Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 18 SEPTEMBA 2025
    Jaridani leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kuhusu masuala ya wanawake, tathmini ya miaka 30 ya harakati za kusongesha haki za wanawake na utamsikia maoni ya Balozi Gertrude Mongella kutoka Tanzania. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali.Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukianza Jumatatu ijayo, Rais wa Mkutano huo Annalena Baerbock  amewaambia waandishi wa habari jijini New York, Marekani kuwa “jukumu letu ni Umoja wa Mataifa uwe thabiti kwa miaka 80 ijayo. Michakato ya kuhakikisha hilo ndio itakuwa jukumu letu mwaka huu, ikiwemo kusongesha ajenda ya marekebisho ya Umoja wa Mataifa. Kwa hiyo tukitaka Umoja wa Mataifa thabiti, basi tunahitaji ahadi kutoka serikali zote duniani.Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayotolewa kila mwaka kabla ya kuanza kwa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu inasema Umoja wa Mataifa umeendelea kusimama imara, ukifanya kazi ya kuendeleza amani, kuchochea maendeleo endelevu, na kupunguza mateso ya kibinadamu licha ya majaribu makubwa. Katika ripoti hiyo Antonio Guterres amesisitiza uimara wa watumishi wa Umoja wa Mataifa, ambao wamejitolea kuleta matumaini na msaada kwa wale wanaohitaji licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu.ripoti ya Hali ya Rasilimali za Maji Duniani iliyotolewa leo inasema ni takriban theluthi moja tu ya mabonde ya mito duniani yaliyokuwa na hali ya “kawaida” mwaka 2024 ilhali mengine yote yalikuwa na kiwango cha juu zaidi cha maji au chini ya kiwango cha kawaida — ikiwa ni mwaka wa sita mfululizo wa kutokuwepo kwa uwiano wa wazi. Ikitolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO, ripoti inasema mwaka 2024 uliokuwa mwaka wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa ulianza na tukio la El Niño ambalo liliathiri vibaya mabonde makubwa ya mito na kusababisha ukame katika maeneo kadhaa ikiwemo kusini mwa Afrika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "MZOEA PUNDA HAPENDI FARASI"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    11 min
  • Agizo jipya la kuhamisha watu katika ukanda wa Gaza ni ‘msumari wa moto kwenye kidonda’
    Wakati Israeli ikiwa imetoa amri mpya ya watu kuhama kutoka jiji la Gaza katika eneo inalokalia kimabavu la Palestina, na kuelekea eneo ililotenga na kuliita ukanda wa kibinadamu kusini mwa Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limesikitishwa na agizo hilo jipya ikisema eneo halina ukubwa wala huduma za kutosha kusaidia wale walioko tayari huko, sembuse wale watakaowasili. Huduma za afya ni tete kama anavyosimulia Flora Nducha kwa taarifa hii. 
    4 min
  • UNDP Zambia: Ukulima kupitia miundombinu inayostahimili mabadiliko ya tabianchi
    Kupitia mradi wa SCRALA uliowezeshwa na  shirika la Umoja wa Mataifa  la mpango wa maendeleo, UNDP, wakulima wadogo nchini Zambia sasa wanaweza kulima mwaka mzima kwa kutumia miundombinu inayostahimili mabadiliko ya tabianchi kama vile mifumo ya umwagiliaji na vituo vya ukusanyaji mazao, jambo linalochangia kuongezeka kwa tija na upatikanaji wa masoko. Sheila Jepngetich anasimulia zaidi.
    2 min
  • 17 SEPTEMBA 2025
    Jaridani leo jaridani tunaangazia haki ya elimu kwa wasichana na wanawake nchini Afghanistan, na kuzorota kwa huduma za afya katika ukanda wa Gaza. Pia tunakwenda nchini Zambia kumulika mradi wa wakulima wadogo.Tarehe kama ya leo, 18 Septemba mwaka 2021 dunia ilishitushwa na kuhuzunishwa na tangazo lililotolewa la uongozi wa Taliban nchini Afghanistan la kukataza wasichana barubaru kuendelea na masomo na kwamba darasa la sita ndio mwisho wa elimu yao. Sasa ni miaka minne na katazo hilo bado limesimama kitu ambacho Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa ni “moja ya dhulma kubwa za wakati wetu.”Wakati Israeli ikiwa imetoa amri mpya ya watu kuhama kutoka jiji la Gaza katika eneo inalokalia kimabavu la Palestina, na kuelekea eneo ililotenga na kuliita ukanda wa kibinadamu kusini mwa Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limesikitishwa na agizo hilo jipya ikisema eneo halina ukubwa wala huduma za kutosha kusaidia wale walioko tayari huko, sembuse wale watakaowasili. Huduma za afya ni tete.Kupitia mradi wa SCRALA uliowezeshwa na  shirika la Umoja wa Mataifa  la mpango wa maendeleo, UNDP, wakulima wadogo nchini Zambia sasa wanaweza kulima mwaka mzima kwa kutumia miundombinu inayostahimili mabadiliko ya tabianchi kama vile mifumo ya umwagiliaji na vituo vya ukusanyaji mazao, jambo linalochangia kuongezeka kwa tija na upatikanaji wa masoko.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • UNICEF yahimiza Taliban kuruhusu wasichana Afghanistan kuendelea na masomo
    Tarehe kama ya leo, 18 Septemba mwaka 2021 dunia ilishitushwa na kuhuzunishwa na tangazo lililotolewa la uongozi wa Taliban nchini Afghanistan la kukataza wasichana barubaru kuendelea na masomo na kwamba darasa la sita ndio mwisho wa elimu yao. Sasa ni miaka minne na katazo hilo bado limesimama kitu ambacho Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa ni “moja ya dhulma kubwa za wakati wetu.”  Leah Mushi na taarifa zaidi.
    3 min
  • 16 SEPTEMBA 2025
    Jaridani leo jaridani tunakuletea mad akwa kina inayoangazia mjadala Mkuu wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno la wiki.Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imesema Israel imetekeleza mauaji ya kimbari Gaza. Ripoti ya tume hiyo hiyo iliyotolewa leo mjini Geneva pia inamtaja Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na maafisa wengine wakuu wa Israel kwa kuchochea vitendo hivyo. Israel imepinga vikali, na kuuita ripoti hiyo kuwa ni “kashfa.” Taarifa hii imetolewa huku mashambulizi makali ya anga yakiendelea usiku kucha mjini Gaza bila dalili za kukoma.Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, shirika hilo limekamilisha makadirio mapya ya bajeti ya mwaka 2026, yakionesha kupunguzwa kwa zaidi ya dola milioni 500. Hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa mageuzi ya UN80, unaolenga kuongeza ufanisi wakati Umoja wa Mataifa ukiadhimisha miaka 80. Bajeti mpya inapendekeza kupunguzwa kwa rasilimali kwa zaidi ya asilimia 15 na nafasi za kazi kwa karibu asilimia 19 ikilinganishwa na mwaka 2025.Huko Nairobi, Kenya leo imezindua maabara ya kisasa ya polio iliyoidhinishwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO katika Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kenya, KEMRI. Kituo hicho, kilichofadhiliwa na WHO na wakfu wa  Gates, kimeelezwa kuwa nyenzo muhimu katika kugundua mapema na kukabiliana na virusi vya polio pamoja na magonjwa mengine yenye uwezekano wa kusambaa, si tu nchini Kenya bali pia katika kanda nzima ya Afrika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo,  mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, anafafanua maana za neno "MJOLI"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    11 min
  • 15 SEPTEMBA 2025
    Jaridani leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, haki za binadamu nchini Sudan Kusini na ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya demokrasia duniani.Kamishina Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, Philippe Lazzarini, ametoa onyo kali kuwa “hakuna sehemu yoyote iliyo salama Gaza, na hakuna mtu aliye salama”akisema      zahma na madhila  yametanda kila kona ya eneo hilo linalokaliwa kimabavu na Israel.Leo ni siku ya demokrasia duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameeleza bayana kuwa demokrasia iko hatarini duniani.Nchini Sudan Kusini ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaendelea kuimarisha mfumo wa mahakama ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wote hata maeneo yote ya nchi hiyo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    11 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners