Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 11 DESEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Sudan Kusini kufuatilia mradi wa kilimo cha mpunga ulivyoleta ustawi kwa jamii ya katikati mwa Sudan unaofanikishwa kwa msaada wa mafunzo wa walinda amani wa UN kutoka Korea Kusini wanaohudumu katika UNMISS kupitia wanasayansi na wakulima wa eneo la Bor katika. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa methali.Mapigano makali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamesababisha vifo vya zaidi ya raia 70, kuwafurusha watu zaidi ya 200,000, na kusitisha msaada wa chakula kwa maelfu. Umoja wa Mataifa unasema hali katika Kivu Kusini imezorota kwa kasi, huku msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP ukisimama na shule zaidi ya 30 zikigeuzwa makazi ya dharura. Katika taarifa yake, Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq, amesema hali imefikia kiwango cha hatari, akionya: “Familia zinazoishi kwa njaa sasa zinagawana chakula chao cha mwisho na watu waliokimbia makazi. Hii ni dharura inayovuka mipaka.” UN inazitaka pande zote kusitisha mapigano mara moja na kuruhusu misaada kufika kwa walio hatarini.Mkutano wa kikao cha 7 wa Baraza La Mazingira la Umoja wa Mataifa UNE-7 unaeelekea ukingoni jijini Nairobi Kenya na miongoni mwa washiriki ni kijana mwanaharakati wa mazingira kutoka asasi ya Umoja wa Mataifa YUNA nchini Tanzania Ally MwamzoraNa leo Umoja wa Mataifa unaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Milima, ukisisitiza umuhimu wa milima kama “kitovu cha maji ya dunia.”  Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, takriban asilimia 70 ya maji safi ya Dunia yamehifadhiwa kama theluji au barafu, yakitoa mito inayosambaza maji ya kunywa, kilimo, viwanda, na umeme wa maji na takriban watu bilioni mbili, ikiwa ni pamoja na jamii nyingi za asili, wanategemea maji ya milima kwa mahitaji yao ya kila siku, maisha, na tamaduni zao. Wataalamu wanasisitiza kuwa kulinda mazingira ya milima ni muhimu ili kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa vizazi vijavyo.Katika kujifunza lugha Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya,  kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "“MWENDAWAZIMU HAPEWI UPANGA"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    12 min
  • Simulizi ya Malaika Oringo, manusura wa usafirishaji haramu wa binadamu
    Kwa manusura wengi wa usafirishaji haramu wa binadamu, msaada hukatika mapema mno. Kutokana na rasilimali chache na mifumo isiyotoa huduma za muda mrefu, wengi hutolewa kwenye mfumo bila kupata usaidizi wa kutosha wa kisaikolojia au utambuzi unaozidi simulizi zao. Malaika Oringo, mama, mwanaharakati, na manusura wa usafirishaji  haramu wa binadamu ameamua kubadilisha hali hiyo. Kama mwanzilishi wa shirika la Footprint to Freedom, linaloongozwa na manusura na linalolenga kuwawezesha na kuwarejesha katika jamii waathiriwa wa usafirishaji haramu wa binadamu, anatetea kuhakikisha sauti za manusura zinakuwa kiini cha utungaji wa sera na hatua za serikali duniani. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
    3 min
  • Vikosi vya UN vya ulinzi wa amani DRC vyakabidhiana majukumu
    Kikosi cha 4 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania kinachohudumu chini ya mwamvuli wa FIB MONUSCO, kimehitimisha rasmi jukumu lake la ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo DRC kwa gwaride maalumu la makabidhiano lililofanywa na Tanzqrf ya 4 pamoja na Tanzqrf ya 5 katika makao makuu ya kikosi hico mjini Beni Mavivi katika jimbo la kivu kaskazini. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Habibu Shaban
    4 min
  • 10 DESEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangaziz siku ya Haki za Binadamu tukikuletea ujumbe wa Volker Türk, Safari ya manusura wa usafirishaji haramu wa binadamu, na vikosi vya 4 na 5 vya ulinzi wa amani kutoka Tanzania nchini DRC.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ametumia Siku ya Haki za Binadamu hii leo kutoa onyo kali akisema ulinzi wa haki za binadamu uko mashakani wakati migogoro na ukandamizaji vinaongezeka kwa kasi isiyo na mfano.Kwa manusura wengi wa usafirishaji haramu wa binadamu, msaada hukatika mapema mno. Kutokana na rasilimali chache na mifumo isiyotoa huduma za muda mrefu, wengi hutolewa kwenye mfumo bila kupata usaidizi wa kutosha wa kisaikolojia au utambuzi unaozidi simulizi zao. Malaika Oringo, mama, mwanaharakati, na manusura wa usafirishaji  haramu wa binadamu ameamua kubadilisha hali hiyo. Kama mwanzilishi wa shirika la Footprint to Freedom, linaloongozwa na manusura na linalolenga kuwawezesha na kuwarejesha katika jamii waathiriwa wa usafirishaji haramu wa binadamu, anatetea kuhakikisha sauti za manusura zinakuwa kiini cha utungaji wa sera na hatua za serikali duniani.Kikosi cha 4 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania kinachohudumu chini ya mwamvuli wa FIB MONUSCO, kimehitimisha rasmi jukumu lake la ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo DRC kwa gwaride maalumu la makabidhiano lililofanywa na Tanzqrf ya 4 pamoja na Tanzqrf ya 5 katika makao makuu ya kikosi hico mjini Beni Mavivi katika jimbo la kivu kaskazini.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    13 min
  • 09 DESEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea ufafanuzi wa umuhimu wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Haki za binadamu kutoka kwa Seifu Magango Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa ambaye anaanza kwa kuzungumzia azimio la tamko hilo la haki za binadamu.Utafiti uliofanywa na Tume ya Ulaya kwakushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa linalaoshughulikia masuala ya wanawake UN Women umebaini kuwa wanawake saba kati ya kumi wakiwemo watetezi wa haki za binadamu, wanaharakati na waandishi wa habari wanakumbana na ukatili mtandaoni.Meneja Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya watoto UNICEF Tess Ingram yupo ziarani Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya kati ambapo hii leo amezungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi na kuwaeleza aliyoshuhudia huko ikiwemo wajawazito walio na utapiamlo kujifungua watoto wenye uzito mdogo au kuzaliwa kabla ya wakati, ambao wengine wanakufa katika vyumba vya wagonjwa mahututi      au wengine hupona lakini watoto hao hukabiliwa na utapimlo au matatizo mengine ya kiafya.Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kutokomeza Ubaguzi wa Rangi CERD, leo imetoa onyo kali kwa Sudan, ikieleza wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la matumizi ya lugha ya kudhalilisha, kauli za chuki na ukiukaji Mkubwa wa haki za binadamu unaochochewa na misingi ya kikabila. Kamati imesem Mashambulizi haswa dhidi ya jamii za Fur, Masalit na Zaghawa, yanadaiwa kufanywa na Kikosi cha Msaada wa Haraka RSF na makundi washirika katika maeneo ya El Fasher, Darfur Kaskazini.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "PEKUPEKU"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • 08 DESEMBA 2025
    Leo katika Jarida la UNMlipuko wa kipindupindu wa mwaka huu nchini DRC ni mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 25.Wananchi wanaojitolea wanavyosaidia wananchi wenzao nchini Sudan.Janga la kibinadamu Sudan haliwezi tena kupuuzwa, wakati ni sasa kulishughulikia.
    10 min
  • UN: Mchango wa watu wanaojitolea ni muhimili wa mabadiliko
    Katika dunia inayohitaji mshikamano ili kufikia maendeleo, mchango wa watu wanaojitolea umeendelea kuwa nguvu muhimu ya kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Kila mwaka tarehe 5 mwezi Desemba, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanaojitolea, mwaka huu ikiwa imebeba maudhui“Kila Mchango Una Umuhimu.”  Maadhimisho ya mwaka huu pia yanazindua rasmi Mwaka wa Kimataifa wa Wanaojitolea kwa Maendeleo Endelevu 2026. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania Sabrina Saidi amezungumza na kijana  ambaye anajitolea katika Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa Tanzania YUNA Je kasema nini?.
    4 min
  • Kutoka changamoto hadi mafanikio: Safari ya Kibra kupitia mfuko wa CERF
    Katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia, jitihada za kuimarisha makuzi na elimu kwa watoto wenye ulemavu zinaendelea kuleta matumaini mapya, kupitia programu inayoungwa mkono na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA,  na Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Mataifa, CERF. Je nini kinafanyika? Sheilah Jepngetich na taarifa zaidi
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners