
Sign up to save your podcasts
Or


Uchaguzi wa wabunge na urais nchini Uganda unafanyika Januari 15, 2026. Rais wa muda mrefu Yoweri Museveni ambaye ameongoza kwa miaka 40, anapambana tena na mpinzani wake mkuu Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine. Upinzani umelalamikia kunyanyaswa, wakati huu mtandao wa Interneti ukizimwa. Je, uchaguzi huu utakuwa huru na haki ? Tunachambua kutoka Kampala.
Rais Donald Trump, Januari 3, 2026, aliagiza operesheni maalum ya wanajeshi wa Marekani nchini Venezuela, kumteka kiongozi wa nchi hiyo Nicolas Maduro. Baada ya kitendo hicho ambacho kimelaaniwa duniani, Maduro alisafirishwa jijini New York na kufunguliwa mashtaka ya kuongoza biashara haramu ya dawa za kulevya nchini Marekani.
Tunachambua hatua hii ya rais Trump, inamaanisha nini ?
Matukio makubwa ya kisiasa tuliyochambua mwaka 2025 ni pamoja na kifo cha aliyekuwa mwanasiasa mashuhuri nchini Kenya Raila Odinga, uchaguzi wenye vurugu uliofanyika nchini Tanzania Oktoba 29 na kutiwa saini kwa mkataba wa kumaliza vita Mashariki mwa DRC, Desemba 04, jijini Washington DC nchini Marekani.
Baada ya shinikizo kutoka kwa Marekani, waasi wa M23/AFC waliondoka kwenye mji wa Uvira, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hata hivyo, rais Felix Tshisekedi ameelezea kitendo hicho kama kiini macho kwa jumuiya ya Kimataifa, kauli ambayo imeungwa na mkono na jeshi la FARDC wanaosema, waasi hao wamejificha katika milima inayopatikana na mji huo. Kuchambua kinachoendelea, tunaungana Mali Ali akiwa jijini Paris na François Alwende akiwa jijini Nairobi.
Hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, si shwari licha ya kutiwa saini kwa mkataba unaolenga kusitisha vita ambavyo vimekuwa vikiendelea kwa muda wa miaka 30. Waasi wa M23/AFC wameudhibiti mji wa Uvira. Marekani inaonya kuichukulia hatua Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao ambao sasa wameahidi kuondoa vikosi vyake katika mji huo, lakini kwa masharti. Tunachambua kwa kina.
Kampeni za uchaguzi nchini Uganda zimezidi kupamba moto kuelekea uchaguzi mkuu January 15 2025 ambapo Rais Yoweri Museveni aliyeingia madarakani mwaka wa 1986, anagombea tena muhula wa saba huku akishindana na wagombea wengine miongoni mwao mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi Ssentamu almaarufu Bobi Wine. Kampeni za mwaka huu zinafanyika huku mgombea wa Upinzani Bobi wine akilalamika kushambuliwa na maafisa wa usalama. Kupata mengi zaidi ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka
Makala ya wimbi la siasa, imeangazia hatua ya viongozi wa Rwanda na DRC ambao siku ya alhamisi desemba 04 watatia saini makubaliano ya amani, mbele ya rais wa Marekani Donald Trump hii ikiwa ni mwendelezo wa mapatano ya amani mashariki mwa DRC yaliyosimamiwa na Marekani yaliyotiwa saini na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili juni 27. Profesa Pacifique Malonga ni mchambuzi wa siasa akiwa Kigali Rwanda, pia Francois Alwende ni mtaalamu wa siasa za maziwa makuu akiwa Nairobi Kenya.
Chama kikuu cha upinzani nchini Kenya cha Orange Democratic Movement-ODM kina kiongozi mpya, Seneta Oburu Oginga, kaka yake kiongozi wa zamani wa chama hicho Hayati Raila Odinga aliyefariki dunia mwezi Oktoba. Je, atafanyaje, kukiunganisha chama hicho ambacho kinaonekana kugawanyika kuhusu ushirikiano wake na uongozi wa rais William Ruto ? Tunachambua.
Nchi za Afrika Mashariki za Kenya, Uganda na Tanzania, zimeendelea kushuhudia ongezeko la visa vya wakosoaji wa serikali kutekwa na kupotezwa. Hivi karibuni, wanaharakati wawili kutoka nchini Kenya, Bob Njagi na Nicholas Oyoo walitekwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita nchini Uganda, baada ya kuhudhuria kampeni za uchaguzi za Bobi Wine, waliachiwa baada ya shinikizo za watetezi wa haki za binadamu. Nani atakomesha utekaji ?
Machafuko yalikumba uchaguzi mkuu wa Tanzania, uliofanyika Oktoba 29, 2025 na rais Samia Suluhu Hassan kutangazwa mshindi kwa kupata asilimia 97.6 ya kura. Chama kikuu cha upinzani CHADEMA, kimesema ushindi wa Samia ni kichekesho cha demokrasia. Anapaswa kufanya nini ili kuirejesha Tanzania katika utulivu wa kisiasa ? Tunachambua.
From the publisher's feed
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners