Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 20 AGOSTI 2025
    Jaridani leo tunaangazia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, na hali ya kibinadamu Gaza na majeraha kwa wenyeji. Makala tunaangazia ukatili wa kingono na mashinani tunakwenda Sudan kumulika jinsi wanavyokabiliwa na unyanyasaji huo wa kingono.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema Afrika inahitaji mageuzi makubwa ya Baraza la Usalama na mfumo wa kimataifa wa fedha ili kufanikisha maendeleo yake na nafasi yake duniani. Akihutubia mkutano wa tisa wa maendeleo ya Afrika TICAD IX nchini Japan, Guterres ameweka vipaumbele vitano.Maelfu ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ambao wamepoteza viungo vyao vya mwili na wanakabiliwa na hali mbaya ya maisha na matatizo makubwa ya kiafya kutokana na ukosefu wa huduma bora za matibabu na viungo bandia wanazohitaji sana.Tunakuletea makala yenye kugusa maisha ya maelfu ya watu kote duniani, ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 19 Agosti limekutana jijini New York Marekani kujadili hali hii inayozidi kuongezeka, na kushuhudia jinsi waathirika wanavyobaki bila msaada wa kutosha kutokana na ukosefu wa rasilimali. Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa na Mwakilishi wake imeonesha ongezeko kubwa la kesi za ukatili wa kingono, jambo linaloibua maswali makubwa kuhusu uwajibikaji na huduma kwa manusura.Na katika mashinani Mwanzilishi na mratibu wa Kundi la Utetezi la Darfur, Ikhlass Ahmed amelielezea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jijini New York kwa njia ya video jinsi wanavyokabiliwa na kuenea kwa kasi kwa unyanyasaji wa kingono.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • 19 AGOSTI 2025
    Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika umuhimu wa wahisani. Pia tunaangazia siku ya Wahudumu wa Kibinadamu Duniani tukikuletea ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaomulika haki zao, na hali ya usalama nchini DRC.Leo ni Siku ya Wahudumu wa Kibinadamu Duniani na Umoja wa Mataifa unasema mwaka 2024 ulikuwa mbaya zaidi, baada ya wahudumu 383 kuuawa kote duniani, hasa Gaza na Sudan. Mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, amesema “Hata shambulio moja dhidi ya mhudumu wa misaada ni shambulio dhidi yeto sote.” Naye Katibu Mkuu António Guterres ameongeza kuwa “Shambulio dhidi ya wahudumu wa misaada ni shambulio dhidi ya ubinadamu hebu tuchukue hatua kwa ajili ya ubinadamu.Huko Geneva Katika hafla maalum ya kuadhimisha siku hii, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Volker Türk, amewakumbuka waliopoteza maisha, wakiwemo wahudumu 22 waliouawa Baghdad mwaka 2003, na kuongeza “Kamwe hatutaacha kusisitiza kwamba serikali au nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wafanye kazi pamoja kuhakikisha wanatoa fursa ya ufikiaji wa kibinadamu kwa watuwenye uhitaji na kunakuwepo na uwajibikaji wa ukiukwaji mkubwa wa sheria za kibinadamu zikijumuisha ulinzi kwa wahudumu wa kibinadamu na wa Umoja wa Mataifa”.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, leo umelaani vikali mashambulizi ya kundi la waasi wa Allied Democratic Forces, ADF kati ya tarehe 9 na 16 Agosti, katika maeneo ya Beni na Lubero, mkoa wa Kivu Kaskazini, yaliyoua raia 52, wakiwemo wanawake na watoto. Mashambulizi hayo yamehusisha utekaji nyara, uporaji, na uchomaji wa nyumba na magari, na kuwaacha wakazi ambao tayari wako katika hali ngumu ya kibinadamu katika mateso zaidi.Na katika mashinani na ikiwa leo ni siku ya wahudumu wa binadamu, huduma na kujitolea kwa wanachama 270 wa Kikozi cha Polisi cha walinda amani kutoka Ghana wanaohudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), wakiwemo maafisa wanawake 63, ilitambuliwa kwa kutunukiwa Nishani ya Umoja wa Mataifa ya Heshima kwa juhudi zao, zikiwa ni pamoja na kuwalinda raia, kuwezesha uwasilishaji salama wa misaada ya kibinadamu, kukuza haki za binadamu na kujenga amani. Bismark Achaab, Msimamizi Mkuu wa Kitengo hicho anatoa shukrani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • Gaza ni tishio lililo kimya - Dkt. Younis
    Umoja wa Mataifa umetenga siku maalum ya kuwashukuru watoa huduma za misaada ya kibinadamu na siku hiyo ni Agosti 19 kila mwaka. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu zinaeleza kuwa mwaka huu wa 2025, watu milioni 305.1 kutoka nchi 72 wanahitaji usaidizi wa kibinadamu ambao utagharibu dola bilioni 47.4. Takwimu hizi zinaonesha umuhimu na uhitaji wa watoa huduma wa kibinadamu.Kuelekeza maadhimisho hayo hapo kesho Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masual ya Watoto UNICEF limetengeneza makala inayoangazia watoa huduma wa misaada ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kimabavu na Israel. Leah Mushi anatujuza kilichopo katika makala hiyo. 
    4 min
  • 18 AGOSTI 2025
    Jaridani leo tunaangazia amani na usalama nchini Ukraine, na ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini. Makala tunaangaazia wahudumu wa kibinadamu Gaza, na mashinani tunamulika afya kwa wanawake wajawazito nchini Tanzani.Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Urusi nchini Ukraine yaliyofanyika usiku kucha, ikiwemo katika miji ya Kharkiv na Zaporizhzhia, yameripotiwa kuua watu 10 wakiwemo watoto watatu, kwa mujibu wa  taarifa  ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa leo.Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la ajira, ILO na mfuko wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD yanatekeleza mradi wa ProAgro YOUTH unaolenga kuongeza ajira kwa vijana katika sekta ya biashara ya kilimo vijijini.Makala Umoja wa Mataifa umetenga siku maalum ya kuwashukuru watoa huduma za misaada ya kibinadamu na siku hiyo ni Agosti 19 kila mwaka. Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu zinaeleza kuwa mwaka huu wa 2025, watu milioni 305.1 kutoka nchi 72 wanahitaji usaidizi wa kibinadamu ambao utagharibu dola bilioni 47.4. Takwimu hizi zinaonesha umuhimu na uhitaji wa watoa huduma wa kibinadamu.Na katika mashinani nampisha Mchanga Omari Kombo kutoka Pemba Zanzibar ambaye ni mnufaika wa mpango mpya wa afya ya uzazi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watotot UNICEF na wadau wake umewasaidia wanawake wajawazito kama kuondokana na upungufu wa damu na kujifungua watoto wenye afya njema.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Kutoka kufanya kazi za ndani hadi kumiliki kampuni ya usafi wa mazingira
    Kutana na Godlove Makunge, kijana huyu wa kitanzania ambaye safari ya maisha  yake imedhihirisha kuwa chochote unachoweka nia na utashi kitafanikiwa. Godlove ambaye elimu yake ni ya kidato cha nne, hakuweza kuendelea na masomo zaidi. Alichukuliwa na mtu mmoja afanye kazi za ndani kutoka Morogoro hadi Lindi na kisha akaishia Mtwara, kusini-mashariki mwa Tanzania ambako huko aliona fursa ya kujipatia kipato kutokana na taka zilizokuwa zinasambaa mitaani. Aliasisi kampuni ya usafi na mazingira iitwayo Shikamana Investment. Sasa kampuni yao ya ubia imeajiri vijana 6. Alishiriki mafunzo ya uchumi rejeleshi yaliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP mkoani Mtwara. Sawiche Wamunza, Sawiche Wamunza Mtaalamu wa Mawasiliano ya Kimkakati UNDP alizungumza na Bwana Makunge baada ya mafunzo hayo ili afahamu amejifunza nini.
    5 min
  • Mazungumzo kuhusu mustakabali wa plastiki yaahirishwa bila muafaka
    Siku 10 za mkutano wa Kamati ya Kimataifa ya Majadiliano (INC) ya kuandaa Mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, ikiwemo katika mazingira ya bahari, zimemalizika huko Geneva, USwisi bila muafaka kwenye nyaraka tarajiwa, ambapo mkutano umeahirishwa hadi tarehe itakayotangazwa baadaye. Sabrina Said ana taarifa zaidi. 
    2 min
  • 15 AGOSTI 2025
    Jaridani leo tunaangazia mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, na vidokezo vya malezi salama ya watoto. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Chad, kulikoni?Siku 10 za mkutano wa Kamati ya Kimataifa ya Majadiliano (INC) ya kuandaa Mkataba wa Kimataifa wenye nguvu kisheria kuhusu uchafuzi wa plastiki, ikiwemo katika mazingira ya bahari, zimemalizika huko Geneva, Uswisi bila muafaka kwenye nyaraka tarajiwa, ambapo mkutano umeahirishwa hadi tarehe itakayotangazwa baadaye.Kuwa mzazi si rahisi kila wakati, lakini usaidizi unaofaa unaweza kuleta mabadiliko ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limekuwa likiendesha mafunzo kwa wazazi juu ya namna bora za kulea watoto. Alinune Nsemwa ambaye ni  mtaalamu wa masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kutoka UNICEF nchini Tanzania ameeleza vidokezo vitatu muhimu vya kuwalea watoto ambavyo vinaweza kuleta utofauti mkubwa.Makala ninakukutanisha na Sawiche Wamunza Mtaalamu wa Mawasiliano ya Kimkakati wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini Tanzania ambaye baada ya mafunzo ya siku tatu ya uchumi rejeleshi katika mkoa wa Mtwara, Kusini-Mashariki mwa Tanzania alizungumza na Godlove Makunge Muasisi na Mkurugenzi wa kampuni ya kuzoa taka na usafi wa mazingira, iitwayo Shikamana Investment. Bwana Makunge anaanza kwa kuelezea mtazamo wa jamii kwake baada ya kuamua kuanza kuzoa taka.Na katika Radwa Ahmed, Mkimbizi kutoka Sudan ambaye alianza kwa kuoka mikate kwa ajili ya familia yake, na kwa ufadhili wa shirika la Umoja wakimbizi Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, ameweza kuigeuza talanta yake kuwa biashara ya kuuza mikate na kuajiri wakimbizi wenzake.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners