Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UNICEF: Vidokezo muhimu vya malezi bora kwa watoto
    Kuwa mzazi si rahisi kila wakati, lakini usaidizi unaofaa unaweza kuleta mabadiliko ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limekuwa likiendesha mafunzo kwa wazazi juu ya namna bora za kulea watoto. Alinune Nsemwa ambaye ni  mtaalamu wa masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kutoka UNICEF nchini Tanzania ameeleza vidokezo vitatu muhimu vya kuwalea watoto ambavyo vinaweza kuleta utofauti mkubwa.
    2 min
  • Vijana waeleza mustakabali wa maisha yao na iwapo wangependa kuwa wazazi
    Wakati dunia ikiendelea kugubikwa na changamoto mbalimbali ikiwemo athari za mabadiliko ya tabianchi na hali mbaya za kiuchumi, vijana wamepaza sauti kueleza wasiwasi wao wa kuwa na Watoto siku za usoni. Tuungane na Leah Mushi katika Makala hii aliyotuandalia kutoka kwenye video ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA ambayo iliwahoji vijana kutaka kufahamu iwapo wangependa kuwa na Watoto kwa siku za usoni.
    3 min
  • 13 AGOSTI 2025
    Jaridani hii leo tunaangazia hakiza binadamu nchini Uganda, na mahakama ya kuhamama kwa ajili ya amani Sudan Kusini. Makala tunaangazia vijana na mpango wa wa kuwa wazazi siku zijazo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya kumulika vijana wakulima.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, (OHCHR), imesema kitendo cha kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye pamoja na mshirika wake Obeid Lutale kunyimwa dhamana mara kwa mara katika kesi inayowakabili ni jambo linalotia hofu kubwa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Mahakama ya kuhamahama iliyopelekwa katika eneo la utawala la Greater Pibor, Kaunti ya Pibor jimboni Jonglei Mashariki mwa Sudan Kusini imeleta haki na amani kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo.Makala wakati hapo jana dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya vijana duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA liliwahoji vijana iwapo wangependa kuwa na watoto hapo baadaye.Na katika mashinani fursa ni yake Emily, mwanachama wa kikundi cha vijana wakulima nchini Kenya wanaolima mbogamboga kupitia mradi uliofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP wa kilimo cha bustani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • 12 AGOSTI 2025
    Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Bahrain, wadau kwa kushirikiaa na ofisi ya Uwekezaji na Uendelezaji Teknolojia, ITPO ya shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO wanachukua hatua kuondolea wanawake umaskini kwa kuimarisha talanta walizonazo. Mengine ni kama yafuatayo..Leo ni siku ya Kimataifa ya vijana duniani maadhinisho yanafanyika jijini Nairobi nchini Kenya chini ya ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewatumia vijana ujumbe maalum akisema “Kwa kijana: Sauti yako, mawazo yako na uongozi ni muhimu.”Je, vijana wanasemaje kuhusu siku hii? Kutoka Dar es Salaam nchini Tanzania, Sabrina Saidi wa Idhaa hii amezungumza na baadhi yao.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani WFP limepokea zaidi ya dola milioni 2 kutoka Japan kwa ajili ya msaada wa chakula nchini Malawi. Kwa msaada huu WFP inatarajia kusambazana tani 1970 za mahindi katika msimu wa mwambo kwa mwaka 2025/ 2026.Na katika mashinani fursa ni yake Maryam Bukar Hassan al maaruf Alhanislam, mshairi kutoka Nigeria ambaye ni mwanaharakati wa haki za binadamu na Mchechemuzi wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Amani. Hivi karibuni alighani shairi lake kwenye tamasha la majira ya joto hapa      jijini New York, nchini Marekani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Jukwaa Biashara lafungua masoko kwa bidhaa za wakimbizi Kakuma, Kenya
    Makala inamulika mnufaika wa Jamii Biashara ambalo ni jukwaa la mtandaoni la masoko lililobuniwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, (ILO) na Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda Kenya, (KNCCI). Jukwaa hili limefungua fursa kwa wakimbizi wanaoshughulika na biashara ndogo ndogo ili kujikimu maisha katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Assumpta Massoi ndiye mwenyeji wako kupitia video ya ILO.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners