Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Mradi wa KiTiKi wainua wakulima wadogo na wakimbizi nchini Tanzania
    KiTiKi yaani Kilimo Tija Kigoma ni mradi wa kuimarisha mnyororo wa thamani ya kilimo cha wakulima wadogo, usawa wa jinsia na amani katika mkoa wa Kioma unaohifadhi wakimbizi zaidi kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Serikali na watu wa Jamhuri ya Korea wamechangia Dola za Marekani milioni 6 kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ili kuimarisha kilimo cha wakulima wadogo na kuimarisha uhakikika wa chakula na lishe miongoni mwa wakimbizi na jamii zinazowahifadhi mjini Kigoma kwa miaka minne tangu mwishoni mwa mwaka juzi 2022. Anold Kayanda kupitia video ya WFP Tanzania anatupeleka mkoani Kigoma kaskazini magharibi mwa Tanzania kusikia manufaa ya mradi wa Kilimo.  
    3 min
  • MONUSCO yafanikisha kufufuliwa kwa kituo cha  Redio na TV cha taifa RTNC mjini Beni
    Wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wana furaha tele baada ya kufufuliwa kwa kituo chao cha Redio na Televisheni ya Taifa, RTNC. Kupitia msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wakazi hao sasa wanaweza kusikiliza na kutazama vipindi vyao wanavyovipenda, waandishi wa habari nao, hawafanyi tena kazi chini ya mti. Kupitia video ya Monusco iliyochapishwa mtandao wa X, John Matemuli, mwandishi wa habari wa kituo hicho cha Redio na Televisheni Beni, kilichositisha matangazo kwa karibu miaka mitano, anafafanua jinsi mambo yalivyokuwa kabla ya kujengwa upya kwa kituo hicho.“Miaka mitano bila Radio na Televisheni ya kitaifa ya Kongo (RTNC) mjini Beni ilikuwa ya machafuko sana. Kulikuwa na wakati ambapo tulikuwa tukifanya kazi hata kutoka juu ya mti, unaweza kuamini! Tulihisi kwamba kulikuwa na hitaji, wananchi na hata baadhi ya viongozi walihisi vivyo hivyo.”Ezechiel Kambale, mkazi wa Beni naye pia anaeleza furaha yake.“Ulipita muda mrefu tangu redio hii kuwa hewani. Lakini sasa nashukuru kwamba wamerudi. Kuna tofauti kubwa ikilinganishwa na zamani, kwa sababu leo, hata kama niko mbali na mji, bado nayapata mawimbi ya redio kana kwamba nipo hapa mjini.”Tulimrudia John na kumuuliza kilichokuwa tofauti kuhusu kituo hicho hasa kabla ya msaada wa MONUSCO.“Kazi ilofanywa hapa imewaridhisha wananchi. Leo, tuna ofisi za usimamizi. Tuna studio za kisasa za televisheni. Tuna studio ya redio kwa ajili ya kutengeneza vipindi  vyetu. Tuna chumba cha habari kilicho na vifaa vya kutosha. Tulikumbana na matatizo ambayo yalihitaji msaada katika ngazi zote, lakini MONUSCO ilitupatia vifaa, ambavyo sasa vinaturuhusu kufanya kazi katika hali bora.”
    2 min
  • 11 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa wa homa ya nyani au mpox barani Afrika na kufufuliwa kwa kituo chao cha Redio na Televisheni ya Taifa, RTNC huko Beni nchini DRC. Makala tanakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Ugonjwa wa homa ya nyani au mpox ukisalia kuwa dharura ya afya ya umma duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasaka zaidi ya dola milioni 21 zitakazotumika hadi mwishoni mwa mwaka huu kuongeza harakati dhidi ya ugonjwa huo miongoni mwa wakimbizi katika nchi zilizokumbwa na dharura ya ugonjwa huo, hususan Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.Wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wana furaha tele baada ya kufufuliwa kwa kituo chao cha Redio na Televisheni ya Taifa, RTNC. Kupitia msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wakazi hao sasa wanaweza kusikiliza na kutazama vipindi vyao wanavyovipenda, waandishi wa habari nao, hawafanyi tena kazi chini ya mti.Makala inatupeleka mkoani Kigoma kaskazini magharibi mwa Tanzania kusikia manufaa ya mradi wa Kilimo Tija Kigoma (KiTiKi) unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa ufadhili wa Watu wa Jamhuri ya Korea.Na mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani kanda ya Afrika, tunamsikia Shane Prigge mkuu wa mnyororo wa usambazaji, WFP Kenya akieleza jinsi UNHAS ambalo ni shirika la ndege la Umoja wa Mataifa la huduma za kibinadamu linavyowezesha mashirika ya kibinadamu kufanya kazi zao.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • UNHCR yatoa ombi la dharura la dola milioni 21.4 kukabili mpox miongoni mwa wakimbizi barani Afrika
    Ugonjwa wa homa ya nyani au mpox ukisalia kuwa dharura ya afya ya umma duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasaka zaidi ya dola milioni 21 zitakazotumika hadi mwishoni mwa mwaka huu kuongeza harakati dhidi ya ugonjwa huo miongoni mwa wakimbizi katika nchi zilizokumbwa na dharura ya ugonjwa huo, hususan Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Assumpta Massoi anafafanua zaidi.UNHCR imetangaza ombi hilo leo la dola milioni 21.4, fedha zinazolenga kusaidia watu milioni 9.9 waliolazimika kukimbia makwao kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo vita. Watu hao wako kwenye nchi 35 barani Afrika.Hatua hii ya UNHCR inakuja baada ya wagonjwa 88 wa mpox kuwa ni wakimbizi na kati yao hao 68 wako DR Congo, taifa ambalo limeripoti idadi kubwa zaidi ya wagonjwa wa mpox duniani. Wagonjwa pia wameripotiwa Jamhuri ya Congo au Congo-Brazaville na vile vile Rwanda.Taarifa ya UNHCR kutoka Geneva, USwisi inasema, ingawa mpox ni ugonjwa wa muda mrefu barani Afrika, ongezeko la wagojwa hasa wenye mnyumbuliko mpya wa mpox yaani Clade 1b umefanya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO kutangaza tarehe 14 mwezi Agosti kuwa mpox ni dharura ya afya ya umma duniani. Na tangu wakati huo watu 20,000 barani Afrika wameshukiwa kuwa na ugonjwa huo.Allen Maina, Mkuu wa Afya ya Umma UNHCR anasema kwa mazingira ya sasa walio hatarini kuambukizwa zaidi ni wakimbizi wanaoishi kwenye mazingira magumu bila maji, wala sabuni na lishe bora.Sasa wanahitaji kusaidia serikali na wadau katika hatua dhidi ya mpox kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma. Hivyo fedha zitaimarisha mifumo ya afya, maji na huduma za kujisafi na kuhakikisha wakimbizi wanajengewa mnepo sasa na siku za usoni.UNHCR inatoa wito kwa wahisani kuonesha ukarimu wao kwa kuwa fedha hizo zitawezesha ujumuishaji wa wakimbizi kwenye mipango ya serikali katika nchi husika ya kujiandaa na kujikinga dhidi ya mpox kwa mujibu wa Mpango wa Afrika dhidi ya mpox ulioandaliwa na kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuia magonjwa, CDC na WHO.
    3 min
  • 10 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Mwanza kaskazini Magharibi mwa Tanzania kupata ufafanuzi wa athari za moshi wa kuni kwa binadamu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na sauti kutoka mashinani.Miaka 63 tangu kifo cha ajali ya ndege cha Katibu Mkuu wa pili wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld huko Ndola Zambia, bado majibu hayajapatikana ya nini kilisababisha ajali hiyo wakati akielekea kusaka amani kwa iliyokuwa Congo, sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limesema kampeni ya chanjo eneo la kaskazini mwa Gaza imeendelea leo jumanne licha ya tukio la jana la jeshi la Israeli kuzuia kwa saa nane msafara wa wafanyakazi waliokuwa wanasafiri kwenda kutoa huduma hiyo.Na leo septemba 10, mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA78 unakunja jamvi baada ya mwaka mzima wa mikutano na mijadala, na hivyo kuashiria kuanza kwa mkutano wa 79  ambapo kuanzia tarehe 22 vitaanza vikao vya ngazi ya juu na Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu. Rais anayemaliza muda wake ni Balozi Dennis Francis kutoka Trinidad na Tobago na anayempatia kijiti ni Philemon Yang kutoka Cameroon.Katika mashinani, tunamulika mwaka mmoja tangu kimbunga Daniel kipige mji wa Dema mashariki mwa Libya na vitongoji vyake na kuleta mvua kubwa iliyosababisha mafuriko yaliyoua zaidi ya watu 5,000, na kuacha makovu hadi sasa. Maelezo ya Hawa Bu Zqeeba aliyempoteza baba yake katika mafuriko hayo yanakupatia taswira halisi ya makovu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
    10 min
  • ECW yarejesha matumaini kwa msichana Fatima wa Nigeria
    Alipokuwa na umri wa miaka 10 mnamo mwaka 2015, Fatima na familia yake walilazimika kutoroka nyumbani kwao Konduga, ili kuepuka mashambulizi kutoka kwa makundi yenye silaha. Konduga iko kilomita 25 kusini mashariki mwa mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria.Familia ya Fatima haikuwa na namna ya kumuandikisha katika shule yoyote rasmi. Alitumia muda wake mwingi kuuza chakula.Shukrani kwa usaidizi wa mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri yaani Education Cannot Wait (ECW) na wadau wake wa kimkakati, Fatima sasa amesajiliwa katika mpango mesto unaolenga kuwapa elimu wasichana walio nje ya shule.Msichana huyu ni mmoja wa walengwa 250 wa programu ya miezi mitano ya kusoma, kuandika na kuhesabu, ambayo imemwezesha kusoma kwa lugha ya Kihausa na hata kuandika jina lake kama anavyoeleza."Niliingia katika shule ya ufundi baada ya kusikia kuihusu wakati nilipokuwa nimeenda kuuza chakua. Mara moja nilihifadhi kile nilichoenda kuuza kisha nikajiandikisha jina langu. Wale ambao tulikuwa hatuendi shule tulitambuliwa na kuchaguliwa. Tulifundishwa jinsi ya kusoma na kuandika. Kabla hapo nilikuwa siwezi hata kuandika jina langu.”Sehemu ya pili ya programu hii mseto ilihusisha kipengele cha ufundi ambapo wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi hupata mafunzo ya ufundi kwa muda wa miezi mitatu. Mpango unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, Norwegian Refugee Council (NRC) na Save the Children."Pia, sasa ninajua namba, na ninaweza kupima watu  ninaposhona." Anasema Fatima ambaye katika kipengengele cha ufundi yeye amechagua ushoni wa nguo.Mpango huu tayari umewanufaisha wasichana balehe 600 tangu kuanzishwa kwake, na kuwapa vifaa vya kuanzia na ujuzi wa kujitegemea. Fatima naye ana matumaini.“Nataka kujifunza stadi hii ili niwahishimishe wazazi wangu na wawe na furaha. Nikimaliza kujifunza nataka kuwa mtu wa kuwashonea ndugu zangu nguo.”Kama ambavyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatoa wito kwa nchi zote kuwekeza katika elimu na kufanya juhudi za kila namna kulinda elimu na maeneo ya kusomea, kulinda wanafunzi na walimu,  Mkurugenzi Mtendaji wa Education Cannot Wait (ECW) Yasmine Sherif, anaeleza namna ambavyo mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri umejizatiti kuendelea kuiunga mkono elimu kote duniani wakati huo akitoa wito kwa kila anayeweza kuwaongezea nguvu afanye hivyo."Kuna ustahimilivu na watoto hawa wamepitia kiwewe na mambo mengi. Ni lazima tuwepo kwa ajili yao, na tunaweza kuona matokeo. Tunatazamia kuufanya tena mpango huu mwaka katika mwaka huu, tunatarajia kufanya hivyo kwa takribani dola milioni 15, kama sio zaidi. Ikiwa nyinyi nyote mtakuja na kutusaidia kuongeza."
    4 min
  • 09 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia suala la elimu katika maeneo ya migogoro, na msaada wa kibinadamu huko Upper Nile nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Nigeria na mashinani nchini Afghanistan, kulikoni??Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kulinda elimu isishambuliwe wakati wa mizozo kutokana na umuhimu wake kwa watoto na jamii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema miaka ya karibuni imeshuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi dhidi ya wanafunzi, walimu na shule duniani kote. Hivyo ndivyo alivyoanza ujumbe wake wa siku hii.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano.Makala inatupeleka Maiduguri nchini Nigeria kusikia namna mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri yaani Education Cannot Wait (ECW) kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) na wadau wengine wanarejesha matumaini kwa waliokosa elimu rasmi hasa kutokana na hali mbayá ya usalama katika maeneo yao.Na katika mashinani, fursa ni yake Faeza, mfanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza biskuti nchini Afghanistan, mradi unaowezeshwa na shirika la WFP akitueleza manufaa ya mradi huo kwa jamii iliyoathirika na vita hasa wanawake na watoto.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • UNMISS: Wananchi wa kaunti ya Nasir watakiwa kuepuka mapigano ili wapelekewe maendeleo
    Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano. UNMISS pamoja na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu walifikia uamuzi wa kusitisha huduma zao katika kaunti ya Nasir kutokana nae eneo hilo kutofikika na pia ukosefu wa usalama uliosababishwa na mapigano ya mara kwa mara baina ya wanajamii wa kuanti hiyo, na pia mapigano na kaunti za jirani.Hata hivyo mwanzoni mwa mwezi huu wa Septemba kilifanyika kikao kilichowaleta pamoja wadau na wananchi baada ya kupatikana uongozi mpya wa kaunti hiyo ambapo katika kikao hicho, wadau wa misaada ya kibinadamu ikiwemo Umoja wa Mataifa waliombwa kurejesha operesheni zao hususan UNMISS, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) na wadau wa Sekta ya afya.Paul Ebikwo ni afisa wa masuala ya kiraia wa UNMISS na akawaeleza anaelewa wasiwasi wao.“Wasiwasi wenu ni wa halali, ni wa kweli, tunaelewa. Lakini mkiongeza mizozo ndani yake, mnafanya mambo kuwa mabaya zaidi, kwa hivyo hebu tufanye maamuzi ya kuachana, na kuweka kando migogoro na sote tufikirie jinsi ya kutatua maswala haya.”Bwana Ebikwo aliongeza kuwa suluhu zote za kuzuia ghasia lazima ziongozwe na wanajamii wenyewe huku akitoa wito kwa makundi ya vijana wanaotumia silaha kujiepusha na mapigano na kutafuta amani.Majadiliano yalihitimishwa kwa wote kukubaliana kuwa na dhamira ya pamoja ya kutafuta njia za kuleta jamii hususani vijana pamoja kwa ajili ya upatanisho na ujenzi wa amani ili kusaidia kurejesha utulivu na kuwezesha jamii katika kaunti ya Nasir kupata ahueni na maendeleo baada ya kuteseka kwa muda mrefu.
    2 min
  • Guterres: Vita huharibu miili, akili na fikra za vijana na watoto
    Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kulinda elimu isishambuliwe wakati wa mizozo kutokana na umuhimu wake kwa watoto na jamii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema miaka ya karibuni imeshuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi dhidi ya wanafunzi, walimu na shule duniani kote. Hivyo ndivyo alivyoanza ujumbe wake wa siku hii. Katibu Mkuu anasema kuanzia Gaza hadi Sudan, Myanmar, Ukraine, Colombia hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kwingineko, vita inasababisha ukatili kwa binadamu, lakini kwa watoto na vijana waliokutwa katikati ya jinamizi la vita, gharama haiwezi kukokotolewa.Anasema ndio maana siku hii inatukumbusha jinsi vita inaharibu miili, akili na fikra za watoto na vijana. Kuanzia majeraha hadi vifo, kutekwa nyara, kulazimika kukimbia, ukatili wa kingono, kutumikishwa vijana na kupoteza fursa. Hatari ni kubwa sana.Anakumbusha kuwa elimu sio tu haki ya msingi ya binadamu, bali ni muhimu kwa ajili ya kutimiza haki nyingine zote za binadamu.Ni kwa mantiki hiyo anataka nchi ziwekeze kwenye elimu na zifanye juhudi zote kuhakikisha wakati wa mizozo elimu na maeneo ya kujifunza yanalindwa, zilinde wanafunzi na walimu na ziwawajibishe wale wote wanaoshambulia shule.Ametumia pia ujumbe huo kuzitaka nchi ziridhie na zitekeleze Azimio la Shule Salama, ziunge mkono Ubia wa Kimataifa wa Kuepusha Mashambulizi dhidi ya Shule na zishikamane na juhudi zote za kuhakikisha watoto na vijana wanaendelea kujifunza iwe wakati wa majanga au wakati majanga yanapokoma.Ametamatisha akisema hebu na tulishe elimu isishambuliwe, tulinde haki ya msingi ya elimu ambayo ni haki ya kila mtoto, kila mtu kokote kule.
    2 min
  • Operesheni dhidi ya makundi yenye silaha likiwemo la CODECO nchini DRC - Brigedia Jenerali Alfred Matambo
    Mkuu wa kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC-MONUSCO anayemaliza muda wake mwezi huu baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja Brigedia Jenerali Alfred Matambo akizungumza na George Musubao, Mwandishi wetu wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, anaeleza matokeo ya moja ya operesheni kubwa za kijeshi 15 walizotekeleza dhidi ya makundi yenye silaha likiwemo la CODECO na kazi za ujumbe huo nchini DRC.
    5 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners