhutubia ni Rais wa Jamhuri ya Kenya William Samoei Ruto ambaye amesema “Dunia iko katika wakati wa changamoto kubwa za kiusalama, ahati ya chata ya Umoja wa Mataifa kuokoa viizazi kutokana na vita iiko katika hatihati.” Aesema nadhariaya wao dhidi yetu ni chachu ya changamoto kubwa ikiwemo vita. Kuanzia Gaza, Darfur, Ukraine, Yemen, Mashariki mwa DRC , Sudan, Sahel na uhalifunchini Haiti,migogoro inasambaratisha maisha na uwezi wa watukuishi katika kiwangocha kihistoria.”Naye Rais wa Malawi Lazarus McCarthy Chakwera, amesema kila nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa inahusiana na nchi nyingine katika mambo matatu, ushirikiano migogoro na ushindani ulio na usawa, hivyo jinsi ya kushughulikia masuala hayo ndio itaamua mustakbali wa vizazi vvya kesho hasa ushirikiano unaofaidisha wote, ushindani ulio na usawa na utatuzi wa migogoro. Amesisitiza kuwa ushirikiano ni kitu cha muhimu sana na mfano mzuri ni nchi yake Malawi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili fursa ni yake Mary Chigumira kutoka Zimbabwe, mmoja wa waafrika aliyefika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa Jijini New York kwa ajili ya Mkutano wa Zama Zijazo uliokamilika hivi majuzi akieleza anavyotamani kujifunza zaidi lugha ya Kiswahili.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    12 min
  • Haya ndiyo tuliyowaeleza viongozi wa ulimwengu - Ibanomonde Ngema na Jerop Limo
    Katika makala ya leo, Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na vijana wawili waliozaliwa tayari wakiwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na hivyo wameamua kujitolea kusukuma mapambano dhidi ya ugojwa huo hatari duniani. Katika mikutano inayoendelea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati huu wa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA79 wasichana hawa wadogo wamepata fursa ya kushiriki katika mkutano wa ngazi ya juu uliondaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi UNAIDS. 
    4 min
  • Viongozi wajadili ongezeko la kina cha baharí; UNEP Tanzania yaonesha njia
    Viongozi wa dunia wakiendelea kuhutubia kwenye Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapa New York, Marekani, kandoni kunafanyika Mkutano wa Ngazi ya Juu  ukimulika madhara ya ongezeko la kina baharí  kutokana na kina cha baharí. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia viongozi wa dunia amewataka wachukue hatua za kijasiri kunusuru maisha na mbinu za kujipatia vipato kwa watu zaidi ya milioni 900 wanaoishi uwanda wa chini wa pwani ulio hatarini kuzama kutokana na kina cha baharí kuongezeka.Kwa Tanzania Umoja wa Mataifa umeanza kuchukua hatua kama unavyosikia kutoka kwa Clara Makenya, Mwakilishi wa shirika la UN la Mataifa la Mazingira, UNEP nchini humo huku tukipata ufafanuzi wa madhara ya ongezeko la kina cha baharí kwenye eneo lao kutoka kwa Segule Segule, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Maji Pangani 
    2 min
  • 25 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa wanaharakati wa malengo ya maendeleo endelevu ambao wamekuja hapa makao makuu ya umoja wa mataifa kuwa sehemu ya utatuzi katika mijadala mikuu ya UNGA79. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakwenda DRC.Viongozi wa dunia wakiendelea kuhutubia kwenye Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapa New York, Marekani, kandoni kunafanyika Mkutano wa Ngazi ya Juu  ukimulika madhara ya ongezeko la kina baharí  kutokana na kina cha baharí.Mjadala mkuu wa wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 79 umeingia siku ya pili hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa nasi tunaendelea kuzungumza na washhiriki mbalimbali wakiwemo kutoka asasi za kiraia kusikia maoni yao kuhusu mkutano huu. Flora Nducha amebahatika kuongea na mmoja wao kutoka nchini Zimbabwe.Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na vijana wawili waliozaliwa tayari wakiwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na hivyo wameamua kujitolea kusukuma mapambano dhidi ya ugojwa huo hatari duniani. Katika mikutano inayoendelea hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati huu wa UNGA79 wasichana hawa wadogo wamepata fursa ya kushiriki katika mkutano wa ngazi ya juu uliondaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi UNAIDS.Na mashinani fursa ni yake mwananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC jimboni Kivu Kaskazini akiwasilisha ujumbe wake kwa viongozi wanaoshiriki mjadala Mkuu wa mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataiafa, UNGA79 hapa New York, Marekani.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • Mwanaharakati Mary: Viongozi wa dunia wasiwape kisogo wanawake na wasichana wa vijijini
    Mjadala mkuu wa wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 79 umeingia siku ya pili hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa nasi tunaendelea kuzungumza na washhiriki mbalimbali wakiwemo kutoka asasi za kiraia kusikia maoni yao kuhusu mkutano huu. Flora Nducha amebahatika kuongea na mwanaharakati mmoja wao kutoka nchini Zimbabwe.Bi. Chigumira ni mwanaharakati  anayepiganiia haki za wanawake na wasichana nchini Zimbabwe kupitia shirikika lale la kiraia la “Unlimited hope alliance” au Muungano wa matumaini yasiokwisha ambao unawasaidia wasichana wenye changamto katika masuala ya elimu, huduma za maji , usafi na usafi wa mazingira  au WASH na kuwawezesha kiuchumi.Bi. Chigumira amekuwa hapa Umoja wa Mataifa kuhudhuria mkutano uliomalizika wiki hii wa Zama Zijazo na kabla hajarejea nyumbani ana ujumbe kwa viongozi wa dunia wanaokutana katika mjadala mkuu wa UNGA79 kuhusu mchango wao katika hataraki za kusaidia wanasichana na wanawake vijijini, “Kwa viongozi tunawaomba wawe sehemu yetu, hatutaki kuwa katika safari hii peke yetu, tunataka kuambatana nao. Endapo tutaambatana Pamoja nao tufafanikisha lengo letu.”Bi. Chigumira amesema hilo litawatia moyo hata wanawake na  wasichana wanaopitia machungu na kukata tamaa, anawashauri akisema, “Kwa wanawake na wasichana ambao mnanisikiliza , asilani hamjachelewa, hata kama maisha yako yaliharibiwa, ulipata mtoto ukiwa na umri wa miaka 14, huo sio mwisho wa safari.”Mkuu huyo wa shirika hilo la kiraia la Unlimited hope Alliance ametoa mfano hai katika shirika lake,  “Tulikuwa na wasichana ambao walipata mimba wakiwa na umri wa miaka 14, lakini sasa wamerejea shuleni , hivyo hamjachelewa hata wale walio katika biashara ya ngono, mnaweza kubadili maisha yenu yaliyoharibika. Njooni kwetu mpate mafunzi ili muweze hata kuanzisha biashara zenu.”Bi.Chigumira anasema anaamini wakijengewa uwezo basi shirika lao litaweza kusaidia wasichana wengi zaidi.
    2 min
  • 24 SEPTEMBA 2024
    Jaridani tunakuletea mada kwa kina ikiwa hii leo Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa mataifa UNGA79 umeng’oa nanga hii na tunakutana na mdau anayepigia chepuo malengo ya maendeleo endelevu hasa haki katika lengo namba 4 la Elimu Bora.Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA79 umeanza leo New York, Marekani ambapo Katibu Mkuu wa Antonio Guterres amesema anashawishika kwamba kuna kweli mbili chungu katika zahma zinazokumba dunia hivi sasa: Mosi-Hali ya dunia si endelevu na hatuwezi kuendelea kama ilivyo na pili; changamoto zilizozoko zinatatulika. Kinachohitajika ni kuweko kwa mfumo wa kimataifa wenye uwezo wa kutatua changamoto hizo.Rais Joe Biden wa Marekani ambaye amesema ni hotuba yake ya mwisho mbele ya Baraza hilo kama Rais wa Marekani na kwamba anatambua changamoto zinazokabili dunia ikiwemo vita, tabianchi na demokrasia. Lakini ana matumaini kuna suluhu kwa kuzingatia yote waliyofanya pamoja kwa miongo iliyopita.Huko Lebanon shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR linaomboleza vifo vya watumishi wake wawili waliouawa huko Bekaa Mashariki baada ya kombora lililorushwa na Israeli kuangukia makazi yao jana Septemba 23. UNHCR imerejelea wito wa Katibu Mkuu wa UN ya kwamba mashambulizi yakome.Na katika mashinani tunamsikia kijana mmoja aliyefika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhudhuria mkutano wa Zama Zijazo uliofunga pazia lake jana, ana wito wa kuwapa viongozi wa ulimwengu ambao wanashiriki katika Mjadala Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa ambao wenyewe umefungua pazialake leo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
    10 min
  • Vijana - Tumechoka na maneno ya viongozi sasa tunataka vitendo
    Jana Jumapili ya Septemba 22 viongozi wa dunia walipitisha Mkataba wa Zama Zijazo. Mkataba huu unalenga kukabili changamoto za karne ya 21 kuanzia mizozo, mabadiliko ya tabianchi, haki za binadamu, hadi taarifa potofu na za uongo. Maeneo Matano makuu ni pamoja na maendeleo endelevu, amani na usalama duniani, sayansi na teknolojia, vijana na vizazi vijavyo na marekebisho ya usimamizi wa dunia, kipengele muhimu wakati huu ambapo taasisi za fedha za kimataifa na Umoja wa Mataifa wenyewe wameshindwa kuja na majawabu ya karne ya 21. Mkataba wa Kimataifa wa Kidijitali unaoelenga pamoja na mambo mengine usimamizi bora wa Akili Mnemba, pamoja na Azimio kwa ajili ya Vizazi Vijavyo linalotaka serikali za sasa kutilia maanani vizazi vijavyo zinapopitisha maamuzi yao ya leo, ni sehemu ya viambatanishi vya Mkataba huu wa Zama Zijazo. Assumpta Massoi ametaka kufahamu maoni ya vijana baada ya hatua hii, na ndio mada yetu kwa kina siku ya leo. 
    8 min
  • 23 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kama nilivyokujulisha leo ambayo ni kipindi maalum kinachojumuisha hotuba za viongozi wa dunia na watetezi wa haki za binadamu ikiwa ni jana Jumapili Septemba 22 viongozi hao walipitisha Mkataba wa Zama Zijazo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Mkutano wa Zama Zijazo uliofanyika kwa siku nne tangu majuzi tarehe 20 ukianza na siku mbili za vijana kukutana na baadaye viongozi wakuu wa ulimwengu, unakunja jamvi hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Kesho Septemba 24 unaanza Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukitajwa kuwa mkusanyiko mkubwa zaidi wa kidplomasia ulimwenguni unaofanyika kila mwaka. Kwa siku sita viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa watahutubia ulimwengu.Leo Jumatatu hali ya mvutano imezidi kutanda Mashariki ya Kati huku ripoti za mamia ya mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Israel dhidi ya Hezbollah yakilenga kusini mwa Lebanon na Gaza ikiwa ni pamoja na kambi ya wakimbizi, wameeleza wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa. Hatua hiyo inakuja wakati afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon Jeanine Hennis-Plasschaert aakianza ziara rasmi nchini Israel kukutana na maafisa wakuu wa serikali, baada ya kusisitiza kwamba "hakuna suluhu ya kijeshi ambayo itafanya pande zote mbili kuwa salama".Na Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali  ya Haki za Binadamu nchini Burundi Fortuné Gaetan Zongo, amehutubia mkutano wa 57 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi hii leo na kueleza kuwa hali ya kibinadamu katika taifa hilo la Maziwa Makuu bado inatia wasiwasi akitolea mfano tukio la mashinikizo kwa wapenzi waliokuwa wanaishi pamoja huko Ngozi, Kayanza na Kirundo mwezi Machi na Aprili mwaka huu.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • Mataifa yahakikishe ulimwengu unakuwa mahali bora kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi - Jerop
    Leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani vijana kutoka kila kona ya dunia wanakutana kuanza kujadili kuhusu mstakabali wao katika zama zijazo. Miongoni mwao ni Jerop Limo kutoka Kenya anayetumia uzoefu wake wa kuishi na Virusi Vya Ukimwi kwa miaka 24 ya umri wake kuhakikisha ulimwengu unakuwa mahali bora kwa watu ambao tayari wanaishi na virusi hivyo. Anold Kayanda amezungumza naye na hapa Jerop Limo anaanza kwa kueleza yale ambayo atawaeleza viongozi wa ulimwengu.
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners