Wimbi la Siasa

Wimbi la Siasa

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Wimbi la Siasa episodes

  • DR Congo: Wanasiasa wachuana kuhusu mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba

    Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kumeundwa miungano miwili ya kisiasa. Kundi la kwanza linaitwa "C4" linalounga mkono mabadiliko ya katiba, chini ya rais Felix Tshisekedi. Nao vigogo wa upinzani wakiongozwa na Martin Fayulu, Moïse Katumbi na wengine, wao wameunda C64" vuguvugu linalopinga marekebisho yoyote na kuilinda katiba ya sasa. Nini hatima ya makundi haya ? Tunachambua.

    10 min
  • Kwanini kampeni za mapema zimeanza nchini Kenya kuelekea uchaguzi wa 2027?

    Siasa za kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, zimeanza kupamba moto nchini Kenya, mwaka mmoja kabla ya wananchi kupiga kura. Rais mstaafu Uhuru Kenyatta amejitokeza waziwazi na kumkosoa mrithi wake William Ruto kwa namna anavyoongoza serikali. Ruto na washirika wake, wanamtaka Uhuru kuachana na siasa. Tunachambua kauli za viongozi hao wa kisiasa.

    10 min
  • Sheria mpya nchini Uganda yalenga vyama vya siasa vya upinzani

    Nchini Uganda, rais Yoweri Museveni ambaye aliapishwa Mei tarehe 12 kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano baada ya kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 40, ametia saini mswada tata unaolenga kudhibiti ushawishi wa kigeni nchini humo kuwa sheria. Ukiukwaji wa sheria hii mpya, adhabu yake ni kifungo cha hadi miaka 10 jela, kwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kuendeleza maslahi ya kigeni dhidi ya taifa la Uganda.

    11 min
  • Tanzania: Ripoti ya Tume imejibu maswali magumu kuhusu ukweli wa Oktoba 29 ?

    Nchini Tanzania Aprili tarehe 23, tume iliyoundwa kuchunguza matukio ya vurugu yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka 2025, ilitoa ripoti yake. Kwa mujibu wa tume hiyo, watu zaidi ya 500 walipoteza maisha, maelfu walijeruhiwa huku uharibifu wa mali wenye zaidi ya thamani ya Shilingi za nchi hiyo Bilioni 125. Je, ripoti hii imejibu maswali magumu kuhusu ukweli wa kilichotokea nchini Tanzania ?  Tunachambua.

    11 min
  • Kwanini Ruben Kigame, anataka kuwa rais wa Kenya 2027 ?

    Uchaguzi Mkuu nchini Kenya ni mwezi Agosti mwaka 2027, lakini wanasiasa mbalimbali wameanza kuonesha nia ya kugombea kiti cha urais. Miongoni mwao ni Ruben Kigame, mwanasiasa, mwanaharakati, mhadhiri, mwandishi wa Habari na mwanamuziki maarufu wa nyimbo za Injili. Yeye ni mlemavu wa Macho, ameamua kujitosa uwanjani, kutafuta uongozi wa nchi ya Kenya. Nini kimemsukuma ?  Wiki hii anazungumza na mwenzangu, Benson Wakoli.

    11 min
  • Mazungumzo mapya kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya DRC nchini Uswizi

    Awamu ya tisa ya mazungumzo ya amani kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yalianza siku ya Jumatatu  Aprili 13 nchini Uswizi. Ujumbe wa Qatar ambao ni wasuluhishi, akiwemo mjumbe wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika Massad Boulos, wanashiriki. Nini Ajenda ya mazungumzo haya ? Raia wa DRC wategeme nini ? Tunachambua.

    11 min
  • Harakati za watetezi wa haki za binadamu Mashariki mwa DRC

    Mashirika ya kutetea haki za binadamu yakiongozwa na Amnesty International, katika ripoti zao, yamekuwa yakionya kuwa maisha ya wanaharakati wa haki za binadamu, wana habari na viongozi wa mashirika ya kiraia yapo hatarini katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa M23, Mashariki mwa DRC. Wiki hii Ruben Lukumbuka, anazungumza na Jack Sinzaera, mwanaharakati maarufu kutoka Kivu Kaskazini.

    10 min
  • Viongozi wa ODM wanaweza kuungana tena baada ya mpasuko wa chama ?

    Chama siasa cha Orange Democratic Movement-ODM kinaendelea kugawanyika, kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2027 nchini Kenya. Tangu kufariki dunia kwa Raila Odinga, mwasisi wa chama hicho kikubwa cha upinzani, viongozi waandamizi wa ODM wameshindwa kuelewana kuhusu kuendelea kumuunga mkono rais William Ruto, anayetarajiwa kuwania tena urais kwa muhula wa pili. Nini hatima ya chama hiki ?

    11 min

About Wimbi la Siasa

From the publisher's feed

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe…

More shows like Wimbi la Siasa

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Siha Njema by RFI Kiswahili

Siha Njema

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners