Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UNICEF yaonya uhaba wa fedha wawaweka na watoto hatarini nchini Sudan
    Leo imetimia siku 1000 tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan, vita vinavyohusisha Jeshi la Sudan SAF na Kikosi cha Wanamgambo wa Sudan cha Msaada wa Haraka RSF. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema mtu mmoja kati ya watatu nchini humo ni mkimbizi ndani ya nchi yake au amekimbilia nje ya nchi huku Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF likieleza mzozo huo ambao umeendelea kusababisha janga kubwa la kibinadamu unawatesa zaidi wanawake na watoto kwani wanabeba mzigo mkubwa wa madhara ya vita. Tuungane na Rashid Malekela kwa taarifa zaidi
    4 min
  • 09 JANUARI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi mkuu nchini Uganda, elimu kwa watoto nchini Sudan leo ikitimia siku 1000 tangu kuzuka kwa vita nchini humo, na juhudi za wanawake za kuhifadhi misitu huko Narok nchini Kenya.Ikiwa zimebakia siku 6 kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Uganda, hii leo Umoja wa Mataifa imetoa ripoti inayobainisha kuwa uchaguzi huo utafanyika katika mazingira yaliyogubikwa na ukandamizaji, vitisho dhidi ya wapinzani wa kisiasa, watetezi wa haki za binadamu, na waandishi wa habari.Leo imetimia siku 1000 tangu kuzuka kwa vita nchini Sudan, vita vinavyohusisha Jeshi la Sudan SAF na Kikosi cha Wanamgambo wa Sudan cha Msaada wa Haraka RSF. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema mtu mmoja kati ya watatu nchini humo ni mkimbizi ndani yanchi yake au amekimbilia nje ya nchi huku Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF likieleza mzozo huo ambao umeendelea kusababisha janga kubwa la kibinadamu unawatesa zaidi wanawake na watoto kwani wanabeba mzigo mkubwa wa madhara ya vita.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, (UNDP), nchini Kenya, kupitia mradi wa kuhimili tabianchi au Climate Promise Guarantee, limewawezesha wanawake wa jamii ya asili katika Kaunti ya Narok, nchini humo kuongoza juhudi za uhifadhi wa misitu huku wakilinda urithi wao wa kitamaduni na kuboresha maisha ya familia zao.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    12 min
  • UNDP Kenya yaunga mkono wanawake wa jamii ya asili Narok katika uhifadhi wa misitu
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, (UNDP), nchini Kenya, kupitia mradi wa kuhimili tabianchi au Climate Promise Guarantee, limewawezesha wanawake wa jamii ya asili katika Kaunti ya Narok, nchini humo kuongoza juhudi za uhifadhi wa misitu huku wakilinda urithi wao wa kitamaduni na kuboresha maisha ya familia zao. Sheilah jepnge’tich na taarifa zaidi.
    4 min
  • 08 JANUARI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC kufuatilia yaliyojiri kwenye kikao mahsusi cha kuimarisha uhusiano mwema na wakazi wa eneo la Beni-Mavivi jimboni Kivu Kaskazini ili kuimarisha ulinzi wa amani wakati huu ambapo kwasasa hatua za kidiplomasia za kutatua mgogoro unaoikumbuka nchi hiyo zikiendelea.Hatimaye matumaini yamerejea ya kuwa na mlo mezani huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP kuweza kupatia raia mgao kamili wa chakula, ikiwa ni mara ya kwanza tangu vita vianze Oktoba 7, 2023.Huko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MINUSCA umesambaza radio zinazotumia nishati ya sola kwa jamii ikiwa ni sehemu ya  usaidizi wake wa kuhakikisha wananchi wanapata taarifa za uhakika na kwa wakati. Katika mkoa wa Nana-Mambéré, MINUSCA imekabidhi radio 600 kwa mamlaka za serikali za mitaa, wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Mkataba wa Amani, viongozi wa kidini, wanawake, vijana, watetezi wa haki za binadamu, vikosi vya ulinzi na usalama, wanahabari, wauza maduka na waendesha bodaboda.Mkuu wa Idara ya Umoja wa Mataifa ya  Operesheni za Ulinzi wa Amani, Jean-Pierre Lacroix akiwa ziarani nchini Lebanon amekuwa na mazungumzo na viongozi wa jeshi la taifa hilo ambapo amewashukuru kwa ushirikiano wao na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa mpito nchini humo, UNIFIL. Wamejadili pia mpango wa unaoendelea wa kupeleka tena vikosi vya UNIFIL kusini mwa Lebanon na jinsi gani ujumbe huo unaweza kuendelea kusaidia jeshi la Lebanon kutekeleza azimio namba 1701 la Baraza la Usalama kuhusu sitisho la uhasama kati ya Israeli na wanamgambo wa Hezbollah.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na ya neno "UMWESO"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    12 min
  • 07 JANUARI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia ukandamizaji wa haki za binadamu na uchaguzi mkuu nchini Uganda, juhudi za Rwanda za kutokomeza Saratani ya shingo ya kizazi, na mafunzo kwa ya kutengeneza kilelezi cha vifaranga au kinengunengu yaliyoendeshwa Kigoma Tanzania.Wakati nchi ya Uganda ikijiandaa na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 15 mwezi huu wa Januari, wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa hii leo wametoa taarifa ikionya kwamba hali ya haki za binadamu nchini Uganda si rafiki kwa uchaguzi wa amani.Saratani ya shingo ya kizazi ndiyo saratani inayowapata wanawake wengi zaidi nchini Rwanda kwani takribani kila mwaka kati ya wagonjwa wapya 1230, 830 hufariki dunia. Ili kupunguza mzigo wa ugonjwa huu na kuokoa maisha, mwaka 2020 Rwanda ilianzisha mkakati wa kitaifa unaoendana na lengo la Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) la kuondoa saratani ya shingo ya kizazi ifikapo 2030.Mafunzo kwa vitendo ya kutengeneza kilelezi cha vifaranga au Kinengunengu yaliyoendeshwa mkoani Kigoma kaskazini-magharibi mwa Tanzania na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, nchini huko yameendelea kusambaa na sasa  yamebisha hodi kwenye viunga vya mji mkuu wa kibiashara Dar es salaam kwa lengo la kusaidia wafugaji kujiongezea kipato badala ya kupoteza vifaranga kwa vifo au kuliwa na kunguru.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    12 min
  • Nchini Tanzania kilelezi cha vifaranga chazidi kusambaa kwa wafugaji
    Mafunzo kwa vitendo ya kutengeneza kilelezi cha vifaranga au Kinengunengu yaliyoendeshwa mkoani Kigoma kaskazini-magharibi mwa Tanzania na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, nchini huko yameendelea kusambaa na sasa  yamebisha hodi kwenye viunga vya mji mkuu wa kibiashara Dar es salaam kwa lengo la kusaidia wafugaji kujiongezea kipato badala ya kupoteza vifaranga kwa vifo au kuliwa na kunguru. Kutoka Tanzania, Rashid Malekela anaripoti.
    5 min
  • Mwelekeo wa kutokomeza saratani ya shingo ya kizazi nchini Rwanda
    Saratani ya shingo ya kizazi ndiyo saratani inayowapata wanawake wengi zaidi nchini Rwanda kwani takribani kila mwaka kati ya wagonjwa wapya 1230, 830 hufariki dunia. Ili kupunguza mzigo wa ugonjwa huu na kuokoa maisha, mwaka 2020 Rwanda ilianzisha mkakati wa kitaifa unaoendana na lengo la Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) la kuondoa saratani ya shingo ya kizazi ifikapo 2030.  Selina Jerobon anafafanua zaidi.
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners