Wimbi la Siasa

Wimbi la Siasa

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Wimbi la Siasa episodes

  • DR Congo: Ni wakati mwafaka wa kuibadilisha katiba ya DRC ?

    Mjadala wa kuibadilisha katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umepamba moto. Wanasiasa wanaoegemea upande wa rais Felix Tshisekedi na chama chake cha UDPS wanaunga mkono mchakato wa katiba kubadilishwa. Upinzani wakiongozwa na naibu Spika wa Bunge la Seneti aliyejiuzulu Modeste Bahati Lukwebo, unapinga. Ni wakati mwafaka wa kuibadilisha katiba ya DRC ? 

    11 min
  • Nini hatima ya vita vya Marekani na Israeli nchini Iran ?

    Ni wiki ya tatu sasa, baada ya Marekani na Israeli zilipoanza kutekeleza mashambulizi ya kijeshi nchini Iran. Mataifa hayo mawili yanasema lengo la mashambulizi hayo ni kuhakikisha kuwa inaharibu kabisa miundo mbinu ya Iran kutengeneza silaha za nyuklia. Rais wa Marekani Donald Trump, anasema vita hivi vitamalizika hivi karibuni, lakini haifahamiki ni lini. Tunachambua.

    11 min
  • Kenya: Je, ushirikiano wa serikali kati ya vyama vya ODM na UDA unafanikiwa ?

    Umepita mwaka mmoja tangu chama tawala nchini Kenya UDA na kile cha upinzani ODM, vilipoingia kwenye makubaliano ya kisiasa na kutaja mambo 10 kama vita dhidi ya ufisadi, kupunguza deni la taifa, ujumuishwaji ulio sawa serikalini kama baadhi ya mambo ya kushughulikia baada ya maandamano ya vijana ya mwaka 2024. Je, mwaka mmoja baadaye mambo hayo yametekelezwa kwa kiasi gani ?  Tunachambua.

    11 min
  • Nini hatima ya vita vya Israel na Marekani nchini Iran ?

    Dunia inashuhudia vita katika ukanda wa Mashariki ya Kati, baada ya Marekani na Israeli kuishambulia Iran, tangu Februari 28. Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu wanataka Iran iache kutengeneza silaha za maangamizi, kuyaunga mkono makundi yenye silaha nje ya Iran na kubadilisha utawala. Kongozi wa kiroho Ayatolla Ali Khamenei, ameuawa katika vita hivyo. Nini hatima ya vita hivi ? Tunachambua.

    10 min
  • Vita vya miaka minne nchini Ukraine, nini suluhu ?

    Imetia miaka minne, tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, katika vita vikubwa tangu vile vya pili vya dunia barani Ulaya. Maelfu ya watu wameuawa, miji na miundo mbinu muhimu imeharibiwa nchini Ukraine. Rais Volodymyr Zelenskyy anasema mwenzake wa Urusi hajatimiza malengo yake ya vita. Kwanini suluhu haijapatikana miaka minne baadaye ?

    10 min
  • Kenya: Kwanini chama cha ODM kimegawanyika kuelekea uchaguzi mkuu 2027 ?

    Joto la kisiasa limeendelea kupanda kwenye chama cha siasa cha ODM nchini Kenya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Chama hicho kilichoanzishwa zaidi ya miaka 20 iliyopita na aliyekuwa Waziri Mkuu Marehemu Raila Odinga, kimegawanyika kwa makundi mawili. Kundi moja linaongozwa na Oburu Oginga, kaka yake Raila, linamuunga mkono rais William Ruto. Kundi lingine, linangozwa na Edwin Sifuna, Katibu Mkuu anayempinga Ruto. Nini hatima ya chama hiki ?

    11 min
  • Mazungumzo ndio suluhu ya changamoto zinazoikabili DRC ?

    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi amesema serikali yake ipo tayari kuongoza mazungumzo kati ya Wakongomani, ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hiyo, hasa utovu wa usalama, mashariki mwa nchi hiyo. Hata hivyo, Chama cha "Ensemble pour la République, kinachoongozwa na mwanasiasa mashuhuri wa upinzani Moise Katumbi, kinasema mazungumzo hayo yanaweza kufanyika tu iwapo yatawashirikisha wadau wote. Rais Tshisekedi, wanaotekeleza mauaji ya raia, hawapaswi kushirikishwa kwenye mazungumzo hayo. Tunachambua.

    11 min
  • Kenya: Nini suluhu ya mzozo wa chama cha ODM ?

    Chama cha ODM kilichoanzishwa na aliyekuwa Waziri Mkuu  nchini Kenya Hayati Raila Odinga, kinapitia mgawanyiko wa kisiasa kuhusu kumuunga mkono rais William Ruto kuwania urais kwa muhula wa pili. Viongozi  wa chama hicho wamegawanyika kuhusu mpango huo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Mvutano  huu unamaanisha nini ?

    11 min
  • Uganda: Museveni achaguliwa tena baada ya miaka 40 madarakani

    Rais Yoweri Museveni, mwenye umri wa miaka 81, na ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 40, alitangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa Januari 15 baada ya kupata asilimia 71.65 ya kura. Mpinzani wake wa karibu Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine mwenye umri wa miaka 43, alimaliza wa pili kwa kupata asilimia 24.72 ya kura. Bobi Wine amedai kuibiwa kura. Ushindi wa rais Museveni unamaanisha nini ?  

    11 min

About Wimbi la Siasa

From the publisher's feed

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe…

More shows like Wimbi la Siasa

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Siha Njema by RFI Kiswahili

Siha Njema

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners