
Sign up to save your podcasts
Or


Nini mustakabali wa eneo la mashariki ya DRC baada ya mkutano wa Luanda ambao uliitishwa na rais wa Angola kushindikana? Tarehe 15/12/2024 Rais Joao Laurenco wa Angola alikuwa amepanga kuwakutanisha marais wa DRC Félix Tshisekedi, na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame, mkutano ambao haukufanyika kwa sababu rais wa Rwanda hakuridhia kushiriki. Ruben Lukumbuka anazungumza na John Banyene wa mashirika ya kiraia mkoani Kivu Kaskazini mashariki mwa DRC na Al Haji Abdulkarim Atiki mchambuzi wa siasa za kimataifa akiwa Daresalaam Tanzania.
Nchini Ghana, rais wa zamani John Dramani Mahama alipata ushindi mkubwa na kumaliza uongozi wa miaka minane wa chama tawala New Patriotic Party (NPP) chake rais Nana Akufo-Addo, anayeondoka madarakani baada ya kuongoza kwa mihula miwili.
Siku 16 za uanaharakati dhidi ya ukatili wa kijinsia ni kampeni inayofanyika kila mwaka kati ya Novemba 25 hadi Desemba 10. Ni kampeni ya siku 16 inayolenga kuhamasisha umma jinsi ya kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. Siku hiyo ilianza kuadhimishwa rasmi mwaka 1991,siku hii inaongozwa na Kituo cha kimataifa cha Wanawake tarehe 10 ilichaguliwa rasmi kuwa siku ya kilele cha maadhimisho haya ikiambatana na siku ya haki za binadamu duniani.
Asante kwa kuendelea kuwa muaminifu kwa radio yako na kwa mtangazaji wako unaweza kumfollow kwa kubonyeza hapa Billy Bilali
Wakaazi wa jimbo la Somaliland, mojawapo wa êneo lililojitenga na Somalia zaidi ya miaka 30 iliyopita, tangu mwaka 2003 wamekuwa wakishiriki kwenye uchaguzi wa kumchagua rais na wabunge wao.
Fursa hiyo pia imekuja Novemba tarehe 13 mwaka 2024 ambapo wapiga kura Milioni 1 waliondikishwa na Tume ya Uchaguzi ya Somaliland wanamchagua rais atakayewatumikia kwa miaka metano.
Wagombea watatu wanatafuta urais wa jimbo hilo, akiwemo kiongozi wa sasa Muse Bihi Abdi, anayetaka muhula wa pili, lakini mpinzani wake mkuu ni Abdirahman Mohamed Abdullahi, maarufu kwa jina la "Irro,”.
Kwenye Makala ya Wimbi la Siasa, tunajadili umuhimu wa uchaguzi wa jimbo la Somaliland na umuhimu wake, kwenye Jumuiya ya Kimataifa, wakati huu, êneo hilo linapotaka kujitawala.
Nchini Musumbuji maandamano yamekuwa yakishuhudiwa baada ya upinzani kukataa kutambua ushindi wa mgombea wa chama tawala Daniel Chapo.
Aliyekuwa mgombea wa upinzani Venancio Mondlane, amekuwa akisisitiza kwamba alipokonywa ushindi, katika makala haya tunazama kujadili kile kinachoendelea nchini Musumbiji.
Wachambuzi wa siasa za kimataifa Lugete Mussa Lugete na Felix Arego wanafafanua hali nchini Msumbiji.
Nchini Kenya bunge la kitaifa na seneti limeidhinisha kuondolewa afisini kwa naibu rais Rigathi Gachagua, kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kueneza siasa za kikabila.
Makala haya yaliandaliwa mapema.
Hatma ya aliyekuwa naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua sasa utaamuliwa na mahakama baada ya mabunge yote mawili kumwondoa madarakani kwa njia ya hoja maalum
Hatua ya kuondolewa Gachagua ni dhihirisho ya kuvunjika kwa uhusiano kati ya rais William Ruto na naibu wake Gachagua ,matukio ambayo si mageni nchini Kenya.
Makala wimbi la siasa inaangazia maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kundi la Hamas, litekeleze shambulio baya zaidi kuwahi kutekelezwa huko Israeli, tukio ambalo lilianzisha vita ambayo imesababisha vifo kwa maelfu ya raia wa Kipalestina na maandamano duniani kote kupinga vita hiyo, wakati huu mzozo huo ukihofiwa kuenea katika mashariki ya kati. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka na waalikwa wake
Makala ya Wimbi la siasa inaangazia tukio la kutekwa na kuuawa, kwa wanasiasa wa upinzani kwenye nchi za Afrika mashariki,tukio la hivi punde likiwa ni kutekwa kwa mwanasiasa mwandamizi wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema Ali Kibao, na baadaye alikutwa ameuawa, na matukio haya yanaripotiwa pia nchini Uganda na DRC. Ungana na Ruben Lukumbuka pamoja na waalikwa wake Jawadu Mohamed ni mchambuzi na mtaalamu wa siasa za Tanzania akiwa Daresalaam Tanzania, pia Frankline M wa CMD nchini Kenya.
From the publisher's feed
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe…

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners