Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UN: Miji inabeba mzigo mkubwa wa migogoro lakini pia ndio kitovu cha Suluhu
    Leo ni Siku ya Makazi Duniani, na Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kuchukua hatua za haraka kujenga miji jumuishi, imara na salama hasa kwa mamilioni ya watu waliolazimika kukimbia makazi yao. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi wanasema miji sasa ndiyo inabeba mzigo mkubwa wa migogoro duniani lakini pia ndiyo kitovu cha suluhisho. Flora Nducha na taarifa zaidi
    4 min
  • 06 OKTOBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya makazi duniani, kazi za walimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu na afya ya uzazi hasa wakati wa kujifungua na kuepusha vifo kupiti uvujaji damu.Leo ni Siku ya Makazi Duniani, na Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kuchukua hatua za haraka kujenga miji jumuishi, imara na salama hasa kwa mamilioni ya watu waliolazimika kukimbia makazi yao. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi wanasema miji sasa ndiyo inabeba mzigo mkubwa wa migogoro duniani lakini pia ndiyo kitovu cha suluhisho.Uongozi wa kugawana majukumu na mashauriano ya kina na walimu ni mambo muhimu katika kuboresha ustawi wa waelimishaji na matokeo ya kujifunza ya wanafunzi, amesema Carlos Vargas, Mkuu wa Kitengo na Mkuu wa Sekretarieti ya Kikosi Kazi cha Kimataifa cha Walimu kwa Elimu 2030 katika UNESCO.Mashirika ya afya duniani yametoa miongozo mipya yenye lengo la kuokoa maisha ya maelfu ya wanawake wanaopoteza maisha kutokana na kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua hali inayojulikana kama postpartum haemorrhage au PPH.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • Kenya: Mradi wa PLEAD Kenya yaleta mabadiliko chanya katika uwezeshaji wa kisheria
    Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Mpango wa Maendeleo, (UNDP) na la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) kwa ushirikiano na viongozi wa sheria nchini Kenya hadi mashinani  wamezindua mpando wa PLEAD unaolenga kuboresha mfumo wa haki katika kaunti 12 nchini humo. Lengo lao ni kuimarisha haki jumuishi kwa kutoa majawabu mbadala badala ya kifungo, kupunguza msongamano wa magereza kwa asilimia 30, na kuondoa mkwamo wa maisha. Sheilah Jepngetich anaeleza zaidi kupitia video iliyochapishwa kwenye chaneli ya Youtube ya UNDP
    5 min
  • UN: Buriani Jane Goodall, mwanamazingira na mtaalamu wa sokwe
    Kufuatia kifo cha Jane Goodall  mwanamazingira, mtaalamu wa sokwe na nyani, halikadhalika mjumbe wa amani kilichotokea Jumatano Oktoba 1 leo tunakurejesha mwaka 2002 alipoteuliwa kuwa mjumbe wa amani,  halikadhalika salamu za rambirambi kufuatia kifo chake. Assumpta Massoi anakuletea taarifa zaidi kuhusu mwanamazingira huyo aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.
    3 min
  • 03 OKTOBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia huduma za afya katika hospital Gaza, mradi wa PLEAD nchini Kenya na mafanikio yako katika kesi za mashinani, na kifo cha Jane Goodall mwanamazingira, mtaalamu wa sokwe na nyani, halikadhalika mjumbe wa amani.Umoja wa Mataifa umeonya kuwa hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza imefikia hatua ya kutisha, huku hospitali zikigeuzwa kuwa uwanja wa mapambano, kukizidiwa na wagonjwa na misaada kukwama. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameaambia waandishi wa habari leo mjini Geneva kuwa kuwa watoto wanakosa hewa ya oksijeni, wagonjwa wanakufa kwenye meza za upasuaji, na risasi zinavurumishwa moja kwa moja ndani ya hospitali.Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Mpango wa Maendeleo, (UNDP) na la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) kwa ushirikiano na viongozi wa sheria nchini Kenya hadi mashinani  wamezindua mpando wa PLEAD unaolenga kuboresha mfumo wa haki katika kaunti 12 nchini humo. Lengo lao ni kuimarisha haki jumuishi kwa kutoa majawabu mbadala badala ya kifungo, kupunguza msongamano wa magereza kwa asilimia 30, na kuondoa mkwamo wa maisha. Sheilah Jepngetich anaeleza zaidi kupitia video iliyochapishwa kwenye chaneli ya Youtube ya UNDP.Kufuatia kifo cha Jane Goodall mwanamazingira, mtaalamu wa sokwe na nyani, halikadhalika mjumbe wa amani kilichotokea Jumatano Oktoba 1 leo tunakurejesha mwaka 2002 alipoteuliwa kuwa mjumbe wa amani,  halikadhalika salamu za rambirambi kufuatia kifo chake. Assumpta Massoi anakuletea taarifa zaidi kuhusu mwanamazingira huyo aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    13 min
  • Gaza: Mashirika ya UN yaonya kuwa hospitali zimegeuka kuwa uwanja wa mapambano
    Umoja wa Mataifa umeonya kuwa hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza imefikia hatua ya kutisha, huku hospitali zikigeuzwa kuwa uwanja wa mapambano, kukizidiwa na wagonjwa na misaada kukwama. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameaambia waandishi wa habari leo mjini Geneva kuwa kuwa watoto wanakosa hewa ya oksijeni, wagonjwa wanakufa kwenye meza za upasuaji, na risasi zinavurumishwa moja kwa moja ndani ya hospitali.  Flora Nducha amefuatilia na hii hapa taarifa yake
    3 min
  • 02 OKTOBA 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ujumbe wa Omon Ukpoma-Olaiya, Kiongozi wa Uwekezaji wa UNCDF kwa Kanda ya Afrika Mashariki, Kusini na Nchi za Kiarabu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi neno la wiki.Haiti, hali ya kibinadamu imefika kiwango cha hatari, amesema Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk. Akihutubia Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Türk amesema Haiti imefika kiwango cha kulipuka kutokana na ukatili na ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu. Amesisitiza kuwa  “Tunaweza na lazima kubadili hali hii kwa ajili ya watu wa Haiti,” akiongeza kuwa “bila hatua za haraka hali mbaya zaidi huenda ikaja kwa Haiti na eneo zima.”Tukielekea Mashariki ya Kati huko Gaza, janga la kibinadamiu linaongezeka ambapo mashambulizi yanayoendelea yameathiri vibaya upatikanaji wa chakula na maji. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA, limeripoti kuwa usambazaji wa chakula kilichopikwa kaskazini mwa Gaza umepungua kwa asilimia 70, huku vituo vinne pekee ndivyo vinavyofanya kazi. Takriban watu milioni moja wanapata maji chini ya lita sita kwa siku, kiwango kilicho chini ya hali ya dharura.Nchini Sudan Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu Volker Türk ameonya kuhusu hali katika mji wa El Fasher, Darfur Kaskazin , akisema mji huo “uko kwenye ukingo wa janga kubwa zaidi ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa kulegeza mzingiro wa kijeshi na kuwalinda raia,” huku Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF) kikiongeza juhudi za kutwaa mji huo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana za maneno "USHINZI NA USHENZI"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    12 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners