Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • VVU: Sindano ya kuzuia kupatikana kwa bei nafuu kuanzia mwaka 2027
    Makubaliano yaliyosimamiwa na mashirika ya kimataifa, likiwemo UNITAID ambalo ni shirika tanzu la shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, halikadhalika Mpango wa afya wa Clinton (CHAI), Wits RHI na Maabara ya Dkt. Reddy, yanalenga kuhakikisha upatikanaji wa Lenacapavir kwa gharama nafuu.Dawa hii, inayodungwa mara mbili pekee kwa mwaka, imeonesha ufanisi mkubwa katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU, jambo muhimu hasa kwa wale wanaopata changamoto kutumia dawa za kila siku.Video ya UNITAID inaonesha maabara yenye teknolojia ya hali ya juu, ambamo wanasayansi wanaandaa dawa hiyo inayotarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kwa mamilioni ya watu walio katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNITAID, Tenu Avafia, anasema hatua hii ni ushindi mkubwa kwa jamii zinazohitaji kinga ya muda mrefu dhidi ya VVU."Tumeitikia wito kutoka kwa jamii na nchi tunazohudumia kwa kuhakikisha dawa hii inapatikana kwa gharama nafuu. Tunatarajia usambazaji wa toleo la bei nafuu la dawa hii kuanza kufikia mwaka 2027, chini ya miaka miwili tu tangu idhini kutolewa katika nchi za kipato cha juu — kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa."Akizungumza kuhusu hatua hii muhimu, Carmen Pérez Casas, Mkuu wa Mikakati Mwandamizi wa UNITAID, anasema:"Kwa kushirikiana na watengenezaji wa dawa mbadala, tumefanikisha bei nafuu mapema zaidi. Lakini bado tunahitaji kusaidia nchi na jamii kwa kuongeza upatikanaji."UNITAID inasema kwa msaada wa mashirika kama PEPFAR ambao ni mfuko wa Rais wa MArekani wa usaidizi wa dharura dhidi ya UKIMWI, pamoja na mfuko wa kimataifa na wakfu wa Gates, hatua hii inaleta matumaini ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU duniani.
    3 min
  • Mwanaharakati Dkt.Owusu: Ni wakati wa sauti zetu vijana zisikilizwe kwa vitendo
    Katika Mkutano wa Vijana wa Umoja wa Mataifa unaofanyika kandoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 unaoendelea hapa New York, viongozi vijana kutoka duniani kote wanataka uwakilishi mkubwa katika maamuzi ya kimataifa.Miongoni mwao ni daktari wa tiba na mwanaharakati wa kijamii wa vijana wa Uingereza na Ghana, Dkt. Khadija Owusu ambaye amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili.Owusu, ambaye pia ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Akaya inayowakilisha wasichana wa zama hizi, anasema vijana hawapaswi kuzungumziwa tu, bali wajumuishwe moja kwa moja katika kuandaa Suluhu za changamoto zinazoihusu dunia wakiwemo na wao "Mara nyingi tunazungumza kuwa tunataka ushiriki zaidi wa vijana wakati umefika wa kuacha kuzungumza tu kuhusu kuhitaji vijana wengi, bali tuwe na vijana wengi."Niko hapa kuwakilisha maelfu ya wasichanaAnasema ushiriki wake katika mkutano huu wa ngazi ya juu wa vijana si wa kibinafsi tu, bali unaakisi sauti za wasichana na vijana wengi wanaosaidiwa na taasisi yake ya Akaya."Niko hapa kuwakilisha si mimi peke yangu, si Uingereza tu, na si Ghana tu, bali Taasisi ya Akaya, na wasichana na vijana wengi tunaowahudumia nchini kote."Owusu anaamini vijana wa Kiafrika, hususan wasichana, wanapaswa kupata nafasi kubwa zaidi katika jmaukwaa ya kimataifa kama Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ili kupaza sauti zao."Bado tunahitaji kuona vijana zaidi kama sisi kwenye vyumba vya mikutano, Waafrika zaidi, vijana zaidi wa Kiafrika na wasichana wa Kiafrika kwenye vyumba vya mijadala, wakishiriki majadiliano kwa sababu tunaleta mabadiliko halisi."Owusu anasema ujumbe wake kwa vijana barani Afrika ni kubeba vipaji vyao, wajiamini, na kuendeleza ndoto zao kwani kila kitu kinawezekana. 
    3 min
  • UNGA80:Hotuba ya Netanyahu yakumbana na upinzani, yeye augeuza ukumbi kuwa darasa
    Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia katika siku yake ya nne hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani leo Ijumaa, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekuwa wa kwanza kuzungumza akitumia muda wake mwingi kushambulia wanamgambowa kipalestina, Hamas na kutetea kila uamuzi wa Israel. Anold Kayanda ameifuatilia hotuba hiyo kwa kina. Ilikuwa majira ya saa tatu na dakika chache hivi asubuhi ya leo saa za New York nchini Marekani ambapo Waziri Mkuu wa Isreal Benjamin Netanyahu amepewa fursa ya kuhutubia na ndipo ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukakosa utulivu. Wajumbe kwa makundi walinyanyuka katika viti vyao na kuondoka huku wakiwaacha maafisa wa Israel wakimpigia makofi kiongozi wao na pia nchi zinazoiunga mkono Israel zikasalia katika viti vyao ikiwemo Marekani.Baadhi ya wajumbe watoka njeKatika eneo la walipotakiwa kukaa wawakilishi wa Palestina kulikuwa wazi, huku katika eneo la Iran ikibakia picha iliyokusanya sura za baadhi ya watu wao waliouawa na mashambulizi ya Israel. Bwana Netanyahu kwa mara nyingine tena ameingia na ubao wenye picha ya ramani ya eneo la Mashariki ya Kati akiutumia kuishambulia Iran na kwa kutumia kalamu akiweka alama ya vema kuonesha namna ambavyo Israel imefanikiwa kupambana na ngome za Irani katika ukanda huo. Katika suti yake, kifuani upande wa kulia, Bwana Netanyahu pia ameweka kibandiko chenye QR Code na akawaambia watu kuwa Israel bado inakumbuka tukio walilofanyiwa na Hamas mwezi Oktoba mwaka juzi na kwamba ikiwa watu wamesahau hilo basi waelekeze simu zao kwenye QR Code hiyo kwenye nguo yake ili iwaoneshe madhara yaliyofanywa na Hamas.Majina ya mateka yakasomwaWaziri Mkuu huyo wa Israel ameyasoma majina ya mateka ambao bado wako mikononi mwa Hamas katika eneo la Ukanda wa Gaza na pia akaueleza mkutano kuwa amesambaza vipaza sauti au spika katika eneo lote la Gaza ili anapoongea leo, azungumze moja kwa moja na mateka huko walikofichwa. Na hapo akabadilisha lugha na kuongea kwa kihebrania akiwaahidi kuwa atawakomboa. Vilevile amedokeza kuwa kwa namna ya kiintelijensia Israel imefanya simu leo ziweze kusambaza hotuba katika ukanda wa Gaza na hivyo akautumia muda huo kupeleka ujumbe mkali kwa Hamas kuwa ataendelea kuwadhibiti. Bwana Netanyahu pia  ameingia ukumbini na vibao viwili vyenye maswali na majibu ya kuchagua japokuwa jibu sahihi kwa mujibu wake na waliojibu kuwa ni All the Above, yaani majibu yote ni sahihi. Maswali yote yalikuwa yakiwatuhumu Iran, Hamas, Al Caeda, Hezbollah na Houthi kuwa pia wanaitakia kifo Marekani na wameua watu wengi Ulaya. Huenda hotuba hii ya Netanyahu ikaingia katika orodha ya hotuba tano ndefu zaidi baada ya ile ya Rais wa Marekani Donald Trump wa Marekani, Ya Mahmoud Abbass wa Palestina na Félix-Antoine Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambao wote hao walitumia zaidi ya dakika arobaini licha ya muda wa hotuba uliopangwa kuwa angalau dakika 15.
    4 min
  • 26 SEPTEMBA 2025
    Hii leo ni hotuba ya Israeli kwenye mjadala mkuu wa baraza kuu, nini kilitokea? Kijana daktari mwanaharakati kutoka Ghana aishiye Uingereza akiwa UNGA80 na matumaini mapya ya kinga dhidi ya maambukizi ya VVU.Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia katika siku yake ya nne hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani leo Ijumaa, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amekuwa wa kwanza kuzungumza akitumia muda wake mwingi kushambulia wanamgambowa kipalestina, Hamas na kutetea kila uamuzi wa Israel. Anold Kayanda ameifuatilia hotuba hiyo kwa kina. Karibu Anold utupe japo kwa muhtasari.Tukisalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, moja ya mikutano ya ngazi ya juu iliyofanyika kando ya mjadala mkuu wa Baraza Kuu, ni ule wa kuadhimisha miaka 30 tangu kuanzishwa kwa program ya Umoja wa Mataifa kuhusu vijana, mkutano ukileta vijana kutoka kona mbali mbali za dunia. Miongoni mwao ni daktari wa tiba na mwanaharakati wa kijamii wa vijana kutoka Uingereza mwenye asili ya  Ghana, Dkt. Khadija Owusu. Amezungumza na Flora Nducha anayetujulisha zaidi katika taarifa hiiKatika hatua kubwa ya kihistoria kwenye mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) dawa mpya ya kudungwa inayoitwa Lenacapavir  inatarajiwa kupatikana kwa gharama nafuu katika nchi 120 zenye kipato cha chini na kati kuanzia mwaka 2027. Dawa hiyo itauzwa kwa kiasi cha dola 40 pekee ikiwa ni gharama ya vidonge vya kila siku vya kujikinga na VVU ambavyo mhusika atatumia kwa mwaka mzima. Sabrina Saidi ana taarifa zaidi.
    10 min
  • 25 SEPTEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalum inayomulika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza NDCs unaoendelea kandoni mwa UNGA80, na tumezungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Mohamed Yakub Janabi.Wakati viongozi wa nchi na serikali wanahutubia wakiwa ndani  ya jengo la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Kiongozi wa Palestina, Mahmoud Abbas ujumbe wake kwa UNGA80 ameutoa kwa njia ya video iliyorekodiwa kutokana na kutopata kibali cha kuingia Marekani. Katika hotuba hiyo amesisitiza kuwa, Ukanda wa Gaza utaendelea kuwa sehemu ya Taifa la Palestina na tuko tayari kuwajibika kikamilifu kwenye uongozi na usalama wa eneo hilo. Hamas hawatokuwa na jukumu lolote kwennye utawala.”.Mapema kabla ya Palestina, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, alihutubia wajumbe akitaka nchi wanachama kujitolea upya kwa misingi ya usawa, mshikamano na ushirikiano wa kimataifa. Amesema hilo ni muhimu kwa kuwa “wakati ambapo hapo awali tulijitahidi kujiuliza ‘Nini ni sahihi’ chini ya sheria ya kimataifa, leo tunashuhudia kwa wazi kuibuka kwa matumizi ya NGUVU ya kitaifa katika kusuluhisha migogoro. Hii ni njia ya giza na ya hatari sana inayotishia utawala wa sheria wa kimataifa tuliokubaliana kwa pamoja kama nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.”Kando ya hotuba za viongozi, kunafanyika maadhimisho ya miaka 30 tangu kupitishwa kwa Programu ya Dunia kwa ajili ya vijana. Je vijana kutoka Malawi wana ujumbe gani? Mwakilishi wao kwenye mkutano huu Rachel Mganga Wanangwa anasema, “Ujumbe kutoka vijana wa Malawi ni wekezeni kwetu, tusaidieni, shirikianeni nasi, na wanashiriki kwenye meza za mazungumzo ili kuhakikisha kuwa sauti zao zinawakilishiwa.”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    12 min
  • Taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu - Volodymyr Zelenskyy
    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu wanachoweza kufanya ni kutoa matamko makali pekee na kwamba kwa sasa duniani sheria pekee za Kimataifa haziwezi kusaidia nchi kujilinda bila ya kuwa na silaha pamoja na marafiki wenye nguvu wa kukusaidia. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.
    4 min
  • ECSA: Diplomasia ya kisayansi kutumika kusongesha Mkataba wa Zama Zijazo Afrika
    Katika siku ya pili ya Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, kando ya hotuba, viongozi wa nchi 9 wanachama wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA watakuwa na mkutano wa kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya, baada ya kujifunza kutokana na COVID-19 au UVIKO19. Mkurugenzi Mkuu wa ECSA Dkt. Ntuli Kapologwe akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa hii ametaja wanachotarajia kwenye mkutano huo..
    8 min
  • 24 SEPTEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia hotuba ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy katika siku ya pili ya mjadala mkuu wa UNG80, na ujumbe wa washiriki wa mkutano huu kutoka Nigeria na Tanzania.Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema taasisi za kimataifa zimekuwa dhaifu wanachoweza kufanya ni kutoa matamko makali pekee na kwamba kwa sasa duniani sheria pekee za Kimataifa haziwezi kusaidia nchi kujilinda bila ya kuwa na silaha pamoja na marafiki wenye nguvu wa kukusaidia.Katika siku ya pili ya Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, kando ya hotuba, viongozi wa nchi 9 wanachama wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA watakuwa na mkutano wa kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya, baada ya kujifunza kutokana na COVID-19 au UVIKO19.Tukisalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Mjadala Mkuu wa UNGA80 mbali ya kusikiza hotuba za viongozi unaambatana na mamia ya matukio na mikutano ya kando. Leo, sauti kutoka pande zote za dunia zinaitaka haki ya kijamii katika moja ya mikutano ya kando na miongoni mwa sauti hizo ni ya  mwanaharakati na mhamasishaji wa masuaa ya wasichana kutoka Nigeria ambaye anasema wasichana vigori hawapaswi kusahaulika.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Wasichana lazima wapewe fursa na kuondolewa vikwazo waweze kufikia uwezo wao: mwanaharakati Yejide Aina
    Tukisalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Mjadala Mkuu wa UNGA80 mbali ya kusikiza hotuba za viongozi unaambatana na mamia ya matukio na mikutano ya kando. Leo, sauti kutoka pande zote za dunia zinaitaka haki ya kijamii katika moja ya mikutano ya kando na miongoni mwa sauti hizo ni ya  mwanaharakati na mhamasishaji wa masuaa ya wasichana kutoka Nigeria ambaye anasema wasichana vigori hawapaswi kusahaulika. Flora Nducha anatujuza zaidi
    3 min
  • 23 SEPTEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalum na mada yetu inamulika maoni kuhusu miaka 80 ya Umoja wa Mataifa. Pia tunakuetea muhtasari wa habari unaofuatilia ujumbe wa viongozi katika mjadala mkuu wa UNG80.viongozi wa dunia wamekutana leo hapa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ikiwa ni siku ya kwanza ya Mjadala Mkuu wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ukiambatana na vikao vya kando vya ngazi ya juu. Katika hotuba yake ya UNGA 80 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa dunia kufanya maamuzi “ni aina gani ya dunia tunataka kujenga pamoja.”Kuanza kwa UNGA maana yake idadi kubwa ya wageni, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa UN anayeshughulikia habari na teknolojia, Bernardo Mariano, amesema wamejipanga kutoa huduma ya internet (Wi Fi) kwa watu 40,000 huku wakihakikisha hotuba za viongozi zinapeperushwa bila hitilafu za kiufundi wala kuvurugwa na mashambulizi ya mtandaoni.Na Hapo kesho Jumatano viongozi wa jumuiya ya Afya ya nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini, ESCA watakutana kumulika Diplomasia ya kisayansi na afya ili kusongesha Mkataba wa Zama Zijazo. Mkurugenzi Mkuu wa ECSA Dkt. Ntuli Kapologwe ameeleza kulikoni?.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    12 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners