Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Chata iliyoanzisha Umoja wa Mataifa miaka 80 iliyopita baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kukutanisha mataifa 50 San Francisco hapa Marekani na kupitisha Chata hiyo, ikilengaa kuzuia vita na kujenga uhusiano mwema baina ya mataifa. Operesheni ya kijeshi iliyofanywa na Marekani tarehe 3Januari nchini Venezuela ambayo ilimchukua Rais wa nchi hiyo Nicolàs Madura na hapo jana walimfikisha mahakamani jijini New York Marekani. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya haki za binadamu OHCHR kupitia msemaji wake Revina Shamdasani akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi amewaeleza kuwa kitendo hicho ni uvunjaji wa sheria za kimataifa na wala kisingizio cha haki za binadamu kisitumike.Tukisalia na Venezuela, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya Kiutu OCHA imeeleza inaendelea kuwasaidia wenye uhitaji nchini humo na mwaka jana ili ainisha zaidi ya wahitaji milioni 8. Msemaji wa OCHA Jens Laerke amewaambia waandishi wa habari jijini Geneva kuwa “Kati ya hao watu milioni nane, "900,000 wamewekwa katika makundi ya juu sana ya wenye uhitaji wa sekta mbalimbali ... kama vile chakula, lishe, elimu, na huduma za afya, kimsingi mambo yote ambayo nchi ya Venezuela halijaweza kutoa kwa raia wake kwa miaka mingi”.Msemaji wa Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anafuatilia akiwa na wasiwasi mkubwa maandamano yanayoendelea nchini Iran. Guterres amesikitishwa na ripoti za vifo na majeruhi kutokana na mapigano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji, akitaka mamlaka zizingatie haki ya kuandamanana na kukusanyika kwa amani.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!