Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Licha ya changamoto mwaka 2025 umekuwa na mafanikio pia:WHO
    Mwaka 2025 umeelezwa kuwa mwaka wa kihistoria kwa sekta ya afya duniani. Hayo ni kwa mujibu wa ujumbe uliotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO,Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, wakati akitoa tathmini yake ya mwisho ya mwaka 2025. Taarifa zaidi na Sabrina Saidi. Karibu Sabrina..(TAARIFA YA SABRINA SAIDI) Asante Flora,Akizungumza kutokea makao makuu ya WHO mjini Geneva, Uswisi, Dkt. Tedros amesema mwaka 2025 umekuwa na mafanikio makubwa pamoja na changamoto nzito kwa afya ya dunia, huku akisisitiza kwamba dunia bado inahitaji uwepo wa WHO. (Clip 1-Sauti ya Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus)“Kweli mwaka 2025 umekuwa mwaka wa mafanikio makubwa na changamoto nyingi kwa afya ya dunia na kwa WHO. Mafanikio makubwa zaidi yalikuwa kupitishwa kwa Mkataba wa WHO wa kukabiliana na milipuko ya magonjwa, ambao ni mfano wa nguvu ya ushirikiano wa kimataifa pale nchi zinapochagua kushirikiana badala ya kugawanyika. Pia, mwaka huu WHO imethibitisha nchi 13 kufanikiwa kutokomeza magonjwa, ikatoa miongozo kuhusu tiba mpya kama Lenacapavir kwa kinga dhidi ya VVU na matibabu ya GLP-1 kwa utipwatipwa,na ikachukua hatua dhidi ya majanga 48 katika nchi na maeneo 79, ikiwemo Gaza, Sudan na Ukraine.”Akizungumzia changamoto, Dkt. Tedros amesema kupunguzwa kwa misaada ya kimataifa na bajeti kumeathiri sekta ya afya duniani, lakini ameeleza kuwa hali hiyo pia inaleta fursa mpya.(Clip 2- Sauti ya Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus)“Lakini ndani ya changamoto hizi pia kuna fursa. Ni fursa kwa nchi kuondokana na utegemezi wa misaada na kujenga mifumo ya afya inayojitegemea, na ni fursa kwa WHO kuwa taasisi imara zaidi na inayojipanga kwa siku zijazo. Dunia bado inahitaji WHO, na WHO itaendelea kushikilia maono yake ya msingi kuhakikisha kiwango cha juu kabisa cha afya kinapatikana kwa wote, si kama upendeleo wa wachache, bali kama haki ya kila mtu.”Dkt. Tedros amehitimisha ujumbe wake kwa kusema kuwa WHO itaendelea kushirikiana na nchi wanachama ili kukabiliana na changamoto za sasa na zijazo za afya duniani.
    3 min
  • UNICEF na washirika wasaidia kuboresha huduma za afya Laascaanood Somalia
    Huko kaskazini mashariki mwa Somalia, eneo la Laascaanood linaendelea kushuhudia maboresho ya huduma muhimu za afya baada ya miaka miwili ya kuvurugika kwa huduma hizo kutokana na mizozo, maboresho haya yanaleta huduma za afya karibu zaidi na akina mama na watoto shukran kwa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF na washirika wake. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.(Taarifa ya Leah)Kwa mujibu wa UNICEF nchini Somalia, mamilioni ya watoto wanakua katika kivuli au mazingira ya ukimya na dharura zilizosahaulika, takribani watoto milioni 1.8 wanahitaji matibabu ya utapiamlo mwaka huu wa 2025. Kila mwaka watoto wapatao 75,000 walio chini ya umri wa miaka mitano hufariki dunia kutokana na magonjwa yanayozuilika na yanayoweza kutibiwa.Miaka miwili ya migogoro imesababisha kusambaratika kwa huduma muhimu huko Laascaanood. Kurejea kwa hali ya utulivu kumeanza kushuhudia urejeshwaji wa taratibu wa huduma hizi muhimu zinazookoa maisha. UNICEF, kwa msaada wa KSRelief na Saudi Esports Federation, inachangia kwenye kutoa huduma jumuishi za afya ya msingi, huku huduma hizo zote zikitolewa chini ya paa moja.Mpaka sasa maelfu ya watu wamefikiwa huku ukisaidia vituo 13 vya afya kama anavyoeleza Dayid Said Ismail Afisa Lishe (Sauti ya Dayid Said Ismail – Evarist)“Mradi huu unasaidia vituo 13 vya afya na unahudumia zaidi ya watu 150,000. Huduma zake zinajumuisha chanjo za watoto, matibabu ya magonjwa kama nimonia na kuhara, pamoja na huduma za magonjwa mengine ya kawaida ya utotoni.”Katika huduma za matibabu tumsikilize Saida Ali Elmi ambaye ni mhudumu wa Afya(Sauti ya Saida Ali Elmi- Sheilah)“Kama mnavyoona, akina mama wengi wamekuwa kwenye foleni tangu saa moja asubuhi na sasa ni saa 5:30 asubuhi. Kwa hiyo wapo hapa kwa ajili ya chanjo za kinga, ikiwemo chanjo za kifua kikuu, surua, polio, pepopunda, kifaduro, pamoja na chanjo mpya iitwayo PCV ya nimonia.”Juhudi hizi zinazofanywa na mashirika haya, tayari zimeanza kuleta matumaini mapya kwa Ayan Hassan Abdi mama mzazi wa Maryam “Nimemleta Maryam kwa sababu alikuwa na homa. Amepatiwa matibabu na pia chanjo. Alifanyiwa vipimo vya homa na kuharisha, na akatibiwa vizuri, Masha’Allah.”
    3 min
  • Guterres: Mwaka mpya 2026 tudumishe mshikamano na amani badala ya mateso
    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa ujumbe mzito wa Mwaka Mpya kwa ulimwengu akisema ulimwengu uko katika njia panda, ukikabiliwa na machafuko, sintofahamu na migawanyiko mikubwa na hivyo kutoa wito kwa wanadamu kuinuka pamoja kwa ajili ya haki, ubinadamu na amani. Karibu Anold Kayanda kwa maelezo zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Katika ujumbe wake wa video uliosambazwa leo asubuhi saa za New York, Marekani, kwa ajili ya mwaka mpya wa 2026, Katibu Mkuu wa Umoja wa Maraifa anauanza ujumbe wake kwa kusema, “tunapoingia mwaka mpya, dunia iko njia panda.”  Amesema dunia inakumbwa na vurugu zinazoendelea, athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi pamoja na ukiukwaji wa kimfumo wa sheria za kimataifa  hali ambayo, kwa mujibu wake, inatishia misingi inayounganisha binadamu kama familia moja ya dunia.Guterres amesema watu kote ulimwenguni wanaendelea kujiuliza iwapo viongozi wao wanasikiliza kilio cha wananchi na kama wako tayari kuchukua hatua za dhati kukabiliana na changamoto hizi.Akigeukia takwimu, Katibu Mkuu ameeleza kuwa matumizi ya kijeshi duniani yamefikia dola trilioni 2.7, ongezeko la karibu asilimia kumi kiwango ambacho ni mara kumi na tatu zaidi ya misaada yote ya maendeleo, na kinacholingana na Pato la Bidhaa za ndani la Bara zima la Afrika.Amesema ongezeko hilo linatokea wakati dunia ikishuhudia mizozo mikubwa kwa viwango ambavyo havijawahi kuonekana tangu Vita Vikuu Vya Pili Vya Dunia.Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu ametoa wito kwa dunia kutumia mwanzo wa mwaka mpya kuweka vipaumbele sahihi, akisisitiza kuwa ulimwengu salama hujengwa kwa kuwekeza zaidi katika kupambana na umaskini badala ya kuwekeza katika vita.Guterres amesisitiza kuwa dunia ina rasilimali za kutosha kuinua maisha ya watu, kuponya sayari na kujenga mustakabali wa amani na haki, endapo tu zitatumika ipasavyo.Kwa mwaka 2026, amewataka viongozi wa dunia kuwa makini zaidi na kufanya uamuzi unaoweka mbele maslahi ya watu na mazingira badala ya kuendeleza mateso.Aidha, amewahimiza raia wote duniani kushiriki kikamilifu katika kujenga dunia bora, akisema mustakabali wa ubinadamu unategemea ujasiri wa pamoja wa kuchukua hatua.Katika kuhitimisha ujumbe wake, Katibu Mkuu ametoa wito wa mshikamano kwa ajili ya haki, ubinadamu na amani duniani.
    3 min
  • 29 DESEMBA 2025
    Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Katika ujumbe wake wa mwaka mpya 2026 Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres ameitaka dunia kushikamana kwa ajili ya amani, maendeleo, na usalama badala ya kuongeza mateso-Huko Somalia kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wakaazi wa Laascanood waboreshewa huduma za afya baada ya kuvurugika kwa miaka miwili-Na Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO amesema mwaka 2025 ulighubikwa na changamoto lukuki za afya ya umma duniani ikiwemo ukata wa ufadhili, lakini kuna matumaini hasa katika suala la utipwatipwa
    10 min
  • 24 DESEMBA 2025
    WHO: Pombe yasababisha kifo cha mtu 1 kati ya 3 kutokana na majeraha barani Ulaya.Gaza: Uhaba wa vifaa tiba unawatesa wagonjwa.UNICEF na wadau wafanikisha kampeni ya chanjo ya Mpox katika kaunti ya Mombasa - Kenya. 
    12 min
  • USIAHI, UKENJA AU UNYENDE
    Hii leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "USIAHI, UKENJA AU UNYENDE"
    1 min
  • 23 DESEMBA 2025
    Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa ambapo hii leo mada kwa kina inaangazia juhudi za kuwa na nishati safi nchini Tanzania ambapo vijana watazungumzia mradi wao wa kuchakata taka za plastiki na kupata nishati safi ya kupikia. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari ukiangazia wakimbizi wa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC, Masuala ya Haki za Binadamu nchini Burundi na Matumaini ya watoto wa Gaza. Mwenyeji wako ni Leah Mushi. 
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners