Wimbi la Siasa

Wimbi la Siasa

By RFI Kiswahili
Download on the App Store

Wimbi la Siasa episodes

  • Rwanda na DRC zawasilisha mapendekezo kuhusu mkataba wa amani

    Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimewasilisha mapendekezo ya rasimu ya mkataba wa amani kwa Marekani, kujaribu kutafuta mzozo wa Mashariki mwa DRC. Nchi hizo mbili zinatarajiwa kutia saini mkataba wa kudumu mwezi Juni, jijini Washington. Harakati hizi, zitazaa matunda ?

    11 min
  • Kenya: Upinzani utamtikisa Ruto uchaguzi wa mwaka 2027 ?

    Wanasiasa wakuu wa upinzani nchini Kenya, wakiongozwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, Aprili 29 2025, walikutana jijini Nairobi kuanza mikakati ya kuunda muungano mpya, kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Je, muungano huu ambao pia umemjumuisha aliyekuwa Waziri wa usalama Fred Matiang’i, unaweza kumtikisa rais William Ruto  wakati wa uchaguzi huo ?

    11 min
  • DRC: Kabila aripotiwa kufikia Goma, huku chama chake kikifungiwa

    Rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila, Aprili 18, aliripotiwa kurejea nchini na kufikia jijini Goma, linalodhibitiwa na waasi wa M 23. Hata hivyo, taarifa hizi hazijathibitishwa rasmi. Serikali jijini Kinshasa, nayo imesitisha shughuli zote za kisiasa za chama chake cha PPRD. Kabila anashtumiwa na serikali kwa kuunga vitendo vya waasi hao.

    11 min
  • Tanzania: CHADEMA yashinikiza mabadiliko kabla ya Uchaguzi Mkuu

    Mwezi Oktoba 2025, wananchi wa Tanzania, watashiriki kwenye uchaguzi Mkuu, kuwachagua madiwani, wabunge na rais. 

    Hata hivyo, chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA, kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, kinashinikiza mageuzi kwenye sheria za uchaguzi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

    Je, kitafanikiwa katika harakati zake ?

    10 min
  • Mkuu wa majeshi nchini Kenya akemea wanaomtaka rais Ruto aondoke

    Mkuu wa Majeshi nchini Kenya, Jenerali  Jenerali Charles Kahariri na Mkuu wa idara ya ujasusi Noordin Haji, wameonya dhidi ya kampeni inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii na mikutano ya hadhara ya –Ruto Must Go- au Ruto lazima aondoke, inatishia hali ya kisiasa nchini Kenya na ni lazima, ikome.

    Je, jeshi la Kenya linaingilia siasa ? Tunajadili…

    11 min
  • Harakati za kumaliza mzozo wa DRC, nani atafanikisha ?

    Wiki hii tunaangazia kinachojiri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya Angola kujiondoa kama mpatanishi wa mazugumzo ya mzozo wa Mashariki mwa  nchi hiyo, rais Paul Kagame na Tshisekedi wakutana Doha na mazungumzo ya kisiasa yanayolenga kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, yazinduliwa jijini Kinshasa.

    Wachambuzi wetu ni Mali Ali, akiwa Paris na Francois Alwende akiwa jijini Nairobi.

    11 min
  • Nani ataisadia Sudan Kusini, isirejee kwenye vita ?

    Sudan Kusini inakabiliwa na wasiwasi wa kujipata tena kwenye vita vipya, kufuatia mzozo wa hivi punde kati ya vikosi vya rais Salva Kiir na Makamu wake wa kwanza wa Riek Machar, baada ya kushambuliana kwenye jimbo la Upper Nile.

    Nini kinaweza kufanyika kuzuia mzozo mpya ?

    Wachambuzi wetu ni Dokta Brian Wanyama, kutoka Kenya na Hamdum Marcel akiwa Mwanza, Tanzania.

    11 min
  • Serikali ya umoja wa kitaifa itasuluhisha mzozo wa DRC ?

    Wakati huu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inapoendelea kukabiliwa na changamoto ya usalama Mashariki mwa nchi hiyo, baada ya waasi wa M23 kuingia katika miji ya Bukavu na Goma, rais Felix Tshisekedi ametangaza mpango wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuwashirikisha wanasiasa wa upinzani.

    Tunajadili iwapo hatua hii itasaidia kutatua mzozo wa mashariki mwa DRC.

    11 min
  • Je, Raila ataegemea upande gani wa kisiasa ?

    Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga , yupo kwenye harakati za mashauriano ya kisiasa na wafuasi wake, kabla ya kutangaza mustakabali wake wa kisiasa baada ya kukosa uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika. Je, Raila ataegemea upande gani ? Tunachambua.

    10 min

About Wimbi la Siasa

From the publisher's feed

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe…

More shows like Wimbi la Siasa

Habari zote by RFI Kiswahili

Habari zote

0 Listeners

Habari RFI-Ki by RFI Kiswahili

Habari RFI-Ki

0 Listeners

Afrika Ya Mashariki by RFI Kiswahili

Afrika Ya Mashariki

0 Listeners

Changu Chako, Chako Changu by RFI Kiswahili

Changu Chako, Chako Changu

0 Listeners

Nyumba ya Sanaa by RFI Kiswahili

Nyumba ya Sanaa

0 Listeners

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii by RFI Kiswahili

Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

0 Listeners

Gurudumu la Uchumi by RFI Kiswahili

Gurudumu la Uchumi

0 Listeners

Siha Njema by RFI Kiswahili

Siha Njema

0 Listeners

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho by RFI Kiswahili

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

0 Listeners

Jukwaa la Michezo by RFI Kiswahili

Jukwaa la Michezo

0 Listeners

Muziki Ijumaa by RFI Kiswahili

Muziki Ijumaa

0 Listeners

Jua Haki Zako by RFI Kiswahili

Jua Haki Zako

0 Listeners

Talisman Brisé by RFI Kiswahili

Talisman Brisé

0 Listeners