Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Tangu 2017 hadi leo warohingya wanahaha bila kujua mustakabali wao
    Leo Agosti 25 ni miaka minane tangu kufurushwa kwa wingi watu wa kabila la Rohingya kutoka katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar. Umoja wa Mataifa unatoa wito wa mshikamano wa kimataifa kuwasaidia kwani mateso kwa watu hao yanaendelea kuwa mabaya zaidi kila uchao. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Asante AssumptaMyanmar (zamani ikiitwa Burma) ni nchi ya Kusini Mashariki mwa Asia yenye zaidi ya makabila 100, inayopakana na India, Bangladesh, China, Laos na Thailand.Warohingya wanafurushwa na kuteswa kwasababu mbalimbali zikiwemo za kihistoria kwa madai kuwa walitoka Bangladesh ingawa wameishi vizazi na vizazi nchini Myanmar. Pia sababu ya imani yao kwa uislamu miongoni mwa sababu nyingine.Ni miaka minane sasa tangu ufurushwaji mkubwa wa jami hii kutoka jimbo la Rakhine pwani ya Magharibi mwa Myanmar. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anaonya kuwa Warohingya na raia wengine bado wanakabiliwa na ukiukaji wa haki za binadamu na kufurushwa. Anaeleza wasiwasi wake kuhusu tarifa za kufukuzwa na kupunguzwa kwa nafasi za hifadhi katika ukanda huo, huku wakimbizi walioko Bangladesh wakikabiliana na upungufu mkubwa wa msaada wa chakula, elimu na huduma za afya.Guterres anasisitiza tena wito wake wa kulindwa kwa raia wote kwa mujibu wa sheria za kimataifa na anataka mshikamano mkubwa wa kimataifa. Hata hivyo ana matumaini kuwa Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Rohingya utakaofanyika New York mwezi ujao utasaidia kupata suluhu za kudumu.Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, anaeleza kuwa jeshi la Myanmar na Jeshi la Rakhine bado wanaendeleza uhalifu mkubwa dhidi ya Rohingya bila kuchukuliwa hatua, kinyume na sheria za kimataifa na maagizo ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki na anatoa wito wa kukomesha matendo hayo ili kuvunja mzunguko wa vurugu.
    2 min
  • Apoteza mwanae akikimbia machafuko
    Machafuko yanayoendelea Kaskazini Mashariki mwa Burkina Faso yamefurusha maelfu ya watu, kukatili maisha na kuwalazimisha wengi kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao. Miongoni mwa simulizi za kugusa ni ya Fadima Bandé mama aliyelazimika kufungasha virago kunusuru maisha yake na wanawe wawili lakini akaishia kupoteza mmoja, je ilikuwaje?  kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Flora Nducha anasimulia zaidi.Katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Dori Mashariki mwa Burkina Faso, sasa ni maskani ya Fadima, maisha hapa ni magumu na hana tena njia ya kujipatia kipato. Kila uchao analazimika kupambana kuhakikisha watoto wake wanapata angalau mahitaji ya msingi, anakumbuka safari ya uchugu kutoka Kijiji kwake Sohlan hadi hapaWakati tunakimbia mmoja wa binti zangu mapacha aliugua baada ya kunyeshewa na mvua kubwa na kupata mafua makali, wakati tayari alikuwa anaumwa utapiamlo. Tulimkimbiza hospitai mjini Sebba lakini akafariki dunia.”Baada ya kupata hifadhi kambini Dori Fadima akajaliwa mapacha wengine wawili ambao sasa wana umri wa miezi tisa na kwa bahati mbaya wote wana utapiamlo kutokana na changamoto ya chakula.“Hapa Dori tumebarikiwa watoto mapacha lakini wametukuta hatua makazi, hatuna chochote na tuna njaa na kibaya zaidi sikuwa hata na maziwa ya kutosha kuwanyonyesha”Watoto wa Fadima wamekuwa wakiishi kwa msaada wa kibinadamu unaotolewa na mashirika mbalimbali ikiwemo UNICEF ambayo sasa inasema hali yao inaweza kuwa mbaya zaidi kutokana na kupunguzwa kwa bajeti ya kimataifa misaada wanayoitoa na hivyo kuhatarisha maisha na mustakabali wa watoto wake. Fadima anasema“Unapotawanywa na machafuko huwezi kufanya kazi, unakuwa kama mtu asiye na ajira na hapo ndio madhila yanapokuwa makubwa zaidi, lakini bado hapa ni bora kuliko ningesalia kijijini kwetu.”Kwa mujibu wa UNICEF Burkina Faso ni moja ya migogoro ya kibinadamu iliyopuuzwa zaidi duniani. Ingawa UNICEF iko hapa kusaidia, lakini  inasema msaada zaidi unahitajika haraka.
    3 min
  • Afrika bado inaathirika kwa kiwango kikubwa, na kwa sasa inakumbwa na Ugaidi - Guterres
    Tarehe 18 Agosti mwaka 2025 siku ya Jumatano, wajumbe 15 wa Baraza la Usalama walikutana kujadili Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kikundi cha kigaidi cha ISIL/Da’esh.Walikabidhiwa ripoti hiyo ya 21 ikimulika vitisho vinavyotokana na kikundi hicho ambacho kirefu chake ni Islamic State in Iraq and the Levant au pia Da’esh. Ripoti ikigusia tishio la kikundi hicho katika maeneo mbalimbali duniani, lakini makala hii initajikita zaidi barani Afrika!
    4 min
  • 22 AGOSTI 2025
    Jaridani leo tunaangazia baa la njaa katika ukanda na huduma za afya katika ukanda wa Gaza. Makala tunafuatilia harakati dhidi ya ugaidi ukimulika ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, na mashinani tunaangazia simulizi za wakimbizi kupitia vyombo vya habari.Zaidi ya nusu milioni ya watu huko Gaza wameripotiwa kukumbwa na baa la njaa, hali ambayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameielezea kuwa “janga lililosababishwa na mwanadamu, shutuma ya kimaadili na kushindwa kwa ubinadamu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, licha ya mazingira magumu linaendelea na juhudi za kuokoa uhai wa kila binadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kimabavu na Israel. Wakati huo huo linatoa wito kwa mataifa mengine kufuata mfano wa Umoja wa Falme za kiarabu, UAE ambao juzi Jumatano wamewapokea baadhi ya wagonjwa mahututi na majeruhi waliobahatika kuhamishwa Gaza ili kupata huduma za kiafya wanazozihitaji.Katika makala Assumpta Massoi anamulika Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika wiki hii hapa makao makuu ya Umoja wa mataifa kuangazia harakati dhidi ya ugaidi ukimulika ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja huo kuhusu kikundi cha kigaidi cha ISIL kijulikanacho pia kama Da’esh.Na katika mashinani fursa ni yake Abraham Mwani mwandishi wa habari za wakimbizi kutoka Radio Pacis miongoni mwa wananufaika wa mafunzo ya UNESCO ya kuwezesha vyombo vya habari kusimulia vyema habari za wakimbizi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    12 min
  • WHO: Mataifa mengine tafadhali fuateni mfano wa UAE kupokea wagonjwa kutoka Gaza
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, licha ya mazingira magumu linaendelea na juhudi za kuokoa uhai wa kila binadamu katika eneo la Ukanda wa Gaza linalokaliwa kimabavu na Israel. Wakati huo huo linatoa wito kwa mataifa mengine kufuata mfano wa Umoja wa Falme za kiarabu, UAE ambao juzi Jumatano wamewapokea baadhi ya wagonjwa mahututi na majeruhi waliobahatika kuhamishwa Gaza ili kupata huduma za kiafya wanazozihitaji. Anold Kayanda anaeleza anawaangazia baadhi yao.
    3 min
  • 21 AGOSTI 2025
    Nchini Tanzania Programu ya Pamoja ya Kigoma, (KJP) inayotekelezwa kwenye mkoa huo ulioko magharibi mwa Tanzania kwa lengo la kujengea uwezo wa kuhimili changamoto zitokanazo na uwepo wa wakimbizi unaendelea kujengea uwezo wenyeji na hivi karibuni zaidi ni mradi wa kuongezea thamani zao la alizeti. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi anakupasha zaidi.
    10 min
  • Ukatili wa kijinsia katika mizozo
    Msikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa leo tunakuletea makala yenye kugusa maisha ya maelfu ya watu kote duniani, ukatili wa kingono katika maeneo yenye mizozo. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 19 Agosti limekutana jijini New York Marekani kujadili hali hii inayozidi kuongezeka, na kushuhudia jinsi waathirika wanavyobaki bila msaada wa kutosha kutokana na ukosefu wa rasilimali.Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa na Mwakilishi wake imeonesha ongezeko kubwa la kesi za ukatili wa kingono, jambo linaloibua maswali makubwa kuhusu uwajibikaji na huduma kwa manusura. Leah Mushi ametuandalia makala ifuatayo ikieleza hayo kwa kina.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners