Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii episodes

  • Rwanda na DRC zasaini mkataba wa amani Washington, chanjo ya ukimwi yaanza Afrika

    Habari kuu wiki hii ni pamoja na mkataba wa amani uliosainiwa kati ya Rwanda na Drc chini ya usimamizi wa Washington, tutaangazia siasa wa Uganda na Tanzania, halkadhalika hali ya kibinadamu nchini Sudan, WHO kuonya kuhusu ongezeko la maambukizo na vifo kutokana na Malaria.

    Tutaangalia hali kule Guinea Bissau baada ya mapinduzi, tutachambua kesi ya ufisadi inayomkabili Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, lakini pia mkutano kati ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa China Xi Jinping.      

    20 min
  • Rais Kagame aishutumu DRC kwa kuchelewesha amani, uchaguzi mdogo Kenya

    Rais wa Rwanda Paul Kagame atuhumu DRC kwa kuchelewesha mchakato wa kumaliza vita mashariki mwa DRC, uchaguzi mdogo nchini Kenya wafuatiwa na kushambuliwa kwa mbunge wa HomaBay Town Peter Kaluma, mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea Bissau, rais wa Marekani Donald Trump asema anapanga kuzuia raia kutoka Nchi zinazoendelea kuingia nchini Marekani,tutaenda Israeli, na maeneo mengine duniani…hayo ni miongoni mwa mengi utakayosikia. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka, kusikiliza zaidi

    21 min
  • Wanafunzi zaidi ya 200 watekwa Nigeria, tume ya kuchunguza vurugu Tanzania yaapishwa

    Habari kuu wiki hii ni siasa za Tanzania zilizosababisha kuundwa kwa tume ya kuchunguza mauaji ya baada ya uchaguzi, kule DRC athari ya mafuriko, tutaangazia ripoti ya WHO kuhusu dhulma dhidi ya wanawake, kule Nigeria tutaangalia utekaji nyara wa wanafunzi zaidi ya 200 pia Mkutano wa G20 kufanyika wikendi hii Afrika Kusini Marekani ikisusia.

    Mkutano wa COP30 wakamilika Brazil bila mwafaka kuhusu kuachana na mafuta kisukuku. 

    20 min
  • Rais Samia atoa msamaha kwa vijana waliokamatwa kwenye maandamano

    Miongoni mwa tarifa utakazoskia katika makala haya ni pamoja na, Rais wa Tanzania Samia Suluhu, ameagiza vyombo vya sheria kuangalia uwezekano wa kuwafutia mashtaka ya uhaini mamia ya vijana waliokamatwa kufuatia vurugu za uchaguzi wa Octoba 29, lakini hayo yakijiri kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa CHADEMA Tundu Lissu ilihairishwa kwa muda usiojulikana.

    21 min
  • Uchaguzi mkuu Tanzania: Waangalizi wasema haukuzingatia vigezo vya demokrasia

    Katika makala yetu leo tunaangazia pakubwa Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania ambapo Rais Samia Suluhu aliapishwa siku ya Jumatatu kuongoza muhula wa pili, hata hivyo ni uchaguzi ambao ulikumbwa na utata huku waangalizi kutoka jumuiya ya Afrika kusini SADC na wale wa umoja wa Afrika AU wakisema haukuzingatia vigezo vya demokrasia.

    Tunaangazia pia taarifa ya Rais Paul Biya, wa Cameroon kuapishwa Alhamisi iliyopita kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa nane, huku upinzani ukiitisha maandamano kupinga matokeo yaliyompa Biya ushindi. Lakini pia tutaangazia kongamano la kimataifa la mazingira, COP30 ambalo linafanyika huko Belem, nchini Brazil, kati ya Novemba 10 na 21.

    21 min
  • Vurugu zaugubika Uchaguzi mkuu nchini Tanzania na hali nchini DRC

    Uchaguzi mkuu uliofanyika katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania, na ambao uligubikwa na maandamano; mkutano wa Paris nchini Ufaransa kuhusu amani ya mashariki mwa DRC na eneo la maziwa makuu, siasa za nchini Kenya, Uganda lakini pia mauaji yaliyotekelezwa na kundi la RSF nchini Sudan, hali nchini Cameroon na Madagascar, kurejewa kwa mashambulizi nchini Ukraine, na huko Israeli dhidi ya Hamas

    21 min
  • Rais W.Ruto amtunuku hayati Raila Odinga, nishani ya juu zaidi, hali mashariki ya DRC

    Hatua ya rais wa Kenya William Ruto kumtunuku aliyewahi kuwa waziri Mkuu na kiongozi wa upinzani nchini Kenya, hayati Raila Odinga, nishani ya juu zaidi nchini, kukamatwa kwa makamu mwenyekiti wa chama cha Chadema nchini Tanzania, John Heche, DRC na Rwanda zakubaliana juu ya mchakato wa upatikanaji wa amani chini ya upatanisho wa Marekani, uchaguzi wa urais nchini Cote D’Ivoire, na rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarcozy wiki hii alianza kukitumikia kifungo cha miaka mitano.

    21 min
  • Kenya yaomboleza kifo cha RAILA, Jukwaa jipya la kisiasa DRC lazinduliwa

    Miongoni mwa matukio makubwa yaliyojiri wiki hii ni pamoja na wakenya kuomboleza kifo cha mwanasiasa mashuhuri aliyewahi kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Raila Amolo Odinga, kuzinduliwa kwa jukwaa jipya la kisiasa : Okoa DR Congo, kuendelea kwa kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu kule Tanzania, kuapishwa kwa kiongozi wa kijeshi wa Madagascar, na matukio mengine duniani.

    21 min
  • Jeshi la Israeli kuondoka Gaza, rais wa DRC aitaka Rwanda kuchangia amani

    Habari kuu wiki hii ni pamoja Israel kuanza kuwaondoa wanajeshi wake kwenye baadhi ya maeneo ya  Gaza, rais wa Ufaransa amteua tena Sebastien Lecornu kuwa waziri mkuu huku kukiwa na mvutano wa kisiasa, rais wa DRC, Félix Tshisekedi, amtaka mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame, kuwaamuru waasi wa M23 kuacha vita mashariki mwa Congo, siasa za kikanda, yaliyojiri huko Morocco, mwanaharakati wa demokrasia nchini Venezuela, Maria Corina Machado, ndiye mshindi wa tuzo ya amani ya Nobeli ya mwaka wa 2025

    21 min
  • Hukumu ya kifo dhidi ya rais mstaafu wa DRC, kampeni za uchaguzi nchini Uganda

    Kumekuwa na hisia mseto kuhusu hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya rais mstaafu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, uzinduzi wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani nchini Uganda, hali ya nchini Tanzania wakati huu wananchi wakijiandaa kushiriki uchaguzi wa oktoba 29 mwaka huu, maandamano ya vijana Gen Z nchini Madagascar, na mashambulio ya mjini Manchester Uingereza.Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi 

    21 min

About Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

From the publisher's feed

Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea…

More shows like Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Wimbi la Siasa by RFI Kiswahili

Wimbi la Siasa

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Siha Njema by RFI Kiswahili

Siha Njema

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners