Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii episodes

  • DRC na waasi wa M23 kukubaliana kuhusu amani ya mashariki, Humphrey polepole akosoa CCM

    Serikali ya Kinshasa na waasi wa AFC/M23 mbioni kusaini makubaliano ambayo kimsingi yanaleta matumaini ya kufikia amani mashariki mwa nchi hiyo, Tanzania yazindua dira ya maendeleo 2050 kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, umoja wa mataifa wasema hali ya kibinadamu nchini Sudan si ya kuridhisha, rais Paul Biya, kiongozi mkongwe sana duniani na umri wa miaka 92 kuwania urais kwa muhula wa nane, umoja wa ulaya kutishia kuiwekea Urusi vikwazo vipya na hali ya nchini Syria

    21 min
  • Rais Ruto aibua hisia kali kwa kuwaagiza polisi kuwapiga risasi ya miguu waandamanaji

    Wiki hii watu wasiopungua 38 waliuawa nchini Kenya kufuatia maandamano ya SabasAba siku ya Jumatatu. Rais Ruto aliibua hisia kali alipowaagiza polisi kuwapiga risasi ya miguu waandamanaji.

    Lakini pia, malalamiko yaliwasilishwa rasmi huko Brussels, dhidi ya wanafamilia tisa wa rais wa DRC Félix Tshisekedi, ambao wana uraia wa Ubelgiji, wakituhumiwa kwa wizi wa madini ya nchi yao.

    Tutakujuza pia taarifa za kikao cha Rais wa Marekani Donald Trump na marais sita wa Afrika magharibi kilichofanyika, lakini pia Uingereza na Ufaransa kutangaza rasmi mpango wa majaribio wa kuwarudisha Paris baadhi ya wahamiaji wanaowasili nchini humo kwa kutumia boti ndogo.

    21 min
  • Rais Kagame na Makubaliano ya Washington DC na mazishi ya Albert Ojwang Kenya

    Yaliyoangaziwa katika makala hii ni pamoja na kauli ya rais wa Kenya kujenga kanisa ndani ya ikulu ya Nairobi, rais Paul Kagame wa Rwanda na mkataba wa amani ulioisainiwa kati ya nchi yake na DRC, waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa kutogombea tena ubunge kuwakilisha jimbo la Ruangwa, hali nchini DRC, Sudan na kauli ya Ufaransa kuwa inatarajia Algeria kumsamehe mwandishi wa vitabu Boualem Sansal aliyefungwa, lakini pia mkutano wa viongozi wa Ulaya kule London Uingereza kufanyika wiki ijayo

    21 min
  • Maandamano mapya yaua 16 Kenya, DRC na Rwanda zasaini makubaliano ya amani

    Wiki hii ulimwengu umeshuhudia matukio mengi ya ajabu na hatari sana kwa usalama wa nchi mbali mbali, kwanza nchini Kenya watu 16 waliuawa katika maandamano ya kuadhimisha mwaka mmoja wa mauaji ya vijana Gen Z, Rwanda na DRC zatia saini mkataba wa amani kumaliza vita vya mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, siasa za Chad, Zambia na pia mashambulizi kati ya Israeli na Iran, pamoja na mkutano wa jumuia ya NATO..na mengine mengi

    21 min
  • Israeli na Iran zaendelea kushambuliana, matukio mengine duniani

    Mashambulio makubwa kwa makombora kati ya Israeli na Iran, na hali inayoendelea hadi sasa, maandamano ya kupinga kifo cha mwanablogu Albert Ojwang yaliyofanyika baada ya naibu Inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat kutangaza kujiuzulu nafasi kupisha uchunguzi, hali ya kisiasa nchini DRCbaada ya waziri wa sheria Constant Mutamba kujiuzulu, na vile vile siasa za ukanda wa Afrika mashariki, Afrika ya magharibi na kaskazini na kwengineko duniani.-

    21 min
  • Mauaji ya mwanablogu nchini Kenya, Marekani yataka Jeshi la Rwanda kuondoka DRC

    Mengi yamejiri nchini Kenya na maeneo mengine wiki hii lakini kubwa ni maandamano ya kupinga mauaji ya kijana Albert Ojwang na kutaka maafisa wa polisi waliohusika wajiuzulu, wiki hii Marekani iliitaka nchi jirani ya Rwanda kuwaondoa wanajeshi wake kwenye ardhi ya DRC kabla ya kusainiwa kwa mkataba wa Washington, pia utasikiliza mengine mengi kwengineko duniani

    21 min
  • Rais mstaafu wa DRC Joseph Kabila mjini Goma, Ngugi wa Thiongo aaga dunia

    Makala ya wiki hii hadi mei 31 imeangazia kuwasili kwa rais mstaafu wa DR Congo Joseph Kabila katika mji wa Goma, kifo cha gwiji wa fasihi raia wa Kenya Ngugi wa Thiong'o kule Marekani, ripoti ya shirika la Amnesty International yasema zaidi ya watu elfu kumi waliuawa nchini Nigeria katika kipindi cha miaka miwili, Sidi Ould Tah kutoka Mauritania ndiye rais mpya wa Benki ya maendeleo ya Afrika, na Israeli kujenga makazi mapya katika ukingo wa Jordan.Ungana na mwandishi wetu Emmanuel Makundi 

    20 min
  • Kabila aondolewa kinga ya kushtakiwa na Seneti ya DRC, Lissu arejeshwa mahakamani Tanzania

    Miongoni mwa taarifa utakazoziskia ni pamoja na; Bunge la seneti nchini DRC lapiga kura ya kumuondolea kinga rais mtaafu Joseph kabila, Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na Mawakili mashuhuri kutoka nchini Kenya, wafukuzwa nchini Tanzania.

    Kwingineko, Mamlaka nchini Libya zagundua miili 58 iliohifadhiwa kwa muda katika chumba cha kuhifadhi maiti na Waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu awatuhumu viongozi wa Ufaransa, Uingereza na Canada kwa kuwapa nguvu kundi la Hamas.

    21 min
  • DRC: Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki wamtaka Rais Felix Tshisekedi kuwaamini viongozi wa dini

    Makala haya yanaangazia taarifa mbalimbali ikiwemo, Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC wamtaka Rais Felix Tshisekedi kuwaamini viongozi wa dini kusaidia kuleta amani na utulivu Mashariki mwa nchi hiyo na pia serikali ya Uganda yawasilisha mswada tata bungeni kuruhusu kesi za kiraia kupelekwa kwenye Mahakama ya kijeshi.

    Taarifa zingine ambazo utaziskia ni uongozi wa kijeshi nchini Mali wasitisha sheria kuhusu vyama vya siasa nchini humo na Mazungumzo ya ana kwa ana kati ya wajumbe wa Ukraine na Urusi yamefanyika wiki hii nchini Uturuki kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2022.

    20 min

About Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

From the publisher's feed

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

More shows like Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Siha Njema by RFI Kiswahili

Siha Njema

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners