Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UN: Dunia ipo katika kipindi cha maamuzi kuhusu mustakbali wa ukimwi
    Kama tulivyokujuza le oni Siku ya UKIMWI Duniani na mwaka huu inaadhimishwa kwa onyo kali kuhusu janga hilo pamoja na wito wa kuchukua hatua. Ikibeba kaulimbiu “Kukabili misukosuko, kubadili mwelekeo wa hatua za UKIMWI,” Umoja wa Mataifa unasema dunia ipo katika kipindi cha uamuzi muhimu katika vita dhidi ya VVU. Flora Nducha na taarifa zaidi
    3 min
  • “VVU si mwisho wa maisha” – Safari ya Pooja Mishra kutoka mshtuko hadi uongozi
    Pooja aliolewa akiwa na umri wa miaka 15, baadaye akiwa mdogo bado akagundua kuwa ana Virusi Vya Ukimwi, VVU, na leo ni Mratibu wa Kitaifa wa Vijana chini ya Muungano wa Kitaifa wa Watu wanaoishi na VVU nchini India (NCPI+), akifanya kazi moja kwa moja na zaidi ya vijana 1,800 kote India. Katika mahojiano yaliyofanywa na Anshu Sharma wa Idhaa ya Kihindi ya Umoja wa Mataifa, Pooja anasimulia safari yake, nafasi ya jamii na familia, na ujumbe wake kwa watu wanaoishi na VVU. Anaposema ART anazungumzia dawa za kufubaza virusi, sawa na ARV lakini katika mkusanyiko wa dawa nyingi kwa pamoja.
    4 min
  • 01 DESEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Siku ya UKIMWI Duniani, simulizi wa mwathirika wa ugonjwa huu amabye aliolewa na umri wa miaka 15, na juhudi za UNICEF Wajir nchini Kenya za kuhakikisha ujumuishwaji wa watoto wenye ulemavu darasani.Leo ni Siku ya UKIMWI Duniani na mwaka huu inaadhimishwa kwa onyo kali kuhusu janga hilo pamoja na wito wa kuchukua hatua. Ikibeba kaulimbiu “Kukabili misukosuko, kubadili mwelekeo wa hatua za UKIMWI,” Umoja wa Mataifa unasema dunia ipo katika kipindi cha uamuzi muhimu katika vita dhidi ya VVU.Pooja aliolewa akiwa na umri wa miaka 15, baadaye akiwa mdogo bado akagundua kuwa ana Virusi Vya Ukimwi, VVU, na leo ni Mratibu wa Kitaifa wa Vijana chini ya Muungano wa Kitaifa wa Watu wanaoishi na VVU nchini India (NCPI+), akifanya kazi moja kwa moja na zaidi ya vijana 1,800 kote India. Katika mahojiano yaliyofanywa na Anshu Sharma wa Idhaa ya Kihindi ya Umoja wa Mataifa, Pooja anasimulia safari yake, nafasi ya jamii na familia, na ujumbe wake kwa watu wanaoishi na VVU. Anaposema ART anazungumzia dawa za kufubaza virusi, sawa na ARV lakini katika mkusanyiko wa dawa nyingi kwa pamoja.Katika Kaunti ya Wajir Kaskazini Mashariki mwa Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Maalum ya Kenya KISE wameanzisha mpango maalum wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu kupata tathmini za kitabibu na kielimu. Mpango huu umeleta matumaini mapya kwa familia nyingi ambazo hapo awali zilikuwa na ugumu wa kupata huduma hizo.Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!
    12 min
  • UNICEF na KISE wawapiga jeki watoto wenye ulemavu katika Kaunti ya Wajir nchini Kenya
    Katika Kaunti ya Wajir Kaskazini Mashariki mwa Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Maalum ya Kenya KISE wameanzisha mpango maalum wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu kupata tathmini za kitabibu na kielimu. Mpango huu umeleta matumaini mapya kwa familia nyingi ambazo hapo awali zilikuwa na ugumu wa kupata huduma hizi kama anavyofafanua Sheilah Jepngetich  katika taarifa hii
    4 min
  • Programu ya Ujana Salama yawezesha vijana Tanzania - UNICEF
    Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF)  kupitia programu yake ya stadi za maisha na mafunzo ya biashara iitwayo Ujana Salama , inayofadhiliwa na mfuko wa maendeleo ya jamii nchini humo TASAF kwa msaada wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imewezesha kikundi cha vijana nchini humo kujitegemea. Mmoja wa vijana wanufaika wa programu hiyo ameweza kujenga mustakabali ambao awali aliouna kama ndoto kupitia masomo ya ushoni. Sheilah Jengetich na taarifa zaidi.
    4 min
  • 28 NOVEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya amani na usalama nchini Guinea-Bissau, utapiamlo nchini Sudan na juhudi za UNICEF za kuwawezesha vijana ili waweze kujikwamua kimaisha nchini Tanzania.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amelaani vikali mapinduzi yanayoendelea nchini Guinea-Bissau akitaka “urejeshwaji wa haraka na usio na masharti wa utawala wa kikatiba” baada ya wanajeshi kutwaa madaraka kufuatia uchaguzi mkuu wa uliofanyika tarehe 23 Novemba.Zaidi ya miaka miwili na nusu ya vita nchini Sudan imewaacha watu milioni 21 karibu nusu ya watu wote wa nchi hiyo wakikabili njaa kali, huku maeneo mawili yakithibitishwa kukumbwa na baa la njaa. Mapigano yamepungua kwa sasa katika baadhi ya sehemu za Khartoum, na masoko yanaanza kufunguliwa tena., Lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP linaonya kuwa hali bado ni tete.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF)  kupitia programu yake ya stadi za maisha na mafunzo ya biashara iitwayo Ujana Salama, inayofadhiliwa na mfuko wa maendeleo ya jamii nchini humo TASAF kwa msaada wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imewezesha kikundi cha vijana nchini humo kujitegemea. Mmoja wa vijana wanufaika wa programu hiyo ameweza kujenga mustakabali ambao awali aliouna kama ndoto kupitia masomo ya ushoniMwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • WFP yaonya jinamizi la vita na njaa nchini Sudan ni mtihani usio na majibu
    Zaidi ya miaka miwili na nusu ya vita nchini Sudan imewaacha watu milioni 21 karibu nusu ya watu wote wa nchi hiyo wakikabili njaa kali, huku maeneo mawili yakithibitishwa kukumbwa na baa la njaa. Mapigano yamepungua kwa sasa katika baadhi ya sehemu za Khartoum, na masoko yanaanza kufunguliwa tena., Lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP linaonya kuwa hali bado ni tete. Flora Nducha na taarifa zaidi
    4 min
  • WFP: Suluhisho bunifu kwa wafugaji wa maeneo yenye ukame nchini Kenya zaleta tija
    Katika maeneo yaliyoghubikwa na athari za mabadiliko ya tabianchi kaskazini mwa Kenya, wafugaji wamekuwa wakikumbwa na changamoto kubwa kwani ukame na mafuriko, vinatishia sio tu mali zao bali pia maisha yao. Lakini kupitia mradi wa bima ya mifugo unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula  duniani WFP, kwa ushirikiano na asasi ya Zoetis na kampuni ya ZEP-RE, jamii zinaanza kupata ahuweni na matumaini mapya. Sheilah Jepngetich na taarifa zaidi.
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners