Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 11 AGOSTI 2025
    Jaridani leo tunaangazia waandishi wa habari waliouawa katika ukanda wa Gaza, na wakimbizi wa Burundi huko Tanzania. Makala inamulika maendeleo na ustawi kwa wakimbizi Kakuma nchini Kenya na mashinani inatupeleka katika kaunti ya Tana River nchini humo, kulikoni?Kufuatia kuuawa kwa waandishi sita wa habari huko Gaza, viongozi wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wamekosoa vikali shambulio hilo lililotekelezwa na majeshi ya Israel usiku wa kuamkia leo.Moja ya changamoto kubwa wanazokutana nazo wakimbizi pale wanapokaa nchi waliyopatiwa uhifadhi kwa muda mrefu ni kukosa nyaraka muhimu za utambulisho. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wakimbizi UNHCR limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanapata suluhu ya changamoto hii. Makala inamulika mnufaika wa Jamii Biashara ambalo ni jukwaa la mtandaoni la masoko lililobuniwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, (ILO) na Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda Kenya, (KNCCI). Jukwaa hili limefungua fursa kwa wakimbizi wanaoshughulika na biashara ndogo ndogo ili kujikimu maisha katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Assumpta Massoi ndiye mwenyeji wako kupitia video ya ILO.Na katika mashinani fursa ni yake Mariam Kazungu kutoka Kaunti ya Tana River nchini Kenya, ambaye anasema Watoto wake wamenufaika kupitia mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa utoaji wa chanjo dhidi ya homa ya tumbo na ugonjwa wa surua.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Ajira ngumu usichague kazi, chupa ni mali - Hauwa
    Huko mkoani Mtwara, kusini mwa Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limeendesha warsha ya siku tatu ya mashauriano kuhusu uchumi rejeshi ili pamoja na mambo mengine kuelimisha vikundi vya wanawake na vijana kuhusu utunzaji wa mazingira na urejelezaji wa taka. Sawiche Wamunza, Mtaalamu wa Mawasiliano UNDP nchini Tanzania amezungumza na mmoja wa washiriki ili kufahamu alichoondoka nacho.
    4 min
  • 08 AGOSTI 2025
    Jaridani leo tunaangazia amani na usalama katika ukanda wa Gaza, na mradi wa mlo shuleni unaowezesha watoto kuendelea na masomo nchini Uganda. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo, ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mpango wa Serikali ya Israel kutwaa kijeshi ukanda wote wa Gaza unaokaliwa kimabavu.Mradi wa mlo shuleni unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula(WFP) nchini Uganda kwa kushirikiana na serikali  umesaiia zaidi ya watoto 255,000 kuendelea na masomo, kujifunza vizuri zaidi na kustawi. Makala inakupeleka Mtwara, kusini mwa Tanzania ambako huko shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limeendesha warsha ya siku tatu ya mashauriano kuhusu uchumi rejeshi ili pamoja na mambo mengine kuelimisha vikundi vya wanawake na vijana kuhusu utunzaji wa mazingira na urejelezaji wa taka. Sawiche Wamunza, Mtaalamu wa Mawasiliano UNDP nchini Tanzania amezungumza na mmoja wa washiriki ili kufahamu alichoondoka nacho.Na katika mashinani Patriciah Akinyi, Mwathirika wa jeraha linaloweza kuzuilika wakati wa kujifungua ambaye pia ni mnufaika wa matibabu ya upasuaji wa kurekebisha jeraha hilo la fistula nchini Kenya inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA, anasimulia kilichomkumba.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    10 min
  • 07 AGOSTI 2025
    Jaridani leo tunaangazia mada kwa kina inayokupeleka katika Hospitali hiyo kusikia wanavyolitekeleza suala la unyonyeshaji hasa kuwaelimisha akina mama wenye hofu ya kunyonyesha kutokana na changamoto zao nyingine za kiafya. Mengine ni kama yafuatayo.Ushahidi unaonesha kuwa unyanyasaji bado ni jambo la kawaida katika huduma kwa wajawazito na watoto wachanga, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, (WHO) hii leo. Mathalani katika nchi nne, utafiti umebaini kuwa zaidi ya asilimia 40 ya wajawazito walikumbana      na kauli chafu wakati wa kujifungua ili hali zaidi ya asilimia 60 walifanyiwa uchunguzi sehemu zao za siri bila idhini yao.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zisizo na bandari za baharini, LLDCs ukiendelea huko Awaza, Turkmenistan, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP limetaka kubadilika kwa fikra ya kwamba nchi hizo kama vile Rwanda na Uganda zina mkwamo wa kibiashara na maendeleo. Mwakilishi wa UNDP nchini Ethiopia Dkt. Samuel Doe akizindua mpango mpya wa kuonesha faida za nchi hizo kwa muunganiko wao kwa njia ya ardhi amesema…. hii leo LLDCs zinatumia vema uwepo wao kimkakati, katikati ya Afrika  na muunganiko wa kikanda kuwa vitovu muhimu vya kuunganisha nchi kiuchumi , biashara na ubunifu. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu leo wamesema ili kuzuia vifo zaidi na mateso kutokana na njaa huko Gaza, Israel inapaswa kurejesha mara moja ruhusa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kibinadamu kuingia bila vikwazo vyovyote eneo la Palestina inalokalia kimabavu.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga,  ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali "SAMAKI WOTE HUNUKA, WALIMSHUKU KAMBALE."Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    11 min
  • Ukame unavyobadili ratiba ya unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama
    Bado dunia ikiendelea kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, Kelvin Keitany wa Radio Washirika, Domus Radio iliyoko huko Kajiado, eneo linalokabiliwa na madhara  ya mabadiliko ya tabianchi, kama vile ukame, anamulika ni kwa jinsi gani madhara hayo yanakwamisha unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama miezi sita ya mwanzo ya uhai bila kitu chochote, Je hali iko vipi Kajiado. Kelvin Keitany na maelezo zaidi.
    3 min
  • 06 AGOSTI 2025
    Jaridani hii leo tunaangazia suala la afya katika ukand wa Gaza, na wito wito wa Umoja wa Mataifa wa kutaka kuachiliwa huru kwa mateka wa Israeli huko Gaza. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa ni siku 668 tangu Hamas ambao ni wanamgambo wa kipalestina wateke waisraeli 250 baada ya kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati, vuta nikuvute ilikuwa bayana kwenye Baraza la Usalama baada ya kikao cha dharura kuitishwa na Israeli kufuatia kuchapishwa kwa picha za mateka wawili walio hoi bin taaban.Leo tuna habari njema kutoka Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kwa mabavu na Israel huko Mashariki ya Kati, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na Umoja wa falme za Kiarabu UAE wamefanikiwa kuingiza dawa, vifaa tiba na damu salama kwa ajili ya matibabu ya wanagaza ambao wanaendelea kuteseka na madhila ya vita. Makala inakupeleka nchini Kenya, hususan kaunti ya Kajiado. Bado dunia ikiendelea kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, Kelvin Keitany wa Radio Washirika, Domus Radio iliyoko huko Kajiado, eneo linalokabiliwa na madhara  ya mabadiliko ya tabianchi, kama vile ukame, anamulika ni kwa jinsi gani madhara hayo yanakwamisha unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama miezi sita ya mwanzo ya uhai bila kitu chochote, Je hali iko vipi Kajiado.Na mashinani fursa ni yake Dkt. Beatrice mwilike, Mkunga Bingwa na Rais wa Chama cha wakunga Tanzania (TAMA) ambaye kupitia mradi unaolenga uzazi salama kwa watoto milioni 10 ifikapo 2030 lililozinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA kwa kusaidiana na serikali ya Denmark, anasema wakunga wanatumia appu na njia za kisasa zinazowapa taarifa sahihi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners