Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • WFP Bigenimana: Nilichokishuhudia Maiduguri Nigeria ni zahma kubwa
    Wahudumu wa kibinadamu wanahaha hivi sasa kufikisha msaada Kaskazini Mashariki mwa Nigeria kwenye jimbo wa Borno mjini Maiduguri ambako maelfu ya watu wametawanywa baada ya bwawa la Alau kufurika na kupasua kingo zake usiku wa manane  wiki iliyopita kutokana na mvua kubwa. Shirika la Umoja wa Matifa la mpango wa chakula duniani WFP ni mdau mkubwa katika kufikisha misaada hiyo na mkuu wa ofisi yake ya Maiduguri Emmanuel Bigenimana anaeleza alichokishuhudia katika Makala hii inayoletwa kwako na Flora Nducha.
    4 min
  • Guterres: Katika Siku hii ya Ozoni, tujitolee kuweka amani kati yetu na sayari yetu
    Pamoja na chapisho lililotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa (WMO) kuangazia ushahidi unaoongezeka kwamba tabaka la ozoni kwa hakika liko mbioni kurejea katika hali nzuri, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake maalumu kwa ajili ya siku ya leo ya Kimataifa ya Uhifadhi wa Tabaka la Ozoni amesisitiza mataifa yote ulimwenguni kuidhinisha na kutekeleza maazimio ya maboresho ya Itifaki ya Montreal yaliyozaa Marekebisho ya Kigali kwa lengo la kupunguza gesi chafuzi zenye nguvu zinazoongeza joto duniani. Katika ujumbe huo, Bwana Guterres ameeleza kwamba Marekebisho ya Kigali ya Itifaki ya Montreal ambayo yanalenga katika kupunguza hydrofluorocarbons (HFCs) ambazo ni gesi zinazoongeza joto duniani yanaweza kuchangia katika kuendeleza juhudi za kukabiliana na tabianchi, kulinda watu na sayari. “Na hilo linahitajika zaidi kuliko wakati mwingine wowote kwani rekodi za joto zinaendelea kuongezeka.” Akasisitiza.Itifaki ya Montreal ilikubaliwa mnamo mwaka 1987 huko nchini Canada na kuanza kutumika mwaka 1989. Maboresho yake yalifanyika mwaka 2016 mjini Kigali Rwanda na marekebisho hayo ya Kigali yakawa sehemu ya Itifaki ya Montreal kuanzia mwaka 2017. Hadi kufikia Aprili mwaka huu 2024 ni nchi 158 pekee zimeidhinisha marekebisho hayo.Guterres anaendelea kueleza kwamba, “iwapo yataidhinishwa kikamilifu na kutekelezwa, Marekebisho ya Kigali ya Itifaki ya Montreal yanaweza kusaidia kuepuka ongezeko la hadi nyuzi joto 0.5 za Selsiasi duniani kufikia mwisho wa karne hii.”Anasema “wakati ambapo ushirikiano kimataifa uko chini ya shinikizo kubwa, Itifaki ya Montreal ya kusaidia kulinda tabaka la ozoni inajitokeza kama ishara yenye nguvu ya matumaini. Ni ukumbusho kwamba nchi zinapoonesha azimio la kisiasa kwa manufaa ya wote, mabadiliko yanawezekana.”Ushahidi wa mafaniko ya Itifaki ya Montreal pia uko katika ujumbe wa Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Inger Andersen alioutoa leo kwa njia ya video akisema,“hatua zilizochukuliwa chini ya Itifaki hii ya Montreal ziliondoa gesi zilizokuwa zinatumika viwandani, gesi ambazo zilikuwa zilizoharibu tabaka la ozoni na ziliongeza joto duniani.”
    2 min
  • 16 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN wa Tabaka la Ozoni, na mssada wa kibinadamu kwa wenyeji wa kisiwa kidogo cha Carriacou, Grenada waliokumbwa na kimbunga Beryl. Makal tunakupeleka nchini Nigeria na mashinani nchini Sudan.Pamoja na chapisho lililotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa (WMO) kuangazia ushahidi unaoongezeka kwamba tabaka la ozoni kwa hakika liko mbioni kurejea katika hali nzuri, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake maalumu kwa ajili ya siku ya leo ya Kimataifa ya Uhifadhi wa Tabaka la Ozoni amesisitiza mataifa yote ulimwenguni kuidhinisha na kutekeleza maazimio ya maboresho ya Itifaki ya Montreal yaliyozaa Marekebisho ya Kigali kwa lengo la kupunguza gesi chafuzi zenye nguvu zinazoongeza joto duniani.Kimbunga Beryl, kilichopiga tarehe 1 Julai 2024, kimewaacha wakazi wa kisiwa kidogo cha Carriacou, Grenada, na athari kubwa . Kufuatia changamoto zinazowakabili wasamaria kutoka maeneo mbalimbali likiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) wamewasaidia kurejesha matumaini kama anavyosimulia Anthony St. Hilaire manusura wa kimbunga hicho.Makala inatupeleka Maiduguri Nigeria ambako mafuriko yanayoshuhudiwa baada ya bwawa la Alau kupasua kingo zake kutokana na mvua kubwa hayajawahi kuonekana katika miaka ya karibuni. Shirika la Umoja wa Matifa la mpango wa chakula duniani WFP ni mdau Mkubwa katika kufikisha misaada kwa waathirika na mkuu wa ofisi yake ya Maiduguri Emmanuel Bigenimana anaeleza alichokishuhudia.Na katika mashinani Aziza, mama wa watoto wanne kutoka Sudan ambaye alikuwa mhudumu wa kibinadamu na sasa amejikuta mkimbizi nchini Uganda baada ya kukimbia nyumbani kwao Sudan kufuatia mapigano yaliyoanza Aprili 2023. Nyumba yao iliporwa kila kitu na sasa akiwa ukimbizi anasimulia maisha yalivyo tangu ahamishwe na kuwa mkimbizi huku akinufaika na msaada kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
    10 min
  • Baada ya kimbunga Beryl Wasamaria na IOM waishika mkono jamii ya Carriacou
    Kimbunga Beryl, kilichopiga tarehe 1 Julai 2024, kimewaacha wakazi wa kisiwa kidogo cha Carriacou, Grenada, na athari kubwa . Kufuatia changamoto zinazowakabili wasamaria kutoka maeneo mbalimbali likiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) wamewasaidia kurejesha matumaini kama anavyosimulia Anthony St. Hilaire manusura wa kimbunga hicho. Anthony aliyekumbwa na hofu kubwa wakati mawimbi makali ya bahari na upepo wa kimbunga Beryl vilipoanza kusambaratisha nyumba yake anasema hakika hali ilikuwa si hali, kwani akijua fika kulikuwa na hatari ya kupoteza maisha ."Awali, upepo ulianza kuvuma kwa nguvu, tukafunga kila kitu. Kisha kina cha bahari kilianza kupandana mawimbi kugonga madirisha na mlango. Ilibidi tufungue mlango ili kupunguza kasi ya upepo na maji."Anthony anaendelea kueleza jinsi alivyorejea nyumbani baada ya kimbunga, na akakuta kila kitu kimekwenda na maji"Haikuwa rahisi. Rafiki yangu mmoja alinipigia simu na kuniambia kuwa kila kitu kimesafishwa. Nilipofika, karibu nilie. Akaniambia usijali, haya ni mambo ya kidunia. Tumebakiwa na jambo kubwa zaidi ambalo ni uhai."Pamoja na maafa hayo na athari zake IOM ikishirikiana na wadau wengine wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha familia zenye uhitaji mkubwa hazikati tamaa , zinakuwa na matumaini na kuapata misaada haraka iwezekanavyo.
    2 min
  • Walinda amani wa Tanzania wang'ara katika ulinzi wa amani nchini Afrika ya Kati, CAR
    Umoja wa Mataifa umewatunuku nishani Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kikosi cha 7 kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR chini ya mwamvuli wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (MINUSCA) kimetunukiwa nishani za Umoja wa Mataifa mnamo tarehe10 Septemba 2024. Afisa Habari wa kikosi hicho, Kapteni Emanuel Ngonela alikuwa shuhuda na ametuandalia makala hii.
    3 min
  • UN: Watoto zaidi ya 560,000 wamepata chango ya polio katika duru ya kwanza ya kampeni ya chanjo Gaza
    Zaidi ya watoto 560,000 wamepokea chanjo dhidi ya virusi vya polio aina ya pili (cVDPV2) kwenye Ukanda wa Gaza katika duru ya kwanza ya kampeni kubwa ya chanjo iliyomalizima jana yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa.Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, watoto waliopokea chanjo hiyo kupitia kampeni ya dharura ya chanjo Gaza ni wale wenye umri wa chini ya miaka 10.Kupitia ukurasa  wake wa mtandao wa X zamani Twitter Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Adhanon Ghebreyesus amesema “Tunafurahia timu zote za wahudumu wa afya, zilizoendesha operesheni hii ngumu. Tunashukuru sana kwa familia kwa imani na ushirikiano wao. Haya ni mafanikio makubwa huku kukiwa na hali mbaya ya kila siku ya maisha katika Ukanda wa Gaza. Hebu fikiria nini kingeweza kufikiwa endapo kungekuwa na ushitishwaji mapigano.”Awamu ya kwanza ya chango ilianza Septemba Mosi na lengo lilikuwa ni katika kila duru kuchanja  zaidi ya watoto 640 000 wa umri wa chini ya miaka 10.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema maelfu kwa maelfu ya watoto wmechanjwa na kukamilika kwa awamu hiyo ya kwanza ya chanjo ni mafanikio makubwa kwa shirika hilo na wadau wote walioshiriki kwani wamefikia lengo kwa asilimia 90 ingawa sasa changamoto ni kutoa dozi ya pili ya chanjo hiyo katika awamu ya pili ya kampeni inayotarajiwa katika wiki zijazo.Dozi za chanjo ya polio zaidi ya milioni 1.6 ziliwasili Gaza ili kukamilisha awamu zote mbili za chanjo inayohusisha wahudumu wa afya zaidi ya 2700.
    2 min
  • 13 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia chanjo za polio katika ukanda wa Gaza, na kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda. Makala inatupeleka nchini CAR na mashinani tutaelekea Gambella, Ethiopia, kulikoni?Zaidi ya watoto 560,000 wamepokea chanjo dhidi ya virusi vya polio aina ya pili (cVDPV2) kwenye Ukanda wa Gaza katika duru ya kwanza ya kampeni kubwa ya chanjo iliyomalizima jana yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa.Mnara wa kudumu wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda umesimikwa kwenye bustani ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York kuhakikisha kilichotokea hakitosahaulika na      asilani kisitokee tena.Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako Umoja wa Mataifa umewatunuku nishani Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kikosi cha 7 kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu chini ya mwamvuli wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo CAR (MINUSCA).Na katika mashinani tutaelekea Gambella, Ethiopia ambapo kupitia video ya UNICEF, tunakutanisha na Ariet, mtoto wa umri wamiaka 10 aliyekumbwa na utekaji baada ya kijiji chake kuvamiwa. Ariet anaeleza jinsi alivyofurahi baada ya kupata msaada wa UNICEF, ili kurejea kwenye maisha ya kawaida.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
    10 min
  • Mnara wa kudumu kukumbuka mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda umewekwa katika makao makuu ya UN
    Mnara wa kudumu wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda umesimikwa kwenye bustani ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York kuhakikisha kilichotokea hakitosahaulika na  asilani kisitokee tena. Hapa katika bustani ya Umoja wa Mataifa mnara huo uliopewa jina “Kumbukumbu ya Mshumaa wa matumaini au Mshumaa wa mautumaini wa Kwibuka” unaonekana bayana hata ukiwa mbali. Na umetengenezwa mithili ya mshumaa Mkubwa uwakao ikiwa ni zawadi maalum kutoka Jamhuri ya Rwanda kwa Umoja wa Mataifa na umesimikwa hapa rasimi jana Alhamisi.Una kitako cha rangi neyusi na maadhindi ya rangi ya dhahabu ukiwa ni mfano wa mshumaa uwkao wa rangi ya kijivu ukiwa umeandikwa maneno  ya kiingereza yakimaanisha “Mauji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda, kumbuka-ungana-upya na Kwibuka mshumaa wa matumaini”Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mnara huu ni ishara ya mnepo na ujasiri wa watu wa Rwanda tangu mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi na wengine wenye msimamo wa wastani ambapo zaidi ya watu milioni 1 waliuawa kufuatia miaka mingi ya taarifa potofu, za uongo, na kauli za chuki zilizochochea mivutano ya kijamii.Wakati wakisimika mnara huo msaididizi wa Katibu Mkuu wa idara ya mawasiiano ya kimataifa Melissa Flemming alifunguka akisema "Mshumaa wa matumaini wa Kwibuka utawaka milele kama kumbusho kwa jumuiya ya kimataifa  na wageni wote wanaokuja hapa kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu haja ya kuzungumza wazi na kusema Hapana kwa chuki.”Mnara huo umesimikwa wakati Umoja wa Mataifa ukijiandaa na mkutano wa zama zijazo utakaoanza mwisho wa wiki ijayo ukifuatiwa na mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 79.
    3 min
  • 12 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania, kulikofanyika mashauriano kuhusu mkutano wa zama zijazo, ambapo baadhi ya washiriki wameeleza walichojadili na walichopendekeza. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na maana ya neno “KILIWAZO”.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X amelaani vikali tukio la jana huko Gaza ambapo vikosi vya anga vya Israel vilishambulia makazi ya wakimbizi wa ndani wapatao 12, 000. Katika shambulio hilo wafanyakazi 6 wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA walifariki dunia na kufanya tukio hilo kuwa lenye vifo vingi zaidi vya wafanyakazi wa UNRWA katika tukio moja.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) na wadau wake, jana Septemba 11 huko Gaza wamefanikiwa kuhamisha wagonjwa 97 na watu wengine 155 wenye majeraha makubwa zaidi. Katika unaotajwa kuwa uhamishaji mkubwa wa wagonjwa tangu ule wa Oktoba 2023 wagonjwa walisafirishwa kupitia Kerem Shalom hadi Uwanja wa Ndege wa Ramon nchini Israel kwa safari ya kuelekea Abu Dhabi, Falme za Kiarabu.Tukisalia huko Gaza, takribani robo moja au watu elfu ishirini na mbili na mia tano ya wale waliojeruhiwa huko Gaza kufikia Julai 23 wanakadiriwa kuwa na majeraha ambayo yatabadilisha kabisa maisha yao na kwa hivyo wanahitaji huduma za uangalizi sasa na hata kwa miaka ijayo. Hiyo ni kwa mujibu wa uchambuzi uliotolewa leo na WHO.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KILIWAZO”.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners