Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 09 Agosti 2024
    Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Flora Nducha akimulika watu wa jamii ya asili, mtoto kunyonyeshwa maziwa ya mama, matumizi ya magunzi ya msonobari kutengeneza mboji salama na mashinani ni  ujumbe wa mshairi mashuhuri duniani kutoka nchini Marekani.Kulinda haki za watu wa jamii ya asili za kujitenga kwa ridhaa na kuishi maeneo yao asilindio ujumbe wa mwaka huu wa siku ya kimataifa ya watu wa jamii ya asili dunia, ujumbe ambao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni sahihi na kila mtu anapaswa kuuzingatia.Afisa wa UNICEF nchini Tanzania akionesha kivitendo kile wanachohamasisha kwa akina mama yaani kunyonyesha watoto wao maziwa ya mama pindi wanapojifungua.Katika makala, Assumpta Massoi anamulika ni kwa vipi magunzi ya mbegu za msonobari yamegeuka lulu huko Tunisia na kuwa chanzo cha kipato kwa mhitimu wa Chuo Kikuu aliyekaa miaka 6 bila ajira.Ujumbe wa mshairi Amanda Gorman kuhusu vita inayoendelea huko Gaza na madhara yake kwa watoto.
    11 min
  • 07 AGOSTI 2024
    Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani, WHO na lile la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA, yamezungumzia umuhimu wa sitisho la mapigano huko Gaza ili kufanikisha utoaji wa chanjo kwa watoto dhidi ya magonjwa hatarishi kama vile polio-Maji safi na salama imekuwa ni mtihani mkubwa  Gaza na kutishia milipuko ya magonjwa limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF huku likifanya kila jitihada kusaidia waathirika-Makala leo inammulika kijana Willy Ng'ang'a kutoka  Kenya anayetumia sayansi kutatua changamoto za mazingira katika jamii kwa kutumia dungusikakati kusafisha maji-Na mashinani  tunaelekea Jijini Dhaka, Bangladesh kusikia ushauri wake Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bi Gwyn Lewis kwa wananchi Bangladesh kuhusu jinsi ya kulijenga upya taifa lao.
    10 min
  • 06 AGOSTI 2024
    Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha  anakuletea -Baada ya wiki kadhaa za maandamano makubwa na machafuko yaliyosababisha vifo vya zaidi ya vijana na raia 300 #Bangladesh sasa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Gwyn Lewis, amesema kufikia leo utulivu kiasi umerejea nchini Bangladesh -Nchini Uingereza ambako maandamano yaliyochochewa na taarifa potofu na za uongo yanazidi kusambaa Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi amesema ghasia hizo ikiwemo dhidi ya wasaka hifadhi zinashtusha na kila mtu bila utofauti wowote ana haki ya kujihisi salama kwenye jamii zao na kuishi huru bila hofu-Leo ikiwa ni miaka 79 tangu MArekani iangushe bomu la atomiki la nyuklia huko Hiroshima nchini Japani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni ajabu kuwa silaha hizo na tishio lake la kuzitumia bado havijaondolewa kwenye matumizi. -Mada kwa kina leo inamulika juhudi za Tanzania katika kutumia sayansi na teknolojia kusongesha lengo namba 16 la maendeleo endelevu linalohusu masuala ya sheria na haki.-Na mashinani tunabisha hodi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR katikashule ya Bombouthi ambayo inalishukuru shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa juhudi za kurejesha elimu
    11 min
  • GAZA: Kutoka Gaza hadi Abu Dhabi kupata matibabu sahihi
    Tangu kuanza kwa mzozo huko Ukanda wa Gaza mwezi Oktoba mwaka jana 2023 baina ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas mzozo ambao umesababisha vifo vingi, majeruhi, watu kupoteza kila kitu na wengine kutekwa, wiki iliyopita Ukanda huo umeshuhudia uhamisho mkubwa zaidi wa wagonjwa ambao wamepelekwa kupatiwa matibabu nje ya nchi.Jumla ya wagonjwa na majeruhi walio mahututi 85 wamefanikiwa kuondolewa kutoka Ukanda wa Gaza kwenda Abu Dhambi katika Falme za kiarabu katika operesheni iliyotajwa kuwa “ngumu sana” iliyotekelezwa kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO wakishirikiana na serikali ya Falme za kiarabu UAE pamoja na wadau wengine. Leah Mushi anatujuza zaidi katika makala haya.
    5 min
  • Hofu yatanda mzozo Mashariki ya Kati kusambaa zaidi
    Kamishina Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za binadamu Volker Türk leo ameonya juu ya ongezeko la hatari ya kusambaa kwa mzozo Mashariki ya Kati na kuzitaka pande zote husika kutoa kipaumbele cha kuwalinda raia. Flora Nducha na taarifa zaidiAsante Assumpta. Katika taarifa yake fupi iliyotolewa mjini Geneva Uswis  Kamishina Mkuu Türk amesema “Nina wasiwasi mkubwa juu ya hatari inayoongezeka ya mzozo mkubwa zaidi Mashariki ya Kati na ninazisihi pande zote husika katika mzozo huu, pamoja na nchi zenye ushawishi, kuchukua hatua za haraka ili kudhibiti hali hii ambayo imekuwa ni ya hatari sana.”Amesisitiza kuwa kwa hali yoyote ile “Haki za binadamu  na hasa ulinzi wa raia lazima iwe kipaumbele cha kwanza.”Kamishina Mkuu huyo wa Haki za binadamu amesema tayari, katika kipindi cha miezi 10 iliyopita ya mzozo huo, raia wengi wao wakiwa wanawake na watoto wamevumilia madhila na mateso yasiyoweza kuvumilika kutokana na mabomu na mtutu wa bunduki unaorindima kila uchao.Hivyo amesema “Kila kitu, na ninamaanisha kila kitu, lazima kifanyike ili kuepusha hali hii kusambaa zaidi na kutumbukia kwenye shimo ambalo litakuwa na matokeo mabaya zaidi kwa raia.”Tangu mzozo huo kuanza Oktoba 7 mwaka jana shirika la Umoja  wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa  Kipalestina UNRWA limesema zaidi ya watu 38,000 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 88,000 kujeruhiwa huku mateka zaidi ya 110 bado wanashikiliwa. 
    2 min
  • 05 AGOSTI 2024
    Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea-Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameonya juu ya ongezeko la hatari ya kusambaa kwa mzozo Mashariki ya Kati na kuzitaka pande zote husika kutoa kipaumbele cha kuwalinda raia-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania limetumia ukurasa wake wa X,  kuelezea mambo muhimu matatu ya manufaa ya maziwa ya mama kwa mtoto. -Makala yetu leo inatupeleka Gaza ambako shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO limesema wagonjwa 85 kutoka Gaza wamesafirishwa kwenda kupata matibabu huko Abu Dhabi katika Falme za kiarabu.-Na mashinani mwanaharakati Plamedie Ndaya kutoka Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, anawashauri wanawake wa Afrika kupigania kutambuliwa kwa haki zao.
    10 min
  • Utipatipwa waongezeka miongoni mwa watoto barani Afrika
    Utipwatipwa ni tatizo la afya la kimataifa na linalokua kwa kasi sana barani Afrika. Kati ya mwaka 2000 na 2016, idadi ya watu wazima wenye utipwatipwa au uzito wa kupindukia barani Afrika ilikaribia kuongezeka maradufu, na mwenendo huo huo sasa unaonekana kwa watoto. Cecily Kariuki wa Idhaa hii kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO amefuatilia kile ambacho mashirika ya Umoja wa MAtaifa na wadau wanafanya ili kukabiliana na changamoto hiyo ya kiafya duniani. Kwako Cecily!
    4 min
  • Utapiamlo una waathiri watoto wa Sudan
    Njaa na utapiamlo unaenea kwa viwango vya kutisha nchini Sudan huku takribani watoto milioni 3.6 wakikakabiliwa na utapiamlo. Wataalamu wa lishe huko Darfur Kaskazini wanaendelea kusaidia familia kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wake. Hata hivyo suluhisho la uhakika ni usitishaji wa mapigano ili kuweza kuruhusu misaada ya kibinadamu kufikia wote wenye uhitaji. Taarifa ya Bosco CosmasHali ya lishe kwa watoto ni ngumu sana katika maeneo mengi ya Darfur Kaskazini nchini Sudan kutokana na mzozo unaoendelea nchini humo pamoja na hali mbaya ya kiuchumi jambo linalowaweka watoto mtegoni, kupata magonjwa ya lishe ikiwemo utapiamlo. UNICEF na wadau wengine wa afya, wanafanya kazi kuhakikisha watoto wanapata tiba stahiki.Halima ni mtaalamu wa lishe huko kitongoji cha Tawila, Darfur kaskazini anasimulia hali ilivyoHALIMA – Sabrina“Nimefanya kazi katika masuala ya lishe tangu mwaka 2017. Watoto wanasumbuliwa sana na utapiamlo. Hakuna chakula cha kutosha kutokana na ugumu wa maisha wanaopitia familia nyingi za Darfur, familia hazina pesa ya kutosha kununua aina mbalimbali za vyakula, kwahiyo mtoto anaweza aina moja tu ya kwa mwezi mzima kama vile, uji. Hakuna matunda wala mboga mboga ama kitu chochote jambo linalosababisha utapiamlo.”Mbali na changamoto wazipatazo watoto, Halima anaeleza magumu anayopitia katika utendaji kazi wake.HALIMA – Sabrina“Ninafanya hii kazi ya kusaidia maisha ya Watoto, tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba hatujapokea mshahara wetu, hapa tupo wanne tu na tunafanya kazi usiku na mchana. Tunawapatia maziwa yenye virutubisho na pia matibabu kwa watoto wanaoharisha na kutapika na matibabu mengine ya kila siku. Hatuna vikonge wala majagi ya kutosha, tunatumia majagi ya kutengenezea maziwa, inaumiza sana kutokuwa na vitendea kazi hivi, iwapo hakutakuwa na chakula cha tiba wala maziwa ya tiba kwa ajili ya kuwapa hawa watoto itakuwa vigumu sana kuwapatia matibabu watoto hawa. Tunawafundisha wazazi hatua za kuchukua wawapo majumbani mwao na pia tunawafundisha kuhusu usafi na lishe. Tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunawapatia dawa na kuokoa maisha ya watoto huku tukiwa na matumaini kuwa watakuwa na afya njema na kupona utapiamlo”UNICEF Pamoja na wadau wengine wa afya wanaendelea kusambaza misaada ya lishe kwa watoto wenye utapiamlo hata katika maeneo ya vita ili kuendelea kuokoa maisha ya watoto hao ambao wapo hatarini zaidi. Misaada hiyo inawanufaisha zaidi ya watoto 240,000 wenye utapiamlo, katika mji wa Darfur.
    2 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners