Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Wachunguzi wa haki za binadamu wataka kuongezwa kwa vikwazo vya silaha Sudan - UN
    Ujumbe Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa  wa kutafuta ukweli nchini Sudan, leo Septemba 6 jijini Geneva, Uswisi, wametoa wito wa kuwekwa vikwazo vya silaha kote nchini Sudan kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kikatili kama vile mashambulizi ya kutisha ya kingono.  Ni mbobevu wa sheria duniani, Mohamed Chande Othman, Mwenyekiti wa Ujumbe huo Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa wa Mataifa wa kutafuta ukweli kuhusu yanayoendelea Sudan akiwaeleza waaandishi wa habari leo kwamba, "tangu katikati ya Aprili mwaka 2023, mzozo wa Sudan umeenea hadi majimbo 14 kati ya 18 na kuathiri nchi nzima na ukanda huo, na kuwafanya Wasudan milioni nane kuwa wakimbizi wa ndani kutokana na mzozo huo, na milioni mbili - zaidi ya milioni mbili – kulazimishwa kukimbilia nchi jirani.”Katika ripoti yao hii ya kwanza tangu Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa lilipounda jopo hilo mwaka jana 2023, wajumbe hawa wamesisitiza kwamba pande zote mbili zinazohasimiana yaani wanajeshi wa Jeshi la Sudan (SAF) na Vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF), pamoja na washirika wao, wanahusika na mashambulizi makubwa, ya kiholela na ya moja kwa moja yaliyohusisha mashambulizi ya anga na makombora dhidi ya raia, shule, hospitali, mitandao ya mawasiliano na miundombinu mingine muhimu ya maji na umeme ikionesha kutozingatia kabisa ulinzi wa wasio wapiganaji.Joy Ngozi Ezeilo, mmoja wa wajumbe wa jopo hilo la wataalamu huru anaeleza kwamba, waathirika walisimulia kushambuliwa wakiwa kwenye nyumba zao na kutishiwa kifo au kuumizwa kwa ndugu au watoto wao kabla ya kubakwa na zaidi ya mtu mmoja.”Wachunguzi hao licha ya kupendekeza uwekaji zaidi wa vikwazo vya silaha kwa Sudan, pia wamehimiza kuanzishwa kwa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani na ama kiwe chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa au mamlaka nyingine ya kikanda.
    2 min
  • 06 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi ya kutisha ya kingono nchini Sudan, na mafunzo ya kidijitali. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Ujumbe Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa  wa kutafuta ukweli nchini Sudan, leo Septemba 6 jijini Geneva, Uswisi, wametoa wito wa kuwekwa vikwazo vya silaha kote nchini Sudan kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kikatili kama vile mashambulizi ya kutisha ya kingono.Uhusiano kati ya teknolojia, elimu, na mabadiliko ya tabianchi ni upi? Hili ndilo limekuwa swala kuu katika mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliopewa jina la Wiki ya Kujifunza kwa Kidijitali au Digital Learning Week uliokamilika jana Alhamisi huko Paris Ufaransa. Mkutano huu uliangazia maswala nyeti ya mchango wa teknolojia katika elimu inayolenga maendeleo.Makala tunaelekea DRC ambako George Musubao, Mwandishi wetu wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akizungumza na Mkuu wa kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC-MONUSCO anayemaliza muda wake mwezi huu baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja Brigedia Jenerali Alfred Matambo. Brigedia Jenerali Matambo anaanza kwa kuzungumzia matokeo ya moja ya operesheni  kubwa za kijeshi 15 walizotekeleza dhidi ya makundi yenye silaha likiwemo la CODECO.Na katika mashinani, Daktari Erick Mashimango aliyeko nchini DRC anatueleza kuwa kuenea kwa ugonjwa wa mpox kwa kasi nchini humo ambako kumegharimu maisha ya ziadi ya watu 600 kumewafanya wananchi kuwa tayari kupokea chanjo.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu! 
    10 min
  • UNESCO: Je AI ina nafasi gani katika kudhibiti habari potofu na za uongo?
    Huko Paris, Ufaransa kumekamilika mkutano wa wiki moja ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ukipatiwa jina Wiki ya Kujifunza Masuala ya Kidijitali au Digital Learning Week ambapo hoja ya Akili Mnemba kudhibiti habari potofu na za uongo imepatiwa kipaumbele.Mkutano huo ulimulika mchango wa teknolojia ya kidijitali katika elimu inayolenga maendeleo badala ya kuyadumaza. Mathalani ni kwa jinsi gani mifumo ya kidijitali inaweza kukabiliana na taarifa potofu kuhusu mabadiliko ya tabianchi.Simon Wanda, Afisa Programu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni amefafanua nafasi ya teknolojia kwenye kukabili taarifa hizo.“Mifumo hii inaweza kuchambua na kutathmini yale yanayowekwa kwenye matandao na kutambua taarifa za uongo au za kupotosha.”Mmoja wa washiriki wa mkutano huo ni Doris Mwikali, Mwanasheria na mtetezi wa elimu kutoka Kenya. Tukamuuliza maoni yake kuhusu nafasi ya teknolojia za kidijitali kwa vijana."Ninafahamu kwamba kuna mazungumzo yanaendelea kuhusu jinsi kampuni za mitandao ya kijamii zinavyopambana  na habari potofu na za uongo. Lakini nadhani kuna zana mpya za akili mnemba zinazotumika na baadhi ya kampuni, kuhakiki  taarifa kwenye mitandao ya kijamii. Ingawa haitakuwa na mchango mkubwa ikilinganishwa na  kampuni za mitandao ya kijamii kuchukua jukumu la kudhibiti habari potofu kwenye majukwaa yao, Bado kuna jukumu kubwa kwa akili mnemba katika uhakiki wa taarifa kwenye mitandao ya kijamii, na hiyo imefanywa na mashirika mengi yasiyo ya kiserikali."Nikarejea kwa Bwana Wanda na kumuuliza maoni yake kuhusu maendeleo ya akili mnemba au AI na ujumuishaji wa sauti kutoka pande zote wakati wa  kusongesha AI.“Zipo jamii nyingi zetu za kiafrika kama wamaasai wa Kenya na Tanzania, ambao kwa muda mrefu wamekuwa na elimu ya asili kuhusu kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ambayo ni elimu inayofaa kutopuuzwa katika makuzi haya ya teknolojia. Hivyo, hili ni suala la kuhoji sana hasa tunapozingatia kwamba maendeleo katika teknolojia yasiegemee eneo moja la elimu tu, ambayo ni elimu ya magharibi, na kupuuza elimu ya kiasili, ambayo ni tunu.”
    3 min
  • 05 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha nchini Bahrain kufuatilia harakati za vijana za kufanikisha haki za watoto waliozaliwa na usonji au Down Syndrome. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na uchambuzi wa methali “Jawabu la kesho andaa leo.”Awamu ya kwanza ya kampeni ya utoaji chanjo ya polio kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 imehamia hii leo eneo la kusini mwa ukanda huo hususan Khan Younis na itakamilika Jumapili hii. Mama mmoja aliyepeleka mtoto wake leo amesema aliposikia tu chanjo inatolewa dhidi ya polio alikimbilia kituo cha jirani cha tiba ili ampatie chanjo kwani anahofia itasambaa kutokana na mazingira machafu ya majitakama wanamoishi. Awamu hii itamalizika Jumapili. Awamu ya Pili itaanza baada ya wiki nne.Nchini China Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anahudhuria mkutano wa China na nchi za Afrika, leo amehutubia mkutano huo na kueleza masuala kadhaa yakusaidia kusongeza nchi za Afrika ikiwemo haja ya kutatua changamoto ya nchi za Afrika kuwa na madeni makubwa na kushindwa kuwekeza katika miradi ya maendeleo, ushirikiano wa kusini -kusini na hitaji la Afrika kuwa na uwakilishi wakudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Na leo ni siku ya Kimataifa ya ukarimu duniani, mfano mmoja tu wa ukarimu unaoendelea sasa duniani ni ule shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA wanaopokea kutoka kila kona ya dunia kuanzia kwa watu maarufu, asasi za kiraia, mpaka watu binafasi, wote lengo likiwa ni kuwawezesha UNRWA kuhudumia wapalestina milioni mbili walio katikati ya mzozo huko Gaza.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, Mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anafafanua methali “Jawabu la kesho andaa leo.”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
    10 min
  • WHO na Zanzibar zashirikiana kutokomeza ugonjwa wa matende
    Huko Zanzibar Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO kanda ya AFrika, linashirikiana na serikali kukabili ugonjwa wa matende ambao ni miongoni mwa magonjwa ya kitropiki yaliyopuuzwa au NTDs. Bosco Cosmas na maelezo zaidi.(Taarifa ya Bosco Cosmas)Video ya WHO kanda ya Afrika inatupeleka Zanzibar, Tanzania nyumbani kwa  Hamis Njani akitembea kwa shida, miguu imevimba. Alipata ugonjwa wa matende akiwa na umri wa miaka 18 lakini sasa WHO imempatia matumaini.(Sauti ya Hamis Njani)“Inaweza kukupata homa siku mbili kwa wiki, kwa hiyo nikashindwa kwenda shuleni.  Wakati mwingine nashindwa kuhudhuria shule kwa miezi hata mitatu. Ninapokwenda kule hospitali, ninapata huduma na mafunzo ya jinsi ya kuishi na haya maradhi kama vile kusafisha, kutumia dawa na mengine yote.”Ugonjwa huu huenezwa na mbu. Husababisha miguu au korodani kujaa maji  .Tangu mwaka 2010 Zanzibar imeendesha kampeni 20 za mgao wa dawa na WHO imetoa dawa kutibu watu milioni 1.5 kila mwaka. Asha Makame ni Mgawaji wa dawa kwenye jamii.(Sauti ya Asha Makame)“Mwanzo ulikuwa mgumu kwa sababu watu walikuwa hawaelewi.  Kwa sasa hivi mwitikio ni mzuri kwa sababu kile kitu watu wamekitumia na wanajua faida yake.WHO imefundisha pia madaktari katika kila hospitali ya wilaya kufanya upasuaji wa kisasa wa mabusha kwa wagonjwa 500.  Dkt. Shali Ahmed ni Meneja Mradi wa NTDs, Wizara ya Afya, Zanzibar.(Sauti ya Dkt. Shali Ahmed - Meneja wa mradi)“Ninaamini kufikia mwaka 2030, hata kabla ya hapo tutakuwa tumekomesha ugonjwa wa matende. Kwa hiyo tunawashukuru sana WHO kwa ushirikiano tunaoupata kwa kupata dawa, mara nyingi tunapata dawa kwa wakati na za kutosha kwa ajili ya nchi nzima.”
    2 min
  • Kemia na ujasiriamali vinavyoambatana katika Chuo Kikuu cha Kenyatta
    Je umeshawahi kujiuliza ni kwa vipi wataalamu wa kemia wanahusiana na ujasiriamali? Kama ndivyo, basi vivyo hivyo kwa Assumpta Massoi akiwa Manama, nchini Bahrain akishiriki Jukwaa la Nne la Uwekezaji kwa Wajasiriamali, WEIF2024 lililoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO, Ofisi ya Uendelezaji wa Biashara, ITPO nchini humo, alikutana na Profesa Ruth Wanjau, Mtafiti na Mshauri wa Masuala ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati katika Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya. Alimuuliza maswali kadhaa ikiwemo ushiriki wake kwenye jukwaa hilo na nini anafanya kusongesha ujasiriamali.
    5 min
  • Afrika yakutana kujadili ukuaji endelevu wa miji kwa mabadiliko ya Afrika
    Mkutano wa siku tatu unaolenga kuendeleza bara la Afrika kupitia ukuaji endelevu wa miji umeanza leo jijini Addis Ababa, Ethiopia kwa ushirikiano wa Muungano wa Afrika, shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani, UN Habitat na Serikali ya Ethiopia. Anold Kayanda ameifuatilia siku ya kwanza ya mkutano huu wa siku tatu na hii ni taarifa yake.(Taarifa ya Anold)Ni mkutano ambao unawapa jukwaa wadau wakuu kutoka kote barani Afrika kuendeleza malengo ya Ajenda ya mwaka 2063 inayosema Afrika Tunayoitaka.Jukwaa hili litachunguza jukumu muhimu la ukuaji wa miji katika kufikia malengo ya Ajenda 2063 na kuunda mustakabali wa miji ya Afrika kwa kuweka mikakati ya kujenga miji ambayo ni endelevu kwa mazingira, inayojumuisha jamii, na inayostahimili uchumi.(Nats)Huyo ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kikanda na Biashara cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa ajili ya Afrika (ECA), Dkt. Stephen Karingi akihutubia mkutano huo anaeleza kuwa ukuaji wa miji wa haraka barani Afrika umekuja na changamoto kama miundombinu duni, kukosekana kwa usawa wa kijamaa na kiuchumi na changamoto za tabianchi na akatumia nafasi hiyo kutoa ahadi kuwa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa ajili ya Afrika (ECA) iko tayari kushirika katika kuzitatua changamoto hizo kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuweka Sera fanisi za Uchumi mkuu na ufadhili kwa ajili ya maendeleo.Mkutano huu utahusisha shughuli mbalimbali ikiwemo mijadala, matukio ya kandoni mwa mkutano na maonesho.Tags: UN-Habitat, Afrika, Africa Urban Forum, Ajenda 2063
    2 min
  • 4 SEPTEMBA 2024
    Ungana na Leah Mushi anayekutea jarida la Umoja wa Mataifa hii leo likiangazia juhudi za Afrika katika kujenga miji endelevu, mapambano ya kutokomeza magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele, matumizi ya sayansi katika nyanja mbalimbali za maisha na mashinani utasikia juhudi za kuhakikisha mipaka ya nchi inaendelea kuwa wazi hata wakati wa majanga ya asili na migogoro. 
    10 min
  • 03 SEPTEMBA 2024
    Karibu kusikiliza jarida ambapo hii leo mwenyeji wako Anold Kayanda anakuletea mada kwa kina inayoangazia nafasi ya vijana katika uongozi. pia utasikia muhtasari wa habari na mashinani inayoangazia kampeni ya utoaji chanjo ya polio  huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati. 
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners