Wimbi la Siasa

Wimbi la Siasa

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Wimbi la Siasa episodes

  • Rais Museveni ateuliwa tena kuwania urais nchini Uganda

    Kiongozi wa muda mrefu nchini Uganda Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 80, ameteuliwa na chama chake cha NRM, kugombea tena urais wakati wa uchaguzi mkuu uliopagwa kufanyika mapema mwaka 2026, baada ya kuwa madarakani miaka 40.

    Hii inamaanisha nini katika siasa za Uganda ?

    11 min
  • Je, mkataba kati ya DRC na Rwanda utaleta amani ya kudumu ?

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda, walitia saini mkataba wa amani, chini ya uangalizi wa Marekani, Juni Juni 27 2025, jijini Washington DC, unaolenga kurejesha amani ya kudumu Mashariki mwa DRC. Nchi hizo mbili zimekubaliana kushirikiana kuyaondoa makundi yenye silaha. Mkataba huu umepokelewa vipi nchini DRC ?

    11 min
  • Je, usitishwaji wa vita kati ya Israel na Iran utadumu ?

    Israel na Iran zimekubali pendekezo la rais wa Marekani Donald Trump, kuacha kushambuliana baada ya vita vya siku 12 vilivyosababisha vifo zaidi ya 600 nchini Iran na zaidi ya 20 nchini Israeli. Israeli ilianza mashambulio hayo, kwa kulenga vituo vya  nyuklia vya Iran  kwa lengo la kuizuia kutengeneza silaha za maangamizi. Je, usitishwaji huu wa vita utadumu ?

    11 min
  • Nini kipo nyuma ya mkataba wa ushirikiano kati ya Kenya na Falme za Kiarabu ?

    Serikali ya Kenya mwezi Januari 2025, ilisaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na nchi ya Falme za Kiarabu kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Mswada huo umezua pingamizi kubwa kutoka kwa wanaharakati, watunga será na wapinzani wa serikali na wanataka wabunge kuufanyia marekebisho.

    Je, kuna siasa gani kwenye mikataba ya Kimataifa inayotiwa saini kati ya serikali ya Kenya na nchi za kigeni ? Edgar Odari Mkurugenzi Mkuu wa, Econews Africa, na Torosterdt Alenga mchambuzi wa siasa za Kimataifa, wanathathmini.

    10 min
  • Trump azuia raia wa nchi 12 kuzuru Marekani

    Rais wa Marekani Donald Trump ameagiza raia wa nchi 12 hasa kutoka Afrika kutozuru nchi hiyo. Agizo hilo lilianza kutekelezwa Juni 9, 2025. Trump anasema amechukua hatua hii kwa sababu za kiusalama. Wakati hayo yakijiri, maandamano yamekuwa yakishuhudiwa katika mji wa Los Angeles, kupinga sera ya Trump ya kuwasaka na kuwafukuza nchini humo, wageni wanaoishi bila vibali. Tunachambua kwa kina.

    11 min
  • Sudan yampata Waziri Mkuu, vita vikiendelea kupamba moto

    Uongozi wa kijeshi nchini Sudan mwishoni mwa mwezi Mei, ulimteua mwanasiasa  na mwanadiplomasia mkongwe Kamil Idris, kuwa Waziri Mkuu mpya wakati huu vita vikiendelea kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF. Tangu kuanza kwa vita Aprili 2023, watu zaidi ya 20,000 wamepoteza maisha, huku wengine Milioni 15 wakikimbia makaazi yao, wakiwemo zaidi ya Milioni nne ambao wamekimbilia katika nchi jirani kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa. Nini hatima ya Sudan ?

    11 min
  • DR Congo: Kabila aondolewa kinga ya kutoshtakiwa, aripotiwa kufikia Goma

    Maseneta nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamemwondolea kinga ya kutoshtakiwa  rais wa zamani Joseph Kabila , ambaye ripoti zinasema alirejea Goma usiku wa Mei 25.Kiongozi huyo wa zamani, ameishtumu serikali ya rais Felix Tshisekedi na kuuita ya  Kidikteta. Hata hivyo, serikali ambayo inamtuhumu kiongozi huyo wa zamani kwa kushirikiana na waasi wa M23.

    11 min
  • Wanaharakati kutoka Kenya wafukuzwa nchini Tanzania

    Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na Mawakili mashuhuri kutoka nchini Kenya, akiwemo Martha Karua na Jaji Mkuu mstaafu Willy Mutunga, walifukuzwa nchini Tanzania, Mei 19, walikokuwa wamekwenda kama mashuhuda wa kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani Tundu Lissu. 

    Rais Samia Suluhu Hassan ameonya kuwa nchi yake haitaruhusu wanaharakati kutoka nje, kuvunja amani ya nchi yake. Tunachambua kilichotokea nchini Tanzania.

    10 min

About Wimbi la Siasa

From the publisher's feed

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe…

More shows like Wimbi la Siasa

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Siha Njema by RFI Kiswahili

Siha Njema

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners