
Sign up to save your podcasts
Or


Makala haya yanaangazia taarifa mbalimbali ikiwemo, Mmarekani Robert Francis Prevost, achaguliwa kuongoza kanisa katoliki duniani, akichukua jina la Papa Leo wa kumi na nne. Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema, chatumbukia katika sintofahamu zaidi kufuatia baadhi ya waliokuwa wajumbe wa kamati kuu ya chama, kutangaza kujiondoa kwenye chama hicho.
Tarifa zingine utakazoskia, silaha za China zilizoagizwa na taifa la Falme za Kiarabu zimepatikana zikitumika na wapiganaji wa RSF nchini Sudan, na nchi jirani za India na Pakistan zashambiliana kwa silaha nzito na kuzua wasiwasi mkubwa katika maeneo ya mipakani.
Makala hii imeamgazia kuuawa kwa mbunge wa Kasipul Charles Ong'ondo Were, kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa kwa pikipiki katika barabara ya Ngong Jijini Nairobi, jumatano, kukamatwa kwa mlinzi wake kiongozi wa chama cha upinzani cha NUP nchini Uganda, nao wawakilishi wa DRC na Rwanda wanaokutana Washington Marekani kusaini mkataba kuelekea makubaliano ya amani ya mashariki mwa DRC, siasa za Tanzania na kushambuliwa kwa kasisi wa kikatoliki na matukio kadhaa ya juma hili kutokea duniani
Makala ya yaliyojiri wiki hii imeangazia mazishi ya kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, DRC na Rwanda zatia saini makubaliano kuhusu njia ya kupatikana amani ya mashariki mwa Congo, siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi wa oktoba, ziara ya rais wa Kenya William Ruto huko China, hali ya vita ya Sudan, vita ya Ukraine na huko Gaza Israeli, ni miongoni mwa Habari kuu za dunia zilizojiri kwa juma hili.
Vita ya sudan Kuingia katika mwaka wa tatu wiki hii, Kenya yatangaza marufuku ya biashara ya figo baada ya ufichuzi, rais wa zamani wa DRC arejea nchini aliwasili mjini Goma huku Marekani ikiitaka nchi ya Rwanda kuondoa wanajeshi wake mashariki mwa nchi hiyo, tumeangazia siasa za Tanzania kuelekea uchaguzi wa Oktoba, kule Sahel na wito wa rais wa Ghana wiki hii akiwataka viongozi wa nchi hizo kuungana pamoja na pia mkutano wa Paris kuhusu hatima ya vita ya Ukraine
Matukio ya wiki: kukamatwa kwa mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania, Tundu Lisu, maadhimisho ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda mwaka 1994, mafuriko jijini Kinshasa huko DRC, hali ya sudan Kusini kutokana na kukamatwa na kuzuiwa nyumbani kwa makamu wa kwanza wa rais Riek Machar, uchaguzi wa Gabon, na pia mzozo wa kibiashara kati ya Marekani na mataifa mengine ulimwenguni ni miongoni mwa Habari kuu za dunia zilizojiri kwa juma hili.
Miongoni mwa matukio makubwa ya juma hili ni pamoja na ziara ya rais wa Uganda Yoweri Museveni, iliyotangulizwa na ziara ya wajumbe wa Umoja wa Afrika, nchini Sudan Kusini baada ya makamu wa rais wa nchini hiyo kukamatwa na kuzuiwa nyumbani kwake, kule DRC waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda waripotiwa kujiondoa katika mji wa Walikale mokowani Kivu kaskazini mashariki mwa DRC, tunaangazia Kenya, Uganda, nchi za Afrika mashariki na magharibi pia kwengineko duniani
Ni juma ambalo limeshuhudia kukamatwa kwa makamu wa kwanza wa rais wa sudan Kusini Riek Machar na kuzuiwa nyumbani kwake, rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye wiki hii aliishutumu Rwanda kwa kupanga kuishambulia nchi yake, waasi wa M23 kukutana na Kiongozi wa Qatar kule Doha,afisa wa polisi ya Kenya kule Haiti kutoweka, utawala wa kijeshi kule Niger kuzindua kipindi cha mpito cha miaka mitano, pia mashambulio ya Israeli kule Lebanon na mkutano wa Ulaya kuhusu Ukraine
Yaliyomo ni pamoja na Mkutano wa ana kwa ana kati ya rais wa DRC Felix Tshisekedi na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame mjini Doha Qatar, mapigano kule Sudan Kusini kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa white Army waliotiifu kwa makamu wa kwanza wa rais Riek Machar, Niger kujivua uanachama wa franchophonie, mashambulio ya Israeli kule Gaza, sintofahamu ya sitisho la mapigano kwa muda mfupi kati ya Urusi na Ukraine ni miongoni mwa habari kuu za dunia zilizojiri kwa juma hili.
Mazungumzo ya ana kwa ana kati ya DRC na waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda kuanza jumanne ya Marchi 18, SADC kusitisha operesheni zake mashariki mwa DRC, mapigano kule Sudan Kusini kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji waliotiifu kwa makamu wa kwanza wa rais Riek Machar, juhudi za kikanda kuyahamasisha mataifa ya Mali, Burkina faso na Niger kurejea tena kama wanachama wa ECOWAS, na sitisho la mapigano kwa muda mfupi kati ya Urusi na Ukraine, ni miongoni mwa yaliyojiri wiki hii
Rais wa Kenya William Ruto na aliyekuwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga wameungana kisiasa rasmi, hali ya mzozo wa mashariki mwa DRC Kuchukua sura mpya, vikwazo vya kiuchumi kuikumba nchi ya Rwanda kufuatia uungwaji mkono wake kwa kundi la waasi la M23, Kiongozi wa kijeshi wa Gabon jenerali Oligui Nguema kuwania urais mwezi ujao, mzozo wa kibiashara kati ya Marekani nchi mataifa kadhaa, lakini pia mzozo wa Ukraine na Urusi.
From the publisher's feed
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners