
Sign up to save your podcasts
Or


Yaliyojiri wiki hii ni pamoja na watu kadhaa wahofiwa kufukiwa na jengo lililoporormoka mtaani Eastleigh jijini Nairobi nchini Kenya, hali ya sintofahamu yaendelea kuzingira kisa cha ebola kilichoripotiwa nchini Nigeria wiki hii, huko DRC mashirika ya kimataifa yaliendelea kuhoji kuhusu dola milioni mia 7 zilizotengewa mapambano ya Ebola, maandamano yanaendelea kufanyika nchini Ufaransa.
Makala hii imeangazia hatua ya rais mstaafu wa DRC Joseph Kabila kuzindua muungano mpya wa uasi wa FRN. Maadhimisho ya miaka 27 tangu alipoaga dunia mwasisi wa taifa la Tanzania mwalimu Julius Kambarage Nyerere, maadhimisho ya mwaka wa kwanza tangu kifo cha aliyekuwa mwanasiasa mashuhuri na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga, ziara ya mfalme wa Hispania Filipe wa Sita kwenye kisiwa cha Ceuta,Trump alisema walifikia makubaliano ya nishati na Urusi
Makala hii imeangazia kisa cha mgonjwa wa ebola aliyetokea DRC kufariki dunia, watu 32 wamepoteza maisha katika ajali ya barabarani mkoani Morogoro nchini Tanzania, na ujumbe wa wawezeshaji wa Umoja wa Afrika kutembelea Kinshasa baada ya kuzuru Kigali Rwanda na Goma, na kwengineko Navy Pillay ndiye mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2026
Miongoni mwa yaliyojiri wiki hii ni pamoja na uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote, huko Lamu, pwani ya Kenya, mapigano yaendelea huko Ethiopia, kifo cha bilionea wa Zimbabwe, kutawazwa kwa mfalme wa Tooro, rais wa Nigeria Tinubu, aahidi kupunguza gharama ya maisha na ajira zaidi, rubani amchoma kisu mwenzake ndani ya ndege iliyokuwa ikielekea Israel, na mengineyo
Taarifa kuu utakayoskia kwenye makala haya ni pamoja na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir avunja serikali kuelekea Uchaguzi mkuu wa mwezi Disemba.
Kwingineko nchini Ethiopia, mapigano mapya yameanza tena kati ya vikosi vya Tigray na jeshi la nchi hiyo. Utaskia pia punde zaidi katika mkutano wa UNGA nchini Marekani.
Raia wa Burundi walivyokumbwa na masaibu jijini Nairobi, Kenya wengine wakaamua kuondoka, ajali ya mioto iliyotokea nchini DRC, kuanzia Kinshasa wakati wa sherehe ya harusi, kuja Bukavu Kivu kusini ambapo wanafunzi wengi walikufa katika moto ulioshika shule moja, huku ajali ya moto ikiripotiwa mjini Goma, Kivu kaskazini; mazishi ya mfalme wa Tooro huko Uganda kufanyika jumamosi hii, hali nchini Tanzania na Kenya, lakini pia yaliyojiri Afrika magharibi, na kwengineko duniani.
Makala hii imeangazia maandamano ya wanaharakati wa Kenya wakidai kuachwa huru kwa wapinzani Tundu Lisu huko Tanzania, na Kiiza Besigye huko Uganda, wanaokabiliwa na mashitaka ya uhaini, ziara ya rais Felix Tshisekedi huko Israeli, umoja wa mataifa kutaka serikali ya Zambia kuacha kukandamiza wapinzani baada ya uchaguzi, na mvutano kati ya Morocco na Uhispania, mashambulio makali kati ya Marekani na Iran baada ya kukwama kwa juhudi za kidiplomasia kati yao.
Makala hii imeangazia kujiuzulu kwa makamu wa rais wa Tanzania Emmanuel Nchimbi, huku bunge limemwidhinisha Deogracias Ndejembi kuwa makamu mpya wa rais, na huko DRC rais Felix Tshisekedi amezindua mazungumzo ya kitaifa ambayo yatadumu kwenye majimbo 26 kabla ya kukamilishwa mjini Kinshasa, akiwatenga waasi wa M23, siasa za Kenya, Sudan na wanajihadi wa Nigeria wanavyojikusanyia fedha, pia mzozo wa mlango bahari wa Hormuz kati ya Marekani na Iran
Makala hii imeangazia ziara ya rais wa DRC Félix Tshisekedi nchini Tanzania, mahakama ya Tanzania yasema kiongozi wa chama cha Chadema Tundu Lissu ana kesi ya kujibu ya uhaini, rais Hakainde Hichilema ndiye mshindi wa uchaguzi mkuu wa Zambia wiki iliyopita, utasikia siasa za Nchini Kenya, Sudan na kampeni za uchaguzi mkuu zilianza siku ya jumatano nchini Nigeria, pia tutaenda huko Senegal, na kwengineko Marekani kuiwekea Iran vikwazo vigumu zaidi vya kiuchumi
Uchaguzi wa urais na wabunge ulivyofanyika nchini Zambia wiki hii, na sasa wananchi wanasubiri matokeo rasmi, baada ya vurugu za siku ya Ijumaa, rais wa Kenya William Ruto aliongoza mazungumzo kuhusu ruwaza ya Kenya 2060, muungano wa upinzani nchini DRC watishia kuitisha maandamano kupinga marekebisho ya katiba; tutaangazia siasa za Tanzania, Sudan, Washington kuiwekea vikwazo Iran kuhusu udhibiti wa mlango Bahari wa Hormuz.
From the publisher's feed
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners