Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 04 SEPTEMBA 2025
    Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa leo Flora Nducha anakuletea-Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi duniani UN-HABITAT lataka wakusanyaji na wachakataji wa taka watambuliwe kwani ni uti wa mgongo wa kuhakikisha mazingira safi na salama mijini-Katibu MKuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameipongeza Papua New Guinea kwa kuwa kisima cha kuvuna hewa ukaa na kuzitaka nchi za G-20 kuwajibika katika kudhibiti mabadiliko ya tabianchi-Nchini Mali, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ameonya juu ya kuzorota zaidi kwa hali ya haki za binadamu. -Na leo katika jifunze Kiswahili Je wafahamu maana ya methali "MASIKINI HANA MIIKO"? basi msikilize mtaalam wetu Dkt. Josephat Gitonga,  ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya,  kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani 
    11 min
  • UNMISS yaimarisha doria jimboni Tambura Sudan Kusini
    Katika jitihada za kuimarisha amani na usalama katika maeneo yaliyoathiriwa na machafuko ya kikabila nchini Sudan Kusini, Umoja wa Mataifa kupitia Ujumbe wake wa amani nchini humo UNMISS wameendelea kuimarisha ulinzi na kuongeza doria za magari usiku na mchana huko Greater Tambura katika jimbo la Equatoria Magharibi.Sabrina Saidi anaangazia juhudi za UNMISS katika kuhakikisha hali ya usalama inarejea na wananchi waliokimbilia katika kambi za wakimbizi kusakama usalama wanarejea makwao.TAARIFA YA SABRINA SAIDI)NAT...Video ya UNMISS inaanza kwa kumulika doria zinazofanywa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko katika kaunti ya Greater Tambura katika jimbo la Western Equatoria, kusini-magharibi mwa nchi ya Sudan Kusini karibu na mipaka ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC na Jamuhuri ya Afrika ya Kati.Tangu mwaka 2021, mizozo ya wenyewe kwa wenyewe, umeendelea kugharimu maisha ya watu wengi na kuwalazimu maelfu kuyakimbia makazi yao.Wananchi waliokumbwa na hofu wamekuwa wakijificha vichakani, wengine wakikimbilia nchi jirani, huku wengi wakitafuta hifadhi katika kambi mbalimbali za wakimbizi wa ndani zilizopo maeneo ya karibu.Ili kuwalinda vyema raia UNMISS wameimarisha uwepo wao katika eneo hilo na kuongeza doria za magari usiku na mchana, wakipita katika barabara mbovu zilizotapakaa tope na kuharibiwa na mvua. Walinda amani hao maarufu kama 'Blue Helmets', wamekuwa wakitembelea kambi mbalimbali za wakimbizi wa ndani na kuzungumza na jamii mbalimbali za kikabila zilizopata hifadhi huko.Tereza Martin ni mmoja wa wakimbizi wa ndani aliyepata hifadhi na hapo, anazungumza kwa hofu na simanzi...CUT: Sauti ya Tereza Martin"Hatuelewi chanzo cha mzozo huu. Tumekuwa tukiishi katika kambi hii kwa takribani miaka sita, tukiishi kwa njaa na mateso. Makazi yetu ya muda ni mabovu. Msimu wa mvua umefanya hali kuwa mbaya zaidi, sasa tunalala juu ya maji ya mvua. Hatuwezi kwenda shambani kwa hofu ya kushambuliwa. Tunaomba serikali na wadau kutuangalia kwa jicho la huruma."NAT....Margret Dominic naye ni mkimbizi wa ndani kambini hapo, anasema doria hizi zinampa amani CUT: Sauti ya  Margret Dominic-"Hatuwezi kutoka nje ya kambi. Tunaweza kulala kwa sababu wanapiga doria usiku. Kama wasingekuwepo, hatujui kama tungeweza hata kupata usingizi."Emmanuel Dukundane ni Afisa wa Masuala ya Kiraia wa UNMISS, anasema wanajenga kambi mpya  katika maeneo ya kimkakati.CUT: Sauti ya Emmanuel DukundaneHili lina maana kubwa sana kwa sababu tuna rasilimali nyingi, na kwa kujiweka katika kambi hiyo mpya, tutaweza kufanya doria zaidi, kufanya mazungumzo zaidi, na kuwezesha mchakato wa upatanisho na amani kwa ujumla."Ingawa UNMISS itaendelea kuisaidia serikali ya Sudan Kusini katika kuwalinda raia wa Greater Tambura, amani ya kweli na upatanisho wa kudumu vinapaswa kukubaliwa na kupatikana kupitia juhudi za jamii husika na viongozi wao wenyewe.
    4 min
  • Wakimbizi Nyarugusu wahamasika kufanya usafi
    Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC wanahakikisha wakimbizi wanaoishi katika kambi za wakimbizi za mkoani Kigoma Magharibi mwa Tanzania ikiwemo kambi ya nyarugusu wanapata huduma muhimu za maji na usafi kupitia ushirikiano wa viongozi wa wakimbizi. Huduma hizo  zimekuwa changamoto kubwa katika kambi za wakimbizi zikichangiwa na ukata wa ufadhili. Flora Nducha na taarifa zaidi (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipoibuka Burundi mwaka 2015, na baadaye mapigano kuighubika upya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, maelfu ya  watu walikimbia na kuvuka mpaka kuingia Tanzania. Leo, wengi wao wanaishi katika kambi za wakimbizi mkoani Kigoma kama vile Mtendeli, Nduta, na Nyarugusu.Lakini maisha kambini hayajakuwa rahisi. Kwa ufadhili mdogo, familia zinapata shida kupata huduma za msingi kama maji safi, makazi, na elimu.Hapo ndipo Shirika la UNHCR, na Baraza la Wakimbizi la Norway NRC, wanapoingia. Tangu mwaka 2016, wamekuwa wakitoa huduma muhimu ikiwemo kufunga mifumo ya maji, kujenga vyoo, na kusambaza sabuni na mahitaji mengine ya usafi.Miongoni mwa wanaofanya mabadiliko kupitia msaada huo ni Ahunga Msama, mkimbizi mwenye umri wa miaka 55 kutoka DR Congo, ambaye ni afisa msimamizii wa huduma za maji, usafi, kujisafi na usafi wa mazingiira WASH katika kambi ya Nyarugusu.(AHUNGA CLIP 1)“Ninasaidia jamii yetu ya kambi ya Nyarugusu ili wawe wanapata maji safi na salama”Ahunga anasema jamii yake iliteseka sana iliteseka sana kwa magonjwa yanayosababishwa na maji machafu ndio maana aliamua kuchukua hatua kulinda afya zao. Kila siku ahakikisha watu wanapata maji safi na huduma za usafi salama.Akiwa pamoja na wakimbizi wenzake, Ahunga anapita nyumba kwa nyumba kufundisha familia jinsi ya kuzuia magonjwa kupitia usafi kwani anaamini elimu ni ufunguo(AHUNGA CLIP 2)“Tunasaidia kuelimisha jamii yetu ili wawe wasafi. Wawe na vyoo, wawe na mabafu, wawe na vichanja na wawe na mashimo ya takataka.”Watu wakielewa, wanaweza kujilinda.Anasema watu wakieelewa ni rahisi kujilinda na juhudi zake zinaokoa maisha na kuhamasisha wengine, zikionyesha kwamba hata katika mazingira magumu, wakimbizi wanaweza kuongoza mabadiliko katika jamii zao na anasema hilo ni la muhimu sana kwani(AHUNGA CLIP 3)“Tunasaidia jamii yetu ili wajilinde na magonjwa ya milipuko”Kwa msaada wa UNHCR na Baraza la Wakimbizi la Norway, maelfu ya wakimbizi katika kambi za wakimbizi za Kigoma sasa wana maji salama, usafi wa mazingira ni bora, na wana matumaini mapya ya maisha.
    3 min
  • UN yatumia kila mbinu kuhakikisha inawafikia waathirika wa tetemeko Afghanistan
    Juhudi kubwa za msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililoipiga Afghanstan mwishoni mwa wiki, zimeendelea leo huku watoa misaada wakikabiliwa hali ngumu ya kuwafikia wanaohitaji msaada kutokana na Barabara kuzibwa na kukatika kwa mawasiliano. Anold Kayanda na taarifa zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Taarifa mpya kutoka kwa timu za tathmini za Umoja wa Mataifa zilizofanikiwa kuwafikia waathirika katika wilaya ya milimani ya Ghazi Abad jana Jumanne kwa njia ya miguu, zimeweka wazi umuhimu wa kuendeleza tena kwa haraka msaada wa kibinadamu.Salam Al-Jabani kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) mjini Kabul anasema, “jambo la dharura ni kuwatoa watu chini ya vifusi na Watu wanasema wanachohitaji kwa haraka ni msaada wa kuwazika waliofariki dunia na kuwatoa waliofunikwa.”UNICEF inasema watoa misaada wake walilazimika kutembea kwa saa mbili ili kuwafikia watu na bado kuna vijiji ambavyo ili kuvifikia unahitaji kutumia saa sita hadi saba na hata helikopta hazijafanikiwa kufika huko.Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP ambao walikuwa wa kwanza kupeleka msaada kwenye eneo la tukio,  Bwana John Aylieff, akiwa mjini Kabul amesema, “WFP inaweza tu kumudu kuwalisha waathirika wa tetemeko la ardhi kwa wiki chache zijazo kabla ya ufadhili kuisha.”Kwa upande wake, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linapeleka msaada muhimu wa dharura kutoka maghala yake yaliyopo Kabul, ikiwemo mahema, blanketi na taa za sola. Pia maelfu ya wanajamii wa eneo hilo wameelekea eneo lililoathirika kusaidia juhudi za uokoaji, wakiwa na maji na chakula.
    3 min
  • 03 SEPTEMBA 2025
    Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa, hii leo utasikia juhudi zinazofanyika kusaidia wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi nchini Afghanistan. Kutoka barani Afrika utasikia juhudi za kulinda raia wa Sudan Kusini wanaoathirika na vita vya wenyewe kwa wenyewe huko jimboni Tambura na kutoka nchini Tanzania utasikia msaada kwa wakimbizi walioko magharibi mwa taifa hilo. 
    10 min
  • 02 SEPTEMBA 2025
    Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia mradi wa FAO Mjini Morogoro, uliokutanisha viongozi wa Serikali kutoka katika Taasisi zinazojihusisha na udhibiti na usalama wa chakula. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.zaidi ya watu bilioni moja duniani wanaishi na changamoto za afya ya akili kama vile msongo wa mawazo na mfadhaiko, kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO. Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema nchi wanachama zinapaswa kushughulikia tatizo hilo kwa “Kuwekeza katika afya ya akili, kwani kuwekeza kwa watu, jamii na uchumi ni uwekezaji ambao hakuna nchi inayoweza kuupuuzia.”Umoja wa Mataifa umetuma salamu za rambirambi na pole kwa wananchi wa sudan kufuatia maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua mkubwa iliyonyesha kwa siku kadhaa ambayo imesababisha maafa katika kijiji cha Tarsin huko Jebel Marra nchini Sudan mwishoni mwa wiki.Nchini Afghanistan ambako idadi ya vifo inaendelea kuongezeka kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea juzi jumapili, wafanyakazi wa misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanafanya kila juhudi kuhakikisha wanafikisha misaada kwa waathirika. Akizungumza na waandishi wa habari kutokea Kabul Afghanistan Indrika Ratwatte ambaye ni mwakilishi wa UN nchini humo amesema “Sio rahisi kufika maeneo yaliyoathirika kitu ambacho kinawafanya majeruhi waendelee kufungiwa.” Ametaja juhudi za haraka zinazofanyika ni pamoja na kuzika miili ya waathirika na kufukia mifugo ili kuzuia magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza kusambaa kwa haraka.”.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua tofauti ya "URAIBU NA HITARI”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    11 min
  • 29 AGOSTI 2025
    Jaridani leo tunaangazia Majaribio ya Nyuklia, na machafuko nchini Sudan Kusini. Makala tunakwenda nchini Nepal na mashinani tunasalia huko huko Sudana Kusini, kulikoni?Dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa yakupinga Majaribio ya Nyuklia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa onyo kali kuhusu kuongezeka kwa hatari za nyuklia kufuatia mvutano wa kisiasa unaondelea duniani na amehimiza kuridhiwa kwa mkataba wa kupiga marufuku majaribio hayo ya kinyuklia.Maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao huko Tambura, jimbo la Equatoria Magharibi, tangu ghasia zilipozuka upya mwaka 2021 nchini Sudan Kusini. Hadi leo, wengi wao bado wanaishi kambini bila chakula cha uhakika, huduma za afya wala usalama huku wanawake na watoto wakibeba mzigo mkubwa zaidi wa mateso hayo.Makala tunakwenda nchini Nepal kumulika suala la waume kwenda kusaka ajira nje ya nchi na kuacha wake zao wakihaha kukimu familia zao katika mazingira ambamo wanawake wanakuwa hawana uthabiti wa kiuchumi limeanza kupatiwa muarobaoni.Na katika mashinani fursa ni yake Anna Pita, Msimamizi wa hospitali ya Kator nchini Sudan Kusini akieleza ni kwa jinsi gani mifumo ya nishati ya jua iliyofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP na wadau wake inabadilisha utoaji wa huduma katika hospitali na vituo vya afya nchini humo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners