Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 01 OKTOBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Kimataifa ya Wazee duniani na mchango wao kwa jamii, hali ya afya katika ukanda wa Gaza, na simulizi ya Balozi Mwema wa UNICEF, Angelique Kidjo.Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako kumefanyika tukio maalum la kuadhimisha siku ya wazee duniani leo Oktoba Mosi, kaulimbiu ikiwa Wazee Wanaendesha Hatua za Kijamii na Kimaisha: Matamanio Yetu, Ustawi Wetu na Haki Zetu. Anayekupeleka ukumbini ni Flora Nducha.Huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanawake katika eneo la Deir al- Balah wanalazimika kutumia majiko ambayo wanachochea taka za plastiki na makaratasi ili kupota moto wa kuweza kupikia chakula. Hali hiyo imesababisha kuenea kwa magonjwa ya kupumua kama vile numonia na pumu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linatoa wito kwa viongozi wa Afrika kufanya uwekezaji wa kifedha wa busara utakaowezesha watoto kupata ujuzi wa msingi wa kujifunza na mustakabali wenye nguvu kwa bara la Afrika. Balozi Mwema wa UNICEF, Angelique Kidjo, katika kuunga mkono wito huo anasimulia safari yake kutoka kujifunza alfabeti hadi kuimba kwa ulimwengu mzima.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    12 min
  • Angelique Kidjo, Mwanamuziki, asimulia safari yake ya elimu akiunga mkono wito wa UNICEF kwa viongozi wa Afrika
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF linatoa wito kwa viongozi wa Afrika kufanya uwekezaji wa kifedha wa busara utakaowezesha watoto kupata ujuzi wa msingi wa kujifunza na mustakabali wenye nguvu kwa bara la Afrika. Balozi Mwema wa UNICEF, Angelique Kidjo, katika kuunga mkono wito huo anasimulia safari yake kutoka kujifunza alfabeti hadi kuimba kwa ulimwengu mzima. Anold Kayanda anaeleza zaidi.
    4 min
  • EAC yasisitiza usalama, uchumi na masuala ya kidijitali katika Mjadala Mkuu wa UNGA80
    Kama unavyofahamu Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 umekunja jamvi rasmi  jana Jumatatu. Na tumepata fursa ya kuzungumza na washiriki mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Veronica Nduva ambaye alizungumza na Flora Nducha kandoni mwa mjadala huo kuangazia mchango wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kutekeleza ajenda ya Umoja wa Mataifa ikiwemo masuala ya Amani na usalama, maendeleo na ushirikiano wa kikanda. Ungana nao.
    10 min
  • 30 SEPTEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ujumbe wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, Veronica Nduva ambaye alizungumza na Flora Nducha kandoni mwa UNGA80. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Ikiwa ni zaidi ya miaka minane tangu zaidi ya wakimbizi 750,000 waislamu wa kabila la warohingya wakimbie Myanmar kuelekea kwenye kambi kubwa nchini Bangladesh, mgogoro huo bado haujapatiwa suluhisho na leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa viongozi wamekutana kusaka suluhu ya kudumu kwa warohingya na makabila mengine madogo nchini Myanmar. Katibu Mkuu Antonio Guterres kupitia Afisa Mtawala Mkuu wa UN Courtenay Rattray amesema, “mgogoro huu, ambao umezidi kuongezeka tangu mapinduzi ya kijeshi Myanmar ya mwaka 2021, unasigina haki za binadamu, utu na usalama wa mamilioni ya watu na unatishia uthabiti wa kikanda. Haitoshi tu kutathmini hali ilivyo. Tunapaswa pia kuendeleza mshikamano na kubuni suluhisho.”Amani nchini DRC imesalia bado ahadi, ni kauli ya Bintou Keita, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC aliyotoa wakati akihutubia Baraza la Usalama lililokutana leo kujadili hali Mashariki mwa DRC. Anasema hali inazidi kuwa tete. “Ghasia zinaendelea kushamiri jimboni Kivu Kaskazini hususan eneo la Rutshuru tangu waasi wa M23 watwae eneo hilo. Kuanzia mwezi Juni na kuendelea ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umepokea maombi lukuki ya watu wakitaka ulinzi kwenye maeneo yanayodhibitiwa na M23.”.Na mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yamesisitiza wito wa kupatikana kwa sitisho la mapigano huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel, ili kupunguza machungu wakati huu ambapo Mpango wa Marekani wa Vipengele 20 unaibua matumaini ya kukomeshwa kwa mapigano. Ricardo Pires, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto, UNICEF amesema, “ni muhimu tupate sitisho la mapigano na misaada iweze sio tu kuingia na kuepusha baa la njaa, bali pia kuelekezwa maeneo ya kusini. Lakini vile vile kuhakikisha watoto na familia zao wanapata malazi bora wakati huu majira ya baridi kali yanakaribia. La sivyo italeta zahma ya afya kwa watoto na familia zao.”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    13 min
  • Ili Afrika ‘iimarike kiafya’ inabidi isiwe tegemezi kwenye masuala ya kifedha: Dkt. Ntuli Kapologwe
    Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA80, inafanyika mikutano mingine ya pembezoni kujadili masuala mengine ya kusongesha maendeleo ya ulimwengu. Wiki iliyopita tulizungumza na Dkt. Ntuli Kapologwe Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA wakati alipokuwa akisubiri kushiriki mkutano  wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kujadili jinsi ya kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya. Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza tena na Dkt. Kapologwe mara tu baada ya mkutano huo
    4 min
  • 29 SEPTEMBA 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia leo Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 tukimulika hotuba za viongozi na mikutano mingine ya pepmbezoni kuhusu malengo ya maendeleo enedelevu, SDGs.Viongozi wa mataifa ya nchi wanachama 16 waliopanda kwenye mimbari ya ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo Jumatatu ya tarehe 29 Septemba 2025 ambayo ndio  ukomo wa Mjadala Mkuu wa mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, (UNGA80) wamepaza sauti zao kuhusu masuala mbalimbali yanayokumba dunia hivi sasa ikiwemo vita Gaza, na hali ya kiuchumi Afrika.Leo Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 hotuba za viongozi ukifunga pazia, Afrika imeweka bayana kauli moja ya mshikamano, kwamba lazima iwe na viti na sauti kwenye Baraza la Usalama na kuahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha dhamira hiyo inatimia. Mchakato ulishaanza na unaendelea kuelekea lengo hilo kama ambavyo Balozi Ekitela Lokaale mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa alivyomfahamisha.Tukisalia hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kandoni mwa Mjadala Mkuu wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA80, inafanyika mikutano mingine ya pembezoni kujadili masula mengine ya kusongesha maendeleo ya ulimwengu. Wiki iliyopita tulizungumza na Dkt. Ntuli Kapologwe Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, ECSA wakati alipokuwa akisubiri kushiriki mkutano  wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kujadili jinsi ya kusongesha diplomasia ya kisayansi ili kuhakikisha bara la Afrika haliachwi nyuma kwenye kukabiliana na changamoto za kiafya.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    12 min
  • Afrika imedhamiria kuhakikisha ina sauti na nafasi Baraza la Usalama la UN: Balozi Lokaale
    Leo Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA80 hotuba za viongozi ukifunga pazia, Afrika imeweka bayana kauli moja ya mshikamano, kwamba lazima iwe na viti na sauti kwenye Baraza la Usalama na kuahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha dhamira hiyo inatimia. Mchakato ulishaanza na unaendelea kuelekea lengo hilo kama ambavyo Balozi Ekitela Lokaale mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa alivyomfahamisha 
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners