Wimbi la Siasa

Wimbi la Siasa

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Wimbi la Siasa episodes

  • Uganda: Mazungumzo kuhusu hatima ya Kizza Besigye

    Waziri wa masuala ya Katiba nchini Uganda Norbert Mao, ametangaza kuwepo kwa mazungumzo ili kupata ufumbuzi wa kuendelea kuzuiwa kwa mwanasiasa  mkongwe wa upinzani Kizza Besigye, anayekabiliwa na mashtaka ya uhaini. Hata hivyo, chama cha siasa cha Besigye  cha People’s Front for Freedom (PFF), kinasema mwanasiasa huyo hana taarifa zozote za kuwepo kwa mazungumzo hayo. Tunachambua

    10 min
  • DRC: Kabila aungana na M23 kuunda vuguvugu jipya la kisiasa na kijeshi

    Baada ya kuongoza nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa karibu miaka 20, rais wa zamani Joseph Kabila, ameungana na waasi wa M23 Mashariki mwa nchi hiyo na kuunda vuguvugu jipya la kisiasa na kijeshi linaloitwa FRN kumpinga rais Felix Tshisekedi na serikali yake. Nini athari za hatua hii ya Kabila na washirika wake  kwa usalama na siasa nchini DRC ? Tunachambua.

    11 min
  • Hali ya siasa nchini Kenya mwaka mmoja baada ya kifo cha Raila Odinga

    Ni mwaka mmoja, tangu kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya na kiongozi wa muda mrefu wa upinzani Raila Odinga. Kufariki kwake dunia, tarehe 15 mwezi Oktoba mwaka 2025, kumeacha pengo kubwa kwenye siasa za nchi hiyo. Chama chake cha siasa alichoasisi cha Orange Democratic movement (ODM), kikishuhudia migawanyiko. Nini hatima ya siasa za Kenya bila uwepo wa Odinga ? Mgeni wetu wiki hii ni Alenga Torosterdt.

    11 min
  • Chanzo cha kuzuka kwa vita vipya Kaskazini mwa Ethiopia

    Tangu tarehe 23 Septemba, mapigano mapya yameendelea kushuhudiwa Kaskazini mwa Ethiopia, kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Tigray. Nini kinaendelea Ethiopia na vita vina vinaweza kuvuka mipaka ? Mchambuzi wetu ni Abdullahi Boru, mtalaam wa masuala  amani , usalama, haki za binadamu katika eneo la Pembe ya Afrika akiwa Washington DC nchini Marekani.

    10 min
  • Suluhu ya njiapanda ya kisiasa nchini Sudan Kusini

    Sudan Sudan inakabiliwa na mzozo wa kikatiba na kisiasa, kuelekea uchaguzi mkuu wa kwanza, uliopangwa kufanyika tarehe 22 mwezi Disemba mwaka huu. Rais Salva Kiir, anayetarajiwa kuwania, amebadilisha sheria ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele kuwa uchaguzi huo unatakiwa kufanyika chini ya Katiba mpya na baada ya sensa ya watu. Nini hatima ya kisiasa Sudan Kusini ?

    11 min
  • Hatima ya serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar

    Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, amezindua Kamati ya pamoja ya majadiliano kati ya chama chake CCM na kile cha upinzani ACT Wazalendo, katika kile kinachoashiria hatua mpya katika mchakato wa maridhiano ya kisiasa katika visiwa hivyo. Hatua hii inakuja baada ya vyama hivyo kusaini tamko la pamoja la makubaliano Julai tarehe 9 mwaka huu, ili kupata maridhiano ya kisiasa. Kwanini imechukua muda mrefu kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ? Tunachambua.

    11 min
  • Kenya yatoa siku 90 kwa wageni wasio na vibali halali kuvitafuta

    Serikali ya Kenya, imewatangazia raia wa kigeni wanaoishi nchini humo bila vibali vya kuishi au kufanya biashara, kuvitafuta ndani ya siku tisini.Hii inafuatia kauli ya rais William Ruto, wiki iliyopita, kuagiza operesheni dhidi ya wachuuzi wanaofanya biashara ndogo ndogo nchini humo. Je, hatua hii ya serikali ya Kenya inamaanisha nini na tishio ya utengamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ?

    11 min
  • Mpango wa rais Tshisekedi kuhusu mazungumzo yatafanikiwa ?

    Mwishoni mwa mwezi wa Agosti, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi, alitangaza mpango wa namna mazungumzo ya kitaifa yatakavyofanyika, kusaidia kuleta utulivu wa kisiasa nchini humo. Mazungumzo hayo yataanzia katika mikoa yote 26, kabla ya yale ya kitaifa kufanyika jijini Kinshasa. Makundi yenye silaha na waasi wa M23/AFC hawatoshiriki kwenye mazungumzo hayo. Je, mpango huu utafanikiwa ?

    11 min
  • DR Congo: Mvutano waendelea kuhusu mpango wa kuifanyia marekebisho katiba

    Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwezi Julai, iliidhinisha sheria tata ya kufanyika kwa kura ya maoni, ili kuifanyia  katiba mabadiliko baada ya kupitishwa na wabunge mwezi Juni. Hatua hii imewakera wapinzani wa rais Felix Tshisekedi, kutoka muungano wa C64 ambao wameitisha maandamano Septemba 15, baada ya kuchelewa kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa. 

    Tunachambua na mbunge Willy Mishiki kutoka upande wa rais Tshisekedi na Emery Damien Kalwira kutoka muungano wa upinzani wa  C64.

    10 min

About Wimbi la Siasa

From the publisher's feed

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe…

More shows like Wimbi la Siasa

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Siha Njema by RFI Kiswahili

Siha Njema

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners