Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 21 NOVEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, mbinu bunifu za kilimo cha kakao nchini Peru, na mradi wa miundombinu wa kupunguza athari ya mafuriko na kugeuza maji ziada kuwa rasilimali muhimu kwa jamii nchini Rwanda.Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ujulikanao kama MONUSCO, leo umelaani vikali mashambulizi makubwa yaliyofanywa na kundi lenye silaha la Allied Democratic Forces ADF kati ya tarehe 13 na 19 Novemba 2025 katika baadhi ya maeneo ya Lubero, jimboni Kivu Kaskazini na kukatili maisha ya raia wengi.Katika msitu wa Amazon upande wa nchi ya Peru, jamii za watu wa asilizimeonesha namna mbinu bunifu za kilimo zinaweza kuongeza uzalishaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Yote haya yanakuja wakati dunia ikiendelea kujadili mustakabali wa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika mkutano wa Umoja wa Mataifa COP30 unaoendelea huko Belém, Brazil.Mwezi Mei 2023, Rwanda nchi iliyozungukwa na milima ilikumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha maporomoko ya ardhi na kusababisha maji kutoka katika milima ya volkano, yakiambatana na mawe mazito kuharibu mashamba, makazi na barabara. Baada ya mafuriko hayo ili kupunguza athari za majanga kama hayo, kwa wakati mwingine Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Rwanda, kwa ufadhili wa Serikali ya Japan, linatekeleza mradi wa Kukabiliana na Majanga Yanayohusiana na Maji katika wilaya za Rutsiro na Burera. Lengo ni kupunguza Athari na kugeuza maji ziada kuwa rasilimali muhimu kwa jamii.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    13 min
  • MONUSCO imelaani vikali mashambulizi ya ADF Lubero nchini DRC yalioua raia 89
    Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ujulikanao kama MONUSCO, leo umelaani vikali mashambulizi makubwa yaliyofanywa na kundi lenye silaha la Allied Democratic Forces ADF kati ya tarehe 13 na 19 Novemba 2025 katika baadhi ya maeneo ya Lubero, jimboni Kivu Kaskazini na kukatili maisha ya raia wengi. Flora Nducha na maelezo zaidi
    3 min
  • 20 NOVEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika Kaunti ya Kajiado iliyoko Kusini na Kusini magharibi mwa jiji la Nairobi nchini Kenya kumulika upatikanaji wa huduma za choo na hasa choo safi na salama ambazo bado ni kizungumkuti kote dunianini.Katibu Mkuu wa Umoja wa, António Guterres,akizungumza na waandishi wa habari hii leo ametoa onyo kali COP30 huko Belém, Brazil, akisisitiza dharura ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Amesema “Jamii zilizo mstari wa mbele zinaangalia zikiesabu nyumba zao zilizozamishwa na mafuriko mavuno yaliyoshindikana, vyanzo vya maisha vilivyopotea na kuuliza kwa kiasi gani zaidi wateseke . Wamesikia visingizio vya kutosha, sasa wanatakahatua”.Leo ni Siku ya mtoto Duniani, mwaka huu ikibeba kaulimbiu “Sikilizeni watoto, simameni kwa ajili ya haki za kila mtoto, kila siku.” Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo ya Hali ya Watoto Duniani 2025 sanjari na maadhimisho haya  inaonya kwamba zaidi ya watoto milioni 417, sawa na mtoto 1 kati ya 5 katika nchi za kipato cha chini na cha kati, wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa mahitaji muhimu angalau katika maeneo mawili ya msingi ya maisha.Mkutano wa wanaharakati vijana wavumbuzi kutoka kila pembe ya dunia umeaanza leo mjini Geneva Uswisi ukibeba mafda kuu “Kutoka Hashtag hadi Hatua”, ukisherehekea vijana wanaobadilisha maisha ya jamii zao kupitia zana za kidijitali na majukwaa ya mtandaoni. Mwaka huu, washindi wa uvumbuzi huo wanatoka nchi mbalimbali, ikiwemo Côte d’Ivoire, India, Lebanon, Japan, na Brazil, wakitambuliwa kwa kazi zao zenye athari kubwa chanya. Waandaaji wa Jukwaa hilo amba oni Umoja wa Mataifa wanasema tukio hili lina lengo la kuhamasisha vijana wengi zaidi kubadilisha ushiriki wao wa mtandaoni kuwa hatua halisi zinazoboresha jamii, kuthibitisha kuwa uanaharakati wa kidijitali unaweza kuleta mabadiliko ya kweli.Na katka kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana za maneno "MTAWALIA.”Mwenyeji wako ni Sabrina Said, karibu!
    11 min
  • Watu bilioni 3.4 hawana huduma salama ya vyoo duniani - WHO
    Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO leo linaadhimisha Siku ya Choo Duniani kwa onyo kali kwamba janga la usafi wa mazingira duniani linagharimu maisha kila siku, na mabadiliko ya tabianchi yanaliweka katika hatari kubwa zaidi huku mamilioni ya watu wakiishi bila huduma muhimu ya choo. Flora Nducha na taarifa zaidi
    3 min
  • 19 NOVEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe katika siku ya Choo Duniani, simulizi za wakinamama wakimbizi wa ndani nchini Sudan, na usugu dhidi ya Viua-Vijasumu (AMR).Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO leo linaadhimisha Siku ya Choo Duniani kwa onyo kali kwamba janga la usafi wa mazingira duniani linagharimu maisha kila siku, na mabadiliko ya tabianchi yanaliweka katika hatari kubwa zaidi huku mamilioni ya watu wakiishi bila huduma muhimu ya choo.Wakinamama wakimbizi wa ndani nchini Sudan wameziomba jumuiya za kimataifa kuwasaidia kuhakikisha vita inaisha nchini mwao ili waweze kuishi kwa amani kwani madhila waliyopitia ni mengi na yanahuzunisha.Usugu dhidi ya Viua-Vijasumu (AMR)unaelezwa kama janga la kimyakimya linalotishia kurudisha nyuma mafanikio ya miongo kadhaa katika tiba na afya. Tunapoadhimisha Wiki ya Kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usugu dhidi ya Viua-Vijasumu au antibiotics, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO Kanda ya Afrika, Profesa Mohamed Janabi, ametahadharisha akisema dawa ambazo hapo awali ziliokoa maisha sasa hazifanyi kazi kama ilivyokuwa na hivyo inabidi kuchukua hatua za pamoja na haraka.Mwenyeji wako ni Sabrina Moshi, karibu!
    11 min
  • Usugu dhidi ya Viua-Vijasumu, AMR ni jukumu la kila mtu – Profesa Mohamed Janabi, WHO Afrika
    Usugu dhidi ya Viua-Vijasumu (AMR)unaelezwa kama janga la kimyakimya linalotishia kurudisha nyuma mafanikio ya miongo kadhaa katika tiba na afya. Tunapoadhimisha Wiki ya Kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usugu dhidi ya Viua-Vijasumu au antibiotics, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO Kanda ya Afrika, Profesa Mohamed Janabi, ametahadharisha akisema dawa ambazo hapo awali ziliokoa maisha sasa hazifanyi kazi kama ilivyokuwa na hivyo inabidi kuchukua hatua za pamoja na haraka. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
    3 min
  • 18 NOVEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Brazil kwenye mkutano wa COP30, ambako Dkt. Richard Muyungi, Mjumbe maalumu kwenye masuala ya mabadiliko ya tabianchi na mazingira kutoka nchini Tanzania anaeleza ni nini bara la Afrika linahitaji.Umoja wa Mataifa umekaribisha kupitishwa kwa Azimio namba 2803 la Baraza la Usalama kuhusu Gaza hapo jana, ukilitaja kuwa hatua muhimu katika kuimarisha usitishaji mapigano. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, anazitaka pande zote kuheshimu kikamilifu makubaliano hayo na kutafsiri kasi ya kidiplomasia kuwa hatua za dharura na za wazi kwa watu walioko katika eneo hilo. Katika taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Guterres, Stéphane Dujarric, amesema Umoja wa Mataifa umejizatiti kuongeza misaada ya kibinadamu na kuunga mkono jitihada zinazoelekezwa katika hatua inayofuata ya usitishaji mapigano.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), hali ya kibinadamu katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini bado ni tete. Mkurugenzi wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, Kanda ya Afrika Patrick Youssef  ambaye amerejea hivi karibuni kutoka DRC amewaleza waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi kwamba raia wa DRC wanaendelea kubeba mzigo mzito wa mapigano, hata wakati shughuli chache za kibiashara zikiendelea kurejea Goma. Ametoa tahadhari kuwa mgogoro huo unakabiliwa na upungufu mkubwa wa ufadhili, ukatili wa kingono unaongezeka, na zaidi ya asilimia 70 ya watu waliojeruhiwa kwa silaha mwaka huu ni raia.Kuanzia leo tarehe 18 inaanza Wiki ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usugu wa Vijiumbemaradhi dhidi ya dawa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linaonya kuwa usugu wa vimelea yaani hali ambapo bakteria, virusi na vijidudu vingine havidhuriki tena kwa dawa tayari unatishia mifumo ya afya, uchumi na uhakika wa chakula. Kwa kaulimbiu “Chukua Hatua Sasa: Linda Leo Yetu, Linda Mustakabali Wetu,” WHO inatoa wito kwa serikali, wahudumu wa afya, wakulima, wadau wa mazingira na umma kuchukua hatua madhubuti kutekeleza ahadi za kisiasa ili kupunguza kuenea kwa maambukizi sugu ya dawa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "UPUNGUFU"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    12 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners