Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 09 SEPTEMBA 2025
    -Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea UNGA79yafikia tamati hii leo na kupisha UNGA80  chini ya uongozi wa Rais mpya Annalena Baerbock-Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyozinduliwa leo imesema matumizi ya kijeshi duniani yalifikia dola trilioni 2.7 mwaka 2024, yakiwa yameongezeka kwa zaidi ya asilimia 9 kutoka mwaka 2023-Mratibu wa Misaada ya Dharura wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher ametangaza leo  dola milioni 1 za kimarekani kutoka  Mfuko wa Dharura wa Umoja wa Mataifa CERF ili kudhibiti mlipuko wa kipindupindu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. -Mada kwa kina inatupeka Pemba Kaskazini kisiwani Zanzibar nchini Tanzania kuangazia mradi wa FAo wa ZJP unavobadili maisha ya wakulima wa ndiziNa katika jifunze Kiswahili utamsikia mlumbi Jorum Nkumbi kutoka Tanzania akifafanua maana ya neno LISANI
    10 min
  • Shirika la Umoja wa Mataifa la afya,WHO laongeza orodha ya dawa muhimu
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limefanya mabadiliko muhimu katika orodha yake ya dawa muhimu duniani au Essential Medicines List – EML na orodha ya dawa muhimu kwa watoto (EMLc) ikijumuisha dawa za kisasa za saratani, kisukari, unene uliopitiliza na magonjwa mengine sugu.Orodha za WHO za dawa muhimu ni nyenzo za mwongozo zinazotumiwa na zaidi ya nchi 150 kupanga ununuzi, bima za afya na upatikanaji wa dawa. Kwa lugha rahisi, dawa zinazoorodheshwa hapa huwa na nafasi kubwa zaidi ya kununuliwa na kutolewa kwa wagonjwa kupitia huduma za umma kwani wanachama wa WHO wanaziweka dawa hizi kama kipaumbele cha kiafya kwa mamilioni ya watu duniani.WHO wakati wakitangaza orodha hiyo mpya waliweka bayana kuwa dawa hizi mpya si za majaribio, bali ni zile ambazo zimethibitishwa kitabibu kuwa zinaokoa maisha, kupunguza madhara ya magonjwa na kuboresha maisha ya wagonjwa.Nini maana yake?Kuongezwa kwa dawa hizi ni hatua ya mbele katika safari ya kuhakikisha afya bora kwa wote. Inamaanisha wagonjwa zaidi wa saratani, kisukari na magonjwa mengine sugu wanaweza kuwa na matumaini ya maisha marefu na bora. Pia ni wito kwa mataifa kuchukua hatua ili kuhakikisha upatikanaji wa dawa unakuwa wa haki na usawa, bila kumwacha mtu yeyote nyuma.Changamoto ya bei na usawa wa kiafyaChangamoto kubwa sasa ni bei kubwa ya dawa hizi mpya, ambazo zinaweza kufanya wagonjwa wengi kushindwa kuzipata.WHO inapendekeza mikakati ya kupunguza gharama na kuhakikisha dawa hizi zinapatikana kwenye ngazi ya huduma za msingi za afya.Deusdedit Mubangizi, Mkurugenzi wa Sera na Viwango vya Dawa WHO, anasema “Sehemu kubwa ya matumizi ya nje ya mfuko wa magonjwa yasiyoambukiza yanaelekezwa kwenye dawa, ikiwa ni pamoja na zile zinazoainishwa kama muhimu na ambazo kimsingi, zinapaswa kupatikana kwabei rahisi kwa kila mtu. Ili kufikia upatikanaji sawa wa dawa muhimu kunahitajika mwitikio madhubuti wa mfumo wa afya unaoungwa mkono na dhamira dhabiti ya kisiasa, ushirikiano wa sekta nyingi na programu zinazozingatia watu ambazo hazimwachi mtu nyuma.”Kwa maneno mengine, dawa hizi haziwezi kuwa za matajiri pekee  lazima mifumo ya afya, serikali na sekta binafsi zishirikiane kuhakikisha kila mtu anayehitaji anapata dawa kwa gharama nafuu.© UNOCHA/Ali Haj SuleimanDaktari akimpatia matibabu mgonjwa wa Saratani huko nchini SyriaSaratani, kisukari na unene uliopitiliza ni changamotoSaratani na kisukari ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo na ulemavu kwa mamilioni ya watu duniani kila mwaka. Kwa mfano, saratani pekee inaua karibu watu milioni 10 kila mwaka.Kuongeza dawa mpya za saratani kama pembrolizumab na atezolizumab, ambazo zinasaidia kinga ya mwili kushambulia chembe chembe za saratani, kunaleta matumaini mapya hasa kwa wagonjwa katika nchi zenye rasilimali chache.Kwa upande mwingine, dawa za kundi la GLP-1 receptor agonists kama semaglutide na tirzepatide zimeingizwa kwenye orodha ili kusaidia wagonjwa wa kisukari cha aina ya pili wanaoishi pia na unene uliopitiliza au matatizo ya moyo na figo. Dawa hizi husaidia kudhibiti sukari, kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na figo, na pia kusaidia kupunguza uzito. 
    4 min
  • Wanavyosema wadau kuhusu Siku ya kujua kusoma na kuandika katika zama za kidijitali
    Ikiwa leo tarehe 8 Septemba ni siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika ambapo Umoja wa Mataifa ulianzisha siku hii ili kuwakumbusha watunga sera, walimu, wadau wa elimu, na jamii juu ya umuhimu wa ujuzi wa kusoma na kuandika katika kujenga jamii yenye elimu, haki, amani na endelevu,  Sabrina Saidi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anaiangazia kauli mbiu ya mwaka huu  "Kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika katika zama za kidijitali" akiwashirikisha baadhi ya wadau wa elimu nchini Tanzania.Amezungumza na baadhi ya wadau kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, SAUT kilichoko jijini Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania.Dismas Nziku ni mwalimu wa masomo ya Biashara na Ujasiriamali  anazungumza kuhusu ni kwa jinsi gani ufundishaji wa zama hizi za kidijitali unavyochochea na kukuza ujuzi wa kusoma na kuandika. "Kwenye dunia ya sasa ujuzi wa kusoma na kuandika kidijitali ni msingi mkubwa kwa mwanafunzi, na miongoni mwa juzi hizi muhimu ni kama vile kujua kutumia vifaa vya kidijitali kama kompyuta, simu janja kwa ajili ya kujisomea na kutafuta maarifa, lakini pia kama mwalimu ninawafundisha wanafunzi kwa njia ya vitendo,kuandaa maswali ya utafiti kwa kutumia internet,kufanya kazi na kufanya kazi ya kikundi mitandaoni."Kuhusu umuhimu wa siku hii kwake na inachangia vipi katika kukuza uelewa wa umuhimu wa kusoma na kuandika shuleni na katika jamii Mwalimu Nziku amesema, "Siku ya Kimataifa ya kujua kusoma na kuandika ni kumbusho muhimu kwamba elimu ni haki ya msingi, na ni msingi wa maendeleo kwa kila mmoja kujua kusoma na kuandika hasa hasa kidijitali, inanipa hamasa kama mwalimu kuendelea kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kusoma na kuandika si kwa ajili ya mitihani tu, bali kwa maisha yao ya kila siku."Didas Karoli ni mwanafunzi katika chuo hicho cha SAUT akisoma shahada ya kwanza ya Mawasiliano kwa Umma, ameeleza kuhusu siku hii na jinsi maendeleo ya kidijitali yanavyochagiza katika kujifunza kwake akisema "Zana za kidijitali zimebadilisha sana upeo wangu katika suala la kujifunza,kutokana na zamani nilikuwa nategemea vitabu lakini hivi sasa natumia tu smartphone au kompyuta na kutengeneza notisi zangu mwenyewe za kujifunzia.Siku ya hii ya kujua kusoma na kuandika ni siku ambayo ni muhimu inafanya watu waweze kujua umuhimu wa kusoma na kuandika."
    3 min
  • Lacroix: Heko MONUSCO na FARDC kwa kulinda raia na kupunguza ghasia za makundi yenye silaha
    Huko Bunia, jimboni Ituri Mashariki Mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC,  Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix, amepongeza juhudi za pamoja za walinda amani wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO na jeshi la serikali ya Congo, FARDC, katika juhudi za kulinda raia na kupunguza ghasia za makundi yenye silaha.Akizungumza wakati wa ziara yake iliyoanza Septemba 6, Mashariki mwa DRC katika jimbo la Ituri Lacroix amesema ushirikiano na kuaminiana kati ya mamlaka za jimbo la Ituri na vikosi vya Umoja wa Mataifa ni msingi muhimu wa kurejesha amani.Anasema “Nipo katika eneo liitwalo Fataki, katika jimbo la Ituri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na hapa kuna kambi ya MONUSCO yenye kikosi cha Nepal, pamoja na kambi ya wakimbizi wa ndani. Maelfu ya watu wanalindwa hapa na wenzetu wa MONUSCO, na wanapatiwa msaada wa kibinadamu pamoja na ulinzi.”Gavana wa Ituri, Jenerali Johnny Luboya, alikaribisha msaada wa MONUSCO katika operesheni za kijeshi na mazungumzo ya amani, yakiwemo dhidi ya kundi la CRP katika eneo la Djugu Ituri ambako mamia ya maelfu ya wakimbizi wa ndani sasa wananufaika na ulinzi wa pamoja wa FARDC na walinda amani wa Umoja wa Mataifa. Lacroix amesema “Katika jimbo la Ituri pekee kuna makambi kadhaa ya wakimbizi wa ndani, ambayo yanalindwa na MONUSCO, ambapo makumi ya maelfu kwa hakika mamia ya maelfu ya watu wanalindwa na wenzetu wa MONUSCO na wanapatiwa msaada.”Mkuu huyo wa operesheni za ulinzi wa amani ameohitimisha kwa kusema ziara hii ni muhimu sana kwani “Nipo hapa kuonyesha kile ambacho MONUSCO hufanya kila siku, tofauti ambayo MONUSCO inaleta katika kuwalinda raia hawa, tofauti kati ya kuwa salama au kuwa katika hatari kubwa, na nilitaka pia kutoa shukrani zangu kwa wenzetu wa MONUSCO. Aidha, nilitaka kuwasikiliza wananchi, hawa wakimbizi wa ndani, pamoja na jamii, na kuona namna ambavyo tunaweza kushirikiana nao zaidi ili kuboresha hali na kupiga hatua katika kukabiliana na ghasia ambazo bado zinaendelea katika eneo hilo.”Baada ya zira yake jimboni Itari Lacrix ameelekea katika mji Mkuu Kinshasa ambako amekutana na na kuzungumza na maafisa wa serikali.
    3 min
  • 08 SEPTEMBA 2025
    Heko MONUSCO na FARDC kwa kulinda raia na kupunguza ghasia za makundi yenye silaha: LacroixSiku ya kimataifa ya kujua kusoma na kuandika.WHO yatoa orodha ya dawa muhimu duniani.
    10 min
  • MINUSCA washiriki kutoa elimu ya usalama barabarani CAR
    Kila mwaka,Wizara ya Uchukuzi na Usafirishaji wa Anga nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR,  kwa msaada wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MINUSCA,huandaa kampeni za usalama barabarani. Na hivi karibuni katika mji mkuu wa nchi hiyo,Bangui, MINUSCA kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya Ndani ISF wameungana kupambana na ajali za barabarani zinazoongezeka kila uchao,doria ya pamoja imefanyika kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara. Sabrina Saidi anatujuza zaidi....​(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Natts ....ongeza hii; katikaa mitaa ya Banguimji mji mkuu wa CAR pisha nikupishe ni nyingi. Kufuatia ongezeko la ajali za barabarani,zinazopoteza maisha ya watu kila uchao, kikosi cha polisi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MINUSCA kimeendesha doria ya pamoja ya usalama kwa kushirikiana na Vikosi vya Usalama vya nchi hii (ISF) katika mji mkuu BanguiOperesheni hii iliyofanyika tarehe 4 mwezi Septemba,mwaka huu imelenga kutoa elimu kwa waendesha pikipiki za abiria maarufu kama "moto taxi" nchini CAR na watumiaji wengine wa barabara kuhusu umuhimu wa kufuata sheria za barabarani.Kwa mujibu wa MINUSCA Hatua hii ina lengo la kuimarisha usalama na kujenga uhusiano mwema kati ya vikosi vya usalama na raia.​Akizungumza kuhusu umuhimu wa hatua hii, Kamanda wa Mkoa wa Plateaux(PLATIU) na Bas-Oubangui(BA OBANGI), Douflé Avi Chico( DOFLE AVII CHIKO BERNAA) Bernard, amesema,CUT- Sauti ya Douflé Avi Chico Bernard“Kwa kushirikiana na MINUSCA, kupitia brigedi yao ya magari, tunafanya kazi ya kuongeza uelewa kwa watumiaji wa barabara, waendesha pikipiki au teksi, ili kupunguza ajali nyingi ambazo kwa bahati mbaya zinagharimu maisha ya watu. Tutaendelea na kampeni hizi kubwa ili kurekebisha hali hii.”​Kwa upande wa watumiaji wa barabara, dereva wa pikipiki za abiria, Jean Terence Bokassa (JANI TEREE BOKASA), ameomba serikali iimarishe udhibiti wa sekta hiyo.CUT- Sauti ya Jean Terence Bokassa“Tunaomba serikali ihakikishe usalama wa waendesha pikipiki za abiria kwa sababu sisi ni watu kama wengine. Tunatoka nje kutafuta riziki, lakini maisha yetu yako hatarini. Tungependa serikali itusaidie kwa kuwafundisha ndugu zetu ambao hawana leseni ya udereva kanuni za barabarani ili kuhakikisha usalama wao.”Nattss.. Sauti za magari honi nk.​Doria hii ya pamoja inaonesha ushirikiano mzuri kati ya Polisi wa Umoja wa Mataifa na ISF, wote wakiwa wamejitolea kulinda raia na kupunguza ajali za barabarani na MINUSCA inasema wananchi wakipata uelewa wa kutosha basio sio tu barabara zitakuwa salama bali pia idadi ya vifo vitokanavyo na ajali za barabarani vitapungua.
    3 min
  • UNICEF: Mateso kwa watoto wa Gaza ni bayana
    Sasa twende Gaza, hii ni hadithi ya maisha, ya watoto wa Gaza wanaokabiliana na baa la njaa, hofu, na kuporomoka kwa kila kitu kinachowaweka hai. Ni hadithi inayoelezwa kupitia macho ya wale wanaoshuhudia mateso kila siku wakiwemo madaktari, akina mama, na wahudumu wa kibinadamu wanaopiga kengele ya tahadhari. Miongoni mwa wahudumu hao ni Tess Ingram afisa mawasiliano wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ofisi ya Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Flora Nducha anasimulia alichokishudia(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Tess aliyefunga safari na kushuhudia hali halisi Gaza akizungumza na waandishi wa habari kutoka mji wa Al Mawasi amesema mwenye macho haambiwi tazama na alichokishuhudia ni cha kutisha kwani jiji hilo sasa linazidi kuzama kwenye lindi la baa la njaa, vituo vya lishe vimefungwa, familia zinalia na kuhaha na watoto wanakufa kila uchao bila msaada.(Tess Ingram- Sheillah)“Jiji la Gaza, kimbilio la mwisho kwa familia za Kaskazini, linakuwa mahali ambapo utoto hauwezi kuishi. Ni jiji la hofu, wakimbizi na mazishi.”Anasema zaidi ya nusu ya vituo vya lishe vya watoto vimefungwa na kina mama wanapofika hospitalini wakiwa wamebeba watoto wao unaoweza kuhesabu mbavu sababu ya kukonda wanaambulia patupu kwani msaada ni haba na kwengine hakuna kabisa.(Tess Ingram 2-Sheilah):“Kilichokuwa hakifikiriki si jambo lijalo ni hali ambayo iko hapa tayari. Kuanguka kwa huduma muhimu na kunawaacha watoto wasiojiweza Gaza wakihaha kusalia uhai.”Tess anasema ukiingia katika vituo vya msaada ndio utatambua wanachokipitia watoto wa Gaza kwani, mateso yanaonekana bayana(Tess Ingram 3-Sheillah)“Saa moja tu ndani ya kliniki ya lishe inatosha kuondoa shaka na shuku yoyote uliyonayo ya endapo Gaza kuna baa la njaa.”UNICEF inasisitiza wito wake kuwa raia walindwe, msaada wa chakula na dawa upelekwe kwa wahitaji bila vizuizi. Kwa sababu watoto wa Gaza bado wako hai na dunia ina uwezo wa kuamua endapo wasalie hai.
    3 min
  • WMO: Ubora wa hewa duniani wazidi kuzorota japo kuna nafuu Asia na Ulaya
    Wakati mabilioni ya watu wakiendelea kuvuta hewa chafu inayosababisha zaidi ya vifo vya mapema milioni 4.5 kila mwaka, wataalamu wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa leo Ijumaa (5 Septemba) wamebainisha madhara ya chembe ndogo ndogo za moshi kutoka katika moto wa nyika ambazo husafiri umbali mrefu duniani kote. Philip Mwihava na maelezo zaidi.(Taarifa ya Mwihava)“Ubora wa hewa hauheshimu mipaka,” anasema Lorenzo Labrador, Afisa wa Kisayansi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani (WMO). Anaendelea kueleza kwamba, “moshi na uchafuzi unaotokana na moto wa nyika katika msimu huu wa kihistoria katika Rasi ya Iberia tayari umepatikana Ulaya Magharibi, kwa hiyo athari zake hazibaki tu kwenye Rasi ya Iberia, bali zinaweza kusambaa kote barani Ulaya.”Akiwasilisha taarifa ya WMO kuhusu Hewa Safi na Tabianchi, ambayo inakusanya data kutoka vyanzo mbalimbali vya kimataifa, leo jijini Geneva, Uswisi Bwana Labrador ametangaza mwendelezo wa mwenendo wa kuzorota kwa ubora wa hewa duniani.Ameonyesha ramani ya dunia ya mwaka 2024 iliyoonesha alama za chembechembe ndogo zinazojulikana kama “PM 2.5” kutokana na moto wa nyika, zikionekana kwa alama nyekundu kwenye maeneo ya Chile, Brazil na Ecuador, pamoja na Canada, Afrika ya Kati na Siberia. Takwimu hizo zinathibitisha mwenendo wa kuendelea kwa kuzorota kwa ubora wa hewa duniani kama ilivyoonekana katika miaka iliyopita.Kwa upande wa habari njema, mwanasayansi huyo wa WMO amesisitiza kupungua kwa uzalishaji wa hewa chafuzi katika baadhi ya maeneo ya dunia.(Sauti ya Labrador) - sauti ya kiume“Tunaona mwenendo wa kuzorota kwa ubora wa hewa hasa kwa kuhusiana na PM 2.5, na pia tunaona kupungua kwa uzalishaji wa hewa chafuzi katika maeneo fulani ya dunia, hasa mashariki mwa China na Ulaya, mwaka baada ya mwaka.”Mfano mzuri uliotolewa katika taarifa ya leo mashariki mwa China, katika miji kama Shanghai, ambako kumepigwa hatua katika kuboresha ubora wa hewa kwa kufungua bustani zaidi na kupanda miti mingi. Na ingawa bado kuna msongamano mkubwa wa magari, mengi sasa ni ya umeme.Hata hivyo WMO inasema licha ya mafanikio hayo, miji michache tu duniani ina viwango vya ubora wa hewa chini ya vile vinavyopendekezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO). Hii inamaanisha kuwa, licha ya maboresho ya karibuni, ubora wa hewa bado ni changamoto kubwa kwa afya ya umma.Umoja wa Mataifa unaongoza juhudi za kupambana na uchafuzi wa hewa majumbani ambao ni mojawapo ya vitisho vikubwa zaidi kwa afya ya umma duniani na hasa ni hatari kwa watoto.
    3 min
  • 05 SEPTEMBA 2025
    Karibu kusikiliza jarida la Habari za Umoja wa Mataifa ambapo leo tunakuletea taarifa kuhusu hali ya hewa na athari za moto wa nyika, tutaelekea Gaza kusikia kutoka kwa mashuhuda wa madhila wayapatayo watoto na wananchi wa Gaza na kisha tutaelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako wanaendesha mafunzo ya usalama barabarani. 
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners