Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 29 AGOSTI 2025
    Jaridani leo tunaangazia Majaribio ya Nyuklia, na machafuko nchini Sudan Kusini. Makala tunakwenda nchini Nepal na mashinani tunasalia huko huko Sudana Kusini, kulikoni?Dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa yakupinga Majaribio ya Nyuklia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa onyo kali kuhusu kuongezeka kwa hatari za nyuklia kufuatia mvutano wa kisiasa unaondelea duniani na amehimiza kuridhiwa kwa mkataba wa kupiga marufuku majaribio hayo ya kinyuklia.Maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao huko Tambura, jimbo la Equatoria Magharibi, tangu ghasia zilipozuka upya mwaka 2021 nchini Sudan Kusini. Hadi leo, wengi wao bado wanaishi kambini bila chakula cha uhakika, huduma za afya wala usalama huku wanawake na watoto wakibeba mzigo mkubwa zaidi wa mateso hayo.Makala tunakwenda nchini Nepal kumulika suala la waume kwenda kusaka ajira nje ya nchi na kuacha wake zao wakihaha kukimu familia zao katika mazingira ambamo wanawake wanakuwa hawana uthabiti wa kiuchumi limeanza kupatiwa muarobaoni.Na katika mashinani fursa ni yake Anna Pita, Msimamizi wa hospitali ya Kator nchini Sudan Kusini akieleza ni kwa jinsi gani mifumo ya nishati ya jua iliyofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP na wadau wake inabadilisha utoaji wa huduma katika hospitali na vituo vya afya nchini humo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Wanawake wa Tambura Sudan Kusini: Tumechoshwa na mzunguko wa vita tunachotaka ni amani
    Maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao huko Tambura, jimbo la Equatoria Magharibi, tangu ghasia zilipozuka upya mwaka 2021 nchini Sudan Kusini. Hadi leo, wengi wao bado wanaishi kambini bila chakula cha uhakika, huduma za afya wala usalama huku wanawake na watoto wakibeba mzigo mkubwa zaidi wa mateso hayo. Kupitia video ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNIMSS Flora Nducha anamulika kauli za baadhi ya wanawake waathirika wanaosihi katika kambi ya wakimbizi wa ndani.
    4 min
  • Maji ni Uti wa mgongo kwa jamii kote duniani - Stephen Tai
    Wiki ya Maji ikifikia tamati leo Agosti 28 na maudhui yakiwa Maji kwa ajili ya Hatua kwa Tabianchi, tunabisha hodi kaunti ya Kajiado nchini Kenya kumsikia mtendaji kwenye mradi wa maji wa Kerarapon Water Association  ambalo ni shirika la kijamii linalohusika na maji na mazingira huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Mtendaji huyo anayeanza kwa kujitambulisha, anazungumza na Kelvin Keitany wa radio washirika Radio Domus nchini Kenya.
    6 min
  • 28 AGOSTI 2025
    Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina, wiki ya Maji ikifikia tamati leo Agosti 28 na maudhui yakiwa Maji kwa ajili ya Hatua kwa Tabianchi, tunabisha hodi kaunti ya Kajiado nchini Kenya kumsikia mtendaji kwenye mradi wa maji wa Kerarapon Water Association  ambalo ni shirika la kijamii linalohusika na maji na mazingira huko kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Mengine ni kama yafuatayo.Ukraine ambapo leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameungama na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kulaani vikali mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani droni yaliyofanywa na Urusi usiku kucha kuamkila dhidi ya miji ya Ukraine na kusababisha vifo na majeruhi kwa raia, wakiwemo watoto, na pia kuharibu majengo ya kidiplomasia jijini Kyiv. Amesisitiza kuwa mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu yao yanakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu, akitaka yakome mara moja na kurudia wito wake wa kusitisha mapigano ili kuelekea amani ya kudumu itakayoheshimu uhuru wa watu, uhuru wa kitaifa na mipaka ya Ukraine kama inavyotambuliwa kimataifa.Kuhusu Mashariki ya Kati Katibu Mkuu António Guterres akizungumza na waandishi wa Habari hii leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa      ameonya kuwa operesheni za kijeshi mjini Gaza zitakuwa na zahma kubwa na amesisitiza “hili lazima likome.” Amesema njaa si tishio tena bali janga la sasa, huku raia, wahudumu wa afya na waandishi wa habari wakiuawa  wakati “macho ya dunia yakitazama.” Guterres ameikumbusha Israel wajibu wake wa kisheria kulinda raia na kuruhusu msaada wa kibinadamu bila vikwazo akisema “Hakuna visingizio tena. Hakuna vizuizi tena. Hakuna uongo tena,”  akitoa wito wa usitishaji mapigano haraka na kuachiliwa kwa mateka wote.Kikosi cha 11 cha Tanzania TANZBATT 11 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO kimetoa msaada wa magodoro kwa raia walioathirika na machafuko ya karibuni katika kijiji Oicha  jimboni Kivu Kaskazini. Miongoni mwao ni Bi Masika Jistine na Mzee Bahati Paluku ambao hawakusita kuonesha furaha yao.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWIJI!.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Mradi wa MONUSCO kwa ushirikiano na PAMI waleta nuru kwa wakazi Nyiragongo, DRC
    Kwa zaidi ya muongo mmoja, eneo la Nyiragongo lililoko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) limekumbwa na hali ya kutokuwepo kwa utulivu wa kudumu kutokana na uwepo wa makundi yenye silaha. Maelfu ya familia wamekimbia makazi yao na watoto wengi kulazimishwa kujiunga na makundi hayo ya kijeshi. Kati ya mwaka 2024 na 2025, kuzuka upya kwa mapigano kunakohusishwa na kuibuka tena kwa waasi wa M23 kumeongeza zaidi hali ya hatari kwa wakazi wa eneo hilo, hasa watoto na vijana. Ili kuleta ahueni kwa wakazi, Umoja wa Mataifa umechukua hatua. Je ni zipi hizo? Ungana basi na Anold Kayanda kwenye makala hii.
    5 min
  • Afisa wa UN ajionea jinsi Tanzania 'inafunda' waendao kwenye operesheni za ulinzi wa amani
    Mratibu Maalum wa Kuboresha Hatua za Umoja wa Mataifa dhidi ya Unyanyasaji wa kingono (SEA) Christian Saunders amefanya ziara nchini Tanzania kuona maandalizi ya vikosi vya operesheni za ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania, Kapteni Mwijage Inyoma Afisa Habari wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) ametuandalia taarifa hii.Ni bendi ya jeshi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ ikiongoza askari wengine kumkaribisha Bwana Christian Saunders hapa katika Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) Kunduchi, Dar es Salaam.Miongoni mwa askari hawa tayari wameandaliwa kwenda katika nchi mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hata nje ili kuusaidia Umoja wa Mataifa kutekeleza moja ya majukumu yake kwa ulimwengu, kuleta na kuitunza amani.Bwana Saunders anasema, “wacha nianze kwa kusema asante. Kusema asante ni jambo muhimu sana, kwa sababu mko tayari kuanza jukumu la kutumwa, iwe mnaenda Lebanon au Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo au kwingineko. Mkiwa mbali na familia zenu, mbali na nchi yenu, katika mazingira yenye changamoto, na wakati mwingine katika hali hatarishi.”Anawapa moyo zaidi askari lakini akiwakumbusha kuwa wao ni kioo cha ulimwengu wazingatie maadili“Na tunathamini sana kujitolea kwenu. Tunathamini sana kwamba mnaenda kuwasaidia ndugu zenu katika nchi nyingine, iwe ni nchi jirani au sehemu iliyo mbali. Mnapokwenda, mnaliwakilisha dunia. Mnawakilisha watu wa dunia.”Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC), Brigedia Jenerali George Itang’are akamthibitishia mgeni kwamba askari hawa wameiva na hakuna kisingizio chochote cha kutozingatia maadili huko wameandako, kisha akawahoji, Nao wanajibu, “twende pamoja, turudi pamoja.” 
    3 min
  • 27 AGOSTI 2025
    Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika maadhimisho ya siku ya Ziwa duniani; Maandalizi ya walinda amani kwenda kuhudumu CAR ma DRC; Msaada wa MONUSCO kwa wakazi wa Kivu Kaskazini; Aliyerejesha fadhila kwa WFP.Leo ni maadhimisho ya kwanza ya siku ya Ziwa Duniani yakibeba maudhui "Ziwa ni uti wa mgongo wa sayari yetu" na ili kuthibitisha hilo tunakupeleka  Mwanza Kaskazini Magharibi mwa Tanzania ambako , Bosco Cosmas kutoka Radio washirika SAUT FM anamulika maoni ya wananchi ni kwa vipi ziwa Victoria limekuwa msaada na mkombozi kwao.Mratibu Maalum wa Kuboresha Hatua za Umoja wa Mataifa dhidi ya Unyanyasaji wa kingono (SEA) Christian Saunders amefanya ziara nchini Tanzania kuona maandalizi ya vikosi vya operesheni za ulinzi wa amani katika maeneo mbalimbali duniani. Kutoka Dar es Salaam, Tanzania, Kapteni Mwijage Inyoma Afisa Habari wa Chuo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) ametuandalia taarifa hii.Anold Kayanda anatupeleka eneo la Maziwa Makuu barani Afrika kusikia harakati za Umoja wa Mataifa kuinua wakazi waliokumbwa kwenye mizozo.Mashinani kutana na Moses Komakech Meneja wa ghala la chakula la shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP lililoko Gulu katika jimbo la Acholi Kaskazini mwa Uganda ambapo baada ya kuwa mnufaika wa mgao wa chakula wa WFP, sasa anaendesha ghala la shirika hilo linalohudumia wakimbizi 800,000.
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners