
Sign up to save your podcasts
Or


Pamoja na Bwana Zephaniah Kivungi, mkurugenzi wa tabianchi katika shirika la CIFF, tunaendelea na awamu ya pili ambapo nilikuahidi kuangazia ni kwa namna gani tunaweza kuhakikisha kuwa biashara ya kaboni zinawakilisha upunguzaji halisi wa gesi chafuzi.
Masoko ya kaboni, yapo kwa ajili ya kuwawajibisha watu na mashirika ambayo shughuli zao zinachangia katika uchafuzi wa hewa, ambapo wanahitajika kugharamia juhudi zinazofanywa na watu mbalimbali au jamii katika kupunguza hewa ya kaboni kwenye anga, kwa mfano upandani wa miti.
Nimemwalika, Zephaniah Kivungi, mkurugenzi wa tabianchi katika shirika la CIFF, ambaye atatusaidia kuelewa zaidi suala hili la masoko ya kaboni katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Madai ya wanaharakati pia yanaitaka serikali kusitisha mipango yoyote ya kutenga maeneo ya misitu kwa ajili ya matumizi mengine, kama vile ujenzi wa barabara, kudumisha marufuku ya ukataji miti ili kulinda misitu iliosalia nchini Kenya, na kuchukua hatua za haraka na thabiti dhidi ya shughuli za ukataji miti kinyume cha sheria na uporaji wa ardhi ndani ya maeneo ya misitu
Licha ya faida za kiuchumi, mashirika ya mazingira na wanaharakati wa mazingira wanasema kiwanda hicho ni tishio kwa mifumo ikolojia ya eneo la Pwani pamoja na riziki ya jamii katika eneo hilo.
Pamoja na Omar Elmawi, wakili wa mazingira na nishati kutoka Mombasa, tunajadili mradi huu wa Dangote ambao ujenzi wake unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 40 ijayo.
Mwaka huu ni maadhimisho ya saba ya siku ya kimataifa ya kutoa hamasisho kuhusu utupaji na upotevu wa chakula, ambao unachangia kati ya asilimia 8–10 ya utoaji wa gesi joto
Lengo la maendeleo endelevu nambari 12.3 linalenga kuona dunia ikipunguza upot’evu na uharibufuwa chakula kwa nusu ifikapo mwaka 2030.
Wananchi katika miji mbalimbali ya dunia wanahimizwa kuacha magari yao binafsi nyumbani na kukumbatia mbinu zingine za usafiri zilizo endelevu kama kutumia baiskeli au kutembea kwa miguu.
Makala haya yanaangazia namna baiskeli za umeme zinaweza kuwa moja ya suluhu ya uchafuzi wa hewa kwenye miji unaotokana na sekta ya usafiri.
Kenya inakabiliwa na changamoto ya plastiki zinazotumiwa mara moja tu kama vile mifuko inayotumiwa sokoni kupakia mboga ambazo huchangia katika uchafuzi wa mazingira licha ya kupigwa marufuku.
Ni Kutokana na hili ambapo wanaharakati wa mazingira wamekuja na mapendekezo mapya ya kukabiliana na tatizo hili, mbali na suluhu la uchakataji.
Moja ya matokeo ya mapendekezo haya ni kuiweka Kenya katika nafasi ya uongozi wa kikanda katika uvumbuzi wa mifumo ya kutumia tena bidhaa.
Hellen Kahaso Dena kutoka shirika la Greenpeace Africa amechambua swala hilo. Sikiliza zaidi kwa kubofya.
Rais akisema wafanyabiashara wa ndani wanahitaji kulindwa. Agizo lake limeibua mjadala kuhusu nafasi ya wageni katika biashara ndogo nchini Kenya.
Matumizi ya ufadhili wa hali ya hewa imekuwa swala kuu kwa wadau wa mazingira, kutokana na mianya ya ufuatiliaji.
Nchini Kenya, shirika la Transparency International, sasa linajaribu kuziba mwanya uliopo ambapowakenya watakuwa wakifuatilia miradi na matumizi ya fedha hizi nchini humo kupitia jukwaa jipya la mtandaoni la Climate Finance Watch Tool.
Kwa wavuvi katika ziwa Niavasha, kama vile Simon Macharia na Joseph Kimani, Magugu maji yamekuwa kero kwa muda mrefu, na wakati mwingine kuwasababishia hasara.
Lakini sasa kutokana na ubunifu wa Joseph Nguthiri, kijana bingwa wa dunia wa Mazingira wa UNEP mwaka wa 2025, na mwanzilishi wa kampuni ya Hyapak wavuvi wanaweza kujipatia kipato zaidi.
From the publisher's feed
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners