Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UN waadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwake
    Umoja wa Mataifa hii leo umeadhimisha miaka 80 tangu kusainiwa kwa Mkataba wake tarehe 26 Juni 1945, tukio lililotoa matumaini mapya kwa dunia iliyokuwa imechoka kutokana na vita kuu mbili za dunia, mauaji ya halaiki na ukoloni. Katika maadhimisho hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema kumbukizi ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa ni fursa ya kukumbuka ujasiri wa waanzilishi wa taasisi hiyo na kuimarisha mshikamano wa kimataifa katika kukabili changamoto zinazokabili dunia hivi sasa. Tuungane na Leah Mushi aliyefuatilia maadhimisho hayo atupatie taarifa zaidi.
    5 min
  • Tumefika hapa UN, tafadhali tusikilizeni - Emily Mohohlo
    Tweet URLKando ya maadhimisho ya siku ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa, hapa makao makuu kumefanyika mashauriano ya faragha yenye lengo la kusaka majawabu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Mashauriano ya leo ni sehemu ya mashauriano 10 yatakayofanyika kuelekea mkutano wa tabianchi wa wakuu wa nchi na serikali utakaofanyika keshokutwa Jumatano hapa Umoja wa Mataifa. Assumpta Massoi amezungumza na mmoja wa watoa mada kwenye mashauriano hayo ambayo matokeo yake yatawasilishwa kwenye mkutano wa viongozi. Katika uwanda wa wageni nje ya jengo la mikutano nakutana na Emily Mohohlo, Mratibu wa shirika la kiraia la Slum Dwellers International kutoka Afrika Kusini linalojikita katika kuhakikisha maeneo ya mabanda mijini yanakuwa jumuishi, yana mnepo na maisha yao yanaboreshwa.Nikamuuliza umuhimu wa mkutano na kusema. “mkutano huu ni muhimu kwangu kwa sababu katika maisha halisia kuna joto kupindukia na linasababisha vifo kwa wanawake na pia kutoweka kwa mbinu zao za kujipatia kipato. Hivyo kwangu naona kama tunaweza kujumuika pamoja katika ngazi ya kijamii na kupata takwimu sahihi na kisha watafiti watusaidie. Tunahitaji wabia kwani tayari tumeshachukua hatua.”Kwa hiyo ujumbe wake kwa washiriki wa mkutano? “Njooni mshirikiane nasi, kwa sababu tuna takwimu kutoka mashinani lakini hatuna uwezo wa kifedha. Tukipata fedha kutoka kwa watafiti itakuwa vema. Tunajua wana takwimu lakini si kutoka mashinani.”Nilipomuuliza umuhimu wa Umoja wa Mataifa wakati huu unatimiza miaka 80 akafunguka, "Ndio sasa una miaka 80, lakini bado hatuoni vya kutosha mafanikio yake mashinani. Huwezi kusaidia mtu mmoja mmoja. Waje kwenye vikundi na itakuwa vema kwa sababu kuna idadi kubwa ya watu.”Akatamatisha na ujumbe kwa Umoja wa Mataifa. “Tumefika hapa, tafadhali tusikilizeni. Hakuna chetu bila kutushirikisha. Asante,”
    3 min
  • 22 SEPTEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa washirirki ya mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, hasa maadhimisho ya miaka 80 ya umoja huo. Pia tunamulika mashauriano ya faragha yenye lengo la kusaka majawabu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi.Umoja wa Mataifa hii leo umeadhimisha miaka 80 tangu kusainiwa kwa Mkataba wake tarehe 26 Juni 1945, tukio lililotoa matumaini mapya kwa dunia iliyokuwa imechoka kutokana na vita viwili vya dunia, mauaji ya halaiki na ukoloni. Katika maadhimisho hayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema kumbukizi ya kuanzishwa kwa UN ni fursa ya kukumbuka ujasiri wa waanzilishi wa taasisi hiyo na kuimarisha mshikamano wa kimataifa katika kukabili changamoto zinazokabili dunia hivi sasa.Tukisalia na maadhimisho ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa , moja ya mchango mkubwa unaotoa kwa dunia tangu ulipoanzishwa mwaka 1945 ni kusaidia mamilioni ya watu wanaolazimika kufungasha virago kukimbia makwao na kuwa wakimbizi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vita. Uganda ni moja ya nchi zinazohifadhi maelfu ya wakimbizi wengi kutoka Sudan, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakisaidiwa chini ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na mengine. John Kibego kutoka Radio washirika Kazi-Njema FM iliyoko mjini Hoima Uganda amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wakimbizi hao akielezea mchango mkubwa wa Umoja wa Mataifa kwake.Kando ya maadhimisho ya siku ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa, hapa makao makuu kumefanyika mashauriano ya faragha yenye lengo la kusaka majawabu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Mashauriano ya leo ni sehemu ya mashauriano 10 yatakayofanyika kuelekea mkutano wa tabianchi wa wakuu wa nchi na serikali utakaofanyika keshokutwa Jumatano hapa Umoja wa Mataifa. Assumpta Massoi amezungumza na mmoja wa watoa mada kwenye mashauriano hayo ambayo matokeo yake yatawasilishwa kwenye mkutano wa viongozi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    12 min
  • Asante UN lakini msichoke kusaka amani ya DRC: Mkimbizi Uganda
    Wakati dunia ikiadhimisha miaka 80 ya Umoja wa Mataifa, moja ya mchango mkubwa unaotoa kwa dunia tangu ulipoanzishwa mwaka 1945 ni kusaidia mamilioni ya watu wanaolazimika kufungasha virago kukimbia makwao na kuwa wakimbizi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vita. Uganda ni moja ya nchi zinazohifadhi maelfu ya wakimbizi wengi kutoka Sudan, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakisaidiwa chini ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na mengine. John Kibego kutoka Radio washirika Kazi-Njema FM iliyoko mjini Hoima Uganda amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wakimbizi hao akielezea mchango mkubwa wa Umoja wa Mataifa kwake. Kwako Kibego.
    5 min
  • Amri ya kuhama 'kaa la moto' kwa WaPalestina Gaza
    Baada ya amri iliyotolewa na jeshi la Israel la kuwataka Wapalestina walioko katika eneo la mji wa Gaza huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel kuondoka eneo hilo kwani linataka kufanya mashambulizi, hali imekuwa mbaya kwa wananchi hususan wazee ambao sasa wanafunga safari kilometa nyingi kuondoka eneo hilo. Leah Mushi anatujuza masahibu wanayo kumbana nao watu hao.
    4 min
  • Balozi Lokaale: Licha ya changamoto  hakuna taasisi mbadala wa UN duniani
    Ilikuwa miezi, wiki na sasa imesalia siku tatu tu kabla ya mjada mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 kun’goa nanga hapa kwenye Makao Makuu jijini New York Marekani ambapo viongozi wa Dunia na wakilishi mbalimbali watashiriki kwenye mkutano wa 80 wa Baraza Kuu. Mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo maadhimisho ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa. Flora Nducha ameketi na mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ekitela Lokaale kuzungumzia Afrika na Umoja wa Mataifa katika miaka na umuhimu wa Umoja huo duniani, hiki ni kionjo tu cha maohojiano hayo akianza na mchango wa Afrika Umoja wa Mataifa
    3 min
  • 19 SEPTEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa ndani wa Palestina Gaza, na ujumbe wa mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ekitela Lokaale kuhusu mchango wa Afrika katika kazi za Umoja wa Mataifa. Pia tunakwenda Tanzania kumulika amani.Baada ya amri iliyotolewa na jeshi la Israel la kuwataka Wapalestina walioko katika eneo la mji wa Gaza huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel kuondoka eneo hilo kwani linataka kufanya mashambulizi, hali imekuwa mbaya kwa wananchi hususan wazee ambao sasa wanafunga safari kilometa nyingi kuondoka eneo hilo.Ilikuwa miezi, wiki na sasa imesalia siku tatu tu kabla ya mjada mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 kun’goa nanga hapa kwenye Makao Makuu jijini New York Marekani ambapo viongozi wa Dunia na wakilishi mbalimbali watashiriki kwenye mkutano wa 80 wa Baraza Kuu. Mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo maadhimisho ya miaka 80 ya Umoja wa Mataifa.Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani, hapo Jumapili tarehe 21 mwezi Septemba 2025, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kushirikiana na baadhi ya wadau nchini humo, umeendesha warsha ya siku moja ya kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Hazina jijini Dar es Salaam kuhusu ya umuhimu wa kuishi kwa amani na kuchukua hatua sasa katika kuidumisha. Warsha hiyo imeongozwa na kauli mbiu  “Chukua hatua Sasa, kwa ajili ya Dunia yenye Amani.”Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
    10 min
  • UN Tanzania yatoa elimu ya amani na utangamano kwa wanafunzi kuelekea
    Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani, hapo Jumapili tarehe 21 mwezi Septemba 2025, Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kushirikiana na baadhi ya wadau nchini humo, umeendesha warsha ya siku moja ya kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Hazina jijini Dar es Salaam kuhusu ya umuhimu wa kuishi kwa amani na kuchukua hatua sasa katika kuidumisha. Warsha hiyo imeongozwa na kauli mbiu  “Chukua hatua Sasa, kwa ajili ya Dunia yenye Amani.” Katika warsha hiyo, baadhi ya wanafunzi wameeleza walichojifunza na namna elimu hiyo inavyoweza kuwanufaisha katika maisha yao ya kila siku. Shuhuda wetu katika mafunzo ni Sabrina Saidi anatupasha ilivyokuwa
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners