Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii episodes

  • Mpasuko ndani ya chama cha ODM, nchini Kenya, huko DRC Monusco kuanza kazi upya

    Mpasuko kushuhudiwa ndani ya ODM, chama cha aliyekuwa kinara wa upinzani nchini Kenya hayati Raila Odinga, ziara ya kaimu mkuu wa tume ya Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Monusco huko Goma mashariki mwa DRC, hali ya nchini Sudan, milio ya risasi kusambaratisha usalama nchini Guinea, Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alikutana na kufanya mazungumzo na rais wa Marekani Donald Trump

    21 min
  • Rais Paul Kagame atoa kauli nzito kwa jumuia ya kimataifa, maombi ya rais Tshisekedi

    Rais wa Rwanda Paul Kagame asema nchi yake haitatizwi na vitisho vya kuwekewa vikwazo na Jumuiya ya Kimataifa, mkutano unaolenga kuimarisha ushirikiano wa kibishara hasa kwenye sekta ya madini kati ya Marekani na nchi za Afrika wafanyika Washington, tumeangazia siasa za Uganda, yaliyojiri nchini Kenya, hali ya kibinadamu yaendelea kuwa mbaya nchini Sudan, rais wa Nigeria Bola Tinubu aagiza wanajeshi kupelekwa katika jimbo la Kwara kulinda amani, mkutano wa Oman kati ya Marekani na Iran.

    21 min
  • Mwaka mmoja watimia tangu waasi wa M23 waidhibiti Goma na siasa za ukanda huu

    Makala hii imeangazia kutomia kwa mwaka mmoja tangu waasi wa AFC/M23 waudhibiti mji wa Goma, Rwanda yaishitaki Uingereza kuhusu mkataba unaohusu wakimbizi, mapigano yashuhudiwa huko Sudan, na katika ukanda wa Afrika magharibi tumeangazia shambulio la watu wenye silaha katika uwanja wa ndege wa Niamey, ECOWAS yaiondolea vikwazo nchi ya Guinea, na tishio la Marekani kuishambulia Iran na mengine zaidi. 

    21 min
  • Jeshi la UPDF kuwaua wafuasi 30 wa chama cha NUP, Gavana Purusi arejea Uvira

    Katika makala utasikia polisi wa Uganda waendelea kuwakamata washirika wa karibu wa mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi Ssentamu baada ya uchaguzi wa wiki iliopita, waasi wa AFC/M23 Kujiondoa kwenye mji wa Uvira mashariki mwa DRCongo, nini kinaendelea? Siasa za Kenya, Tanzania na hali ya sasa nchini Sudan; wanajihadi kuwateka waumini zaidi ya mia moja na sitini wakiwa kanisani kule Nigeria, na kutamatika kwa jukwaa la Uchumi duniani huko Davos

    21 min
  • Watu zaidi ya 10 wauawa katika machafuko Uganda, M23 watangaza kuondoka Uvira

    Makala hii imeangazia uchaguzi wa nchini Uganda matokeo yakisubiriwa kutolewa leo, mkutano wa Lome nchini Togo kuhusu mustakabali wa amani ya mashariki mwa DR Congo, hali ya nchini Sudan, Somalia, na ugunduzi wa kaburi la pamoja lenye miili ya wahamiaji 21 huko Libya, hotuba ya rais Macron mbele ya maafisa wa jeshi la nchi yake na kauli ya Marekani kuhusu waandamanaji wa Iran

    21 min
  • Nini kinaendelea baada ya Maduro kukamatwa? siasa za Tanzania na mengineyo

    Miongoni mwa matukio makubwa ni pamoja na kukamatwa kwa aliyekuwa rais wa Venezuela Nicolas Maduro, kubanduliwa kwa timu ya taifa ya DRCongo kwenye michuano ya AFCON 2025, vifo vya wakimbizi wa Congo Kinshasa katika kambi huko Burundi, siasa za Tanzania, Kenya na Uganda kuelekea uchaguzi wa January 15 hali ya nchini Sudan kusini, Rais Faustin Archange Touadera kutangazwa mshindi wa Uchaguzi wa urais hivi karibuni na kauli ya Urusi kuhusu washirika wa Ukraine, Ulaya

    21 min
  • Ulimwengu waukaribisha mwaka wa 2026 katika mazingira tofauti

    Makala hii imeangazia namna dunia ilivyoukaribisha mwaka mpya wa 2026, kampeni za uchaguzi wa mwezi huu nchini Uganda kushika kasi, siasa za Kenya: kiongozi wa chama cha ODM atangaza kuwa atagombea kiti cha urais mwaka ujao, hali ya mashariki mwa DRC, Israeli kulitambua eneo la Somaliland kama taifa huru,nchi kadhaa za Afrika zatangaza kuwazuia raia wa Marekani kuzuru nchi zao na mkutano wa rais wa Ukraine Volodmir Zelensky na rais wa Marekani Donald Trump

    21 min
  • Matukio makubwa ulimwenguni katika wiki ya mwisho ya mwaka 2025

    Matukio makubwa ya wiki hii ni pamoja na maadhimisho ya sikukuu ya krisimasi duniani mataifa kadhaa yakikabiliwa na shida za kiusalama, kasi ya kampeni za uchaguzi nchini Uganda, waasi wa AFC/M23 na mapigano yao mkowani Kivu kusini mashariki mwa DRC, kesi ya uhaini inayomkabili makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Riek Macxhar kuahirishwa hadi January 06; mashambulizi ya vikosi vya Marekani dhidi ya wanamgambo wa Islamic State nchini Nigeria, na pia hali nchini Ukraine na Cambodia.

    21 min
  • Waasi wa AFC/M23 watangaza kujiondoa mjini Uvira kwa masharti

    Miongoni mwa matukio makubwa ya wiki hii ni pamoja na waasi wa AFC/M23 kutangaza kujiondoa kwenye mji wa kimkakati wa Uvira mkowani kivu kusini mashariki mwa DRC hatua ambayo imetiliwa mashaka, shirika la kimataifa la Amnesty lasema polisi nchini Tanzania walitumia nguvu kupita kiasi kudhibiti waandamanaji kipindi cha uchaguzi, wafuasi wa rais wa Tunisia, Kais Saied waandamana kuonesha ungwaji mkono huku mzozo wa kisiasa ukizidi, Umoja wa ulaya EU kuiipa Ukraine mkopo wa Yuro Bilioni 90

    21 min
  • Waasi wa M23 waudhibiti mji wa Uvira DRC na maadhimisho ya uhuru nchini Kenya

    Makala hii imeangazia kwa sehemu kubwa hali iliyojiri kwenye mji wa Uvira mkoani Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Kenya kutoka kwa mkoloni wake Uingereza,nacho chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania chasema watu zaidi ya elfu mbili waliuawa wakati wa machafuko ya wakati wa uchaguzi wa octoba 29, na mengine mengi

    20 min

About Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

From the publisher's feed

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

More shows like Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Siha Njema by RFI Kiswahili

Siha Njema

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners