Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 26 NOVEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia usafirir endelevu, udhalilishaji wa mtandaoni tukikuletea ujumbe kutoka Uganda, na ufugaji endelevu unaowawezesha wafugaji katika maeneo kame ya Isiolo na Garissa nchini Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafiri Endelevu Duniani kwa kuonya kwamba mifumo ya usafiri duniani ambayo ni muhimu kwa uchumi na maisha ya kila siku inayochochea dunia kuelekea janga la tabianchi na kwa hivyo siku hii inatukumbusha kwamba njia ya kuelekea mustakabali bora inategemea mifumo safi na yenye uendelevu wa usafiri.Siku 16 za uhamasishaji kupinga ukatili dhidi ya wanawake zikiendelea leo tunakupeka mjini Hoima Magharibi mwa Uganda kusiki maoni kutoka kwa wa mji huo kuhusu ukatili mtandaoni yakienda sanjari na kauliimbiu ya kampeni ya ya mwaka huu isemayo “Ukatili wa mtandaoni ni ukatili halisi na hakuna visingizo kwa ukatili mtandaoni”.Katika maeneo yaliyoghubikwa na athari za mabadiliko ya tabianchi kaskazini mwa Kenya, wafugaji wamekuwa wakikumbwa na changamoto kubwa kwani ukame na mafuriko, vinatishia sio tu mali zao bali pia maisha yao. Lakini kupitia mradi wa bima ya mifugo unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula  duniani WFP, kwa ushirikiano na asasi ya Zoetis na kampuni ya ZEP-RE, jamii zinaanza kupata ahuweni na matumaini mapya.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri Endelevu: Katibu Mkuu UN atoa wito wa mabadiliko ya haraka
    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafiri Endelevu Duniani kwa kuonya kwamba mifumo ya usafiri duniani ambayo ni muhimu kwa uchumi na maisha ya kila siku inayochochea dunia kuelekea janga la tabianchi na kwa hivyo siku hii inatukumbusha kwamba njia ya kuelekea mustakabali bora inategemea mifumo safi na yenye uendelevu wa usafiri. Flora Nducha na maelezo zaidi.
    4 min
  • 25 NOVEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, na leo zinaanza siku 16 za uanaharakati kuelimisha umma kuhusu janga la ukatili wa kijinsia, tunamsikia  mmoja wa waathirika wa ukatili wa kingono.Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa onyo kali kuhusu ongezeko la ukatili mtandaoni dhidi ya wanawake na wasichana.Ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya wanawake UN Women na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC inaonya kwamba mwaka 2024, wanawake na wasichana 50,000 waliuawa na wapenzi au jamaa sawa na mwanamke mmoja kila dakika 10.Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) inaonya kwamba uchumi wa Eneo la Palestina Linalokaliwa kwa Mabavu na Israel umerudi nyuma miaka 22 kwa muda usiozidi miaka miwili kwani umeingia katika hali mbaya zaidi ya mdororo kuwahi kurekodiwa, huku miongo ya maendeleo ikifutwa na operesheni za kijeshi zilizodumu kwa muda mrefu pamoja na vizuizi vya muda mrefu.Katika kujifunza lugha Kiswahili hii leo,  mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "MADUYUNI"Mwenyeji wako ni Sabrina Said, karibu!
    13 min
  • Mashindano ya mpira wa miguu kwa waliokatwa viuongo Gaza yafana
    Mashindano ya mpira wa miguu yanayofahamiaka kama Hope Championship kwa watu waliokatwa viungo katika Ukanda wa Gaza yamemalizika majuzi baada ya siku nne mfululizo za michuano. Mashindano haya yanaandaliwa na Chama cha Soka cha Watu Waliokatwa Viungo cha Palestina kama sehemu ya juhudi za kuwasaidia majeruhi na kuthibitisha ushiriki wao endelevu katika shughuli rasmi za michezo. Anold Kayanda anaripoti.
    4 min
  • Ushauri nasaha wamwezesha mkimbizi nchini Kenya kurejea maisha ya kawaida
    Tukielekea katika siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake hapo kesho Novemba 25 leo tunakupeleka Kenya kwake Geradline Ndayisenga, raia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) ambaye sasa anaishi ukimbizini kwenye eneo la Kitengela, Kaunti ya Kajiado nchini humo, anasema kama si usaidizi wa ushauri wa nasaha alioupata kutoka shirika la kiraia la Forum for Women Development, Democracy and Justice, FODDAJ nchini humo, basi hajui maisha yake  yangalikuwa vipi. Je ilikuwaje? Tuungane na Sheilah Jepngetich kwa simulizi zaidi.
    3 min
  • 24 NOVEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya maendeleo na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika, mashindano ya mpira wa miguu yanayofahamiaka kama Hope Championship kwa watu waliokatwa viungo katika Gaza na ukatili wa kijinsia.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo ametoa ujumbe mzito kwenye Mkutano wa Muungano wa Afrika AU na Muungano wa Ulaya EU, unaofanyika mjini Luanda, Angola akionya kuwa dunia “inabadilika kwa kiwango cha kutisha,” huku janga la tabianchi, ukosefu wa usawa na mvutano wa kimataifa vikichochea misukosuko mipya duniani.Tukielekea katika siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake hapo kesho Novemba 25 leo tunakupeleka Kenya kwake Geradline Ndayisenga, raia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) ambaye sasa anaishi ukimbizini kwenye eneo la Kitengela, Kaunti ya Kajiado nchini humo, anasema kama si usaidizi wa ushauri wa nasaha alioupata kutoka shirika la kiraia la Forum for Women Development, Democracy and Justice, FODDAJ nchini humo, basi hajui maisha yake  yangalikuwa vipi.Mashindano ya mpira wa miguu yanayofahamiaka kama Hope Championship kwa watu waliokatwa viungo katika Ukanda wa Gaza yamemalizika majuzi baada ya siku nne mfululizo za michuano. Mashindano haya yanaandaliwa na Chama cha Soka cha Watu Waliokatwa Viungo cha Palestina kama sehemu ya juhudi za kuwasaidia majeruhi na kuthibitisha ushiriki wao endelevu katika shughuli rasmi za michezo.Mwenyeji wako ni Sabrina Said, karibu!
    12 min
  • Mradi wa FAO wajenga mnepo baada ya mafuriko nchini Rwanda
    Mwezi Mei 2023, Rwanda nchi iliyozungukwa na milima ilikumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha maporomoko ya ardhi na kusababisha maji kutoka katika milima ya volkano, yakiambatana na mawe mazito kuharibu mashamba, makazi na barabara. Baada ya mafuriko hayo ili kupunguza athari za majanga kama hayo,kwa wakati wmingine Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Rwanda, kwa ufadhili wa Serikali ya Japan, linatekeleza mradi wa Kukabiliana na Majanga Yanayohusiana na Maji katika wilaya za Rutsiro na Burera. Lengo ni kupunguza Athari na kugeuza maji ziada kuwa rasilimali muhimu kwa jamii. Kufahamu zaidi kuhusu mradi huo ungana na Sheilah Jepngetich
    4 min
  • Jamii za asili Peru zaongeza uzalishaji wa kakao kwa mbinu bunifu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
    Katika msitu wa Amazon upande wa nchi ya Peru, jamii za watu wa asilizimeonesha namna mbinu bunifu za kilimo zinaweza kuongeza uzalishaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Yote haya yanakuja wakati dunia ikiendelea kujadili mustakabali wa hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika mkutano wa Umoja wa Mataifa COP30 unaoendelea huko Belém, Brazil.
    5 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners