
Sign up to save your podcasts
Or


Jukwaa la kubadili mtazamo wa Afrika jijini Kigali limewataka vijana wa Afrika kujitokeza na kubadili mustakabali wa maisha yao badala ya kutegemea viongozi wa sasa.
Tunakuuliza msikilizaji , vijana wana nafasi gani kuleta mabadiliko ya siasa na uchumi?
Skiza maoni ya mskilizaji.
Nchini Kenya, serikali imesema wizi wa fedha kupitia njia ya simu umeongezeka zaidi mwaka huu ikilinganishwa na miaka ya awali. Kuimarika kwa teknolojia ukitajwa kuwa kichocheo.
Je nani anapaswa kuwajibikia pesa za mwananchi zinapoibwa kupitia simu ?
Skiza maoni ya mskilizaji.
Serikali ya DRC na waasi wa AFC/M23 wamebaliana kuhusu mpango wa mazungumzo ya amani, hatua inayotoa nafasi ya kutekelezwa kwa mkataba wa amani wa Doha na Washington, ili kumaliza vita mashariki mwa nchi hiyo.
Skiza maoni ya mskilizaji.
Nchini Zambia, Rais Hakainde Hichilema, amechaguliwa kwa muhula wa pili, akimshinda mpinzani wake wa Karibu Brian Mundubile. Hata hivyo kumeshuhudiwa malalamiko ya dosari kadhaa ikiwemo udanganyifu, wizi wa kura na vitisho, mambo yanayoripotiwa wakati wa chaguzi nyingi barani Afrika.s
Ripoti ya wataalam wa hali ya hewa imeonya kuwa Afrika inakabiliwa na uwezekano wa aslimia 81 wa kukumbwa na hali ya hewa ya El Nino. Katika ripoti hiyo, eneo la Kusini mwa Afrika linatarajiwa kukumbwa na
Mwishoni mwa juma lililopita, upinzani nchini DRC kupitia vuguvugu la C64 ulitangaza kuwa utafanya maandamano Septemba 15 kupinga mchakato wa marekebisho ya katiba.
Tangazo lao walilitoa baada ya muda waliokuwa wameutoa kwa Rais Felix Tshisekedi kuitisha mazungumzo ya kitaifa kupita.
Mwaka mmoja kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, imetoa kanuni mpya za ufadhili wa kampeni za wagombea mbalimbali.Mgombea urais atatakiwa kutumia kiasi cha shilingi za Kenya zisizozidi Bilioni 6 huku vyama vya siasa vikitakiwa kutokuvuka matumizi ya bilioni 25 za Kenya.Tumemuuliza mskilizaji ,anazungumzia vipi kanuni hii ?na nchini mwake , kuna utaratibu kama huu?
Na Hannah Nalianya
Kila Ijumaa rfi Kiswahili inakupa nafasi kuchangia mada yoyote kuhusiana na matangazo yetu.
Skiza maoni ya Juma hili
Fainali ya kombe la dunia katika mchezo wa soka, itawakutanisha mabingwa watetezi Argentina na Hispania waliowahi kushinda taji hili mwaka 2010.
Mechi hiyo itapigwa siku ya Jumapili nchini Marekani.
Unatarajia nani ataibuka mshindi katika mechi hiyo na kwanini.
Skiza ya mskilizaji
Na Hannah Naliaka
Safari ya Ufaransa kutinga fainali za kombe la dunia imefikia tamati baada ya kushindwa mabao 2-0 na Uhispania katika nusu fainali ya kwanza.
Unazungumziaje mechi hiyo ?
Skiza maoni ya mskilizaji.
From the publisher's feed
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners