Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Viongozi wa kimataifa washikamane kuhakikisha ulimwengu wenye usawa wa kijinsia - Dorice Mkiva
    Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani ambako mkutano wa Zama Zijazo umen’goa nanga leo kwa siku mbili za kuchua hatua kabla ya kikao cha ngazi ya juu siku ya Jumapili na Jumatatu. Leo Vijana wanapata fursa ya kupaza sauti zao kuhusu dunia na mustakbali wautakao. Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na kijana mwenye ulemavu kutoka Tanzania ambaye ni mmoja wa wazungumzaji  wa mkutao wa leo. Anaanza kwa kujitambulisha.
    3 min
  • 20 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia uondoaji wa taka katika ukanda wa Gaza, na ujumbe wa vijana ambao watashiriki mijadala mikuu hapa makaomakuu ya Umoja wa Mataifa. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu na mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini, kulikoni?Hali inazidi kuwa si hali huko Ukanda wa Gaza kwani sasa raia wanakwepa sio tu mashambulizi na magonjwa bali pia nyoka, panya na wadudu ambao wanasambaa kutokana na mazingira machafu. Watu wanajihifadhi kwenye maeneo ya wazi bila mifumo ya majitaka au ya kuondoa maji ya mvua. Timu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina imefika kupuliza dawa ili kulinda wananchi hao.Leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani vijana kutoka kila kona ya dunia wanakutana kuanza kujadili kuhusu mstakabali wao katika zama zijazo. Miongoni mwao ni Jerop Limo kutoka Kenya anayetumia uzoefu wake wa kuishi na Virusi Vya Ukimwi kwa miaka 24 ya umri wake kuhakikisha ulimwengu unakuwa mahali bora kwa watu ambao tayari wanaishi na virusi hivyo.Makala inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani ambako mkutano wa Zama Zijazo umen’goa nanga leo kwa siku mbili za kuchua hatua kabla ya kikao cha ngazi ya juu siku ya Jumapili na Jumatatu. Leo Vijana wanapata fursa ya kupaza sauti zao kuhusu dunia na mustakbali wautakao.Na katika mashinani Balozi Mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Tendai Mtawarira, mwanamichezo nguli mstaafu wa mpira wa raga mzaliwa wa Zimbabwe lakini alichezea Afrika Kusini, akizungumzia alichokishuhudia katika safari yake ya kwanza nchini Sudan Kusini.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • UNRWA: Nyoka, panya na wadudu vyatishia wakazi wa Gaza
    Hali inazidi kuwa si hali huko Ukanda wa Gaza kwani sasa raia wanakwepa sio tu mashambulizi na magonjwa bali pia nyoka, panya na wadudu ambao wanasambaa kutokana na mazingira machafu. Watu wanajihifadhi kwenye maeneo ya wazi bila mifumo ya majitaka au ya kuondoa maji ya mvua. Timu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina imefika kupuliza dawa ili kulinda wananchi hao. Tuko Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, video ya UNRWA inaonesha wafanyakazi wa shirika hilo wamefika kwenye makazi ya muda ya wakimbizi wa  ndani. Katika eneo hili majitaka yamezingira makazi ya wakimbizi kwani hakuna mifumo ya kuyaondoa.Kando kidogo, mama anaonekana akimsafisha mwanae kwa kutumia maji yaliyohifadhiwa kwenye dumu.Mama huyu ambaye jina lake halikupatikana anasema, nilifurushwa kutoka jiji la Gaza hadi hapa Khan Younis. Tumefika kwenye eneo lililokuwa wazi, kwa hiyo uwepo wa panya na wadudu unahatarisha maisha ya watoto wangu. Nina hofu kubwa ya afya ya watoto wangu kutokana na wadudu na panya.Sasa anaonekana afisa mmoja wa UNRWA akiwa na wenzake wakipita hema kwa hema wakigawa dawa za kuua wadudu hao.Afisa huyu anasema wamewapatia ushauri na mwongozo wa jinsi ya kutumia dawa hizo.Halikadhalika wamepuliza dawa za kuulia wadudu na pia kuondoa taka zilizokuweko karibu na makazi ya wakimbizi hao wa ndani.UNRWA inasema viwango vya juu vya joto, na uweko wa makazi hayo kwenye eneo la wazi ni mazingira rafiki kwa panya, nyoka na wadudu wengine.Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, tangu vita ianze Gaza, tarehe 7 Oktoba mwaka 2023, zaidi ya watu milioni 1.9 wamefurushwa makwao.
    2 min
  • 19 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tuankuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Sudan Kusini kufuatilia changamoto za kibinadamu na jinsi ambavyo mashirika ya Umoja wa Mataifa yanavyozitatua. Pi atunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo na ufafanuzi wa methali.Licha ya kuongezeka kwa majanga duniani, kuanzia umaskini hadi dharura ya tabianchi, Umoja wa Mataifa umesalia na azma yake ya kusongesha amani, maendeleo endelevu na kupunguza machungu yanayowapata binadamu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika ripoti yake ya mwaka ya utendaji wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo jijini New York, Marekani kabla ya kuanza kwa Mjadala Mkuu wa  mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA79.Shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi, UNAIDS hii leo limetoa ripoti yake huko Geneva, Uswisi ikionesha kuwa mzigo wa madeni unaokabili nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara unasababisha zibakie na fedha kidogo kugharimia huduma za afya, pamoja na huduma muhimu zaidi dhidi ya Virusi vya Ukimwi, VVU. Idadi kubwa ya watu wanaoishi na VVU duniani wako eneo hilo lakini mzigo wa madeni unarudisha nyuma maendeleo yaliyopatikana ya kutokomeza Ukimwi ifikapo 2030.Tukisalia na suala hilo hilo la UKIMWI, UNAIDS inasema vijana wawili wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na pia wana ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, Ibanomonde Ngema kutoka Afrika Kusini, na Jerop Limo kutoka Kenya, wako njiani kuja New York, Marekani kushiriki UNGA79 na Mkutano wa Zama Zijazo kwa lengo la kusihi viongozi wa dunia kushirikiana na vijana katika kutokomeza Ukimwi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Mke ni nguomgomba ni kupalilia.”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
    11 min
  • Pamoja na kuahirisha uchaguzi tunachoimbea Sudan Kusini ni amani: FAO Meshack Malo
    Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO nchini Sudan Kusini limesema licha ya uchaguzi mkuu kuahirishwa nchini humo hadi 22 Desemba 2026 kitu kikubwa kwa taifa hilo changa zaidi barani Afrika ni amani. Akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili katika Makala hii Meshack Malo mwakilishi wa FAO Sudan Kusini amesema kuahirisha uchaguzi huo ambao awali ilikuwa ufanyike 22 Desemba mwaka huu 2024 ni  uwamuzi wa Wasudan na wana sababu za msingi, hivyo jumuiya ya kimataifa itaendelea kushirikiana nao na kuliombea amani taifa hilo.
    4 min
  • Mfuko wa Kimataifa yatoa karibia dola milioni 10 kukabiliana na mpox DRC
    Kutokana na ombi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (the Global Fund) leo umetangaza kuchangia dola za Marekani milioni 9.5 kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa mpox katika majimbo sita kati ya yale yenye viwango vya juu zaidi vya maambukizi nchini humo.  Tangazo hilo lililotolewa leo Septemba 18 katika makao makuu ya Mfuko huo wa kimataifa unaofahamika kama The Global Fund, mjini Geneva, Uswisi imeeleza kuwa fedha hizo zinaelekezwa katika katika jimbo la Equateur, Ubangi Kusini, Sankuru, Tshopo, Kivu Kusini, Kivu Kaskazini na Kinshasa, jimbo lenye msongamano mkubwa wa watu milioni 17.
    2 min
  • 18 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia juhudi za Umoja wa Mataifa za kukabiliana na ugonjwa wa MPOX barani Afrika. Makala inatupeleka nchini Sudan Kusini kuangazia uhairishwaji wa uchaguzi na mashinani nchini Sudan ambapo vilabu vinatumiwa kuimarisha ulinzi wa wasichana.Kutokana na ombi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (the Global Fund) leo umetangaza kuchangia dola za Marekani milioni 9.5 kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa mpox katika majimbo sita kati ya yale yenye viwango vya juu zaidi vya maambukizi nchini humo.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Burundi linasema asilimia 33 ya wagonjwa wa homa ya nyani au mpox nchini humo ni watoto wa kwenda shule wenye umri wa kuanzia miaka 5 hadi 19, na hivyo kuwa changamoto mpya wakati familia zinajiandaa kwa mwaka mpya wa masomo.Makala leo inatupeleka Sudan Kusini ambako mwishoni mwa wiki serikali ilitangaza kuahirisha uchaguzi mkuu ambao ulikuwa ufanyike 22 Desemba mwaka huu 2024.Mashinani tuko katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam nchini Sudan ambako shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA) linatumia vilabu kufanikisha ulinzi wa wasichana walio hatarini. Sasa Ikhlas Mousa Andulkareem ambaye ni mfanyakazi wa kijamii katika shirika lisilo la kiserikali la Nada ALAzhar, linalopata usaidizi kutoka UNFPA anatueleza jinsi eneo salama kwa wanawake na wasichana litawanufaisha waathiriwa kwenye kambi hii ya Zamzam.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • UNICEF Burundi yachukua hatua mpox isivuruge muhula wa masomo kwa watoto
    Nchini Burundi shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana na serikali kuhakikisha mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nyani au mpox nchini humo hauthiri watoto kurejea shuleni wakati huu ambapo asilimia 33 ya wagonjwa wakiripotiwa kuwa na umri wa kati ya miaka 5 hadi 19. Cecily Kariuki anatupa maelezo zaidi kupitia  video hii ya UNICEF inayotupeleka hospitali ya Prince Louis Rwagasore iliyoko mji mkuu wa taifa hilo la Maziwa Makuu, Afrika, Bujumbura..Video ya UNICEF inaanzia kwenye uwanja wenye mahema yenye nembo ya shirika hilo. Moja kwa moja tunaingia ndani, daktari akitoa maelekezo kwa akina mama walioko na watoto wao wanaougua mpox. Miongoni mwao ni Primitive Nibitanga, mama watoto wawili. Primitive anasema tumelazwa kwa zaidi ya wiki mbili sasa. Nilienda kituo cha afya lakini hawakuweza kumtibu mtoto wangu. Majirani walinishauri nije hapa kliniki. Nilifika na kulazwa. Mtoto wangu alikuwa mahututi, lakini wauguzi walijitahidi kwa kadri ya uwezo wao na haikuchukua muda alipona. Bahati mbayá siku tatu baadaye dada yake alipata dalili zile zile na tukarejea tena hapa.”Daktari Fidel Cishahayoanahusika na usimamizi wa matibabu ya mpox katika hospitali hii ya Prince Rwegasore. Anasema “hatua ya kwanza ilikuwa kutenga hili eneo kwa sababu tulikuwa tunapokea wagonjwa wa mpox na wanaoshukiwa kuwa na maambukizi. Kwa hiyo tuliandaa ili kuwa na eneo la wagonjwa na washukiwa. Tuliandaa pia timu ya wahudumu, wakiwemo madaktari na wauguzi kutoka idara nyingine kwa ajili ya mpox. Wanaopona wanaruhusiwa na kushauriwa kujitenga kwa angalau wiki tatu.” UNICEF tayari imeomba dola milioni 58.8 kusaidia kupambana na mlipuko wa mpox barani Afrika ikiwemo nchini Burundi. Mwakilishi wa UNICEF nchini Burundi France Bégin amesema fedha hizo pamoja na mambo mengine zitasaidia kuwalinda watoto ili warejee shuleni licha ya mlipuko. Vile vile kuepusha kuvurugwa zaidi kwa fursa za wanafunzi kusoma kwani mwaka mpya wa masomo umeanza tarehe 16 mwezi huu wa Septemba.
    2 min
  • 17 SEPTEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Nairobi Kenya ambako tutamsikiamwanamuziki nyota, mjasiriamali na mwanaharakati wa haki za wanawake Lizi Ogumbo. Pia tunakuletea habari kwa ufufpi na mashinani.Vurugu dhidi ya wapinzani wa serikali nchini Venezuela zimefurutu ada, imesema tume huru ya uchunguzi ikitaja kukamatwa, ukatili wa kingono na utesaji kama mbinu zitumiwazo na serikali ya Rais Nicolas Maduro ili aendelee kuweko madarani.Mwaka 2024 ukiripotiwa kuwa na idadi kubwa ya chaguzi kwenye nchi zaidi ya 60 ambako zaidi ya watu bilioni 1 watapiga kura kuchagua viongozi wao wa umma, wataalamu wa Umoja wa Mataia wanaelezea hofu yao juu ya kitendo cha watu kutoweshwa katika kipindi hicho ili kunyamazisha demokrasia, kitendo ambacho wamesema kinabinya uhuru wa kupiga kura.Na hii leo matokeo ya utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa yameonesha kuwa licha ya majanga yanayoendelea kukumba dunia, nchi wanachama zimeendelea kujizatiti kuanzisha huduma za serikali mtandao ili wananchi waweze kupata huduma mbali mbali kidijitali, ambapo ripoti inazitaja Denmark, Estonia na Singapore kushika nafasi ya juu kati ya nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa, kwa mawanda na ubora wa huduma za serikali mtandaoni.Katika mashinani Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP nchini Bangladesh Stefan Liller anatueleza kiwango cha athari za mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners