Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Mscan yawezesha wajawazito vijijini Uganda kupata huduma za uchunguzi
    Baada ya kuhitimu shahada ya udaktari nchini mwake Uganda, huko Afrika Mashariki, Daktari mmoja alibaini kuwa hiyo haitoshi, bali alienda mbali zaidi kubuni kifaa kinachosaidia wajawazito hasa wale wanaoishi maeneo ya ndani zaidi kufahamu hali ya afya ya watoto wao tumboni, na hivi sasa kifaa hicho kinaelekea kupata hakibunifu kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la Hakibunifu, WIPO. Assumpta Massoi anasimulia zaidi.
    3 min
  • 14 JANUARI 2026
    Hii leo jaridani tnaangazia uchumi wa dunia unaoendelea kukua ila maendeleo katika kupata kazi zenye ubora na staha yamekwama, pia tunaangazia afya ya uzazi nchini Uganda na homa ya bonde la ufa (RVF) kwa mifugo nchini Tanzania. Licha ya uchumi wa dunia kuendelea kukua, maendeleo katika kupata kazi zenye ubora na staha yamekwama, huku mamilioni ya wafanyakazi wakisalia katika lindi la umaskini na ajira zisizo rasmi. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani (ILO)iliyotolewa hii leo huko Geneva Uswisi.Baada ya kuhitimu shahada ya udaktari nchini mwake Uganda, huko Afrika Mashariki, Daktari mmoja alibaini kuwa hiyo haitoshi, bali alienda mbali zaidi kubuni kifaa kinachosaidia wajawazito hasa wale wanaoishi maeneo ya ndani zaidi kufahamu hali ya afya ya watoto wao tumboni, na hivi sasa kifaa hicho kinaelekea kupata hakibunifu kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la Hakibunifu, WIPO.Mfumo wa kubaini mapema homa ya bonde la ufa (RVF) iliyobuniwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini Tanzania imewezesha wizara, wakulima, na madaktari wa mifugo kuchukua hatua za mapema, hivyo kulinda maisha na mali dhidi ya ugonjwa huo unaoshambulia mifugo na binadamu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • 13 JANUARI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika mwaka mpya 2026 kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel ambao wanaendelea kukabiliwa na hali ngumu ya maisha katika kambi za wakimbizi na katika makazi ambayo ni magofu na vifusi vya nyumba zilizoharibiwa wakati wa vita baina ya Jeshi la Israel na Wanamgambo wa Hamas.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema licha ya sitisho la mapigano huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, maisha ya watoto bado yako katika hali tete, huku zaidi ya watoto 100 wakiwa wameuawa tangu Oktoba mwaka jana lilipoanza sitisho hilo.Vinywaji vyenye sukari na vileo vinazidi kuwa nafuu kwa bei kutokana na viwango vya kodi kwa muda mrefu kuwa vya chini katika nchi nyingi, jambo linalochochea unene kupita kiasi, ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya moyo, saratani na maradhi mengineyo hasa miongoni mwa watoto na vijana balehe, zimesema ripoti mpya mbili zilizotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hususan jimboni Ituri, mashariki mwa nchi hiyo ambako ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umepatia mafunzo ya ujasiriamali wafungwa kwenye gereza kuu lililoko Bunia, ambao ni mji mkuu wa jimbo hilo.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "MAHULUCHI"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    10 min
  • Mkuu wa UNHCR ahimiza mshikamano na suluhu zaidi kwa wakimbizi Kenya
    Katika ziara yake ya kwanza rasmi iliyofanyika nchini Kenya kama Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi, Barham Salih ametoa wito wa kuimarishwa kwa mshikamano wa kimataifa na uwekezaji endelevu ili kuwasaidia wakimbizi kujenga upya maisha yao, akionya kuwa upungufu mkubwa wa ufadhili unatishia kurudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana kwa juhudi kubwa katika ulinzi na kujitegemea kwa wakimbizi. Flora Nducha na taarifa zaidi  
    4 min
  • 12 JANUARI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia wito wa kuimarishwa kwa mshikamano wa kimataifa na uwekezaji endelevu kwa wakimbizi nchini Kenya, usugu wa Viuaji- Vyasumu au AMR na utekelezaji wa mradi wa kusambaza nishati ya umeme na vifaa vya nishati nchini Chad.Katika ziara yake ya kwanza rasmi iliyofanyika nchini Kenya kama Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi, Barham Salih ametoa wito wa kuimarishwa kwa mshikamano wa kimataifa na uwekezaji endelevu ili kuwasaidia wakimbizi kujenga upya maisha yao, akionya kuwa upungufu mkubwa wa ufadhili unatishia kurudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana kwa juhudi kubwa katika ulinzi na kujitegemea kwa wakimbizi.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani linaendelea na juhudi za kupambana na changamoto ya usugu wa Viuaji- Vyasumu au AMR na sasa imetoa miongozo na taratibu za kuhakikisha kuna matumizi sahihi ya dawa na wahudumu wa sekta ya afya katika nchi wanachama wanaendelea kuwapatia mafunzo ili kuzitumia kwa usahihi na kwa uwajibikaji.Nchini Chad, utekelezaji wa mradi wa kusambaza nishati ya umeme PAAET umefanikisha vifaa 145,000 vya nishati ya sola kusambazwa kwa gharama nafuu kwa kaya zilizoko majimbo 23 ya taifa hilo na sasa maisha yamekuwa bora.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • WHO na juhudi za kupambana na usugu wa Viuajijasumu
    Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani linaendelea na juhudi za kupambana na changamoto ya usugu wa Viuaji- Vyasumu au AMR na sasa imetoa miongozo na taratibu za kuhakikisha kuna matumizi sahihi ya dawa na wahudumu wa sekta ya afya katika nchi wanachama wanaendelea kuwapatia mafunzo ili kuzitumia kwa usahihi na kwa uwajibikaji. Tupate tarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners