
Sign up to save your podcasts
Or


Baadhi ya habari ambazo tumezipa uzito ni pamoja na mkutano wa 80 wa baraza kuu la umoja wa mataifa wiki hii ambapo viongozi wa dunia walipata nafasi ya kutoa hotuba zao, kujiuzulu kwa spika wa bunge la DRC Vital Kamerhe, na kuendelea kwa mapigano mashariki mwa nchi hiyo, kuidhinishwa kwa wagombea wa kiti cha urais nchini Uganda kuelekea uchaguzi wa mwakani, Peter Mutharika kurejea madarakani baada kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu, kura ya maoni ya Guinea, na mambo mengine mengi.
Baadhi ya habari ambazo tumezipa uzito ni pamoja na vurugu katika bunge la DRC na mchakato wa kumuondoa spika wa bunge hilo na maafisa wengine, mashindano ya dunia ya baiskeli kung’oa nanga siku ya Jumapili mjini Kigali, mji mkuu wa Rwanda, siasa za Uganda kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani, tumeangazia hali nchini Tanzania, Sudan kusini, uchaguzi wa Malawi, kura ya maoni kule Guinea kuhusu marekebisho ya katiba na ziara wa Marekani huko Uingereza.
Karibu kwa makala ya Yaliyojiri wiki hii. Baadhi ya habari ambazo tumezipa uzito wiki hii ni makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini ashatkiwa kwa uhaini na mauaji, ajali ya boti nchini DRC.
Tutaangalia hatma ya mkutano wa hali ya hewa nchini Ethiopia, Vilevile onyo la vifo vya malaria kuongezeka mwaka huu kutokana na kupunguzwa kwa misaada ya kigeni.
Wiki hii taarifa zilizokuwa gumzo kwenye vyombo vya habari ni kuhusu hukumu dhidi ya aliyekuwa waziri wa sheria nchini DRC, Constant Mutamba, nitakujuza pia kuhusu kampeni za uchaguzi mkuu nchini Tanzania, tutaangalia pia ajali ya boti nchini Nigeria iliyoua watu 30. Kimataifa, tutaangazia punde zaidi katika mzozo wa Urusi na Ukraine.
Kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa urais wa mwezi oktoba mwaka huu nchini Tanzania, kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame dhidi ya mzozo wa mashariki mwa DRC, mapigano makali kati ya jeshi la Congo FARDC na washirika wao wazalendo maeneo ya milima ya Fizi, hali nchini Sudan, ziara ya rais wa senegal jijini Paris ufaransa, Urusi yaendeleza mashambulio huko Kiev Ukraine licha ya shinikizo za Kimataifa na mengineyo.
Ni juma ambalo limeshuhudia mkutano kati ya rais wa Marekani Donald Trmp na rais wa Ukraine Volodmir Zelensky akisindikizwa na viongozi wa Ulaya, michuano ya CHAN kwenye nchi tatu za Afrika Mashariki yaendelea, mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu juma hili yalishutumu jeshi la Rwanda likishirikiana na waasi wa M23 kuwaua raia wa kawaida Binza wilayani Rutshuru mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, mkutano wa kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika au TICAD ulifunguliwa jijini Yokohama, Japani.
Mkutano wa Geneva washindwa kupata mkataba wa kimataifa kuhusu taka za plastiki, takriban watu 31 wakiwemo raia 19 waliuawa katika mapigano kati ya jeshi la Kongo na wanamgambo wa CRP wa Thomas Lubanga katika eneo la Djugu mkoani Ituri kaskazini mashariki mwa DRC, michuano ya CHAN 2024 kwenye nchi za Afrika Mashariki, hali ya Sudan, Somalia na mkutano wa rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, huko Alaska.
Miongoni mwa taarifa utakazoziskia ni pamoja na; sintofahamu yaendelea kuhusu kuanza kwa mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Kinshasa na Muungano wa Vikosi vya Kidemokrasia vya Ukombozi wa Kongo AFC/M23, Rais wa DRC, Felix Tshisekedi amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri na kujumuisha upinzani.
Tutakueleza punde zaidi katika uchaguzi wa Tanzania. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Afrika Magharibi na eneo la Sahel, yasema hali ya usalama katika eneo hilo inasalia kuwa ya wasiwasi mkubwa na kimataifa Rais wa Marekani, Donald Trump, asema huenda hivi karibuni akakutana ana kwa ana na rais wa Urusi, Vladmir Putin, kuzungumzia mzozo wa Ukraine.
Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo juma hili zilifanya mkutano wa kwanza wa kamati ya pamoja ya usimamizi , kesi ya rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila ilisikilizwa kwa mara ya pili mjini Kinshasa, serikali ya Tanzania, ilipiga marufuku raia wa kigeni kufanya biashara ndogondogo, hali nchini Sudan kusini na Sudan, hatua ya rais wa Cote D’Ivoire kutangaza nia ya kuwania urais kwa muhula wa nne na kwengineko duniani.
Kesi ya rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila ilifunguliwa mjini Kinshasa, waziri wa zamani wa sheria nchini DRC Constant Mutamba alikana mashtaka dhidi yake Kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma, ripoti moja wiki hii ilisema Watu 65 waliuawa nchini Kenya kufuatia maandamano ya vurugu kati ya mwezi juni na julai, hali nchini Sudan kusini na Sudan lakini pia tutaangazia Afrika magharibi na mengine mengi
From the publisher's feed
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners