Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Tiba asilia zina nafasi muhimu katika kuimarisha mifumo ya afya duniani - WHO
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linasema tiba asilia na tiba jadidifu zina nafasi muhimu katika mifumo ya afya duniani, hasa katika kinga, huduma za usaidizi wa magonjwa na kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa jamii. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Tiba Asilia, Jadidifu na Jumuishi cha WHO, Dkt. Sung Chol Kim, katika mahojiano maalum kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Tiba Asilia unaoendelea huko New Delhi, India. Sabrina Saidi na taarifa zaidi..
    3 min
  • 19 DESEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi wa Barham Ahmed Salih wa kuwa Kamishna Mkuu ajaye wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Tiba asili, na haki za binadamu nchini Sudan. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amekaribisha hatua ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ya hapo jana kumchagua Rais Mstaafu wa Iraq, Barham Ahmed Salih wa kuwa Kamishna Mkuu ajaye wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, kwa muhula wa miaka mitano ijayo.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linasema tiba asilia na tiba jadidifu zina nafasi muhimu katika mifumo ya afya duniani, hasa katika kinga, huduma za usaidizi wa magonjwa na kuongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa jamii. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Tiba Asilia, Jadidifu na Jumuishi cha WHO, Dkt. Sung Chol Kim, katika mahojiano maalum kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Tiba Asilia unaoendelea huko New Delhi, IndiaUmoja wa Mataifa unaendelea kuonesha wasiwasi mkubwa kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo la Darfur, Sudan, ukionya kuwa mashambulizi yanayolenga makundi maalum ya watu yanaweza kuashiria hatari kubwa zaidi ya mauaji ya kimbari.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    10 min
  • 18 DESEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ya vijana wanaotafuta fursa za mafunzo kwa vitendo. Umoja wa Mataifa ni moja ya mashirika ya kimataifa yanayotoa fursa hii kwa vijana kutoka duniani kote kuja hapa Makao Makuu jijini New York Marekani au hata katika nchi husika.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo imefichua mauaji ya kutisha, ubakaji na matumizi ya njaa kama silaha ya vita katika kambi ya Zamzam, Darfur, Sudan. Kwa mujibu wa ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR, raia wasiopungua 1,013 waliuawa katika mashambulizi ya siku tatu ya wanamgambo wa RSF mwezi Aprili, huku zaidi ya watu 400,000 wakilazimika kukimbia makazi yao.Leo, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemulika mchango mkubwa wa mamilioni ya wahamiaji duniani, wakati uhamiaji ukiendelea kuwa mgumu zaidi kutokana na migogoro, majanga yanayohusiana na tabianchi na shinikizo za kiuchumi. Ameeleza kuwepo kwa viwango vya juu zaidi vya watu waliolazimika kuhama makazi yao na idadi kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa ya vifo vya wahamiaji wakiwa safarini, huku akisisitiza kuwa uhamiaji salama na unaosimamiwa vyema unaweza kuchochea ukuaji wa uchumi, ubunifu na maendeleo katika nchi za asili na zinazopokea wahamiaji. Guterres amesema, “Uhamiaji unapokuwa salama na unasimamiwa vyema, si janga la kuogopa, bali ni nguvu kubwa ya kuleta mema.”.Na Ama K. Babebrese Balozi mwema wa kitaifa wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM mwenye asili ya Ghana ambaye sasa ni muhamiaji nchini Uingereza, katika siku hii ya uhamiaji ametoa ujumbe maalum akisema "Napenda kumtia moyo kila mtu kwamba tunaweza kuwa tofauti, hadithi zetu za uhamiaji ni tofauti tumetoka kwenye mazingira tofauti lakini kitu cha muhimu ni kwamba kama jamii sisi ni kitu kimoja. Uhamiaji ndio hadithi yangu”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • Wakimbizi kutoka DR Congo wanazidi kumiminika nchini Burundi
    Kuongezeka kwa machafuko katika jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kumesababisha watu wengi kuyahama makazi yao ndani na kumbilia kusaka hifadhi nchi Jirani ya Burundi. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi limeeleza mpaka sasa karibu wakimbizi 64,000 tayari wamewasili Burundi, na idadi ikitarajiwa kuongezeka. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi
    3 min
  • 17 DESEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia tiba asili, machafuko katika jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na ubakaji unaotumika kama silaha ya vita nchini humo humo.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaweka mkazo mpya wa kisayansi katika tiba asili au mitishamba, wakati mawaziri, wanasayansi na viongozi wa jamii za asili kutoka zaidi ya nchi 100 wakikutana mjini New Delhi India kuanzia leo kuangazia mchango wa tiba za asili.Kuongezeka kwa machafuko katika jimbo la Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kumesababisha watu wengi kuyahama makazi yao ndani na kumbilia kusaka hofadhi nchi Jirani ya Burundi. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi limeeleza mpaka sasa karibu wakimbizi 64,000 tayari wamewasili Burundi, na idadi ikitarajiwa kuongezeka.Ubakaji unaotumika kama silaha ya vita huacha majeraha yasiyofutika ya mwili,  akili na ya roho. Katika ushuhuda huu wenye nguvu, manusura mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa anaishi kama mkimbizi nchini Burundi, anasimulia safari yake ya maumivu baada ya kunusurika ukatili wa kingono uliomsababishia majeraha makubwa ya mwili, ikiwemo fistula, pamoja na makovu ya kina ya kihisia.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    12 min
  • Ubakaji kama silaha ya vita - Safari ya manusura wa DRC katika kupata uponyaji na heshima
    Ubakaji unaotumika kama silaha ya vita huacha majeraha yasiyofutika ya mwili,  akili na ya roho. Katika ushuhuda huu wenye nguvu, manusura mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa anaishi kama mkimbizi nchini Burundi, anasimulia safari yake ya maumivu baada ya kunusurika ukatili wa kingono uliomsababishia majeraha makubwa ya mwili, ikiwemo fistula, pamoja na makovu ya kina ya kihisia.Sheilah  Jepng’etich na taarifa zaidi
    4 min
  • Kutetea mazingira ni ndoto yangu kubwa - Frida Amani
    Frida Amani, msanii wa muziki wa kizazi kipya wa kwa hip hop au muziki wa kufokafoka almaarufu kama rap kutoka nchini Tanzania, ambaye pia ni mtangazaji na mwanamazingira, amepata heshima kubwa ya kuwa Balozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa wa Mazingira UNEP, akiwa na jukumu la kuhamasisha kurejesha ikolojia duniani. Akizungumza katika mahojiano maalum na UN News Kiswahili kandoni mwa mkutano wa 7 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA7 uliokunja jamvi mwishoni mwa wiki, Frida amesema “Ni nafasi kubwa sana ambayo nimeipata. Sio kwangu tu, ni kwa ajili ya vijana wenzangu”. Tuungane na Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa Stella Vuzo na mchechemuzi huyu katika makala hii.
    9 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners