Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 21 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa COP16 katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia na ufugaji nyuki Turakana nchini Kenya. Pia tunakupeleka nchini Somalia kufutilia programu wa WFP wa mlo shuleni na mashinani inatupeleka nchini Lebanon.Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng’oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili.Kila siku, mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda shule wakiwa na njaa, wengi wao wakiteseka na utapiamlo sugu ambao huathiri ukuaji wa kiakili na utendaji wao katika masomo. Wanaobahatika huweza tu kumaliza masomo yao na kufanikiwa maishani kutokana na programu ya ‘mlo ya shuleni’ inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP). Mfano wa wanufaika hao ni El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa sasa wa WFP nchini Somalia.Makala inatupeleka Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame ambako mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.Mashinani fursa ni yake Waffiyah Diyah kutoka Lebanon ambaye ni muathirika wa vita vilivyolazimisha maelfu ya watu kufangasha viragoanaelezea hali ya familia yake baada ya kukimbia mashambulizi na kupoteza kila kitu, lakini sasa anapokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM).Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • COP16: Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Baionuai waanza nchini Colombia
    Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng’oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili. COP16  kwa siku 12, viongozi na wadau kutoka kote duniani wanatarajiwa kujadili  namna ya wanadamu kuishi kwa amani na asili ya ulimwengu, kama wasemavyo nchi  mwenyeji Colombia kwa lugha ya kihispanyola Paz con la Naturaleza yaani amani na asili.Washiriki, kwa kina watajadili utekelezaji wa mkakati wa Kimataifa wa Kunming-Montreal kuhusu bayoanuai, makubaliano ya kihistoria ya mwaka 2022 ya kusitisha na kubadili upotevu wa asili. Pia watachunguza jinsi ya kuelekeza mabilioni ya dola kwa nchi zinazoendelea ili kuhifadhi na kudhibiti bioanuai kwa uendelevu. Na watajadili sheria za msingi ambazo zinaweza kuhitaji kampuni za kibinafsi kufidia mataifa.Katika sherehe za ufunguzi wa mkutano huu hapo jana, kwa njia ya video, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye pia anategemewa kuhudhuria siku za mwishomwisho za mkutano huu, amewaeleza wajumbe akisema, “mkakati wa Kimataifa wa Bioanuwai unaahidi kurekebisha uhusiano na dunia na mifumo yake ya ikolojia. Lakini hatuko kwenye mstari. Jukumu lenu katika COP hii ni kubadilisha maneno kuwa vitendo.”
    2 min
  • Nchi zote pamoja na mashirika ya kimataifa ikiwemo UN yanawajibika kukomesha ukaliwaji wa Palestina
    Tume hiyo huru imeyasema hayo katika taarifa mpya ya msimamo wa kisheriia iliyotolewa mjini Geneva Uswis kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina ikiwemo Jerusalem Mashariki ambayo imeweka wazi maoni ya tume kuhusiana na wajibu wa serikali na jinsi Baraza Kuu na Baraza la Usalama linavyoweza kutambua na kutekeleza mbinu na hatua sahihi zinazohitajika kwa kazi hiyo hadi mwisho wa ukaliwaji huo, na kwa haraka iwezekanavyo.Tume ihiyo imebaini kwamba maoni ya ushauri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu matokeo ya Kisheria yanayotokana na sera na desturi za Israel katika eneo linalokaliwa la Palestina ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki ni wenye mamlaka na usio na utata kwa kusema kwamba kuendelea kuwepo kwa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu ni kinyume cha sheria na sheria ya kimataifa.Taarifa hiyo ikitolewa Geneva Gaza kwenyenyewe hali inaendelea kuwa tete, kwa mujibu wa Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestinna UNRWA Phillipe Lazzarini, kwani shule nyingine ya UNRWA imeshambuliwa leo Jabalia Kaskazini mwa Gaza, watu kadhaa wameripotiwa kuuawa na miongoni mwao Watoto wengi waliokuwa wakipata hifadhi katika jengo hilo.Lazzarini amesema hili ni shambulio la tatu dhidi ya majengo ya UNRWA kwa wiki moja. Na pia wafanyakazi wa shirika hilo wanaendelea kuuawa sasa wameffikia 231 tangu kuanza kwa vita hii Oktoba mwaka jana.Naye msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF James Elder akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo amesema “Gaza ni mfano halisi wa ulimwengu wa kuzimu duniani kwa watoto milioni moja wa eneo hilo. Na hali inazidi kuwa mbaya, siku baada ya siku, tunapoona athari za kutisha za mashambulizi ya anga ya kila siku na operesheni za kijeshi za Israek kwa watoto wa Kipalestina.”Nalo shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA likiangazia Ukingo wa Magharibi limesema “Vikosi vya Israel vimekuwa vikitumia mbinu mbaya za vita katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kuibua wasiwasi mkubwa juu ya matumizi ya nguvu kupita kiasi na kuongeza mahitaji ya kibinadamu ya watu.” Ameelezea wasiwasi kuhusu mashambulizi ya walowezi wa Israel dhidi ya Wapalestina na miti yao ya mizeituni wakati huu wa mavuno ya kila mwaka.
    3 min
  • Mbegu za asili zinanisaidia kukabili mabadiliko ya tabianchi - Mkulima
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO linapigia chepuo uwepo wa mifumo ya uzalishaji chakula inayoendana na kila eneo husika, mathalani kilimo kitumie mbegu za asili za eneo husika kama mbinu ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Kupata aina tofauti tofauti za mbegu za asili kwa eneo husika kunainua kipato cha wakazi wa vijijini na kuongeza mnepo majanga yanapotokea. Na hicho ndio anafanya mkulima kutoka Tanzania ambaye wakati wa maonesho ya siku ya chakula duniani huko mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa Tanzania alieleza kwa nini ameamua kuchukua hatua hiyo. Assumpta Massoi anasimulia zaidi.
    4 min
  • UN Ripoti: Uwezekano wa kifo cha Dag Hammarskjöld kuwa ni hila unaongezeka kutokana na taarifa mpya
    Ripoti nyingine mpya ya tathimini ya uchunguzi wa hali na mazingira ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1961 Dag Hammarskjöld imetolewa leo ikiwa na vipengele vinne vipya vikiongeza uwezekano kwamba kifo hicho cha ajali ya ndege kilikuwa ni hila. Asante Anold kwanza ikumbukwe kuwa hii sio ripoti ya kwanza na huenda isiwe ya mwisho ya kutathimini hali na mazingira yliyochangia ajali ya ndege iliyokatili maisha ya Dag Hammarskjöld tarehe 17 Septemba 1961 akiwa njia kuelekea Congo ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cngo DRC, kujadili usitishwaji wa uhasama ila ni ripoti ya karibuni zaidiRipoti inasema mwenyekiti wa jopo la tathimini ya uchunguzi jaji mkuu wa zamani wa Tanzania Mohamed Chande Othman amepokea taarifa mpya muhimu kutoka kwa nchi wanachama ambazo zinajumuisha maeneo haya Mosi:  uingiliaji unaowezekana wa Nchi Wanachama wa mawasiliano husika.Pili: Uwezo wa wanajeshi wa Katanga, au wengine, wa kufanya shambulio linalowezekana kwenye ndege ya SE-BDY,Tatu: kuwepo kwa askari wa kigeni na wafanyakazi wa kijasusi katika eneo hilo la tukioNa nne: Taarifa zaidi mpya zinazohusiana na muktadha na matukio yanayozunguka kifo hicho mwaka 1961.Jaji Othman amemkabidi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ripoti hii ya tathimini ambaye naye ameiwasilisha kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.Na kufuatiia tathimini hii Guterres amesema anaizingatia ingawa kihistoria kumekuwa na nadharia nyingi zilizotolewa kama sababu inayowezekana ya ajali hiyo, na anazichukulia nadharia hizo nyingi kuwa zisizo na uthibitisho.Hata hivyo mwenyekiti wa jopo la tathimini anasema  nadharia nyingine ambayo inabaki na inakubalika ni kwamba shambulio la nje au tishio lilikuwa sababu ya ajali.Pia amesema kuwa dhana mbadala zinazoonekana kuwepo ni kwamba ajali hiyo ilitokana na hujuma, au makosa ya kibinadamu yasiyokusudiwa.Katibu mkuu amekaribisha ushirikiano uliotolewa na baadhi ya nchi wanachama katika tathimini hiyo lakini bado jopo la tathimini linaaminikuna baadhi ya nchi wanachama wana taarifa muhimu ambazo hawajataka kuzitoa.
    3 min
  • 18 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia eneo linalokaliwa kwa mbavu la Kipalestina, na ndoto Mchezaji kijana wa soka zilizokatizwa na vita katika ukanda wa Gaza. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani Kenya, kulikoni?Tume Huru ya Kimataifa ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina leo imesema mataifa yote na mashirika ya kimataifa, ikiwa ni amoja na Umoja wa Mataifa, wana wajibu chini ya sheria za kimataifa wa kukomesha uwepo haramu wa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, wakati mashambulizi Gaza yakishika kazi na kuongeza madhila kwa raia.Katika ufukwe wa Al- Mawasi, magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, mchezaji mpira wa Klabu ya Soka ya Rafah Services anaendelea na mazoezi yake ili kuendeleza uthabiti wa mwili kama mchezaji wa soka wa kulipwa wa klabu hiyo muhimu wakati huu mashambulizi ya makombora yakiendelea kwenye eneo hilo.Makala inatupeleka Tanzania hususan mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki ambako Assumpta Massoi amezungumza na mhifadhi wa mbegu za asili, mahojiano yaliyofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini humo. Mhifadhi mbegu anaanza kwa kujitambulisha.Na mashinani fursa ni yake Nosizi Reuben Dube ambaye kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), amefanikiwa kupata shahada ya chuo kikuu, akiwakilisha tumaini kwa jamii yake, ambayo imeishi Kenya kwa zaidi ya 50 bila uraia hadi walipotambuliwa hivi karibuni na serikali ya Kenya na kuwapatia vyeti vya uraiaMwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 
    11 min
  • Mohamed hajakata tamaa ya kuwa mwanasoka maarufu - Gaza
    Katika ufukwe wa Al- Mawasi, magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, mchezaji mpira wa Klabu ya Soka ya Rafah Services anaendelea na mazoezi yake ili kuendeleza uthabiti wa mwili kama mchezaji wa soka wa kulipwa wa klabu hiyo muhimu wakati huu mashambulizi ya makombora yakiendelea kwenye eneo hilo. Jua linazama hapa kwenye ufukwe wa Al Mawasi, kwenye bahari ya Mediteranea, wengine wakiwa wanaogelea, na kwa mbali mahema ya waliosaka hifadhi baada ya kufurushwa kaskazini mwa Gaza, mmoja anaonesha mbwembwe za dana dana ya mpira, anajitambulisha."Naitwa Mohamed Abu Jalda, mchezaji wa Klabu ya Rafah Services katika daraja la kwanza. Nilikuwa na ari kubwa ya kuwa mchezaji mkubwa wa soka kama wengine walioko nje ya Ukanda wa Gaza, lakini kutokana na vita, tamaa yangu na maisha yangu yalicheleweshwa, sasa nina zaidi ya miaka 20, nikijaribu kuwa mchezaji wa soka, lakini siwezi kwa sababu naishi Gaza ambapo kuna mapigano ya mara kwa mara. Kila siku nahisi kama ninakufa; Mungu atujalie uvumilivu kuhimili maisha haya."Mohamed amekuwa akiwa na ndoto ya kucheza soka ya kulipwa tangu akiwa na umri wa miaka 10 na sasa ana umri wa miaka 20 anaona ndoto inayoyoma, lakini ana matumaini.."Wakati wowote nikipata muda na kutamani kucheza soka,ninakuja ufukweni, kwani ni sehemu pekee naweza kucheza kama mchezaji mwingine. Natumai Mungu atanijalia kufanikiwa kuwa mchezaji wa soka, na najivunia kuwa mpalestina kutoka Gaza. Natamani kucheza soka nje ya Gaza na timu ya taifa ya Palestina, kwa sababu ni haki yangu."
    2 min
  • 17 OKTOBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia juhudi za vijana hasa katika kuboresha mifumo ya elimu katika matumizi ya teknolojia ambapo Gloria Anderson, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Shirika la TEDI anatufafanulia zaidi.Leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza umaskini duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema umaskini umesalia kuwa baa la dunia ukiathiri mamia ya mamilioni ya watu duniani kote.Huko MAshariki ya Kati, awamu ya pili ya utoaji wa chanjo dhidi ya polio imekamilika eneo la kati mwa Gaza, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema watoto 181,429 wamepatiwa. Wengine 148,064 wamepatiwa matone ya vitamini A. Ingawa hivyo vituo vinane vya afya vitasalia wazi ili kuendelea kutoa chanjo kwa familia zilishindwa kufikisha watoto wao katika siku tatu za chanjoMkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti amezuri Rwanda kujionea harakati za taifa hilo kukabili homa ya Marburg ambapo amepongeza serikali na wadau kwa ushirikiano kudhibiti mlipuko na kusema, tumeona idadi ya wagonjwa ikianza kupungua, halikadhalika idadi ya vifo baada ya wiki kadhaa za kazi ya kujituma.Katika kujifunza lugha ya kiswahili. matamshi sahihi ya lugha husaidia kufikisha ujumbe sahihi. Kinyume cha hivyo ujumbe utakuwa sivyo ndivyo na ndio maana hii leo, mbobezi wa lugha ya Kiswahili, Joramu Nkumbi kutoka Tanzania anafafanua tofauti ya maana ya maneno Ajali na Ajari, hasa pale yatakapotamkwa na mzungumzaji anayechanganya herufi ‘R’ na ‘L’Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    12 min
  • Asante WFP sasa najua kuandika na kusoma jina langu – Mkimbizi DRC
    Mbali na usaidizi mkubwa kwa watu waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro mashariki mwa DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linatoa msaada kupitia miradi iliyo ndani ya mfumo wa kuzuia na kupunguza hatari za unyanyasaji wa kijinsia unaohusishwa na uhakika wa kupata chakula.  Takriban wanawake 40 waliokimbia makazi yao wanaoishi katika kambi ya Bulengo jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC wamenufaika na mafunzo ya kusoma na kuandika tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2024. Walengwa waliojifunza kusoma na kuandika wanashuhudia kwamba yamebadilisha maisha yao. Mwandishi wetu wa habari mashariki mwa DRC, George Musubao alisafiri kutoka Beni hadi Goma katika kambi ya Bulengo kuzungumza na mmoja wao.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners