Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 05 AGOSTI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, uwekezaji kwenye mustakabali yao, kauli mbiu ya Wiki ya unyonyeshaji duniani iliyoanza tarehe Mosi mwezi huu wa Agosti na itakunja jamvi tarehe 7.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Wanawake, UN Women na la watoto, UNICEF yamewaeleza waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi kuwa hali ya njaa Sudan inazidi kuwa kali zaidi. Salvator Nkurunziza, Mwakilishi wa UN Women Sudan amesema kwamba UN Women inashauri zipewe kipaumbele kaya zinazoongozwa na wanawake, pamoja na makundi kama wanawake wajawazito, wanaonyonyesha, na wasichana balehe katika kila aina ya msaada wa chakula.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo katika ufunguzi wa Mkutano kuhusu nchi zisizo na Bahari LLDC3 unaofanyika Awaza, Turkmenistan amewasihi viongozi  kufikiria upya maendeleo kwa mataifa yasiyo na bahari akisema, “leo tunakusanyika hapa kuthibitisha ukweli kwamba jiografia haipaswi kamwe kuamua hatima ya nchi.” Tukirejea Geneva, Uswisi unakofanyika mkutano utakaweka mwelekeo wa jinsi ya kukabiliana na uchafuzi unaotokana na plastiki duniani, Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira Duniani, UNEP, ameonya kwamba, “uchafuzi wa plastiki tayari upo katika mazingira, baharini, na hata katika miili yetu. Tukizidi kuendelea kwa mwelekeo huu, dunia yote itazama katika uchafuzi wa plastiki.”Na mashinani leo tuko katika shoroba za makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambapo wageni hutoka kila pembe ya Dunia kutembelea jengo hili la kihistoria. Mwalimu Maria Rulands ni mmoja wao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    11 min
  • Raia wanaendelea kuuawa katika ukanda wa Gaza wakihaha kusaka chakula
    Simulizi za huzuni, majonzi na kukata tamaa zinaendelea kila uchao huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel hasa wakati huu ambapo raia wanaokwenda kusaka chakula wanakumbwa na mashambulizi yanayosababisha vifo. Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa uliripoti kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa na mamia kadhaa walijeruhiwa katika siku mbili pekee Wakisaka chakula. Simulizi zaidi anayo Assumpta Massoi.
    3 min
  • 04 Agosti 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na mlipuko wa kipindupingu nchini Sudan. Makala tunafuatilia ziara ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kazakhstan na mashinani tunamulika unyonyeshaji Sudan Kusini.Simulizi za huzuni, majonzi na kukata tamaa zinaendelea kila uchao huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel hasa wakati huu ambapo raia wanaokwenda kusaka chakula wanakumbwa na mashambulizi yanayosababisha vifo. Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa uliripoti kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa na mamia kadhaa walijeruhiwa katika siku mbili pekee Wakisaka chakula.Zaidi ya watoto 640,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wapo hatarini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huko Kaskazini mwa Darfur, nchini Sudan.. Katika makala Anold Kayanda anatupeleka Asia ya Kati ambako Umoja wa Mataifa na Kazakhstan wamesaini makubaliano ya Kazakhstan kuwa mwenyeji wa Kituo cha Kikanda cha Umoja wa Mataifa cha Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa ajili ya ukanda wa Asia ya Kati na Afghanistan..Na mashinani nawapisha wanafunzi wawili,Wanga pamoja na Kifaya ambao ni wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Askofu Abangite iliyopo jimbo la Yambio,kusini Magharibi mwa Sudani Kusini karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Wakizungumza na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF nchini humo wameeleza umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • IMF yatoa mtazamo mpya wa Uchumi wa dunia kwa mwaka 2025/ 2026
    Mnamo mwezi April mwaka huu Shirika la Fedha la Kimataifa IMF lilitoa makadirio na mtazamano wa uchumi wa dunia ambapo lilieleza pamoja na mambo mengine kuongezeka kwa vikwazo vya biashara kunasababisha kushuka kwa kasi kwa ukuaji wa uchumi wa dunia mwelekeo ambao ulielezwa kuathiri nchi nyingi duniani.Tarehe 29 Julai IMF ikatoa ripoti mpya, ambapo tathmini mpya ya mwelekeo wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026 ikionesha matumaini tofauti na hali ilivyoonesha miezi mitatu mitatu iliyopita. Leah Mushi amefuatilia ripoti hiyo nakutuandalia makala hii akieleza kwa kina.
    4 min
  • Ndoto ya Sahar ya kushamiri kimaisha yatwamishwa na mashambulizi ya Israeli Gaza
    Harakati za kila uchao kwa raia wa Gaza huko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli za kukimbilia chakula huku mashambulizi yakiendelea zimeendelea kusababisha vifo na majeruhi ambapo majeruhi wa hivi karibuni aliyetajwa ni Sahar, mtoto mwenye umri wa miaka 14 aliyepata ulemavu akikimbilia kupokea msaada wa chakula. Ripoti ya Selina Jerobon inayotokana na video iliyochapishwa mtandao wa X na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipaletina, UNRWA, inafafanua zaidi.
    3 min
  • 01 AGOSTI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya wakimbizi wa ndani katika ukanda wa Gaza, na mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi. Makala tunamulika mtazamo mpya wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026, na mashinani tunakwenda nchini Somalia, kulikoni.Harakati za kila uchao kwa raia wa Gaza huko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli za kukimbilia chakula huku mashambulizi yakiendelea zimeendelea kusababisha vifo na majeruhi ambapo majeruhi wa hivi karibuni aliyetajwa ni Sahar, mtoto mwenye umri wa miaka 14 aliyepata ulemavu akikimbilia kupokea msaada wa chakula.Mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi, jana Julai 31 umefika tamati baada ya siku tatu za mijadala ambazo zimezaa Azimio la kihistoria linalotoa wito wa "ushirikiano wa kimataifa ulio thabiti na wenye ufanisi zaidi" ili kuendeleza amani, haki, na ustawi. Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, (IPU), Tulia Ackson kupitia hotuba ya kufunga mkutano huo uliondaliwa kwa ushirikiano wa IPU na Umoja wa Mataifa akadokeza kilichomo katika azimio hilo. Katika makala Leah Mushi anatuletea habari njema kutoka shirika la fedha la kimataifa IMF kuhusu mtazamo mpya wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026.Na mashinani tutakupeleka nchini Ethiopia, kumulika harakati za kujikwamua kiuchumi katikati ya janga la ukame.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
    11 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners